Somo la 3: Kuelewa Asili ya Mwanadamu

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Mwanzo 2-3, Mhubiri 12, Mathayo 17
Swahili
Year: 
2022
Quarter: 
4
Lesson Number: 
3

Somo la 3: Kuelewa Asili ya Mwanadamu

(Mwanzo 2-3, Mhubiri 12, Mathayo 17)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2020, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Unapozifikiria sheria za usalama barabarani, ninatarajia kwamba usingependa polisi wa usalama barabarani akusimamishe na kukuandikia adhabu. Lakini, unaamini kwa dhati katika usimamizi na utekelezaji wa sheria za usalama barabarani kwa watumiaji wengine wa barabara. Ni kweli? Vipi kuhusu maisha baada ya kifo? Ungependa kuishi milele, lakini kuna watu wengi ambao badala yake una uhakika hawapaswi kuhusishwa na uovu milele. Biblia inazungumzia nini kuhusu hii mada? Je, wanadamu wana asili ya milele? Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tujifunze zaidi!

I.  Roho

A.  Soma Mwanzo 2:7. Kitu gani kilimfanya mtu kuwa “kiumbe hai?” (Kupokea pumzi ya uhai kutoka kwa Mungu.)

B.  Soma Mhubiri 12:1. Hii inazungumzia nini juu ya kuzeeka? (Ukiishi maisha marefu kiasi cha kutosha, kuna muda utayazungumzia maisha kwa kusema, “Sina furaha” na maisha.)

C.  Vifungu vinavyofuatia katika Mhubiri 12 (vifungu vya 2-5) vinatoa taswira ya vile inavyofanana kwa mtu kuwa mzee. Hebu tusome Mhubiri 12:5-7. Unapojikita kwenye kifungu cha 6, je, inaonekana kama kifo ndio hatma? (Kwa dhahiri mambo haya yanaonekana kuwa ndio ukomo.)

1.  Linganisha Mhubiri 12:7 na kile tulichokisoma hivi punde katika Mwanzo 2:7. Je, huku ni kugeuza mchakato? (Inaonekana hivyo.)

II.  Mwili

A.  Soma Mwanzo 3:22-24. Unahusianishaje suala hili na mjadala wetu juu ya roho? Je, ni lazima tuwe na vyote viwili, yaani, roho (pumzi) na Mti wa Uzima ili kuendelea kuishi?

1.  Alimradi mwili wako haurejei mavumbini, unaendelea kuwa na roho yako?

B.  Soma Ufunuo 22:1-2. Kwa nini Mti wa Uzima uko mbinguni? Je, hali yetu mbinguni inafanana na hali waliyokuwa nayo Adamu na Eva kule Edeni? (Mantiki inasema kuwa haitofautiani – kutokufa kwetu mbinguni kunategemeana na kuendelea kula kutoka kwenye mti wa uzima.)

1.  Hiyo inazungumzia nini kuwahusu wale wote ambao hawataingia mbinguni? (Hawawezi kuendelea kuwepo.)

2.  Hii inazungumzia nini juu ya utegemezi wetu wa roho juu ya mwili wetu? (Mwili wetu ni wa muhimu kwenye mwendelezo wa uhai wa roho yetu. Kama hili lisingekuwa kweli, tusingehitaji Mti wa Uzima.)

III.  Roho na Mwili

A.  Tukiangalia tena Mwanzo 2:7 na Mhubiri 12:7 inaonekana kama roho na mwili havihusiani. Mungu alipopulizia “pumzi ya uhai” puani mwa Adamu, je, alimpulizia “Adamu” kama mwanadamu tofauti?

1.  Tafakari juu ya jambo hili: je, kila mtu ambaye amewahi kuishi ni mtu aliyeumbwa mawazoni mwa Mungu na kisha akapandikizwa katika roho tofauti ili kuunganishwa na mwili wetu wakati tukiwa hai?

B.  Soma Yeremia 1:4-5 na Wagalatia 1:15. Vifungu hivi vinazungumzia nini juu ya Mungu kutujua kabla hatujazaliwa? (Vinaelezea kwa umahsusi kwamba Mungu alikuwa na habari zetu kabla hatujazaliwa.)

1.  Je, huu ni uthibitisho Mungu alipopuliza pumzi yake kwa Adamu, alipulizia utambulisho (identity) mahsusi ndani ya mwili wa Adamu? (Ndiyo.)

2.  Au, hii ni kauli ainasafu (generic) kwamba Mungu anaufahamu mustakabali na mustakabali huo unatujumuisha na sisi? (Jinsi Yeremia 1:5 ilivyoandikwa inazungumzia mwingiliano (uhusiano) wa Mungu na Yeremia kabla hajazaliwa.)

C.  Soma Mwanzo 1:26. Huyu “wetu” ambaye Mungu anamzungumzia kama kuwaumba wanadamu ni nani? (“Wetu” anaonekana kuwa Mungu Baba, ambaye anamjumuisha Roho Mtakatifu.)

1.  Je, Roho Mtakatifu ana jukumu linalojitegemea? (Ndiyo. Katika Yohana 16:7 Yesu anasema kuwa asipoondoka Roho Mtakatifu hatakuja. Angalia pia Yohana 16:13.)

a.  Je, hiyo inaashiria kwamba kama tumeumbwa kwa mfano wa Mungu roho yetu ina jukumu linalojitegemea? (Inaonekana hivyo – tunapoanza kuvuta hewa ya oksijeni (ambayo imo tumboni) hiyo pumzi ya Mungu inapandikiza utambulisho (identity) wa pekee (unique).)

b.  Unadhani Roho Mtakatifu anaweza kuwepo bila uwepo wa Mungu Baba? (Hapana. Mfanano huu unaimarisha dhana ya kwamba roho inauhitaji mwili ili iweze kujitosheleza.)

D.  Soma Yohana 3:5-6. Hii inarejelea “roho” ya nani? (Hii ni rejea ya ubatizo. Mwili ni wetu, lakini Roho ni Roho Mtakatifu.)

E.  Soma Warumi 8:15-16. Ikiwa Roho Mtakatifu “huzishuhudia” roho zetu, je, hiyo inamaanisha kuwa roho yetu ina mchakato wa fikra inayojitegemea? (Lazima.)

F.  Soma 1 Wakorintho 6:15-17 na 1 Wakorintho 6:19. Vifungu hivi vinahusu dhambi ya zinaa na vinatuambia kuwa dhambi zote si sawa, dhambi hii ni mbaya zaidi. Kwa nini? (Kwa sababu katika tendo la ngono mnaunganishwa na “kuwa mwili mmoja.” Tatizo ni kwamba tayari umeshaunganishwa na Mungu.)

1.  Hebu tuchimbue zaidi hii dhana ya kuunganishwa na Mungu na kuwa “roho moja naye.” Muunganiko huu unatokeaje? (Kifungu cha 19 kinatuambia kuwa unatokana na “Roho Mtakatifu aliye ndani yenu.”)

2.  Je, hii inamaanisha kuwa tuna roho inayojitegemea? (Hili ni gumu kidogo kulielewa, lakini inaonekana kwamba roho yetu inayojitegemea inaunganishwa na Roho Mtakatifu.)

G.  Kama Mungu alipulizia pumzi kwa Adamu anayejitegemea (na wewwe unayejitegemea) katika mwili wake, je, unakumbuka kuwa na ufahamu kabla hujazaliwa? (Hapana. Tunakumbuka tu kuyafahamu mambo tulipokuwa na miili yetu.)

1.  Hiyo inatufundisha nini juu ya ufahamu wakati roho yetu inaporejea kwa Mungu (Mhubiri 12:7)? (Kinachorejea kwa Mungu ni upekee (unique) wako, lakini sio ufahamu wako.)

H.  Hebu tupitie upya kile tulichokisoma na kukijadili ili tuone kama tunaweza kufikia hatma ya uelewa wetu kuhusu roho yetu iliojengwa juu ya Biblia (na mantiki). Mungu alipomuumba Adamu alimpulizia utambulisho (identity) mahsusi ndani yake. Lakini, utambulisho huo usingeweza kuendeelea pasipo uwepo wa mwili, ambayo ndio sababu ya Mti wa Uzima katika bustani ya Edeni na Mbinguni. Roho yetu ni sawa na Roho Mtakatifu na roho hizi mbili zinachangamana. Je, unakubaliana na hili?

IV.  Vifungu Vyenye Matatizo

A.  Soma 2 Wakorintho 5:6-9. Paulo anazungumzia nini kuhusu ufahamu “pamoja na Bwana?” (Anaonekana kusema kuwa tutakuwa na ufahamu “mbali na mwili.” Muktadha ni muhimu. Ukisoma 2 Wakorintho 5:1-10 Paulo anarejelea “maskani” kama mwili wetu. Mjadala wake unalinganisha maisha ya duniani na maisha ya mbinguni. Haashirii roho isiyokufa inayojitegemea kwani anahitimisha mjadala kwa rejea ya hukumu ya mwisho.)

B.  Soma Zaburi 115:17-18. Vifungu hivi viwili vinaonekana kukinzana. Wafu hawasifu, lakini mtunga Zaburi anamsifu Mungu “tangu leo hata milele.” Je, hii inamaanisha kuwa wenye haki ndio kamwe hawafi na wana roho ya ufahamu? (Hii inasomeka kupita kiasi kwenye vifungu hivi. Ujumbe ni rahisi, wafu hawashuhudiwi na waishio wakimsifu Mungu. Hata hivyo, wenye haki wana matarajio ya uzima wa milele (katika ulimwengu utakaofanywa upya) na hivyo masifu ya milele.)

C.  Soma Mhubiri 9:5. Kifungu hiki kinaonekana kuwa maarufu sana kinachosema “ingia kwenye Biblia” kuonesha kuwa hatujui lolote baada ya kifo. Kiangalie kwa ukaribu zaidi. Je, unaamini kuwa wafu “hawana ijara tena?” Je, unaamini kuwa Mungu amewasahau wenye haki waliofariki? (Hiki ni kifungu kinachoogofya kukinukuu kwa sababu kikichukuliwa kiuhalisia, inamaanisha kuwa hakuna mbingu.)

D.  Soma Mhubiri 9:2-3. Je, hii inaonekana kuwa kweli? (Kwa dhahiri hapana ikiwa unaamini kuwa Mungu huwatunuku wale wanaomchagua. Kifo sio mwisho wa mambo. Ukisoma sura yote utaona kwamba Sulemani anaonekana kuwa na mfadhaiko. Hitimisho lake (Mhubiri 9:7-9) ni kuishi kana kwamba hakuna kesho, kwa sababu kesho haipo. Huo sio ujumbe wa Biblia.)

E.  Soma Mathayo 17:1-4. Je, Musa na Eliya wako hai na salama kabisa? (Bila shaka.)

1.  Soma Kumbukumbu la Torati 34:5-7. Kwani Musa hakufa? (Alikufa.)

2.  Ikiwa wafu hawana ufahamu, unaelezeaje suala la Musa kuwa hai na salama na kumsalimia Yesu? (Yuda 9 inatuambia kuwa Mikaeli aliudai “mwili wa Musa.” Hivyo, Mungu anaweza kuwafufua wafu na kuwachukua mbinguni.)

F.  Soma Mathayo 27:51-53. Hii inazungumzia nini kuhusu wafu? (“Watakatifu” wanaweza kufufuliwa kabla ya ujio wa Yesu Mara ya Pili.)

G.  Rafiki, tunapaswa kuhitimisha nini juu ya asili ya wanadamu? Ninadhani kwamba Mungu anapandikiza ndani yetu roho ya pekee (unique) inayorejea kwa Mungu wakati kifo kinapotokea. Roho hii inahitaji mwili uwe na ufahamu, na hilo linatokea pale tu Mungu anapoamua kuufufua mwili wetu.

V.  Juma lijalo: Tumaini la Agano la Kale.