Karama za Kiroho kwa Ajili ya Uinjilisti na Ushuhudiaji

(Matendo 1, 2, 8 & 13, Yohana 20, Yoeli 2)
Swahili
Year: 
2012
Quarter: 
2
Lesson Number: 
3

Utangulizi: Je, ni kweli kwamba sote tuna angalao karama moja ya kiroho? Juma lililopita tulijibu kuwa “ndiyo.” Lakini je, tunajenga dhana isiyo na dhamana? Ili uwe na karama ya kiroho ulipaswa kwanza uwe umeshampokea Roho Mtakatifu, sawa? Ninapoliangalia jambo hili kwa undani zaidi ndivyo ninavyozidi kusumbuliwa nalo. Juma hili somo letu litakuwa tofauti kidogo. Badala ya sisi kusoma Biblia, na mimi kupendekeza hitimisho, nina uhakika kabisa kuwa nipo sahihi, juma hili tutakuwa tukisaidiana kupata majibu kwa pamoja. Nina tatizo na sina uhakika sana na suala hili. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tuone kile tunachoweza kujifunza kuhusiana na kile inachomaanisha kumpokea Roho Mtakatifu!

  1. Roho Mtakatifu na Yesu
    1. Soma Matendo 1:1-5. Je, tunajifunza nini kuhusu kubatizwa kwa ubatizo wa Roho Mtakatifu? (Yesu aliuhaidi. Tunauhitaji. Sio ubatizo wa maji.)
      1. Kwa nini wanafunzi walimhitaji Roho Mtakatifu?
    2. Hebu tuangalie kisa kifupi hapa. Soma Mathayo 3:11. Je, nini kinachotabiriwa kuhusu Yesu na Roho Mtakatifu? (Kwamba matokeo ya imani katika Yesu ni kutuletea Roho Mtakatifu.)
    3. Soma Yohana 16:5-11. Je, unamlinganishaje Roho Mtakatifu na Yesu? (Yesu anasema kuwa Roho Mtakatifu ni wa hadhi ya juu! Yesu anasema kwamba “ni vizuri” yeye anaondoka, kwa sababu “Mfariji” (Roho Mtakatifu) hatakuja kama yeye hataondoka. Haitakuwa vyema kwa Yesu kuondoka isipokuwa kama Roho Mtakatifu ni “bora.”)
      1. Inaonekana jambo lisiloweza kufikirika ya kwamba kingine kingeweza kuwa bora zaidi ya kuwa na Yesu kuweza kuishi nasi. Je, Yesu anamaanisha nini kwa kauli hii? (Yesu anaorodhesha mambo ambayo Roho Mtakatifu atayafanya. Lakini, mantiki inaniambia kuwa Roho Mtakatifu ni “bora” kwa sababu anaweza kuwepo mahali pote kwa wakati mmoja.)
      2. Kama Yesu ndiye mbadala wa Yesu kuishi pamoja nawe, ni muhimu kiasi gani kupokea ubatizo wa Roho Mtakatifu? (Bila Roho Mtakatifu tunazama. Ni wa muhimu sana.)
    4. Soma Yohana 16:13-15. Je, hii inapendekeza nini kuhusu uhusiano uliopo kati ya Roho Mtakatifu na Yesu?
  2. Kuipokea Karama
    1. Soma Matendo 1:12-14. Je, wanafunzi walijiandaaje kumpokea Roho Mtakatifu? (Maombi ya mara kwa mara.)
    2. Soma Matendo 2:1-4. Je, wanafunzi walijuaje kuwa walikuwa wamepokea ubatizo wa Roho Mtakatifu? (Usingewezaje kujua! Sauti kali, ghadhabu, moto, na ushuhudiaji wa wazi wa wanafunzi.)
      1. Je, unafahamu kuwa unaye Roho Mtakatifu maishani mwako?
      2. Kama hufahamu, basi jibu ni “hapana,” sawa? Au ndivyo hivyo?
      3. Je, umewahi kuwa na uzoefu wa sauti kali, ghadhabu, moto au utokewaji wa hadharani? (Rafiki, nakwambia kuwa swali langu linanisumbua akili. Ninaamini kuwa Roho Mtakatifu ananiongoza kuyaandaa masomo haya, lakini sijawahi kuwa na uzoefu wa sauti kali, ghadhabu, moto au utokewaji wa hadharani.)
    3. Hebu tuangalie mafungu mengine mawili ambayo huenda hujawahi kuyagundua katika siku za nyuma. Soma Yohana 20:19-23. Je, Yesu aliwapatia nini wanafunzi? (Aliwavuvia karama ya Roho Mtakatifu, na ikawapatia uwezo.)
      1. Je, palikuweppo na udhihirisho wa hadharani? (Hakuna udhihirisho uliorekodiwa.)
      2. Soma tena Matendo 1:1-2. Je, nani aliyewapa maelekezo mitume? (Yesu alimtumia Roho Mtakatifu!)
      3. Baada ya ufufuo wa Yesu, mara mbili wanafunzi wanapewa msaada na Roho Mtakatifu. Je, kwa nini baadaye Yesu aliwaambia kuwa “wasubiri” “kubatizwa kwa Roho Mtakatifu?” Matendo 1:4-5.
        1. Je, wanawezaje kupokea uwezo au karama za Roho Mtakatifu pasipo sauti, ghadhabu au moto?
        2. Je, sauti kali, ghadabu na moto vinapaswa kuwa ndio matamanio yetu?
  3. . Kisa cha Karama
    1. Soma Matendo 6:1-4. Je, ni vigezo gani wanavyovitafuta kwa wale watu saba? (Miongoni mwa mambo menngine, aliyejawa Roho Mtakatifu.)
    2. Soma Matendo 6:5-6. Utabaini kuwa Filipo ni sehemu ya kundi hilo. Fungu halisemi kuwa alikuwa “amejawa…. Roho Mtakatifu.” Kwa nini? Je, hiyo sio sehemu ya vigezo? Hii inapendekeza kuwa kuna viwango vya karama ya Roho Mtakatifu, na Filipo hayumo kwenye kiwango cha Stefano.)
    3. Soma Matendo 8:5-8. Hapa tunamwona Filipo tena. Je, amejawa Roho Mtakatifu?
    4. Soma Matendo 8:9-11. Filipo anatenda miujiza na Simoni anatenda miujiza. Kama ulikuwa unamchunguza Simoni, je, ungejuaje kama Roho Mtakatifu ndiye alikuwa chanzo cha uwezo wake?
      1. Soma 1 Petro 4:10. Je, hii inatufundisha nini kuhusu matumizi ya karama za kiroho? (Karama za kiroho ni kwa ajili ya kuwatumikia watu wengine. Kwa vile Simoni alikuwa anajitukuza yeye mwenyewe, hii ilikuwa dalili kuu kwamba hakuwa akitumia uwezo wa Roho Mtakatifu.)
    5. Soma Matendo 8:12-13. Je, nini kilichotokea kwa mchawi? (Alipokea imani (aliamini)! Akabatizwa.)
    6. Soma Matendo 8:14-17. Je, nini kinachokosekana kwenye huduma ya Filipo? (Roho Mtakatifu hakuwa amewashukia watu.)
      1. Je, unawezaje kulielezea hili? Filipo amejawa Roho Mtakatifu. Tuliona kuwa aliwekewa “mikono” naye akatenda miujiza mikubwa. Je, wale anaowabatiza wanawezaje wasiwe na karama ya Roho Mtakatifu?
        1. Soma Mathayo 28:19-20. Kwa hakika Filipo lazima alikuwa anabatiza kwa mujibu wa maelekezo ya Yesu kuhusu ubatizo. Je, maelekezo yale hayahakikishii ubatizo kwa jina la Roho Mtakatifu?
      2. Angalia tena Matendo 8:17. Je, ni Petro na Yohana pekee ndio wangeweza kuwawekea watu mikono ili kuwapelekea Roho Mtakatifu?
        1. Je, Filipo hakujumuishwa? Kama ndivyo, je, kwa nini mtu aliyejawa Roho Mtakatifu asijumuishwe?
        2. Kama Filipo hakujumuishwa, je, kwa nini hakuwawekea mikono wale aliowabatiza?
    7. Soma Matendo 8:18-19. Simoni anawaona waamini wengine waliopokea karama ya Roho Mtakatifu. Je, Simoni ana lengo kubwa, sawa? Anataka kushiriki Roho Mtakatifu na watu wengine.
    8. Soma Matendo 8:20-23. Njia mojawapo tunayoitumia kupima unyofu wa ibada kwa Mungu ni kwa jinsi tunavyotumia fedha zetu. Simoni anataka kuachana na fedha zake ili aweze kumpata Roho Mtakatifu. Je, kuna ubaya gani katika hilo? (Je, unaweza kumnunua Mungu? Roho Mtakatifu ni zawadi, kama wokovu. Hatuwezi kudai Roho Mtakatifu, au “kubadilishana” kitu chochote ili kumpata.)
      1. Kwa nini Petro anasema kuwa Simoni hajumuishwi kwenye hii karama? (Yeye ni mkali na mtumwa wa dhambi.)
        1. Je, tunaweza kutengwa kumpokea Roho Mtakatifu maishani mwetu kwa sababu kama hizi?
        2. Je, Simoni hana karama zozote za Roho?
    9. Hebu tupitie upya tena ili tuone jinsi ambavyo Roho Mtakatifu anatujia. Soma tena Matendo 8:15-17. Je, tunakipataje kile ambacho Simoni alikitaka kwa udi na uvumba? (Kwa mara nyigine tena tunaona kuwa maombi ni ufunguo. Hata hivyo, Petro na Yohana pia kwa namna fulani ni wa muhimu katika hili.)
    10. Ukiendelea kusoma zaidi katika hii sura, utaona kisa cha kushangaza jinsi ambavyo Roho Mtakatifu anamwongoza Filipo kwa Mweka Hazina wa Kikushi. Je, ni kwa jinsi gani Filipo anaweza kuongozwa namna ile na Roho Mtakatifu, lakini wale anaowabatiza hawajampokea Roho Mtakatifu? (Tulipotambulishwa pale awali kwa huyu Filipo, tulifahamishwa (kwa ulinganifu) kuwa ana karama ya Roho Mtakatifu kwa kiwango kidogo kuliko Stefano. Sasa, inaonekana kuwa anayo karama ndogo (au karama nyingine tofauti hivi) kuliko Petro na Yohana.)
  4. Nguvu Kamili ya Roho Mtakatifu Sasa?
    1. Soma Yoeli 2:28-29. Je, ni nani anayestahili kumpokea Roho Mtakatifu kwa uwezo? (Sisi sote.)
    2. Soma Matendo 2:14-17. Je, Petro anaielezeaje sauti, upepo na moto wa Roho Mtakatifu? (Anasema huu ni utimilifu wa Yoeli 2.)
      1. Wengine wanasema kuwa hivi leo hatuna uwezekano wa kumpata Roho Mtakatifu mwenye “nguvu kamili.” Je, hiyo ni kweli? (Kama Matendo 2 ndio “siku za mwisho,” tunaishi katika siku za mwisho!)
    3. Rafiki, vipi kuhusu wewe? Je, Roho Mtakatifu amekushukia? Je, amekushukia kwa nguvu? Kama sivyo, kwa nini usiombe hilo litokee?
  5. Juma lijalo: Uinjilisti na Ushuhudiaji Kama Mtindo wa Maisha.