Somo la 10: Kulipa Fadhila

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Luka 12
Swahili
Year: 
2023
Quarter: 
1
Lesson Number: 
10

Somo la 10: Kulipa Fadhila

(Luka 12)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2020, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Somo letu juma hili linahusu kile tunachopaswa kukifanya “katika miaka ya mwisho wa uhai wetu.” Ikiwa “ulipaji fadhila” katika kichwa cha habari unaelekezwa kwa wazazi badala ya watoto, je, hiyo haikifanyi kichwa cha habari kuwa cha ajabu sana? Kwani wazee sio maskini? Je, kilio cha “nipo kwenye mpango wa kipato kamili” sio wito kwa ajili ya kutengewa kiwango cha kifedha kinachoridhisha? Vipi kuhusu punguzo la bei katika maeneo mbalimbali kwa wazee? Je, hiyo haioneshi kwamba wao ni wahitaji? Ukweli ni kwamba wazee wengi, hususan wale waliozingatia mafundisho ya Biblia juu ya fedha, kwa kiasi kikubwa wamejiwekea akiba kwa ajili ya uzee wao. Wazee hao wanapaswa kufanyia nini mali zao katika miaka yao ya mwisho hapa duniani? Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tujifunze zaidi!

I.  Mkulima

A.  Soma Luka 12:16-17. Yesu anayaelezeaje mavuno ya mkulima? (Yesu anasema mkulima alikuwa tajiri. Kinachoashiriwa ni kwamba alikuwa tajiri kabla Yesu hajaelezea kilichofuatia.)

B.  Soma Luka 12:18-19. Je, huu ni mpango mzuri wa kibiashara? Je, huku sio kuweka akiba kwa ajili ya siku zijazo? Je, hii haifanani na kile alichokifanya Yusufu kwa maelekezo ya Mungu? Angalia Mwanzo 41:47-49.

C.  Soma Luka 12:20-21. Mungu anamuita mkulima huyu mwenye busara kuwa “mpumbavu!” Tunatakiwa kujadili maswali machache ili kuwa na uelewa mzuri wa utambulisho huo.

1.  Je, kuna sababu yoyote kuamini kwamba mkulima huyu ni mzee na hii inatufundisha jambo kuhusu uzee na fedha? (Hakuna uthibitisho kuwa mkulima huyu ni mzee – tofauti na kwamba mkulima alifariki usiku ule. Mfano huu unaweza kuwafundisha Wakristo wa umri wowote juu ya jinsi ya kushughulika na faida.)

2.  Angalia tena Luka 12:19. Je, kuna ubaya wowote na hili? Je, hii haionekani kama mkulima alijipanga kustaafu “kwa miaka mingi?”

3.  Linganisha na Luka 12:21. Kwa nini Mungu anamuita mkulima huyu “mpumbavu?” Je, ni kwa sababu alijiwekea akiba kwa ajili ya siku zijazo? (Hapana. Shtaka halisi ni kwamba alijiwekea akiba “kwa ajili yake” na “hakujitajirisha kwa Mungu.”)

a.  Inahitajika nini kujitajirisha kwa Mungu? (Kama tulivyojifunza, Malaki 3 inaweka alama ya kumrejeshea Mungu asilimia 10 ya kipato.)

b.  Unadhani kwamba Mungu anazungumzia fedha anapotoa mashtaka kuwa mkulima hakujitajirisha kwa Mungu? (Kisa hakizungumzii chochote kuhusu kama mkulima alitoa zaka katika malimbuko yake, lakini kinatuambia kwa uhakika jinsi mkulima alivyodhamiria kutumia muda wake. Mpango wa mkulima haujumuishi kauli yoyote juu ya kutumia muda wake na Mungu.)

c.  Unadhani Mungu alimuua mkulima kwa sababu kwa upumbavu wake alishindwa kutekeleza wajibu wake kwa Mungu? Kumbuka hiki ni kisa!

D.  Sidhani kama tunaweza kukielewa vizuri kisa alichokielezea Yesu kama tutashindwa kugundua sababu ya Yesu kukielezea kisa hicho. Soma Luka 12:13-15. Je, hawa wanaweza kuwa watoto wa mkulima ambaye kwa sasa ni marehemu? (Kwa kuwa Yesu anaelezea kisa cha mkulima, jibu ni “hapana,” lakini kweli hizi zinaweza kuendana na kisa.)

1.  Una mtazamo gani juu ya jibu la Yesu katika Luka 12:14? Je, kwa upande wako jambo hili linaonekana kuwa sahihi? Je, ni kweli kwamba hatuna haja ya kumjibu Yesu? (Yesu anasema tu kwamba yeye sio hakimu.)

E.  Luka 12:15 inabeba ujumbe mkuu kwenye mjadala wetu wote hadi kufikia hapa kumhusu mkulima. Yesu anatoa tahadhari gani? (Kutotamani.)

1.  Kwa nini? (“Uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu alivyo navyo.”)

2.  Je, hiyo ni tafsiri ya tamaa – kujikita kwenye umiliki wa vitu (au kutokuwa navyo) badala ya mambo mengine maishani?

a.  Tafakari jinsi tafsiri hiyo ya tamaa inavyoendana na kweli hizi. Badala ya kumwomba Yesu mwongozo wa kiroho, mtu huyu anaomba msaada wa kugawiwa fedha kutoka kwa ndugu yake.

F.  Soma tena Luka 12:16. Yesu anaelezea kisa cha mkulima ili kufafanua jibu lake kwa mtu huyu. Kwa kuzingatia hilo, hebu niambie kuwa unadhani kisa cha mkulima kinamaanisha nini? (Hatupaswi kujikita kwenye mali zetu badala ya uhusiano wetu na Mungu. Kwa nini? Kwa sababu mali zetu zinaweza kupotea kufumba na kufumbua, wakati uhusiano wetu na Mungu ni wa milele.)

1.  Je, kisa hiki kina lolote la kuwaambia wazee walio na mali nyingi?

2.  Je, kisa hihi kina chochote cha kuwaambia wazee wasio na mali nyingi?

3.  Je, umegundua kwamba watu wasio na mali nyingi mara nyingi wanajikita kwenye uzingativu wa umiliki mali kuliko wanaomiliki mali? Je, ni kama ajali tu kwamba Yesu alimwambia mtu asiye na urithi kuwa “ajilinde na choyo?”

4.  Je, kisa hiki kina fundisho kwa vijana wadogo? (Lazima kina fundisho. Kijana mdogo aliye na mgogoro wa urithi ndiye aliyeanzisha mjadala.)

G.  Baada ya kutafakari mjadala wetu wa kisa cha mkulima na muktadha wake, mkulima alipaswa kusema nini katika Luka 12:19 ambacho kingekuwa bora zaidi kuliko kile alichokisema? (Angeweza kusema, “Sina haja ya kujipatia chakula ili kuishi miaka mingi. Nitatumia muda huo kuutangaza ufalme wa Mungu, kupumzika zaidi, kufurahia kula na kunywa, na maisha yangu yatajawa furaha.)

II.  Urithi

A.  Kifo cha mkulima kwa muktadha wa mgogoro wa mtu juu ya urithi unaibua suala la jinsi ambavyo mkulima angepaswa kutafakari uwezekano wa kifo chake. Soma 1 Timotheon 5:8. Je, wazee wenye mali wanapaswa kuwapatia watoto wao mali hizo? (Tunatakiwa kuitegemeza familia. Hata hivyo, muktadha wa maelekezo haya ni kuwasaidia wale walio maskini.)

1.  Katika kutafakari uamuzi wetu juu ya fedha zetu pale tunapofariki, je, kujitajirisha kwa Mungu bado ni suala la kulizingatia? (Lazima kizingatiwe kisa cha mkulima.)

B.  Hebu tuangalie visa vinavyozungumzia kuwagawia watoto wetu mali. Soma Mithali 13:22. Chukulia kwamba watoto wako hawahitaji mali zako. Je, hii inamaanisha kwamba tuwapatie tu mali hiyo kwa sababu ya kuwajali na kuwafikiria wajukuu?

1.  Je, kwa umahsusi tunapaswa kuwategemeza wajukuu wetu?

C.  Soma 2 Wakorintho 12:14. Je, wazazi wana wajibu wa kuwagawia mali watoto wao? (Kwa kiwango kidogo hiki ndicho anachokisema.)

D.  Soma Zaburi 103:13. Kama umejibu “ndiyo” kwa swali lililotangulia, je, hili ni suala la huruma badala ya wajibu?

E.  Soma Hesabu 27:9-11. Tafakari juu ya kile kinachoandikwa hapa. Je, hii ni amri ya kuacha urithi, au amri juu ya nini kinatokea pale unapoacha urithi?

F.  Soma Kumbukumbu la Torati 21:17. Je, unadhani jambo hili bado linahusika kwa Wakristo wa leo? (Mtoa maoni mmoja alibainisha kuwa hapa ndipo mahala pekee katika Biblia panapoelezea kuwa mzaliwa wa kwanza anapaswa kupewa mafungu mawili. Kuna rejea nyingine zinazozungumzia “haki za uzaliwa wa kwanza,” zinazojumuisha vitu zaidi ya urithi wa mali. Katika Mwanzo 25:5-6 Ibrahimu alimpa Isaka yote aliyokuwa nayo, hata kama Isaka hakuwa mzaliwa wa kwanza wa kiume wala mwanaye wa pekee wa kiume.)

G.  Soma Mwanzo 49:3-4, na 1 Mambo ya Nyakati 5:1-2. Hapa kuna fundisho gani la jinsi tunavyopaswa kuwaachia watoto wetu mali? (Hii ni kuzingatia ustahili.)

H.  Soma Mithali 13:11. Hii inatoa tahadhari gani juu ya kuwahamishia mali watoto wetu mara tu baada ya kufariki kwetu? (Inaweza kuwa tatizo kwa sababu wanaweza kuipoteza/kuitapanya.)

I.  Soma 1 Timotheo 6:17. Ni urithi gani bora tunaoweza kuwaachia watoto wetu? (Kumtumaini Mungu badala ya fedha.)

J.  Rafiki, maisha yetu hayahusishi vitu tuavyovilimiki. Vinaweza kupotea ndani ya muda wa kufumba na kufumbua. Kwa nini, kulingana na 2 Wakorintho 4:18, tusiubadili mwelekeo wetu ili kujikita kwenye uhusiano na Mungu? Hiyo ni baraka ya milele.

III.  Juma lijalo: Kusimamia Nyakati Ngumu.