Somo la 10: Unyenyekevu Ndani ya Tanuri (Kalibu) 

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Mathayo 5:5, Zaburi 37, 1 Petro 5
Swahili
Year: 
2022
Quarter: 
3
Lesson Number: 
10

Somo la 10: Unyenyekevu Ndani ya Tanuri (Kalibu) 

(Mathayo 5:5, Zaburi 37, 1 Petro 5) 

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2020, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza. 

Utangulizi: Yesu anafundisha katika Mathayo 5:5 “Heri wenye upole; maana hao watairithi nchi.” Je, hilo ni sahihi kwako? Wapole hawashindi chochote, hivyo lazima warithi kutoka kwa washindi? Nimeyatumia maisha yangu kama mpambanaji katika mfumo wa sheria na ninawafundisha wapambanaji wa siku zijazo. Hilo halionekani kama ni upole. Je, inawezekana kwamba nimechukua njia ya upole muda wote na sikulitambua hilo? Hebu tuone kile ambacho Roho Mtakatifu anaweza kukifanya ili itusaidie kuelewa suala hili vizuri zaidi tunapoendelea kuchambua kile kinachosemwa na Biblia kuhusu upole! 

I.  Kuuelewa Upole 

A.  Soma Zaburi 37:11. Hii inatufundisha nini kuhusu kauli ya Yessu katika Mathayo 5:5? (Ananukuu Zaburi 37:11! Ni vigumu sana kuelewa muktadha wa kile anachokisema Yesu katika Mathayo 5:5, lakini tunao muktadha mzuri tunaotakiwa kuuchimbua zaidi katika Zaburi 37.) 

B.  Soma Zaburi 37:1-2. Kwa nini unapaswa kuwa na amani pale unapojaribiwa kuwatamani watenda maovu? (Watenda maovu wana maisha yenye ukomo.) 

C.  Soma Zaburi 37:3-4. Tukimtumaini, kumfuata, na kumtii Mungu, “tukifanya urafiki na uaminifu,” matokeo yake ni yepi? (Mungu atatupatia haja za mioyo yetu.) 

1.  Je, unaweza kuona mfanano kati ya kuwa na haja za moyo wako na kuirithi nchi? 

D.  Soma Zaburi 37:5-6. Matokeo ya haki ni yepi? (Kumtumaini Mungu. “Naye atafanya.”) 

1.  Je, hiyo inamaanisha tusifanye chochote? Tukae tu na kutazama kwa upole? (Tunaambiwa “kukabidhi njia zetu kwa Bwana.” Tukifanya hivi Biblia inaahidi kuwa “haki” yako itatokeza “kama nuru.” Hiyo inaonekana kama nimepewa wito wa kufanya jambo fulani. Vinginevyo, hakutakuwa na chochote cha kukitokeleza nuruni.) 

E  Soma Zaburi 37:7-8. Tunaambiwa tuache kufanya nini kwa umahsusi? (Tuwe wavumilivu. Usikasirike. Usiwe na wasiwasi kwa sababu inaweza kukusababishia utende jambo ambalo ni ovu.) 

F.  Soma Zaburi 37:9. Hiki ni kifungu kingine kinachoahidi kwamba “tutairithi nchi.” Tunatekelezaje hilo? (“Tunamngoja Bwana.” Watenda maovu watakatiliwa mbali na Mungu.) 

G.  Soma Zaburi 37:10-11. Utafafanuaje kuwa “mpole” katika muktadha tuliojifunza? (Inamaanisha kumtegemea Mungu badala ya kujitegemea wenyewe. Inamaanisha kumtumaini Mungu.) 

1.  Nuru inanipambazukia. Kwa kutambua kwamba Mungu alikuwa pamoja nami kwenye kesi zenye mvutano/mgogoro mkubwa imekuwa msingi wa kunifanya niweze kudhibiti msongo – achilia mbali kuhusu ushindi. Je, mtazamo huo unamfanya mtu kuwa mpole? 

H.  Zaburi 37:12-20 inaendelea na ufafanuzi wa jinsi waovu wanavyokula njama za uovu dhidi ya wenye haki lakini Mungu anavunja mikono ya waovu huku akiwacheka. Soma Zaburi 37:21-22. Hii ni kauli nyingine inayohusu sisi kuirithi nchi. Kifungu hiki kinasema kuwa tunapaswa kufanya nini ili kuirithi nchi? (Uwe mwaminifu na mkarimu kwenye masuala ya fedha.) 

I  Soma Zaburi 37:27-29 na Zaburi 37:34. Hizi ni kauli mbili zaidi kuhusu watu wa Mungu kuirithi nchi. Zinasema nini juu ya wale wanaoirithi nchi? (Hii inarudia mada ile ile kwamba wale wanaompenda na kumtii Mungu wanatunzwa na kulindwa na Yeye, wakati waovu wanaangamizwa.) 

J.  Kwa kuwa sasa tunaiona taswira pana ya muktadha wa kauli ya Yesu kuwahusu wapole, utafasilije (define) suala la kuwa mpole? (Mtu anayemtumaini Mungu pale anapokabiliana na uovu.) 

K.  Je, uligundua rejea za kuwa imara na kumsubiria Mungu? Je, hiyo inamaanisha kuwa maisha yangu ya upambanaji yalitumika vibaya na kwamba ninapaswa kustaafu kufundisha wapambanaji wa siku zijazo? Kabla ya kujibu swali langu soma Kumbukumbu la Torati 20:1, Mika 5:9 na uyatafakari maisha ya Mfalme Daudi, mwandishi wa Zaburi 37. (Tunatakiwa kuyatafakari mafundisho ya Biblia kwa ujumla wake. Mungu ana wafuasi wapambanaji wengi, ambao Mfalme Daudi anaweza kuwa mkuu. Alishirikiana na Mungu kuushinda uovu.) 

L.  Kwa hiyo, hii inafanyaje kazi? Tunawezaje kuwa wapambanaji na wakati huo huo kuwa wapole? Kimsingi, ninazungumzia juu ya “mpambanaji kiutamaduni,” na sio kuhusu kuwadhuru kimwili watu waovu. Je, unaweza kuona mifano yoyote kwenye Biblia inayofafanua mchanganyiko huu wa upambanaji na upole? (Kitabu cha Esta ni mfano mzuri sana. Mungu anaushinda uovu mkubwa uliodhamiriwa kwa watu wake. Esta ni msingi wa kisa kinachoendana na “mpambanaji kiutamaduni” ambaye anasimama kidete kuwatetea watu wake katika muktadha wa hatari sana. Soma Esta 9:12-13. Tunaona kwamba wapiganaji halisi pia wanatumiwa na Mungu kuushinda uovu.) 

II.  Kuuelewa Unyenyekevu 

A.  Watu wengi wanaweza kufasili (define) upole kuwa ni unyenyekevu. Zaburi 37 inalizungumziaje hilo? (Kumsubiria Mungu na kumtumaini Yeye ni matendo yanayoendana na unyenyekevu. Wafuasi wa Mungu humsubiria Mungu.) 

B.  Soma Mathayo 23:12, Yakobo 4:10, na 1 Petro 5:6. Kama kweli wewe ni mtu mnyenyekevu kwa nini utake kukwezwa? 

1.  Je, vifungu hivi ni kwa ajili ya watu wenye majivuno (au watu wanaotamani kuwa na ujivuni) ili kuwapatia mwelekeo wa kukwezwa? 

2.  Je, unapaswa kuwa mnyenyekevu kwa kuwa tu hiyo ndio njia nzuri ya kuendesha maisha yako? Ikiwa ndivyo, kwa nini Biblia inaahidi kwamba utaishia kukwezwa? 

C.  Hebu tupitie upya 1 Petro 5:6. Tafsiri ya Biblia ya “Vulgate Latin” pamoja na tafsiri nyingine za kale inasema kuwa wanyenyekevu watainuliwa “kwa wakati wake.” Hiyo itakuwa lini? (Mbinguni.) 

1.  Je, inaleta mantiki kwamba jinsi wanyenyekevu wanavyokwezwa ndivyo watakavyokwenda mbinguni? 

2.  Kama unadhani hilo ni kweli, tafakari tena asili ya mbingu. Jambo gani linakufanya kuwa mtu wa pekee hapa tena sasa hivi? Je, ni akili zako, mwonekano wako, uwezo wako kimuziki, uwezo wako kimichezo, uwezo wako wa kufanya biashara, au ujuzi wa aina fulani? 

D.  Soma Wafilipi 3:20-21. Tutakapofika mbinguni, tutapewa miili ya namna gani? (Kifungu hiki kinatuambia kwamba miili yetu ya “unyonge,” (ikimaanisha unyenyekevu, itafanana na mwili wenye utukufu wa Yesu!) 

E.  Soma 1 Wakorintho 15:52. Namna nyingine ya kutafsiri “kisichooza” ni “kisichoharibika.” Je, sote tutapewa karama inayofanana? (Kama tuna kasoro katika maeneo fulani ya mwili, kwa mfano akili, ninatambua kwamba huo ni uharibifu utakaorekebishwa.) 

F.  Sehemu ya Tamko la Uhuru wa Marekani inasema “Kweli hizi zinajidhihirisha, kwamba watu wote wameumbwa sawa.” Ukitumia muda wako darasani utatambua kwamba hilo sio kweli. Sote tuna fursa sawa, lakini watu wengine ni werevu zaidi au wana tamaa ya kufanya mambo makuu kuliko wengine. Je, utakubaliana kuwa kule mbinguni, Biblia inasema kwamba kiuhalisia kauli hii itakuwa ya kweli? 

1.  Kama umejibu, “ndiyo,” wanyenyekevu wanakwezwaje mbinguni sote tutakapokuwa sawa? (Lazima hii iwe inamaanisha kwamba sote tunakwezwa – yaani wote watakaofanikiwa kufika mbinguni.) 

2.  Je, hii inatufanya tuwe na fasili tofauti ya unyenyekevu wa kweli? Kwamba mtu mpole hayuko radhi kuwa “chini ya,” bali kuwa “sawa na” wengine? 

G.  Soma Zaburi 62:9. Kitu gani kinawafanya masikini na matajiri kuwa sawa? (Wote wanategemea pumzi (kupumua). Dhana ya kwamba kuwa tajiri hukufanya uendelee kupumua ni “kujidanganya.”) 

H.  Soma 1 Petro 1:24-25. Kwa nini Paulo anatulinganisha na majani na maua? (Tuna ukomo mkubwa sana wa muda. Utakumbuka tulizungumzia hilo kuhusu waovu.) 

1.  Kwa nini neno la Mungu ndilo lenye ujumbe mzuri wa kweli? Petro anataka tutoke na fundisho gani kutoka kwenye tofauti hii? (Ahadi za Mungu kwenye Biblia ni za milele. Mpango wa Mungu ni wa milele.) 

I.  Hebu tusimame kidogo na tutafakari mfanano kati ya kuwa mpole na kuwa mnyenyekevu. Je, sifa za kuwa mpole na mnyenyekevu ni sawa na kuwa mnyonge au duni kwa namna fulani? (Kuwa mpole inamaanisha kwamba unamtegemea Mungu kwa ajili ya ushindi, na sio kujitegemea mwenyewe. Kuwa mnyenyekevu inamaanisha kuwa unatambua kwamba mafanikio maishani hutoka kwa Mungu na ni ya kupita (ya muda mfupi), ilhali uhusiano wetu na Mungu hudumu milele.) 

J.  Rafiki, Mungu anatuwazia mambo makuu. Kama unatamani kuinuliwa, kama unatamani kuushinda uovu, kama unataka kutenda mambo makuu kwa ajili ya Mungu, somo letu juma hili linatufundisha kuwa upo mchakato. Mchakato huo unaanza (na kuhitimisha) kwa kutofautiana na Mungu. Tunamtii. Tunamtumaini. Tunafuata mwongozo wake. Tuna mtazamo wa kwamba kila kitu kinatoka kwake. Ukifanya hivyo mambo makubwa yatakujia. 

III.  Juma lijalo: Kusubiria Tanurini (Kalibuni).