Somo la 10: Mioto ya Kuzimu

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Isaya 66, Marko 9, Ufunuo 20
Swahili
Year: 
2022
Quarter: 
4
Lesson Number: 
10

Somo la 10: Mioto ya Kuzimu

(Isaya 66, Marko 9, Ufunuo 20)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2020, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Je, watu huwa wanaifikiria jehanum kwa dhati kabisa? Vitabu vingapi na wahusika wangapi kwenye sinema husema, “tunaonana jehanum?” Kama kweli mzungumzaji anadhani kuwa jehanum ni mahala ambapo moto huwaka milele, kauli hiyo isingetolewa kirahisi namna hiyo. Kama jehanum kuna mateso ya milele watu makini wangetoa kipaumbele kikubwa kuepuka wenda jehanum. Badala yake, watu wengi (nikiwemo mimi) wanatafakari kwa kuzingatia kuikosa mbingu.  Na je, jehanum inamzungumziaje Mungu? Kisa cha injili kinasema kuwa Mungu anatenda zaidi ya haki kwa wanadamu pale alipojitoa ili kutupatia nafasi ya kuuchagua uzima wa milele. Je, “zaidi ya haki” pia inaweza kuwa zaidi ya isivyo haki? Miaka sabini ya dhambi inastahili mateso ya milele? Hebu tuzame kwenye Biblia zetu na tuone kile inachokisema kuhusu jehanam!

I.  Vita vya Funza

A.  Soma Isaya 66:23. Je, umewanukulia watu wengine kifungu hiki ili kuthibitisha kwamba hata mbinguni Sabato itatunzwa?

B.  Soma Isaya 66:24. Kama umejibu, ndiyo, kwenye swali lililotangulia, je, uliendelea kunukuu kifungu hiki? (Huenda hapana!)

1.  Je, kifungu hiki kinathibitisha waliopotea wanateswa kwenye “moto” ambao “hautazimika?”

2.  Hebu tuangalie kisa hiki kwa kina. Kifungu kinasema kuwa ni nini mustakabali wa wale wanaomuasi Mungu? (Watakufa. Wamekufa.)

a.  Je, mauti ndio yanayoamua mustakabali uliopo kati ya Shetani na Mungu katika jaribu la Eva? (Soma Mwanzo 3:3-4. Shetani alimwambia Eva amuasi Mungu na kumuahidi kuwa uasi haukuishia kwenye kifo. Ulikuwa ni uongo katika kipindi hicho na bado ni uongo hata sasa.)

C.  Angalia sentensi ya mwisho ya Isaya 66:24. Funza na moto wa nani hautazima? (Moto sio wa mwanadamu, unatoka kwa Mungu. Hivyo, hakuna sababu ya kudhani kuwa funza anamilikiwa na mtu yeyote tofauti na Mungu. Kwa ufupi hii inaelezea uharibifu wa mwili – ama unachomwa au unaliwa na funza.)

D.  Soma Marko 9:47-48. Yesu anaongezea nini kwenye Isaya 66:24? (Haongezei chochote. Ananukuu tu sehemu yake.)

E.  Mara zote muktadha ni muhimu. Soma Marko 9:42. Je, kumsababisha mtu kutenda dhambi ni jambo baya sana? (Ndiyo.)

1.  Yesu anaposema “afadhali mtu huyo,” mbadala wake ni upi? (Chochote kile ambacho kwa kawaida huwatokea wadhambi.)

2.  Je, Yesu aliamini katika mateso ya milele jehanum? (Asingeweza kuamini hivyo kwa sababu kila mtu angependelea kuzama majini ili aweze kuchomwa milele.)

F.  Soma Marko 9:43-47. Ngoja niulize swali lenye uhalisia kivitendo. Je, ni dhambi kuamua kutomtii Mungu, au ni sawa tu kama kamwe hukuwahi kuifanyia kazi?

G.  Soma Mathayo 5:27-29. Hapa tunaona maelezo mengine kwenye kauli ya Yesu. Je, Yesu anasema kwamba kitendo pekee ndicho dhambi? (Hapana. Anasema kuwa kama unadhamiria kuzini ni sawa na kuufanya uzinzi huo.)

1.  Katika muktadha huo, lengo la kung’oa jicho lako au kukata mkono wako ni nini? (Yesu anajihusisha kwenye mbalagha (utiaji chumvi). Hawezi kuwa anamaanisha kwa dhati kwamba ujitie upofu au ujisababishie ukiwete kwa sababu kwa kufanya hivyo hakutakomesha uwezo wako wa kutenda dhambi.)

2.  Je, inaleta mantiki kuhitimisha kwamba Yesu pia anajihusisha kwenye utiaji chumvi pale anapozungumzia “moto wa jehanum usiozimika?” (Ndiyo. Lakini, utaona kwamba moto ndio hauzimiki, na sio kuungua kwa mwili wako.)

II.  Ziwa la Moto

A.  Soma Ufunuo 20:4-6. Kifungu hiki kinasema kuwa ni nini hatima ya wafu waovu hadi kufikia hapa? (Ni wafu katika makaburi yao. “Wamefufuka” katika ufufuo wa pili baada ya miaka elfu.)

1.  Je, walikuwa wakiungua jehanum wakiwa na ufahamu? (Sio kwa mujibu wa kifungu hiki.)

B.  Soma Ufunuo 20:7-9. Shetani anawakusanya waovu kuzishambulia Yerusalemu Mpya na watakataifu. Mwisho wao ni upi? (Moto “ukawala.” Hii ni rejea ya kwanza ya kukabiliana kwao na moto, na moto huo hauwatesi, unawala.)

1.  Ni nini chanzo cha moto unaowala waovu? (Moto “ukashuka kutoka mbinguni.” Huu sio moto wa jehanum kutoka vilindini mwa dunia. Haya sio mateso. Haya ni maangamizi ya waovu.)

C.  Soma Ufunuo 20:10. Chukulia kwamba baada ya kufa waovu wanakwenda jehanum moja kwa moja ambapo wanateswa kwa moto. Je, watateswa kwa muda mrefu zaidi kuliko ibilisi? (Ndiyo, kwa sababu ibilisi anaingia kwenye moto katika kipindi cha mwisho wa dunia. Tunaweza kuona jinsi jambo hili lisivyo na mantiki au maarifa ya kisheria. Shetani anateseka kidogo kuliko wapotevu waliokufa maelfu ya miaka iliyopita? Hilo haliwezi kuwa sahihi.)

1.  Biblia inasema kuwa nani atateswa milele? (Shetani.)

a.  Je, hii inaonekana kuwa ni haki?  (Shetani ndiye mwanzilishi wa uovu na amekuwa akisababisha taabu kwa maelfu ya miaka.)

D.  Soma Ufunuo 20:14-15 na 1 Wakorintho 15:25-26. Jehanum inawezaje kutupwa katika ziwa la moto? Mauti yanawezaje kutupwa katika ziwa la moto? (Hapo awali waovu walimezwa na moto kutoka mbinguni. Kilichosalia ni mfumo wa mauti. Ninaelewa jambo hili likisema kwamba mambo yote yanaishia hapa. Uovu wote umetokomea moja kwa moja.)

1.  Je, Shetani pia ametokomea? (Hili ni swali makini zaidi, lakini ninadhani kwamba hata yeye hatimaye anamezwa ili kwamba mauti na jehanum vinaweza kusemwa kiukweli kwamba vimefikia mwisho.)

III.  Mtazamo wa Mungu

A.  Soma Ezekieli 18:32. Ni nini mtazamo wa Mungu kwa waovu? (Anawataka wamgeukie na waishi.)

1.  Mungu anasema kuwa njia mbadala ya kumgeukia ni ipi? (Kifo.)

2.  Je, Mungu asiyetamani mtu yeyote afe anadhamiria kuwatesa katika moto milele? (Mateso ya milele hayaendani kabisa na ufafanuzi wa mtazamo wa Mungu.)

B.  Soma Ezekieli 18:23. Ni nini jibu la swali hili fasaha? (Mungu anatutaka tujibu kwamba hafurahii kifo cha mwovu. Kwa dhahiri basi, hafurahii mateso ya waovu.)

C.  Soma Waebrania 9:25-28. Je, hii inatuambia kuwa Yesu alichukua nafasi yetu? Kwamba aliteseka kwa ajili ya dhambi zetu? (Ndiyo!)

1.  Sijawahi kusikia hoja hii hapo kabla, lakini hebu itafakari. Waebrania 9:26 inajenga hoja kwamba Yesu hakuwa na haja ya kufa kwa “kujirudiarudia” kwa sababu yeye sio mwana kondoo halisi na alijitoa kafara mwenyewe. Lakini, ikiwa adhabu ya kweli ya dhambi ni kuungua milele jehanum, je, huko sio “kujirudiarudia” ambako Yesu alipaswa kuteseka? (Ikiwa adhabu sahihi kwa dhambi ni mateso ya milele, basi Yesu hakuteseka mateso hayo kwa ajili yetu. Hii ni hoja yenye nguvu kwamba mauti, na sio mateso ya milele, ndio adhabu ya dhambi.)

D.  Soma Mhubiri 9:1-2. Haya ni maneno ya Sulemani. Je, amevuviwa na Roho Mtakatifu kutoa kauli hii juu ya mustakabali ujao? (Ikiwa Sulemani anasema kuwa mustakabali wetu wa milele ni ule ule, bila kujali kama sisi ni wema au wabaya, kwa dhahiri hilo haliendani na maandiko ya Biblia – hususani kwa mambo ambayo tumekuwa tukijifunza katika mfululizo wa masomo haya.)

E.  Soma Mhubiri 9:3. Je, hili linaendana na maandiko ya Biblia? (Ikiwa anamaanisha kwamba sote tunakufa, basi hilo ni kweli.)

F.  Soma Mhubiri 9:4-5. Je, hili ni kweli? (Ingawa inaweza kuwa kweli kwamba kuwa hai ni afadhali kuliko kuwa mfu, ni uongo wa dhahiri kwamba wafu wenye haki “hawana ijara tena.”)

1.  Je, unanukuu Mhubiri 9:5 kuelezea hali ya wafu? (Ikiwa unafanya hivyo, acha kwa sababu kifungu hicho kina kauli ya uongo wa dhahiri.)

G.  Soma Mhubiri 9:7-9. Je, Mungu anaidhinisha kila tunachokifanya? Je, maisha ndio kila kitu tulichonacho na hivyo tunapaswa kuyaishi kikamilifu?

H.  Soma Mhubiri 9:10-11. Ni nini lengo la kufanya kazi “kwa nguvu zako zote” ikiwa, kama inavyoelezwa katika kifungu cha 11, haileti tofauti yoyote kwa sababu muda na bahati vinaweza kusababisha mambo yakaenda mrama?

1.  Je, maisha yanakatisha tamaa zaidi kwa sababu baada ya kazi yetu yote nzuri sote tunakwenda jehanum? 

I.  Tunapaswa kuzielewaje kauli anazozitoa Sulemani zisizoendana na injili? (Tunaweza kuamini kwamba Biblia ni neno la Mungu lisilo na dosari kwa kuelewa kwamba vifungu tofauti vinatumika katika namna tofauti. Yesu alielezea kisa kilichopo katika Luka 16 kuhusu Lazaro na Tajiri kufafanua kwamba wanadamu wataukataa ushahidi wa ufufuo wake. Hata Sulemani mwenye hekima na tajiri alipitia mateso ya sonona na kuandika mambo ambayo hakuyaamini. Hatupaswi kupotoka kwa kunukuu kauli zake zilizokuwa na msongo wa mawazo.)

J.  Rafiki, Mungu anakupenda na hakuwazii mateso ya milele endapo utakataa ofa yake ya rehema ya uzima wa milele. Lakini, kwa nini uwe mpumbavu? Mchague Yesu na chagua uzima wa milele. Kwa nini usifanye hivyo sasa hivi?

IV.  Juma lijalo: Udanganyifu wa Wakati wa Mwisho.