Somo la 5: Habari Njema ya Hukumu

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Ufunuo 20, Waefeso 2, Mathayo 22
Swahili
Year: 
2023
Quarter: 
2
Lesson Number: 
5

Somo la 5: Habari Njema ya Hukumu

(Ufunuo 20, Waefeso 2, Mathayo 22)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2023, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Fikiria jambo hili la kufurahisha kuhusu hukumu. Kila mtu anataka watu wengine wahukumiwe kwa kile walichokitenda (au kile wanachodhani kuwa wamekitenda). Lakini hakuna mtu anayetaka kuhukumiwa. Je, umewahi kujisemea, “Ninatamani gari la polisi lingekuwa hapa ili washuhudie jinsi mtu huyu anavyoendesha gari?” Kwa upande mwingine, je, huwa unafurahia pale gari la polisi lililo nyuma yako linapokuwashia vimulimuli vya taa kukuashiria kuwa usimame na kuegesha gari pembeni mwa barabara kwa kukiuka sheria ya usalama barabarani? Tumekuwa tukijifunza Ufunuo 14:7 ambayo inaonya kwamba “saa ya hukumu yake imekuja.” Je, inawezekana kwamba hukumu hii ni kwa ajili ya watu wengine na sio kwa ajili yako? Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia ili tujionee!

I.  Vitabu

A.  Soma Ufunuo 20:11. Unadhani ni nani yuko kwenye kiti hiki cha enzi? (Mungu.)

1.  Ni kwa vipi mbingu na nchi zinakimbilia pahala? Na kwa nini zikimbie? (Zingatia ufafanuzi wa kiti cha enzi, ni “kikubwa” na “cheupe.” Nadhani hiyo maana yake ni kwamba kinatisha na kinaangaza. Kitu gani hutokea kwa nyota na mwezi jua linapochomoza na kuangaza? Zinapotea. Hicho ndicho kinachotokea hapa. Taswira ya kiti cha enzi inatisha na kuangaza sana kiasi kwamba hatuwezi tena kuona nchi na anga.)

B.  Soma Ufunuo 20:12. Tunaona “vitabu” vya aina gani hapa? (Kuna “vitabu” na kisha kuna “Kitabu cha Uzima.” Vyote vinafunguliwa.)

1.  Taarifa gani inamaanishwa kwa taswira ya maneno ya “vitabu kufunguliwa?” (Vitabu huandika taarifa na kumbukumbu. Ukifungua kitabu utaangalia taarifa iliyoandikwa ndani yake.)

2.  Aina gani ya taarifa imo ndani ya vitabu hivi? (Kumbukumbu ya kile ambacho wale wanaohukumiwa wamekitenda.)

a.  Hii inakuambia nini kuhusu aina ya hukumu ya Mungu? (Mungu sio dikteta. Kuna ushahidi wa kimaandishi. Watu hawa hawahukumiwi kwa kuzingatia hadhi, fedha, ushawishi, rushwa, au kumbukumbu ya uongo. Wanahukumiwa kutokana na matendo yao yaliyoandikwa)

C.  Hebu turukie chini na kusoma Ufunuo 14:15. Matendo yako yakiwa yanapitiwa kwenye hukumu, matokeo yake ni yepi? (Unatupwa kwenye ziwa la moto.)

1.  Hiyo inatuambia nini kuhusu asili ya matendo yaliyowekwa kwenye kumbukumbu? (Kwa ujumla lazima yatakuwa mabaya. Taswira iliyopo ni kwamba matendo mabaya ya watu hawa yameandikwa, wanahukumiwa kutokana na matendo haya mabaya, na kisha wanaangamizwa kwa moto.)

D.  Yote haya yanatisha kuyasikia. Hebu tuangalie tena Ufunuo 20:12 na Ufunuo 20:15. Kitabu gani ni cha kipekee? (Kitabu cha Uzima.)

1.  Kitu gani kimeandikwa kwenye Kitabu cha Uzima? (Biblia inasema kuwa majina yameandikwa. Hii inamaanisha kuwa majina na wala sio matendo, ndio yameandikwa. Kimsingi, kwenye vitabu vingine kumbukumbu ya matendo bila majina haina maana yoyote. Lakini uhalisia haufafanui kwa nini Kitabu cha Uzima kinabainishwa kwa umahsusi kwamba kinajumuisha majina.)

E.  Hebu tuangalie vifungu vingine kwenye mjadala huu. Soma Waefeso 2:4-5. Tuna tumaini gani ikiwa matendo yaliyoandikwa kwenye vitabu ni mabaya? (Hakuna tumaini lililojengwa juu ya matendo yetu. Tunafanywa kuwa hai kwa sababu ya neema tuliyopewa na Yesu.)

F.  Soma Waefeso 2:6. Je, maoni haya yanahusu kipindi baada ya hukumu? (Itakuwa hivyo. Wale waliookolewa kwa neema wapo na Yesu mbinguni.)

G.  Soma Waefeso 2:7-9. Je, wale waliookolewa kwa neema wameokolewa kwa matendo yao? (Hapana. Kwa mahsusi matendo yamekanushwa.)

1.  Tukisoma Waefeso 2 ndani ya Ufunuo 20 inatuambia nini kuhusu hiki Kitabu cha Uzima? (Kina majina ya wale waliookolewa kwa neema. Hakina kumbukumbu ya matendo kwa kuwa watu hawa hawahukumiwi kwa matendo yao.)

2.  Hebu tuliangalie hili kwa mtazamo wa kiuhalisia zaidi. Ufunuo 20:12 inarejelea idadi isiyo kamili ya vitabu kwa ajili ya kuweka kumbukumbu ya matendo, isipokuwa Kitabu kimoja tu cha Uzima. Hii inatuambia nini, kwa mtazamo wa kiuhalisia, kuhusu kama Kitabu cha Uzima kinaweka kumbukumbu ya matendo? (Kuandika jina lako huchukua nafasi ndogo zaidi kuliko kuandika matendo yako katika kipindi chote cha maisha yako.)

II.  Kisa cha Yesu Kuhusu Hukumu

A.  Soma Mathayo 22:1-2. Kisa hiki kinahusu nini? (Ufalme wa Mbingu. Kwa kuwa tutaona kwamba kisa hiki kinaelezea kigezo cha kuingia kwenye Ufalme, hivyo basi kinatuhabarisha juu ya hukumu iliyotolewa kwa ajili ya kuingia.)

B.  Soma Mathayo 22:3-4. Hii inasemaje kuhusu namna tunavyoingia mbinguni? Je, tunapaswa kuitikia wito? (Unatakiwa kupewa mwaliko. Hii haituambii jinsi kundi hili lilivyochaguliwa ili kupewa mwaliko.)

1.  Mfalme anasisitiza kwa kiasi gani katika kuwapata waalikwa kuhudhuria?

C.  Soma Mathayo 22:5-7. Hii ni hukumu ya kutisha! Kwa dhahiri hawaendi mbinguni. Wageni hawa watarajiwa walifanya nini kiasi cha kustahili hukumu? Hawakujali na pia walikuwa na chuki kutokana na mwaliko wa Mfalme. Walishughulishwa zaidi na mambo mengine na hawakumpa Mfalme kipaumbele.)

D.  Soma Mathayo 22:8. Hukumu ni ipi kwa wale ambao hawakuja? (“Hawakustahili.” Tutarudi kwenye jambo hili.)

E.  Soma Mathayo 22:9-10. Kifungu hiki kinatuambia jinsi kundi hili lilivyochaguliwa ili kupokea mwaliko kwenye harusi. Kigezo hicho kilikuwa ni kipi? (Kila aliyepatikana na aliyekuwa tayari kuja.)

1.  Tunaambiwa kwa umahsusi kwamba jambo gani halikuwa kigezo cha kuwaalika kundi hili jipya la wageni? (matendo yao. Tunaambiwa kuwa wageni “waovu kwa wema” walialikwa na kuja.)

2.  Kitu gani basi kinamaanishwa katika Mathayo 22:8 kuhusu “kustahili?” (Inamaanisha kuitikia mwaliko.)

F.  Soma Mathayo 22:11-13. Ilikuwaje mtu huyu hakualikwa kwenye harusi? (Hakuwa amevaa “vazi la harusi.”)

1.  Kwa kuwa kisa hiki kinahusu Ufalme wa Mbingu, hii inatuambia nini kuhusu aina ya hukumu – hususan kwa mtu huyu mmoja? (Ni mtu ambaye, kwa kuzingatia maelezo ya Ufunuo 20, anatupwa kwenye ziwa la moto.)

2.  Hebu tuangalie yale tuliyojifunza. Tunao wale walioshinda kila aina ya jaribu ili kukubaliwa kuingia mbinguni na wale waliohukumiwa hukumu ya uangamivu. Elezea jinsi waovu walivyoshindwa kuingia mbinguni? (Wanaangukia kwenye makundi kadhaa. (Wanampuuzia Mfalme, wanapendelea kujishughulisha na mambo yao badala ya kutumia muda wao kwenye harusi ya Mfalme, wanakuwa na uadui na watumwa wa Mfalme au wanawachukia watumwa wa Mfalme na kuwaua. Kuna kundi jingine, mtu aliyekubali mwaliko wa Mfalme lakini akashindwa kuvaa vazi la harusi.)

G.  Angalia tena Mathayo 22:11-12. Tunatakiwa kulielewa hili vazi la harusi! Unadhani wageni walipataje vazi la harusi? (Wageni hawakuja na vazi la harusi kutoka nyumbani kwa sababu kisa hiki kinasema kuwa walikusanyika kutoka “njia panda za barabara.” Mwanzoni mwa safari yao hawakujua kuwa walikuwa wanakwenda kuhudhuria harusi muhimu. Hitimisho pekee lenye mantiki ni kwamba Mfalme alitoa mavazi ya harusi.)

1.  Kila mtu alikuwa amevaa vazi la harusi isipokuwa mtu huyu mmoja. Unadhani kwa nini mtu huyu alitekewa alipoulizwa aliingiaje ndani ya ukumbi bila kuwa na vazi la harusi? (Hakuwa na utetezi wala kisingizio.)

a.  Hiyo inatuambia nini kuhusu vazi la harusi? (Hatuna sababu yoyote ya kutolipokea kutoka kwa Mfalme. Mwitiko huu unasisitiza dhana ya kwamba watu wema na waovu wanakubaliwa ikiwa watavaa vazi la harusi. Kama suala lilikuwa ni endapo mtu huyu alikuwa mwovu au mwema, basi kwa dhahiri tungesikia hoja kutoka kwake. Angalia, kwa mfano, uamuzi ulioandikwa katika Mathayo 7:21-23.)

H.  Ili kuangalia kwa kina zaidi hili vazi la harusi, soma Ufunuo 19:8, Isaya 61:10, Isaya 64:6, na Zekaria 3:4. Ufunuo 19:8 inalirejelea vazi kama “matendo ya haki ya watakatifu.” Hata hivyo, vifungu vingine vinasema kuwa vazi linaloakisi matendo yetu ni “vazi chafu.” Tunapaswa kuelewa nini kutokana na vifungu hivi ambavyo yumkini vinakinzana? (Ukichukua kile tulichojifunza katika Waefeso, kwamba matendo yetu hayatuokoi, ukiongezea na kukubalika kwa wageni wema na waovu kwenye harusi ambao walikuwa tayari kuvaa vazi, rejea ya vazi katika Ufunuo 19:8 inaonekana kuwa tofauti kabisa. Ukiiangalia kwa ukaribu zaidi, kanisa ndilo linalovaa vazi hili, na linaweza tu kumaanisha kuwa matendo ya haki ya watakatifu yanaliakisi vizuri kanisa.)

I.  Soma Mathayo 22:14. Wageni harusini “walichaguliwaje?” (Walijichagua wenyewe. Walikubali kuja na walikubali vazi la harusi.)

J.  Rafiki, hii ndio hukumu isio na kifani ambayo sote tunaitaka, ikiwatokea wengine na sio kwetu. Kwa nini? Kwa sababu tumepokea na kukubali wito wa Mfalme wa kwenda mbinguni na tumepokea vazi lake la haki badala ya kuyategemea matendo yetu. Hii ni ofa nzuri sana. Je, utaipokea sasa hivi?

III.  Juma lijalo: Saa ya Hukumu Yake.