Somo la 3: Injili ya Milele

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Ufunuo 14
Swahili
Year: 
2023
Quarter: 
2
Lesson Number: 
3

Somo la 3: Injili ya Milele

(Ufunuo 14)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2020, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Jambo gani linakujia akilini unapokitafakari kitabu cha Ufunuo? Watu wengi wanachukulia kwamba hawawezi kukielewa. Wanyama wa kutisha, masumbufu na vitisho vitakavyotokea duniani, na maonyo ya mambo yatakayotokea yanaonekana kuwa ya kutisha. Kwa nini Mungu alimhamasisha Yohana kwa ujumbe huu? Je, ni ili kuwapa wafuasi wa Mungu tumaini na utambuzi wa kile kitakachotokea katika siku zijazo? Katika nyakati nilizokuwa nikitizama soka niliibua tabia ya kurekodi mchezo wa mpira wakati ukichezwa. Timu yangu ikishinda, ningeutazama mpira. Kitendo hiki kilinifanya niwe mtulivu. Hata kama mambo mabaya yalitokea wakati mchezo ukiendelea, nilijua kuwa hatimaye mambo yangekuwa mazuri. Hiki ndicho ninadhani Mungu anakiwazia katika kushiriki nasi kitabu cha Ufunuo – anataka kutupatia kiwango cha ujasiri na imani juu ya mambo ya kutisha yanapotokea duniani. Hebu tuzame kwenye somo letu la Ufunuo ili tujiandae kuelewa kwa utulivu matukio ya nyakatiza mwisho!

I.  Lengo

A.  Soma Ufunuo 1:1. Maoni ya Albert Barnes yanasema kuwa “Ufunuo” maana yake ni “uchi.” Una maoni yoyote kwa nini hili ni jina zuri la kitabu? (Dhana iliyopo ni kwamba mustakabali hauko wazi. Kivuli cha mambo yajayo kimetolewa.)

1.  Ni nani chanzo cha hii taarifa mpya? (Mungu alimpatia Yesu ambaye alimtuma malaika kumpatia Yohana. Yohana alikuwa mmojawapo wa wanafunzi kumi na wawili ambaye alikuwa pamoja na Yesu.)

B.  Soma Ufunuo 1:3. Je, itakuwa vizuri zaidi kuendelea kutojua habari za hii taarifa mpya? (Hapana. Tumebarikiwa kuwa makini na wasikivu wa suala hili na kulikumbuka kwa sababu ni la muhimu katika kipindi kifupi kijacho.)

C.  Soma Ufunuo 14:6. Ujumbe huu unatolewa kwa nani? (Wale wote wanaoishi duniani!)

1.  Je, sio ujumbe wa muhimu kwa mtu yeyote? (Ni kwa ajili ya “kila taifa na kabila na lugha na jamaa.” Mtu yeyote anayesema kuwa ujumbe huu haumhusu atakuwa amekosea.)

2.  Je, hii ni injili mpya? Je, ni “habari iliyotokea hivi punde?” Habari mpya? (Hapana. Ni injili ya “milele.” Mara zote ujumbe huu umekuwa ni injili.)

3.  Unadhani kwa nini taswira ya malaika huyu inaonekana kama “anaruka moja kwa moja juu?” (Hii ni taswira ya mwendo wa kasi na ujumbe ulioelekezwa kwetu.)

II.  Malaika wa Kwanza

A.  Soma Ufunuo 14:7. Ujumbe huu umejumuishwa kwenye sentensi moja! Hebu tuiangalie kwa kina zaidi. Kwa nini tumche na kumtukuza Mungu? (“Saa ya hukumu yake imekuja.”)

B.  Soma Danieli 7:9-10. Hukumu hii ni ipi? (Inaonekana kuwa hukumu ya mwisho inayorejelewa katika Ufunuo 14:7.)

C.  Soma Danieli 7:13-14. Nani anayeshinda hukumu hii? (Wale wanaomtumikia Yesu. Wao ni sehemu ya ufalme wa milele.)

D.  Hebu tujikite kwenye nusu ya mwisho ya Ufunuo 14:7. Ni kwa msingi gani Mungu anadai utii wetu kwake? (Yeye ni Mungu Muumbaji wetu.)

1.  Uumbaji huu unaelezewa katika kitabu cha Mwanzo sura ya 1 na 2. Je, ni lazima tukubali maelezo ya kitabu cha Mwanzo kujumuishwa kwenye kundi hili la waabudu? (Ikiwa huamini msingi mahsusi ya kuabudu kwako, sioni ni kwa namna gani unaweza kuitwa muabudu. Aina hiyo ya uabudu ni ulaghai.)

2.  Hivi leo kuna mambo yanayobishaniwa sana ambayo yanahusishwa moja kwa moja na maelezo ya uumbaji. Suala mojawapo ni kuhusu mianzo – je, wanadamu waliumbwa kwa mkono wa Mungu au ni matokeo ya mabadiliko yaliyotokea pole pole? Suala jingine linahusu ndoa, je, ndoa ilibuniwa kuwa kati ya mwanaume na mwanamke wanaokuwa “mwili mmoja?” Suala la tatu linahusu jinsia. Je, kuna jinsia mbili pekee, au hili ni suala linalobadilika umbo kabisa, hivyo jinsia inaweza kubadilika?

a.  Je, ni muhimu kuyakubali maelezo ya Biblia kwenye masuala yote haya ili kuwa muabudu wa kweli?

3.  Ikiwa umejibu kuwa mtazamo wa muabudu wa kweli lazima uendane na maelezo ya Biblia, je, hili ni jambo linalopaswa kuhubiriwa na kufundishwa na Wakristo? Na je, hiyo itakuwa sehemu ya ujumbe wa Malaika wa Kwanza?

4.  Ikiwa jibu lako kwenye swali la awali ni “hapana,” unadhani ni nini yaliyo maudhui ya ujumbe wa Malaika wa Kwanza?

E.  Angalia tena nusu ya mwisho ya Ufunuo 14:7 kwa mtazamo tofauti kidogo. Je, unaweza kuona uhusiano wowote wa kimantiki kati ya wito wa kumwabudu Mungu na huu ufafanuzi wa shughuli za Mungu? (Shughuli hizi ndizo zinazomstahilisha Mungu kuabudiwa. Zinaakisi uwezo wake, mamlaka yake juu ya uumbaji.)

1.  Kuna sinema maarufu ya mwaka 1939 iitwayo “The Wizard of Oz.” Matokeo yake ni kwamba mchawi mkuu na mzuri ajabu alikuwa mlaghai. Alikuwa ni mtu tu akiendesha mashine iliyotoa taswira ya uongo ya uwezo na nguvu. Je, hivi ndivyo wanavyochukulia wale wasioyaamini madai ya Mungu ya kuwa na uwezo? Je, bado unaweza kudai kuwa wewe ni Mkristo kama unaamini madai yanafanana na mtu aliye nyuma ya pazia kwenye sinema ya “Wizard of Oz?” (Imani hii inaonekana kuwa ya kawaida na iliyozoeleka, na sielewi mantiki yake.)

III.  Injili ya Milele

A.  Angalia tena Ufunuo 14:6-7. Biblia inaipa jina sentensi hii moja kama “injili ya milele.” Je, hivyo ndivyo unavyoielewa injili: Mungu Muumbaji wetu ameanza kutoa hukumu yake?

1.  Je, hiki sio kinyume tu cha namna tunavyopeleka injili: Mungu wetu mwenye upendo aliishi na kufa kwa ajili yako ili uweze kuepuka matokeo ya hukumu ya mwisho? Kwa nini usimkiri yeye kama Mwokozi wako sasa hivi?

B.  Soma 1 Wakorintho 15:1-2. Paulo anasema kuwa alihubiri nini? (“Injili.”)

1.  Ni nini matokeo ya kuipokea injili ya Paulo? (Wanaokolewa.)

C.  Soma 1 Wakorintho 15:3-5. Namna ambayo Pulo anafafanua injili anayoihubiri ni namna iyo hiyo ambayo na mimi ninashiriki injili na wengine. Hii inaonekana tu kuwa kinyume na injili ya milele aliyoishirikisha Malaika wa Kwanza. Unaweza kupatanisha mambo haya mawili?

D.  Soma Warumi 3:21-24. Je, hii ni injili? (Ndiyo! Ni injili kama ninavyoielewa na kuifundisha.) 

1.  Je, hii pia ni tofauti na injili ya milele iliyotangazwa na Malaika wa Kwanza? (Kwa dhahiri inaonekana kuwa tofauti sana.)

E.  Ninaiamini Biblia. Inaonekana kuwa vigumu kupatanisha injili ya Malaika wa Kwanza na injili iliyohubiriwa na Paulo katika 1 Wakorintho na Warumi. Hebu tuanze kwa kujiuliza kitu gani kimeachwa nje ya ujumbe wa injili iliyotangazwa na Malaika wa Kwanza? Kweli gani za msingi zinakosekana kwenye ile sentesi moja? (Anguko la wanadamu. Kuingia kwa dhambi. Yesu kutuokoa. Malaika wa Kwanza anamtangaza Yesu kama Muumbaji na kisha anarukia kwenye historia yote iliyosalia hadi kwenye hukumu ya mwisho.)

1.  Je, hizi ni taarifa zisizo za msingi, yaani, taarifa zilizoachwa na Malaika wa Kwanza? (Hapana. Ni za muhimu.)

2.  Hebu subiri kidogo. Je, umuhimu wa taarifa unageukia kwenye chimbuko la uamuzi wako?

F.  Chukulia kwamba unazungumzia juu ya mashindano makubwa ya magari unayoyamiliki. Unaelezea uzuri wake na uwezo wake ilipotengenezwa kwa mara ya kwanza. Unaelezea juu ya mashindano muhimu yajayo na unatangaza kuwa gari hili litashinda mashindano hayo. Hata hivyo, unashindwa kubainisha kwamba gari hili lilikuwa limeharibika sana, injini ilikuwa mbovu, na bodi ya gari na injini zimetengenezwa upya kabisa. Je, maelezo haya mafupi kuhusu uwezo na ushindi yangekuwa ya muhimu sana? (Ninadhani jibu ni “ndiyo.” Masuala ya msingi ni hali ya sasa ya gari na ukweli kwamba gari hili litashinda. Kama ungekuwa unalinunua gari tofauti na kutarajia ushindi historia ya gari katika kipindi fulani ingekuwa ya muhimu. Hivyo ndivyo ninavyopatanisha kauli za Malaika wa Kwanza na Paulo kuhusu injili. Malaika wa Kwanza anaelezea kilicho cha muhimu sasa hivi, na sio kufundisha juu ya njia ya kupata wokovu.)

G.  Soma Mathayo 28:19-20. Unahusianishaje vifungu hivi na ujumbe wa Malaika wa Kwanza? (Yesu anarejelea “mwisho wa nyakati.” Malaika wa Kwanza anatoa uharaka kwenye injili. Mungu Muumbaji wetu anayasogeza mambo karibu na mwisho wake.)

H.  Rafiki, mwisho unakuja. Ikiwa huamini inachokisema Biblia kuhusu mwanzo wa dunia, yumkini usiweze kuamini maelezo ya nyakati za mwisho. Ikiwa una mashaka, kwa nini usimwombe Roho Mtakatifu, sasa hivi, ayaongoze mawazo yako katika kweli yote?

IV.  Juma lijalo: “Mcheni Mungu na Kumtukuza.”