Somo la 9: Yesu, Mpatanishi wa Agano Jipya

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Waebrania 9, Warumi 3, Waefeso 3
Swahili
Year: 
2022
Quarter: 
1
Lesson Number: 
9

 Somo la 9: Yesu, Mpatanishi wa Agano Jipya

(Waebrania 9, Warumi 3, Waefeso 3)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2020, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Unazifahamu dini ngapi? Kila dini ninayoifahamu inahusisha kafara ya namna fulani. Kafara hiyo ni sadaka kwa mungu wa dini hiyo au namna fulani ya malipizi ya dhambi. Kitu unachokimiliki kinatolewa. Ukristo ni tofauti kwa maana ya kwamba hatupati wokovu wetu kwa matendo yetu. Kutoa mali zetu hakutupatii uzima wa milele. Hata hivyo, tunayo dhabihu. Lakini dhabihu yetu ni tofauti kabisa na ile ya dini nyingine. Mungu wetu anajitoa kafara yeye mwenyewe, hatumtolei kafara. Hebu tuzame kwenye somo letu la Waebrania na tujifunze Zaidi!

  1.    Damu Itakasayo
    1.    Soma Waebrania 9:11-12. Hebu tuelewe vizuri mazingira haya. “Hema kamilifu zaidi” ni lipi?
      1.    Kitu gani kimo ndani ya hili “hema?” (“Patakatifu.”)
      1.    Nani aliyelitengeneza hema hili? (Halikuwa ya ulimwengu huu, na haikutengenezwa kwa mikono ya mwanadamu.)
      1.    Lengo la hili hema ni lipi? (Hema hili linaonekana kama hekalu la duniani lililojengwa wakati wa safari ya wana wa Israeli kutoka Misri. Kama hema takatifu la duniani, lengo lake ni kundoa dhambi za watu, ili kupata “uzima wa milele.”)
      1.    Tafsiri ya Biblia ya ESV inatafsiri “hema” kile ambacho tafsiri zingine zinasema ni “hekalu.” Kiuhalisia kwa Kiebrania inamaanisha kofia ya nguo au hema. Kwa kuwa hapa ni mahala pa kuishi, baadhi ya watafsiri wanadhani ni sahihi kuliita hekalu. Kwa nini hekalu la mbinguni liitwe “hema?” (Hekalu la jangwani lililojengwa wakati wa safari ya wana wa Israeli, lilitengenezwa kwa kuzingatia maelekezo ya Mungu, kiuhalisia lilikuwa ni hema. Rejea hii inaendana na kile kilichotendwa kupitia kwa Musa na kile kinachoendelea mbinguni.)
    1.    Soma Waebrania 9:13-14. Damu ya Yesu iliyomwagika kwa ajili yetu inatufanyia nini? (“Itasafisha dhamiri zetu na matendo mafu.”)
      1.    Hiyo inamaanisha nini?
        1.    Je, “matendo mafu” ni juhudu zetu za kuupata wokovu? Je, ni matendo maovu? Je, ni yote mawili?
      1.    Utaona kwamba kifungu cha 14 kinasema kuwa damu ya Yesu inapatikana “kwa Roho wa milele.” Hii “Roho wa Milele” ni kitu gani? (Roho Mtakatifu.)
      1.    Utaona kuwa mwishoni mwa kifungu cha 14 kinasema kuwa tunasafishwa matendo yetu mafu “tupate kumwabudu Mungu aliye hai.” Lengo la kafara ya Yesu kwa ajili yetu ni lipi? (Tumwabudu/tumtumikie.)
        1.    Ikiwa haya “matendo mafu” ni juhudi zetu za kuupata wokovu wetu, je, Mungu anatamani tumtumikie kwa namna gani?
        1.    Je, unakumbuka mjadala wetu wa Waebrania 6:12? Mungu anatuwazia “ukomavu,” ikimaanisha kuelewa pambano la kiroho kati ya wema na uovu. Tunaenda mbali zaidi ya kujiangalia nyakati zote ili kusahihisha upungufu wetu. Unaweza kusema kuwa Roho Mtakatifu anaingiaje kwenye pambano hili?
  1.   Wokovu Umepatikana
    1.    Hebu turukie kidogo mbele na tusome Waebrania 10:9-10. Je, mapenzi ya Yesu, utayari wa kufa kwa ajili yetu, unatutendea nini? (“Umetutakasa, mara moja tu.”)
    1.    Soma Waebrania 10:14. Hii ni ahadi nzuri sana. Je, kifungu hiki kinasema kuwa Yesu amekufanya kuwa “mkamilifu?” (Ndiyo, “umekamilishwa hata milele.”)
      1.    Je, tabia yako ndivyo inavyopaswa kuwa? Je, wewe ndiye Mkristo mkamilifu? (Hapana. Kifungu hiki pia kinasema kuwa “tunatakaswa.”)
      1.    Unawezaje kuwa “mkamilifu” na bado uko kwenye mchakato wa kutakaswa? (Tunatangazwa kuwa wakamilifu kutokana na kile ambacho Yesu amekitenda kwa ajili yetu pale msalabani. Lakini, maisha yetu ni kazi inayoendelea.)
    1.    Hebu turejee kwenye Waebrania 9 na tusome Waebrania 9:26. Unazielewaje kauli za kwamba Yesu “mara moja tu amefunuliwa” ili “azitangue dhambi?”
      1.    Dhambi bado iko hai miaka elfu mbili baadaye. Tunalielezeaje hili? (Kuhukumiwa kwako kutokana na dhambi zako kumekoma. Kumekomeshwa na Yesu bado anafanyia kazi tatizo la dhambi maishani mwako, lakini si kwa lengo la kuupata wokovu wako. Wewe ni mkamilifu sasa hivi.)
    1.    Soma Waebrania 9:27-28. Lengo la Yesu kwetu ni lipi? (Kuwaokoa wale wanaomngojea kwa hamu.)
      1.    Hii inatufundisha nini kuhusu mtazamo wa waliokombolewa?
  1. Mtazamo wa Wokovu
    1.    Soma Warumi 3:21-22. Nani anayestahili kukitegemea kile ambacho Yesu amekitenda msalabani? (“Wote waaminio.”)
    1.    Soma Warumi 3:23-24. Tunapaswa kuwa na mtazamo gani kwa Wakristo wengine? (Sote tumepewa dhabihu. Hatuko juu ya mtu mwingine. Hakuna “tofauti” (kif.22) kwenye suala la wokovu wetu.)
    1.    Soma Warumi 3:27-28. Nani anayestahili kujivunia wokovu wake? (Hakuna hata mtu mmoja! Yesu alitupatia wokovu, hatukujipatia sisi wenyewe.)
    1.    Soma Warumi 3:31. Je, hii inamaanisha kuwa kuitii sheria sio suala la muhimu tena? (Sio kwenye wokovu wetu. Lakini ukweli kwamba Yesu alikufa ili kutimiza matakwa ya sheria inaonyesha kuwa ni muhimu.)
      1.    Rejea nyuma na usome tena sehemu ya mwisho ya Warumi 3:21. Inamaanisha nini kusema kwamba Sheria na Manabii wanashuhudia haki ya Mungu? (Kama sheria haikuwa ya muhimu, Mungu angeipuuzia badala ya kuifia. Tunatakiwa kuwa na hilo kama sehemu ya mtazamo wetu.)
    1.    Soma Waefeso 3:14-16. Paulo yuko kwenye mateso anapoandika hili. Mtazamo wetu kwa Mungu unapaswa kuwaje pale tunapokabiliana na magumu? (Tunatakiwa kumgeukia Mungu na atatupatia Roho wake Mtakatifu ili kutuimarisha.)
      1.    “Utajiri wa utukufu wake” unahusikaje na msaada huu? (Mungu amekufa kwa ajili yetu. Yesu ametukomboa. Kwa kumbukumbu hii, je, tunaweza kumtumaini kutenda jambo jema? Naam!)
    1.    Soma Waefeso 3:17-19. Upendo wa nani unaelezewa hapa? (Upendo wa Yesu. Paulo anatufundisha kuwa katika nyakati zote, hususani nyakati za uhitaji, tunatakiwa kutafakari kafara ya Yesu kwa ajili yetu. Tafakuri hiyo inatubadilisha. Inatujaza upendo. Inatupatia mtazamo sahihi.)
    1.    Soma waefeso 3:20. “Nguvu itendayo kazi ndani yetu” ni ipi? (Roho Mtakatifu.)
      1.    Je, uwezo wa Roho Mtakatifu una ukomo?
      1.    Utaona kwamba tunachomwomba Mungu kimo ndani ya uwezo wa Roho Mtakatifu. Hiyo inatufundisha nini kuhusu maombi yetu? (Hakuna ukomo kwenye kile ambacho Mungu anaweza kututendea.)
      1.    Angalia pia lugha inayorejelea kile “tunachokiomba au kukifikiria.” Hii inazungumzia nini juu ya kile ambacho tungependa Mungu atutendee? (Inasema kuwa malengo yetu ni ya chini sana. Mungu anatuwazia mengi kwa ajili yetu kuliko vile tunavyoweza kudhania.)
        1.    Je, huu ndio uzoefu wako? (Huu ni uzoefu wangu. Takribani miaka ishirini iliyopita nilifanya uamuzi wa kuyaelekeza maisha yangu kwenye ufundishaji. Niliwazia kufundisha katika ngazi ya chuo kwenye shule inayomilikiwa na kanisa. Mungu alinifungulia milango kufundisha katika shule ya sheria ya Kikristo masomo ambayo nilikuwa nikishughulika nayo mahakamani! Lilikuwa jambo zuri sana, na zaidi ya nilivyodhania.)
    1.    Rafiki, Yesu amekuhakikishia wokovu wako. Ametenda kile usichoweza kukitenda. Yesu alifanya hivi kwa sababu amejawa upendo kwa ajili yako. Je, utaikubali ofa yake ya wokovu? Je, utalitumaini pendo lake kwa ajili yako? Kwa nini usijitoe kufanya hivyo sasa hivi?
  1.   Juma lijalo: Yesu Anafungua Njia Kupitia Kwenye Pazia.