Somo la 5: Upatanisho Mlalo: Msalaba na Kanisa

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Waefeso 2:11-22
Swahili
Year: 
2023
Quarter: 
3
Lesson Number: 
5

Somo la 5: Upatanisho Mlalo: Msalaba na Kanisa

(Waefeso 2:11-22)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2023, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: “Upatanisho Mlalo?” Hiyo inaonekana kama hisabati za jiometri (geometry). Kabla wale wanaotaabishwa na hisabati hawajapata changamoto miongoni mwetu, hapa tunazungumzia kuhusu uhusiano na sio hisabati. Kwa umahsusi, uhusiano wetu na watu wengine na sio uhusiano wa “juu” kati yetu na Mungu. Hii leo hili ni suala tatanishi. Katika Ufunuo 2:20-21 tulisoma juu ya mshiriki wa kanisa ambaye, pamoja na mamo mengine, “anawafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini.” Kanisa hilo la Thiatira linaonywa “kutomvumilia” mshiriki huyo kwa sababu hatatubu. Hii leo tuna makanisa ambayo sio tu kwamba yanavumilia dhambi ya uzinzi, bali “wanajivunia” dhambi hiyo. Kweli kabisa wanajivunia? Tunawaoneshaje upendo wale wanaotuzunguka bila kuvuka msitari na kuwa kanisa la “Thiatira?” Tatizo katika Efeso lilikuwa lipi na lilitatuliwaje? Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tujifunze zaidi! 

I.  Mwingine

A.  Soma Waefeso 2:11. “Watu wa Mataifa kwa jinsi ya mwili” ni kitu gani? Na kwa nini Paulo anarejelea “tohara ya mwilini iliyofanyika kwa mikono?” (Kwa kuwa wanadamu wanaweza kutengeneza hizi tofauti (kutahiriwa au kutotahiriwa) inaonekana kama Paulo anadhani utofauti huu ni bandia.)

1.  Unaona mfanano gani katika jamii yetu leo? (Tofauti za juujuu zilizojengwa juu ya mionekano inayoweza kubadilika. Hiyo itajumuisha uvaaji, nywele, mapambo ya nje.)

2.  Anachokizungumzia Paulo sio sawa na jinsi tunavyopachika nywele zetu kwa sababu tohara ilikuwa na maana muhimu ya kiroho. Jambo gani litakuwa mfanano wa kisasa? (Hebu tuangalie nyuma kabla hatujaangalia mbele. Wayahudi waliwachukulia watu wa Mataifa kama watu waliotengwa, waliokataliwa na Mungu. Hii leo mfanano utakuwa ni wapagani au Wakristo waliopo makanisani tunaowachukulia kuwa na mafundisho duni.)

B.  Soma Waefeso 2:12. Kuna tatizo gani kubwa zaidi kwa Waefeso kuwa watu wa Mataifa? (Hawakuwa na Mungu, na hawakuwa na tumaini. Mungu hakuwa amewaahidi, bali aliwaahidi watu wake – Wayahudi. Hizi sio tofauti bandia.)

II.  Kumwondosha Mwingine

A.  Soma Waefeso 2:13. Sasa watu wa Mataifa wamewekwa karibu. Kivipi? (“Kwa damu yake Kristo.” Hii ni rejea ya dhahiri kwa kile ambacho Yesu alitutendea pale msalabani.)

B.  Soma Waefeso 2:14. Kifungu kinasema kuwa kwanza Yesu “ndiye amani yetu.” Mtu anawezaje kuwa amani?

1.  Tunaona kidokezo kwenye hilo swali hapo juu kwenye kauli ambayo Yesu “alitufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja.” Yesu aliwafanyaje watu wa Mataifa na Wayahudi kuwa “wamoja?” (Hawakuwa tena watu wa Mataifa au Wayahudi, bali walifanyika kuwa Wakristo – sasa ni wamoja. Hivyo ndivyo ambavyo Yesu “mwenyewe” alivyo amani yetu.)

2.  Kifungu hiki pia kinasema kuwa Yesu “amevunjavunja katika mwili wake” tofauti kati ya Wayahudi na Mataifa. Hilo lina ukweli gani? (Yesu aliwafia Wayahudi na Mataifa. Aliwapa Wayahudi njia mpya ya kumwendea Mungu na aliwapa Mataifa njia ya wokovu.)

C.  Soma Waefeso 2:15. Ni kwa jinsi gani “sheria ya amri” inasababisha mgawanyiko kati ya Wayahudi na Mataifa? (Kuzishika sheria na amri ndiko kulikowafanya Wayahudi wajihisi kuwa bora kwa Mataifa. Kulikuwa na ukweli mkubwa kwenye hisia kwamba walikuwa na faida – angalia Waefeso 2:12.)

1.  Ni kwa jinsi gani “kuiondosha sheria ya amani” husababisha “hao wawili kuwa mtu mpya mmoja?” (Soma Warumi 8:1-4. Sidhani kama Paulo anataka kukomesha Amri Kumi, bali anatufundisha kuwa Yesu alizishika Amri Kumi kwa ajili yetu. Alifanya hivyo kwa Wayahudi na Mataifa. Kwa muktadha huo hakuna sababu kwa mtu yeyote kujihisi kuwa ni duni.)

D.  Soma Waefeso 2:16. Msalaba ni fursa sawa ya chanzo cha wokovu. Ukweli huo unaukomeshaje uhasama? (Wayahudi na Mataifa walikuwa maadui kwa sababu mmoja alijihisi kuwa bora, na mwingine alichukia kitendo hicho. Msalaba unasawazisha uwanja wa mchezo. Hakuna tena “mwingine.”)

III.  Kuitumia Kanuni Leo

A.  Soma Waefeso 2:17-18. Tunakuwaje na njia sawa ya kumkaribia Mungu? (Kupitia kwa Yesu tunayo njia kupitia kwa Roho Mtakatifu kwenda kwa Mungu Baba.)

1.  Hebu tujadili utatanishi niliouibua kwenye sehemu ya utangulizi. Kuna mpambano unaoendelea kanisani kwangu na kwa watu wengine kuhusu jinsi tunavyopaswa kukabiliana na wadhambi wanaojivunia dhambi yao. Kanisa la Kimethodisti limegawanyika kutokana na suala hili. Je, tunapaswa kutumia fundisho la Paulo kuhusu kuwapatanisha Wayahudi na Mataifa kwenye swali la sasa kuhusu jinsi ya kukabiliana na wale wanaojivunia dhambi yao? Je, hilo linaweza kupatanishwa kwa njia ile ile?

2.  Soma Warumi 8:4-6. Je, wale wanaoongozwa na Roho wataitangaza dhambi au kujivunia kwayo? (Hapana. Tunaitwa “kuenenda” kwa kufuata mambo ya Roho na sio kwa kufuata mambo ya mwili.)

3.  Vipi kuhusu Paulo kuwaambia Wayahudi kwamba kujivunia utii wao kulikoma pale ambapo kila mmoja anapoelewa kuwa anaokolewa kwa utii wa Yesu? Je, hiyo haihusiki kwenye hali na mazingira ya sasa? (Sio Wayahudi wala Mataifa waliokuwa wakamilifu katika utii wao. Yesu pekee ndiye mkamilifu. Hivyo, majivuno katika utii hayapo. Lakini hiyo haimaanishi tutangaze na kushadadia dhana ya kujivunia dhambi. Angalia Warumi 8:6. Ikiwa kujivunia utii hakupo, tunawezaje kudhani kuwa majivuno ni dhambi?

B.  Soma Warumi 8:12-13. Je, wale wanaoishi kwa kuzingatia uongozi wa Roho Mtakatifu wanajali kuhusu utii? (Ndiyo. Kifungu cha 13 kinasema kuwa “twayafisha matendo ya mwili.” Hakisemi kuyahamasisha matendo ya mwili.)

1.  Kama tungeingia kwa kina kwenye vuguvugu la majivuno, nadhani tungegundua kuwa wachache wanahoji kuwa wanadamu wanapaswa kujivunia dhambi zao. Bali, hoja yao ni kwamba kile wanachokihamasisha sio dhambi. Kukiri hilo kunarahisisha mjadala.

2.  Baadhi ya watu wanaweza kulalamika kwa kitendo cha mimi kuibua suala hili. Kama pambano limekolea, je, unapaswa kusimama kwenye msitari wa mapambano ukiwa na sare zako zilizovaliwa vizuri, au unapaswa kusogea eneo halisi la mapigano?

3.  Je, kuna dhambi zaidi ya moja kanisani ambayo mdhambi anadai kuwa anajivunia?

C.  Soma Waefeso 2:19-21. Katika kipindi cha Paulo kiuhalisia Mataifa walizuiliwa kuingia katika hekalu Yerusalemu. Hali yao ya sasa ikoje kama Wakristo? (Wao ni sehemu ya jengo la hekalu!)

1.  Hebu tuangalie kwa kina hii inamaanisha nini. Ikiwa sisi ni sehemu ya hekalu la Mungu, je, kuna mahali mahsusi kwa ajili yetu sote? (Sote tuna wajibu mahsusi wa kuwa hekalu. Angalia 1 Wakorintho 12.)

2.  Ni nini lilikuwa lengo la hekalu Yerusalemu? (Palikuwa ni mahali alipokaa Mungu. Ni mahali palipompa Mungu utukufu.)

a.  Ikiwa sasa wewe ni sehemu ya hekalu jipya, je, hivyo vipengele vya hekalu la Yerusalemu vinahusika kwako? Je, Mungu anakaa ndani yako? Je, utampa Mungu utukufu?

D.  Angalia tena Waefeso 2:21. Je, “jengo lote” ndilo kanisa leo?

1.  Kama umejibu kuwa, “ndiyo,” kwenye swali lililotangulia, basi je, unapaswa kuabudu tofauti na kanisa? (Mjadala tuliokuwa nao unajielekeza kwenye mchangamano (fellowship.) Tunakuwa na mtazamo sahihi dhidi ya watu wengine, na tunatengeneza hekalu la Mungu linalostahili.)

2.  Utalifafanuaje “kanisa?” (Mara zote nimekuwa mshiriki wa madhehebu yanayoamini kuwa mafundisho yake ni bora kuliko ya madhehebu mengine. Nilipokuwa mtu mzima nilitambua kuwa madhehebu mengine mengi yana mtazamo kama huo. Kwa nini basi wawe na madhehebu?)

a.  Ni kwa jinsi gani dhana ya madhehebu iathiri dhana ya kila Mkristo kuwa sehemu ya jengo la hekalu? (Ninadhani madhehebu yako sawa. Unaabudu na watu ambao kwa ujumla wana uelewa kama wako kuhusu Biblia. Kisicho sawa ni kudhani kuwa wewe ni bora zaidi kwa sababu ya madhehebu yako. Haya ni marudio ya uhasama kati ya Wayahudi na Mataifa.)

E.  Soma Waefeso 2:22. Mungu anakaaje ndani yako na katika jengo la kanisa? (“Katika Roho.” Lazima tuhakikishe kuwa tumemkaribisha Roho Mtakatifu maishani mwetu. Bila kufanya hivyo basi kiukweli sisi ni “yule mwingine.”)

F.  Rafiki, katika uhusiano mlalo kati ya Wakristo sisi ni wamoja katika Yesu. Hatuna uhasama na hatujivuni kutokana na mafundisho ya kiimani au matendo yetu. Kristo pekee ndiye aliyetuokoa. Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu ndiye sehemu ya hekalu la Mungu. Je, utaungana na hekalu hilo? Je, utaitegemea kafara na maisha ya Yesu? Je, utaishi kwa kumzingatia Roho Mtakatifu? Kwa nini usichukue uamuzi huo sasa hivi?

IV.  Juma lijalo: Siri ya Injili.