Somo la 9: Yakobo Mtwaa Mahali Pa Wengine

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Mwanzo 25–29
Swahili
Year: 
2022
Quarter: 
2
Lesson Number: 
9

Somo la 9: Yakobo Mtwaa Mahali Pa Wengine

(Mwanzo 25–29)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2020, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Je, umewahi kuyasikia maneno, “Lile ulitendalo ndilo likupatalo?” (What goes around, comes around?) Katika maisha nimebaini kwamba mambo mabaya ambayo watu wanayasababisha kwa wengine yanaishia kuwa mabaya hayo hayo ambayo watu hao wanaishia kuyapata mikononi mwa watu wengine. Juma hili tunaliona hili likitokea kwenye somo letu la Yakobo na Esau. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tujifunze zaidi!

  1.    Uzao wa Isaka
    1.    Soma Mwanzo 25:19-21. Jiweke kwenye nafasi ya Isaka. Biblia inahabarisha kuwa Rebeka, mkewe, ni tasa. Unapoyatafakari maisha yako, je, unayatafakari maisha ya wazazi wako? Je, unatafakari jinsi walivyoshughulika na mambo yanayofanana na hayo?
      1.    Kama niko sahihi juu ya mawazo ya Isaka, unadhani alikuwa na mwitikio gani kwa maombi yake kujibiwa mara moja? (Lazima alishukuru.)
      1.    Je, kuna kumbukumbu yoyote hadi kufikia hapa inayomwonyesha Isaka kutokuwa mwaminifu kwa Mungu au kuanguka kiimani? (Sio katika tulichokisoma hadi kufikia hapa. Juma lililopita tulijifunza kwamba Isaka aliruhusu kufungwa kamba wakati wa maandalizi ya kuuawa kutokana na amri ya Mungu. Baba yake, Ibrahimu, alikuwa shujaa wa imani katika kipindi hicho, lakini inaonekana kuwa vivyo hivyo kwa Isaka.)
    1.    Soma Mwanzo 25:22-24. Tunajifunza nini kuhusu tabia ya Rebeka? (Rejea zote zinazomhusu hadi kufikia hapa ni chanya sana. Anamwendea Mungu na swali lake, naye Mungu anamjibu!)
      1.    Zingatia kifungu cha 23. Hii inatufundisha nini juu ya uhuru binafsi wa uchaguzi? (Inatufundisha kwamba kwa asili tunafahamu, kwamba baadhi ya watu wanazaliwa wakiwa na manufaa fulani. Hata hivyo, hilo halituwekei ukomo wa uhuru wetu binafsi wa uchaguzi.)
    1.    Soma Mwanzo 25:25-26. Hebu tupitie jambo tulilolijadili hapo awali. Mwanzo 25:21 inaonyesha kama vile Rebeka alikuwa mjamzito mara tu baada ya Isaka kumwomba Mungu. Tunajifunza nini hapa? (Mwanzo 25:20 inatuambia kuwa Isaka alikuwa na umri wa miaka 40 walipooana. Na Mwanzo 25:26 inatuambia kuwa alikuwa na umri wa miaka 60 wakati mapacha walipozaliwa.)
      1.    Isaka alisubiria kwa muda wa theluthi moja ya maisha yake ili kuwapata wanaye. Hiyo inatufundisha nini?
    1.    Hebu tuchukue njia ya mzunguko kidogo ili kuangalia kama Isaka ni shujaa wa imani. Soma Mwanzo 26:6-7. Je, Isaka anamtumaini Mungu? (Hapana, kama ilivyokuwa kwa baba yake Abramu, anautegemea na kuutumaini uongo. Yumkini huo ucheleweshaji wa miaka ishirini ulidhamiria kumsaidia katika imani yake.)
    1.    Soma Mwanzo 25:27–28. Unaona tatizo gani hapa? Je, sasa tunaona kasoro za kitabia kwa Isaka na Rebeka?
      1.    Kiuhalisia kifungu kinasema kuwa Isaka alimpenda Esau kwa sababu ya chakula. Jiweke kwenye nafasi ya Isaka. Je, ungempenda mwindaji mwenye makunyanzi tofauti na mtu “mpole” anayependelea kukaa hemani? (Esau anaonekana kuwa kama “mtu wa baba” (a man’s man). Maoni ya Adam Clarke yanatusaidia kuliangalia jambo hili kwa utofauti. Anataarifu kuwa Yakobo alikuwa anafuga na kutunza ng’ombe, “jambo lililochukuliwa kama ajira sahihi kabisa katika nyakati hizo za zamani.” Hii inatuambia kuwa Yakobo ni msomi, akiishi kwa kutegemea kujifunza ufugaji. Esau anaishi kwa kutegemea ushindi.)
  1.   Udanganyifu
    1.    Soma Mwanzo 25:29-31. Hii inazungumzia nini juu ya tabia ya Yakobo? (Ndugu mlafi, asiye na upendo kiasi gani! Jibu sahihi linapaswa kuwa “Ndiyo, ndugu yangu! Nimekula nyama nyingi ya wanyama uliowawinda. Siku yako ilikuwaje?”)
    1.    Soma Mwanzo 25:32-34. Hii inazungumzia nini juu ya tabia ya Esau? (Hayuko makini. Haoni thamani ya haki ya uzaliwa wa kwanza.)
      1.    Nani kati ya ndugu hawa wawili ana hali mbaya zaidi? (Kura yangu inamwangukia Yakobo. Esau anaonekana si mkomavu. Yakobo ni mlafi mwenye hila.)
    1.    Hebu turukie hadi kwenye sura mbili mbele. Soma Mwanzo 27:6-7. Isaka ana dhamira gani kwa Esau? (Anataka kumbariki.)
      1.    Je, baraka hii ni sawa na haki ya uzaliwa wa kwanza? (Soma Kumbukumbu la Torati 21:15-17. Uzaliwa wa kwanza ni “mafungu mawili” ya mali za baba.)
      1.    Je, ni jambo la pekee kwamba Isaka anamwambia Esau peke yake juu ya mpango wake? Hamwambii mkewe na wala haandai kusanyiko la kifamilia juu ya suala hili la baraka?
    1.    Soma Mwanzo 25:23. Mungu anaahidi nini linapokuja suala la vijana wawili? (Hii haionekani kama haki ya uzaliwa wa kwanza.)
    1.    Soma Mwanzo 27:8-12. Kwa nini asiamini baraka za Mungu badala ya kuutumaini uongo?
      1.    Ni aina gani ya baraka uipatayo kutokana na udanganyifu?
      1.    Ungependekeza mpango gani mbadala kwa Yakobo na Rebeka? (Rebeka alipaswa kumwambia Isaka kile alichoambiwa na Mungu kuhusu wana wawili na nani atakayemtumikia mwingine. Kwa upande mwingine, ukweli kwamba Isaka anamwambia Esau kwa siri kuhusu baraka inaashiria kwamba Isaka anajua kile ambacho Mungu anakitaka.)
    1.    Soma Mwanzo 27:13. Je, Rebeka analaaniwa ikiwa ni matokeo ya jambo hili? (Ndiyo, kwa maana ya kwamba Yakobo anaondoka na anakufa kabla hajarejea. Kamwe hamwoni mwanaye tena – kijana ampendaye.)
    1.    Soma Mwanzo 27:15-20. Je, ungefanya hivi? Je, ungedai baraka za Mungu ili kuunga mkono udanganyifu wako?
    1.    Soma Mwanzo 27:21-24. Utaona kwamba Isaka ana mashaka makubwa juu ya mwana anayembariki. Kwa nini hawaiti watu wengine ili kuthibitisha utambulisho wa mtu anayetaka kumbariki? (Hii ni ishara nyingine kwamba anajaribu kufanya jambo hili kwa siri.)
    1.    Soma baraka yenyewe katika Mwanzo 27:28-29. Je, hii ni haki ya uzaliwa wa kwanza? (Sio kwa umahsusi. Badala yake, kama ikitolewa kwa Esau moja kwa moja itakinzana na ahadi ya Mungu (Mwanzo 25:23) kwamba Esau atamtumikia Yakobo.)
    1.    Baada ya Isaka kumbariki Yakobo, Esau anawasili na chakula chake kwa ajili ya kupata baraka yake. Soma Mwanzo 27:32-33 na Waebrania 11:20. Inawezekanaje kusema kuwa Isaka “kwa imani” akambariki Yakobo?
      1.    Kwa nini Isaka anasema kuhusu Yakobo, kwamba “naye atabarikiwa?”
      1.    Na, kwa nini Isaka alitetemeka sana alipoutambua udanganyifu? (Sioni sababu kwa nini Isaka hakuweza “kutatua” tatizo la udanganyifu mara moja, isipokuwa kwamba alijua kuwa alikuwa anaenenda kinyume na mapenzi ya Mungu. Hiyo ilimsababisha atetemeke na kukiri kwamba baraka itasalia kwa Yakobo.)
    1.    Soma Mwanzo 27:41-43. Baraka hii inageuka na kuwaje hadi kufikia hapa?
  1.      Ahadi
    1.    Soma Mwanzo 28:10-15. Ahadi iliyotolewa kwa Ibrahimu na Isaka sasa inatolewa kwa Yakobo. Je, hiyo ni sahihi? (Tuliona kwamba Ibrahimu, Sara, Isaka, na Rebeka wote walikuwa na shida katika kuamini ahadi za Mungu. Wote waliutegemea uongo. Uongo wa Yakobo unaonekana kuvuka mipaka, lakini matokeo yanaendana na ahadi ya Mungu kwa Rebeka. Mungu anatenda kazi na watu wenye upungufu.)
  1.   Linakurudia (It Comes Around)
    1.    Kama anavyopendekeza mama yake, Yakobo anakimbilia kwa mjomba wale, Labani. Soma Mwanzo 29:15-19. Yakobo anaingia kwenye makubaliana na Labani ya kufanya kazi kwa miaka saba, je, Yakobo alikuwa mzuri na makini kwenye majadiliano? Kwa kupata malipo yake kabla ya kazi?
    1.    Soma Mwanzo 29:20-25. Je, kila mtu katika familia ile sio mwaminifu?
    1.    Soma Mwanzo 29:26. Kama Labani anasema ukweli kuhusu mil ana desturi za nchi yake, kwa nini hakubainisha hilo wakati walipoingia mkataba? Kwa nini, kama anavyouliza Yakobo, alimdanganya?
    1.    Soma Mwanzo 29:27-30. Unalinganishaje udanganyifu na Labani na ule wa Yakobo?
      1.    Chukulia kwamba Yakobo anakataa kumdanganya baba yake, na Mungu anafanyia kazi matokeo kama alivyoahidi. Je, unadhani Isaka angetuma ujumbe kwenda kwa Labani kwa ajili ya kumtafutia Yakobo mke? Je, Isaka angetenda jambo hilo hilo ambalo Ibrahimu alimtendea?
    1.    Rafiki, mdanganyifu anadanganywa! Udanganyifu wa mwisho unatokana na udanganyifu wa nyuma kabisa. Ninaamini kwamba endapo Yakobo na Rebeka wangemtumaini Mungu, baadaye Yakobo angempata Raheli kama mke wake na kumpeleka nyumbani. Rebeka angeishi na Yakobo na Raheli. Je, utadhamiria, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, kumtumaini Mungu na sio udanganyifu?
  1.    Juma lijalo: Yakobo-Israeli.