Somo la 13: Kristo Ndani ya Tanuru (Kalibu)

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Mathayo 2, 12, 23, 26 & 27
Swahili
Year: 
2022
Quarter: 
3
Lesson Number: 
13

Somo la 13: Kristo Ndani ya Tanuru (Kalibu)

(Mathayo 2, 12, 23, 26 & 27)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2020, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Hakuna mtu anayewapenda watu wa hovyo. Hakuna mtu anayependa kufedheheshwa. Hakuna mtu anayependa kuambiwa kuwa hana hadhi, na zaidi sana asingependa kuambiwa hivyo na watu ambao hadhi yao inatiliwa shaka. Hakuna mtu anayependa kuaibishwa. Hakuna mtu anayependa kuteseka kwa maumivu makali. Hakuna mtu anayependa kuuawa na watu waovu tena wenye vurugu. Pamoja na hayo, Yesu aliyapitia yote haya na kuzidi kwa ajili yetu. Tunaishi kwenye utamaduni usio wa kawaida. Kama kitu fulani hakifanyi kazi tunakitupilia mbali tu na kutafuta kingine kipya. Hebu fikiria kama ungetambua kuwa kifaa chenye hitilafu ulichokuwa ukikitumia kitakusababishia madhara makubwa. Kwa dhahiri ungekitupilia mbali na kununua kingine. Jambo la kushukuru ni kwamba, Yesu hakututupilia mbali na kuwaumba watu wapya, walio na shukurani zaidi na wasio hatarishi. Alichotutendea Yesu hakiwezi kuelezewa kwa lugha na uelewa wa kawaida. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tulijadili suala hili!

I.  Kuanzia Mwanzoni Kabisa

A.  Soma Mathayo 1:18-19. Rejesha saa ya akili yako miongo michache nyuma. Je, unawakumbuka watoto ambao mimba zao zilitungwa kabla wazazi wao hawajaoana? (Nilipokujwa kijana mdogo, hii ilikuwa ni kashfa (scandal). Hii leo katika baadhi ya jamii hili ni jambo la kawaida. Tunajua kwamba ilikuwa kashfa katika zama za Yesu kwa sababu Yesu alikumbushwa hili mara kwa mara katika kipindi cha uhai wake (angalia Yohana 8:41).)

B.  Soma Luka 2:7. Umewahi kusikia tusi, “Ulizaliwa kwenye kihenge?” Yesu alizaliwa wapi? (Kuna mjadala unaohusu kama alizaliwa kwenye kihenge au pangoni, lakini Biblia iko wazi kwamba kwanza alilazwa na kupumzishwa kwenye hori la kulishia ng’ombe.)

C.  Soma Mathayo 2:1-2. Je, wasomi walitaka kujua zaidi habari za kuzaliwa kwako? Je, nyota ilikuwepo iliyotangaza ujio wako? (Wakati huo huo kipindi Yesu anapitia mazingira dhalili, pia ana mambo yasiyo na kifani yanayoendana na kuzaliwa kwake. Anaitwa “Mfalme wa Wayahudi.”)

D.  Soma Mathayo 2:3. Kwa nini “Yerusalemu yote” ifadhaike kwa kile walichokitaarifu wasomi (mamajusi)? (Wana mfalme mpya?)

E.  Soma Mathayo 2:4-6. Viongozi wa dini wanaamini kuwa Yesu anaweza kuwa nani? (Masihi aliyeahidiwa!)

F.  Soma Mathayo 2:7-8 na Mathayo 2:11. Je, mamajusi wanadhani kuwa Yesu ni Mfalme wa unabii? (Wanamsujudu. Wanaamini Yesu ni Masihi/Mfalme.)

G.  Soma Mathayo 2:12-13 na uilinganishe na Ufunuo 12:4-5. Je, kisa hiki kinaonekana kama kisa cha kusisimua? Unatangazwa kuwa Mfalme na mamajusi (wasomi) na kisha unatakiwa kuikimbia nchi kwa sababu Mfalme wa nchi aliyepo madarakani anataka kukuua?

H.  Soma Mathayo 2:16. Watu wangapi wasio na hatia wanadhuriwa na Shetani? Unaweza kufikiria kina cha huu uovu?

1.  Tafakari kisa hiki kwa wale ambao hii leo wanapitia mabalaa makubwa ambayo hayaonekani kuwa na mantiki. Je, uwepo wa uovu una maelezo ya kutosha?

II.  Wakati wa Huduma Yake

A.  Soma Mathayo 12:22-23. Watu wa kawaida wanauchukuliaje muujiza huu? (Wanauliza kama Yesu ni Masihi. Angalia Mathayo 1:1 na Isaya 35:4-5.)

B.  Soma Mathayo 12:24. Viongozi wa dini wanaashiria nini kumhusu Yesu? (Kwamba Yesu ni wakala wa Shetani.)

1.  Zingatia kile tulichokisoma ambacho Herode alikifanya chini ya ushawishi wa Shetani. Je, hili ni shtaka la kutisha kulitoa dhidi ya Yesu?

C.  Soma Mathayo 12:25-26. Kwa nini Yesu anatetea hadhi yake kwa njia ya hoja yenye mantiki?

D.  Soma Mathayo 12:27-28. Yesu anatoa madai gani yasiyo ya moja kwa moja? (Kwamba yeye ni Masihi.)

1.  Utaona kwamba viongozi wa dini wanadai kuwa Yesu ni wakala wa Shetani na Yesu anajibu kwamba yeye ni Masihi. Fikiria watu wengi ambao leo hii wanasema kuwa alikuwa “mtu mwema” au “nabii” au jambo linalofanana na hilo. Je, ni jambo jema kwamba watu wanaomdunisha Yesu hii leo wana mtazamo chanya zaidi kwake? (Hapana. Inaonesha kuwa wana ujinga wa kutozijua kweli. Wale walioona kile alichokifanya Yesu walijua kwamba nguvu isiyo ya kawaida (miujiza) ndio ufafanuzi wa pekee. Swali lilikuwa tu kwamba ni muujiza upi huo?)

E.  Soma Mathayo 12:31-32. Je, umewahi kuwasikia watu wanaosema baadhi ya “waponyaji kwa njia ya imani” ni wakala wa Shetani? Shutuma za aina hiyo ni za hatari kiasi gani? (Nitasita sana kusema kwamba mtu anayedai kutumia uwezo wa Roho Mtakatifu kufanya uponyaji kimsingi anafanya kazi kwa njia ya pepo. Yesu anaashiria kwamba dhambi hii haitasamehewa.)

F.  Soma Mathayo 23:37-39. Utume wa Yesu ni kwa Wayahudi. Unaweza kusema Yesu alidhani kuwa huduma yake inaendeleaje? (Vibaya. Hili ni jambo la kusikitisha!)

1.  Jiweke kwenye nafasi ya Yesu. Mambo yote tuliyoyajadili yamekutokea, na sasa mwishoni mwa kazi yako watu uliofanya kazi kuwaongoa “hawako tayari!” Ungejisikiaje?

III.  Mwisho

A.  Soma Mathayo 26:19-21 na Mathayo 26:33-34. Yuda anamsaliti Yesu na Petro anamkana Yesu. Yesu anazifahamu kweli hizi. Hii inafananaje na huzuni ya Yesu kwamba wale aliokuja kuwakomboa, “hawakuwa radhi?” (Hili ni jambo baya zaidi. Jambo jingine ni kushindwa kushawishi. Huku ni kushindwa kwa wale walio karibu naye, wale waliokuwa wenzake katika kazi yake.)

B.  Soma Mathayo 26:38-40. Ukimwambia rafiki yako kuwa una huzuni sana kiasi kwamba unaweza kufa, hivyo unataka “akuchunge” kwa saa moja, ungetarajia nini kwa rafiki wa kweli?

1.  Kama atalala, utauthaminishaje urafiki wenu?

2.  Je, Yesu ana wasiwasi kuvuka saa chache zinazofuata? (Angependa kuepuka yale yatakayotokea, kama itawezekana. Wanafunzi wake wanamsaliti, na washirika wake wa karibu wanaonekana kutomjali sana.)

C.  Soma Mathayo 27:15-17 na Mathayo 27:20. Hii inaathirije nafsi ya Yesu? Hisia zake za kuhitajika? Makutano walimpendelea mfungwa mwenye kuvuma kwa ubaya dhidi ya Yesu linapokuja suala la kama Yesu anapaswa kufa. Kama ungekuwa Yesu, je, ungekuwa unajiuliza kama watu hawa waliyaona mambo yote mema uliyowatendea?

1.  Unadhani hili liliathirije dhamira ya Yesu kupitia kifo cha kutisha ili kuwakomboa watu hawa? Watu wanaopendelea kumuua badala ya mfungwa mwenye sifa mbaya?

D.  Soma Mathayo 27:22-23. Pilato anasema kuwa haki inabainisha kuwa mtu huyu anapaswa kuishi. Unadhani hilo liliathirije dhamira ya Yesu kupitia kifo cha kutisha ili kuwakomboa watu hawa? (Lazima mambo yote haya yangemshawishi Yesu kuwaacha wanadamu wapokee haki waliyostahili – kifo cha milele.)

E.  Soma Mathayo 27:27-31. Angalia kwa undani habari za mashambulizi kwa Yesu. Mara mbili walimvua nguo mbele ya “batalioni yote.” Wakamvisha kama Mfalme na kumdhihaki. Wakamtemea mate. Wakamvika taji ya miiba juu ya kichwa chake. Chukulia kwamba mtu anayekudai fedha amekufanyia hivi. Je, ungemwambia kuwa humdai chochote?

1.  Vipi kama kweli ulikuwa mfalme na watu waliokudhihaki, kukutemea mate, na kukujeruhi walikuwa na hadhi ya chini yako? Je, ungewapumzisha baadhi ya majukumu? Je, ungewalipa madeni yao?

F.  Soma Mathayo 27:35-36 na Mathayo 27:39-42. Unapaswa kuhitimisha nini kimantiki kutokana na ukweli wakati Yesu anaponing’inizwa msalabani, nguo zake zinagawanwa miongoni mwa askari? (Lazima hili linamaanisha kuwa anapitia mateso ya ufidhuli na kuning’inia uchi msalabani.

1.  Kama ungekuwa kwenye nafasi ya Yesu, ungeshawishika kiasi gani kwamba wewe ni Mwana wa Mungu?

G.  Soma Mathayo 27:43. Dharau kwenye maneno “kama anamtaka,” ni dhana ya kwamba Mungu hampendi Yesu. Kwamba Yesu anasema uongo kuhusu kuwa “Mwana wa Mungu.” Kama wazazi wako walikuwa wanakupenda, ungekuwa na mwitiko gani kwa watu wanaokuambia kuwa hukupendwa?

H.  Soma Mathayo 27:46. Je Yesu anaamini kwamba Mungu hampendi? Kwamba viongozi wa dini walikuwa sahihi kuwa Mungu “hamtaki?” (Hii inaonesha kwamba Yesu anajihisi kutengwa na Mungu na hii inasababisha kukata tamaa kwa hali ya juu.)

1.  Je, ungeweza kusimama imara katika mazingira haya?

I.  Rafiki, kama unatilia shaka kuwa Yesu anakupenda, fikiria kile ambacho tumetoka kujifunza! Yesu anatupenda kwa namna ambayo maneno ya wanadamu hayawezi kuuelezea upendo huo vya kutosha! Je, utayatoa maisha yako kwa Mungu aliyeyatoa maisha yake kwa ajili yako?

IV.  Juma lijalo: Tunaanza mfululizo mpya ya masomo juu ya kifo na tumaini letu lijalo.