Somo la 10: Yesu Anafungua Njia Kupitia Kwenye Pazia

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Kutoka 12, Mambo ya Walawi 23, Waebrania 10 & 12
Swahili
Year: 
2022
Quarter: 
1
Lesson Number: 
10

Somo la 10: Yesu Anafungua Njia Kupitia Kwenye Pazia

(Kutoka 12, Mambo ya Walawi 23, Waebrania 10 & 12)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2020, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Je, una “mapazia” yoyote maishani mwako? Mojawapo ya mgahawa mmoja ninaoupenda sana umewekwa kwa namna ambayo sharti upite kwenye pazia ili uweze kuingia ndani. Sina uhakika kuna mazingira ya usafi kiasi gani kwa kila mtu kujigusisha kwenye pazia hili. Yapo mapazia mengi ya kisomi maishani mwangu. Mapazia hayo yanahusisha mafundisho ambayo nina maoni yangu kuyahusu, lakini kila ninapojifunza zaidi ninatambua kuwa sina uelewa sahihi. Hekalu la jangwani, hekalu la Yerusalemu, yote mawili yalikuwa na pazia lililotenganisha patakatifu na vyumba vya patakatifu pa patakatifu. Hilo ndilo pazia tunalolichimbua juma hili. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tujifunze zaidi kuhusu kinachomaanishwa na mapazia haya maishani mwetu!

I.  Sikukuu na Ishara

A.  Soma Kutoka 12:3, Kutoka 12:5-7, na Kutoka 12:12-13. Kufuata maelekezo haya juu ya kumtoa kafara mwana-kondoo (au mbuzi) kuliwafanyia nini watu wa Mungu? (Kuliwaepusha wazaliwa wao wa kwanza kuuawa malaika alipopita juu na wazaliwa wa kwanza wa Kimisri waliuawa.)

B.  Soma Kutoka 12:14, Yohana 19:13-15, na Mathayo 27:45. Unaona uhusiano gani kati ya kusherehekea kipindi malaika alipopita juu na kusulubiwa kwa Yesu? (Kusherehekea kipindi alichopita malaika, na damu iliyowaokoa wazaliwa wao wa kwanza, kunatokea wakati ule ule Yesu anaposulubiwa.)

1.  Hebu tuliangalie hili kwa kina. Angalia tena Kutoka 12:6 na uilinganishe na Mathayo 27:46. Unajifunza nini juu ya muda ambao matukio hayo mawili yanatokea? (Kitabu cha Kutoka kinasema mwana-kondoo kwa ajili ya Pasaka alichinjwa “jioni.” Maoni ya “Vincent’s Word Studies” yanabainisha kuwa “saa tisa” iliyozungumziwa katika Mathayo 27:46 ilikuwa ni majira ya saa 9 za alasiri. Maoni ya John MacArthur yanafafanua kuwa Musa alielekeza kuwa kafara ifanyike “jioni” na Mwanahistoria wa Kiyahudi, Josephus, anafafanua kuwa ilikuwa ni utamaduni kumtoa kafara mwana-kondoo majira ya saa 9 za mchana.)

2.  Je, ni jambo litukialo kulingana na jingine kwa nasibu (coincidence) kwamba Yesu alikufa msalabani katika muda ule ule ambao mwana-kondoo wa pasaka alipochinjwa?

C.  Soma Mambo ya Walawi 23:4-6 na Mambo ya Walawi 23:15-16. Sikukuu ya Mkate Usiotiwa Chachu ilianza lini? (Siku ya Sabato baada ya Pasaka na inaendelea kwa juma zima.)

1.  Angalia rejea ya siku hamsini baadaye.  Hii ni Sikukuu ya Mavuno, pia ikijulikana kama “Pentekoste” (angalia Matendo 2:1) kwa Wakristo.)

D.  Soma Matendo 1:3-5 na Matendo 2:1-4. Badiliko gani linatokea kwenye Ukristo? (Hii ni karama iliyoahidiwa ya Roho Mtakatifu katika nguvu.)

E.  Uhusiano sahihi kati ya kifo cha Yesu na Pasaka, na uhusiano wake kwenye hizi sikukuu nyingine mbili unatufundisha nini? (Kwa hakika Yesu ndiye Mwanakondoo wa Pasaka aliyeahidiwa. Mungu anatumia Sikukuu ya Mavuno kama mwanzo wa mavuno mapya ya roho kwa njia ya uwezo wa Roho Mtakatifu.)

F.  Hebu tuangalie uhusiano mwingine. Soma Mathayo 27:50-51. Jambo gani linatokea Yesu anapokata roho? (Pazia la hekalu linapasuka vipande viwili.)

1.  Pazia hili lilikuwa sehemu gani? (Soma Kutoka 26:33. Lilitenganisha kati ya patakatifu na patakatifu sana. Hakuna muumini wa Kiyahudi ambaye angechana pazia kwa sababu waliogopa kifo kama wangeingia mahali patakatifu sana. Angalia Mambo ya Walawi 16:2.)

2.  Tunapaswa kuhitimisha nini kuhusu pazia kupasuka kutoka juu hadi chini? (Mtu asiye wa ulimwengu huu alitenda jambo hili. Pazia hili lilikuwa zito. Mwanadamu angejaribu kulipasua kuanzia chini, badala ya kulichana kuanzia juu. Na kwa kuongezea, hili lingekuwa jambo la hatari kwa mwanadamu kutokana na hatari ya kuingia kwa bahati mbaya mahali patakatifu sana.)

G.  Soma Waebrania 10:19-20. Kifungu hiki kinaashiria nini kuhusu asili ya pazia lililopasuka na yule aliyelipasua? (Mungu alilipasua. “Njia ile aliyotuanzia iliyo mpya…… ipitayo katika pazia.”)

II.  Pazia

A.  Hebu tuangalie zaidi kupasuka kwa pazia. Soma Waebrania 10:19-22. Inamaanisha nini kwa sisi “kupaingia patakatifu?” (Patakatifu sana ndipo mahali alimokuwemo Mungu. Hapa ndipo mahali ambapo mtu wa kawaida angekufa kama angeingia kwa sababu ya kuwepo kwa Mungu. Yesu ametufungulia “njia mpya iliyo hai” ikiwa ni matokeao ya kafara yake.)

B.  Soma Zekaria 3:1-2. Shetani amesimama wapi? (Mkono wa kuume wa Kuhani Mkuu.)

1.  Kuhani Mkuu yuko wapi? (Mbele ya “malaika wa Bwana,” na kumbukumbu ya Mungu kuongea inaashiria kuwa hii ni njozi ya mbinguni.)

C.  Soma Ufunuo 12:7-9. Hii inaweka kumbukumbu ya habari gani?

1.  Unafahamu jambo hili lilitokea nini?

D.  Soma Ufunuo 12:10-11. Hii inatuambia nini kuhusu kazi ya Shetani mshitaki? (Alipaswa kuhama. Hayupo tena mbinguni. Ametupwa chini duniani.)

1.  Hebu tulitafakari hili kidogo. Unadhani kwamba kupasuka kwa pazia, kunakoashiria kuingia kwetu mbele za Mungu, kunahusiana na kundoka kwa Shetani kutoka mbele za Mungu? (Inaonekana vinahusiana. Shetani ameondoka. Yesu anaturuhusu kuingia mbele za Mungu. Bwana asifiwe!)

III.  Kuingia Kwetu

A.  Soma Waebrania 12:21. Tukio gani linahusisha Musa kutetemeka kwa hofu? (Soma Kutoka 19:16-19. Hii inarejelea kipindi cha kutolewa kwa Amri Kumi katika Mlima Sinai. Watu walitakuwa “waonane na Mungu.” Kilikuwa kipindi cha hofu kwa sababu uwezo wa Mungu ulikuwa unadhihirishwa.)

B.  Soma Kutoka 19:21. Nini kingetokea kama watu wangemwangalia Mungu? (Wangeangamia.)

C.  Soma Waebrania 12:22. Utaona kwamba kifungu cha 22 kinaanza kwa kusema “bali ninyi.” Hii inaashiria badiliko gani? Picha imebadilikaje? (Hii ni taswira ya mbinguni. Inatutambulisha kwenye dhana ya kwamba sasa tuna uzoefu tofauti kabisa tofauti na ule waliokuwa nao watu katika Mlima Sinai.)

1.  Ni kwa namna gani uzoefu unatofautiana? Hii inalinganishwaje na kwenda mahali ambapo Mungu anakaa kule mbinguni? (Mwonekano huu mpya ni wa sherehe. Panaonekana kama mahali ambapo watu na malaika wanafurahia.)

D.  Soma Waebrania 12:23-24. Utaona hii inazungumzia kuwa tunakwenda “kwa Mungu.” Je, unadhani hii inamaanisha kwamba tunamwona Mungu? (Hicho ndicho kinachoashiriwa. Sasa tunaweza kumwona Mungu na tusife.)

1.  Unalihusianishaje hili na pazia kupasuka na patakatifu sana kufunguliwa kwa ajili ya kuangaliwa? (Vifungu hivi vinaendana na dhana ya kwamba Yesu anaturuhusu kuingia patakatifu sana pa hekalu – mabali abapo uwepo wa Mungu uliweza kupatikana. Hekalu hili lipo mbinguni ambapo tunamwona Mungu.)

E.  Soma Yohana 5:24. Chini ya mfumo wa kale, watu wangekufa kama wangemwona Mungu. Kwa nini? (Kwa sababu walikuwa wadhambi na yeye ni Mungu mtakatifu.)

1.  Unaona nini kwenye kifungu hiki kinachoelezea kwa nini sasa tunaweza kuingia mbele za Mungu? (Tumevuka kutoka mautini hadi kwenye uzima wa milele. Hatuingii hukumuni.)

2.  Jambo gani linahitajika kwetu ili kuweza kuvuka? (Kulisikiliza neno la Mungu na kumwamini Yesu.)

F.  Rafiki, je, ungelipenda hilo litokee sasa hivi? Je, ungependa kupita kwenye pazia, upite kutoka mautini hadi kwenye uzima ili uweze kusimama mbele za Mungu? Kwa nini usifanye uamuzi huo sasa hivi?

IV.  Juma lijalo: Yesu, Mwanzilishi na Mwenye Kutimiza Imani Yetu.