Somo la 2: Matanuru Yajayo

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
1 Petro 4-5, Warumi 1, Yeremia 9
Swahili
Year: 
2022
Quarter: 
3
Lesson Number: 
2

Somo la 2: Matanuru Yajayo

(1 Petro 4-5, Warumi 1, Yeremia 9)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2020, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Baadhi ya watu wanashtukizwa mara kwa mara kuliko watu wengine. Watu wanaochukua tahadhari huwa wanautafakari mustakabali na hushtukizwa kwa nadra sana. Watu wasiojali wanashtukizwa mara kwa mara kwa sababu huwa hawayatafakari mambo yaliyo mbele yao. Kwa namna moja au nyingine kila mtu huwa anashtukizwa. Somo letu juma hili linahusu kushtukizwa na majanga. Je, kuna namna ya kujiandaa kwa ajili ya kushtukizwa? Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tujifunze zaidi!

  1.    Kushtukiza (Surprise)
    1.    Soma 1 Petro 4:12. Unadhani Petro anatutaka tufanye nini ili kuepuka kushtukizwa na “jaribu zito?” (Anatuonya. Kama umeonywa, una uwezekano mdogo wa kushtukizwa.)
      1.    Petro anatuambia kuwa majaribu mazito sio “jambo geni.” Juma lililopita tulijifunza Zaburi 23 iliyotuambia (Zab: 23:6) kwamba “wema na fadhili [zitatufuata] siku zote za [maisha yetu].” Kwa nini tusishtukizwe kwenye majaribu mazito?
    1.    Soma 1 Petro 4:13-14. Je, vifungu hivi vinatoa jibu kwenye swali la kushtukizwa? (Kifungu cha 14 kinatuambia kuwa ikiwa “Roho wa utukufu na wa Mungu” anatukalia, tutarajie matusi na mafedhehesho.)
      1.    Je, kuna manufaa yoyote kwa mtu kupitia majaribu? (Kifungu cha 13 kinatuhakikishia kuwa tukiyashiriki mateso ya Kristo, tutafurahia atakapoyatwaa mamlaka.)
    1.    Petro anaanza sura hii kwa kutoa jibu kwenye swali la kwa nini hatupaswi kushtukizwa wakati wa mateso. Soma 1 Petro 4:1-2. Kwa nini hatupaswi kushtukizwa? (Yesu alipitia mateso nasi tunapaswa kukubali mtazamo wake juu ya mateso. Maoni kadhaa niliyoyapitia hayakubaliani nami, lakini ninadhani vifungu hivi pia vinatuambia kuwa tunapoziacha “tamaa za wanadamu” tunaweza kutarajia mateso zaidi.)
    1.    Soma 1 Petro 4:3-4. Tunaona sababu gani hapa ya “kudhuriwa?” (Tunapowaacha marafiki wetu wa siku nyingi wanaoishi maisha ya kifisadi, watasema mambo mabaya kutuhusu.)
  1.   Hakuna Mshtuko (No Surprise)
    1.    Soma 1 Petro 4:15. Kitu gani kingine kinasababisha mateso? (Kutenda maovu. Kujishughulisha na mambo ya watu wengine. Kuua na kuiba.)
      1.    Je, kwa kawaida hivi ndivyo huwa unayaangalia mateso, kwamba yanatokana na kutokuwa mtiifu? (Mara kwa mara huwa ninaandika kwamba Amri Kumi zilitolewa ili kuyafanya maisha yetu yawe mazuri. Amri hizo, Zaburi 23:2, zinatuelekeza kwenye “malisho ya majani mabichi” na “maji ya utulivu.”)
    1.    Soma 1 Petro 4:16-18. Mateso yetu yatafananishwaje na wale wanaoteseka kwa kutenda maovu? (Kinachoashiriwa hapa ni kwamba kila mtu anapata mateso, lakini mwovu anateseka zaidi kutokana na maovu ayatendayo.)
      1.    Unapokabiliana na jaribu zito, ni jambo gani la kwanza unalopaswa kulifanya? (Tafakari kwa nini unapata mateso. Je, ni kwa sababu umetenda jambo baya, au kwa sababu ulikuwa mwaminifu kwa Mungu?)
    1.    Soma Mathayo 10:14-15. Kama ulikuwa unateseka kazini kwako kwa sababu ulijaribu kuwaongoa wafanyakazi wenzako, je, utahitimisha kwamba ulikuwa unateseka kwa kutenda jambo jema? (Kifungu hiki katika kitabu cha Mathayo kina maelekezo mazuri. Kinatuambia kuwa katika juhudi zetu za kiinjilisti hatutakiwi kuendelea kuwaudhi watu. Washirikishe injili na endapo hawataipokea, “kung’uteni mavumbi ya miguuni mwenu” na msonge mbele.)
    1.    Soma 1 Petro 5:1-3. Je, hii ni kanuni ya jumla, kwamba hata kama tunadhani kuwa tunateseka kutokana na kumfuata Yesu, tunatakiwa kuwa makini ili kuwa na uhakika kuwa sisi si chanzo cha mateso yetu? (Kifungu hiki kinatuambia kuwa hata mchungaji wa mifugo anaweza kufanya makosa katika uongozi.)
  1.      Adui Wetu
    1.    Soma 1 Petro 5:8. Ni nani aliye mwanzilishi wa mateso yetu? (Shetani.)
      1.    Je, umewahi kuwasikia watu wakimlaumu Mungu kwa mateso ya ulimwengu huu?
      1.    Kwa nini useme kwamba Shetani ndiye chanzo kikuu cha mateso? (Tunateseka kwa sababu Shetani anatushambulia, au tumetenda jambo lisilo sahihi (ambalo pia linahusianishwa na Shetani), au mtu mwingine ametenda jambo lisilo sahihi (kwa mara nyingine, pia linahusianishwa na Shetani.)
    1.    Soma 1 Petro 5:9. Unapendekezaje kwamba tumpinge Shetani? Hii inatuambia kuendelea kuwa thabiti katika imani yetu, lakini utatumiaje imani yako ili kumpinga Shetani?
    1.    Soma 1 Petro 5:10. Je, huu ndio msingi wa kumpinga Shetani kwa “imani thabiti?” (Lazima “imani” inamaanisha imani kwa Mungu. Imani yetu kwa Mungu inatuambia kuwa mateso yetu ni ya muda mfupi tu. Mungu atasahihisha mambo mbinguni, au hata kabla ya hapo.)
    1.    Soma 1 Petro 5:11. Jambo gani linamaanishwa kwenye kifungu hiki? (Mungu ndiye mdhibiti wa mambo. Ana mamlaka.)
    1.    Soma 2 Wakorintho 12:7-9. Nani anawajibika na “mwiba” wa Paulo? (Anasema kuwa Shetani ndiye anayewajibika.)
      1.    Kwa nini Mungu hakuuondoa mwiba huu kwa kuwa yeye ndiye mdhibiti wa mambo yote? (Paulo anasema ulimsaidia kuepuka udanganyifu na kwamba uwezo wa Mungu “hutimilika katika udhaifu.”)
        1.    Hii inatufundisha nini juu ya uhusiano kati ya Shetani na Mungu linapokuja suala la mateso? (Shetani anawajibika, sio Mungu. Lakini, Mungu ana mamlaka na kuna nyakati anaruhusu mateso kwa sababu anazozijua yeye.)
  1.   Ghadhabu ya Mungu
    1.    Soma Warumi 1:18. Hebu subiri kidogo! Ni punde tu tumejadili kuwa mateso yanatoka kwa Shetani, hayatoki kwa Mungu. Je, Petro na Paulo (mwandishi wa kitabu cha Warumi) hawakubaliani?
      1.    Aina gani ya watu wanahisi ghadhabu ya Mungu? (Wale wanaoukandamiza ukweli.)
    1.    Soma Warumi 1:21-25. Ghadhabu ya Mungu inashukaje? (Vifungu hivi vinatuambia kuwa mdhambi anaikataa kweli ya Mungu, fikra yake inazingirwa, na Mungu anawaacha wadhambi katika “tamaa za mioyo yao.”)
      1.    Je, hii ni sawa na Mungu kumpiga mtu kwa ugonjwa? (Hapana. Huyu ni mtu akijipiga mwenyewe – na Mungu analiruhusu jambo hilo. Mungu anamruhusu mtu afanye kile anachojisikia.)
    1.    Soma Warumi 1:23 na Warumi 1:26-27. Angalia mpangilio wa tatizo. Kwanza wanadamu wanayakataa mamlaka ya Mungu na kuyabadilisha mamlaka hayo na kitu kingine kilichotengenezwa na wanadamu. Baada ya kuyakataa mamlaka ya Mungu, kisha wanakataa mpangilio wake wa kujamiiana. Wanabadili “matumizi ya asili” kwa ajili ya uhusiano wa kisenge. Je, umeuona uendeleaji (progression) huu katika maisha ya watu unaowafahamu?
      1.    Hii leo watu wanajenga hoja kwamba Paulo anaandika juu ya wanaume watu wazima wakifanya ngono na vijana wadogo, na sio juu ya uhusiano wa kibasha kwa jinsia zote mbili. Hiyo inatoa ufafanuzi gani juu ya mpangilio wa tatizo tulioujadili hivi punde? (Mamlaka ya Mungu yanaenda mbali zaidi hadi Edeni, ambapo Mungu alianzisha ndoa kama uhusiano wa maisha yote kati ya mwanaume na mwnamke wanaokuwa “mwili mmoja.” Angalia Mwanzo sura ya 2. Mara unapoyakataa mamlaka ya Mungu, uko huru kujenga hoja zinazokinzana na vifungu vya wazi vya kitabu cha Warumi.)
    1.    Soma Yeremia 9:23-24. Ni muhimu kiasi gani kumjua Mungu? (Kifungu hiki kinasema kuwa tunapaswa “kumfahamu na kumjua” Mungu.)
      1.    Tunapaswa kujua nini kumhusu Mungu? (Kwamba “anatenda wema, na hukumu, na haki katika nchi.”)
        1.    Inamaanisha nini kwa Mungu kutenda “haki?”
    1.    Soma Yeremia 9:25-26. Unaelewa hii kumaanisha jambo zaidi ya Mungu kuwaruhusu tu wanadamu kupitia mateso yatokanayo na matokeo ya chaguzi zao wenyewe? (Kifungu kinasema kuwa Mungu “atawaadhibu” wale wanaojidai kumfuata Yeye kwa nje (sio kutoka moyoni). Hiyo inaonekana kama mpango madhubuti kwa upande wa Mungu.)
    1.    Soma Yeremia 9:5-7. Kifungu hiki kinazungumzia juu ya kuwasafisha watu wa Mungu. Aina gani ya watu inaelezewa kuwa ndio wanaohitaji utakaso? (Ni vigumu sana kubainisha kuwa hawa ni watu wa Mungu, “Hujidhoofisha ili kutenda uovu,” wana lundo la “hadaa kwa hadaa.” Hawa ni watu wabaya. Hawa sio watu wanaojaribu kumfuata Mungu na wanahitaji “utakaso” kidogo.)
    1.    Rafiki, somo hili linaonesha kuwa sote tunaweza kupata majanga. Shetani ndiye mwanzilishi wa misiba, na tunajiletea majanga kwa kuchagua kufuata njia ya Shetani. Lakini, hata wale wanaomfuata Yesu wanaweza kupitia mateso. Mungu anaahidi kuwa mateso yetu yatakuwa ya muda mfupi, na kwamba hatimaye atayarekebisha. Je, utafanya uchaguzi leo wa kupunguza mateso yako, na kumfuata Yesu?
  1.    Juma lijalo: Kizimba cha Ndege.