Uinjilisti na Ushuhudiaji Kama Mtindo wa Maisha

(Yohana 17, Marko 5)
Swahili
Year: 
2012
Quarter: 
2
Lesson Number: 
4

Utangulizi: Mtu yeyote anayeitizama dunia kwa uaminifu kabisa na kuviangalia viwango vya Mungu anafahamu kuwa kuna pengo kubwa sana kati ya hivi vitu viwili. Ukiwa kama shuhuda, kama mwinjilisti, basi unasimama kati ya hizo pande mbili. Wewe ndio kiungo kati ya dunia na Ukristo. Kati ya dunia na uzima wa milele. Kuna angalao tatizo moja kubwa kuhusiana na mahali uliposimama. Yesu anatuambia katika Yohana 17:14 kwamba ulimwengu unatuchukia. Je, utakuwaje kiungo sahihi wakati unapokabiliana na chuki? Je, tunajihusishaje na chuki? Hebu tukimbilie kwenye somo letu la Biblia na tuone kile tunachoweza kujifunza!

  1. Mpango wa Yesu wa Pambano
    1. Soma Yohana 17:1-4. Yesu anatoa ombi zuri ajabu linaloelezea kile alichokwishakifanya duniani na mpango wake wa baadaye. Je, utume mkuu wa Yesu ni upi? (Kumpa Mungu utukufu.)
      1. Je, fungu hili linasema kuwa Yesu alimpa Mungu utukufu kwa namna gani? (Kwa kukamilisha kazi ambayo Mungu alimpatia ili aifanye.)
      2. Je, ni kazi gani hiyo? (Ni daraja. Kuwapeleka waliopo ulimwenguni kwenye uzima wa milele.)
      3. Je, mtu analivukaje hili daraja? (Uzima wa milele hupatikana kwa kumjua Yesu.)
      4. Kama sisi ni wanagenzi/wanafunzi wa Yesu, je, ni kiashiria gani tulichonacho kuhusiana na kazi yetu? (Tunahitajika kumpa Mungu utukufu kwa kuwasaidia watu kumjua Mungu. Kuwasaidia watu kuvuka hili daraja.)
    2. Soma Yohana 17:13-14. Je, Yesu alitusaidiaje kumjua Mungu? (Kwa kutupatia neno la Mungu.)
      1. Je, unadhani inamaanisha nini kwa kauli ya kwamba Yesu alitupatia neno la Mungu? (Yohana 1:1 inanijia akilini. Yesu ndiye mwenye uhalisia wa Mungu. Maisha na mafundisho ya Yesu vinatusaidia kumjua Mungu.)
      2. Je, mwitikio wa ulimwengu kwenye neno la Mungu ukoje? (Dunia inawachukia.)
      3. Je, unajisikiaje kuhusiana na wewe kuchukiwa? (Yesu anasema anataka kutupatia furaha!)
      4. Je, hii inafanyaje kazi? Wanachukia, wewe unacheka? (Ukielewa kuwa sababu ya chuki ni kwamba wewe uujue ukweli, basi hapo unaweza kujisikia vizuri maishani.)
    3. Katika Yohana 17:14 Yesu anazungumzia kuhusu maelekezo yake, neno lake. Je, tulijifunza nini juma lililopita kuhusiana na elimu yetu tunayoendelea nayo? (Soma Yohana 16:7-13. Katika kazi yetu kama kiungo kati ya wapagani na uzima wa milele, katika kazi yetu kama wanagenzi/wanafunzi wa yesu, hakutuachia kitabu cha kutupatia maelekezo. Alituachia Roho Mtakatifu. Kama vile ambavyo tunamwendea Yesu kwa ajili ya mashauri, vivyo hivyo tunapaswa kumwendea Roho Mtakatifu. Kumbuka kuwa ni Roho Mtakatifu aliyekifanyia kazi kitabu!)
    4. Soma Yohana 17:15-18. Kwa kuongezea na chuki, je, ni kitu gani kingine tunachotakiwa kupambana nacho? (Mwovu.)
      1. Je, “mwovu” ana nini mawazoni mwake kwa ajili yetu? (Chochote kiwacho kile, kilichopo mawazoni mwa Yesu ni kutuepusha na mwovu.)
      2. Je, mojawapo ya kinga zetu kuu ni ipi? (Yesu anaomba ili kwamba tutakaswe (kuwekwa wakfu) kwa maneno ya Mungu. Kwa mara nyingine tena, hii inajielekeza kwa Roho Mtakatifu kama kinga yetu kuu.)
    5. Hebu tusome mafungu matatu ya muhimu sana: Waefeso 6:12, Mathayo 9:36 na Luka 14:26.
      1. Neno lililotafsiriwa kama “chuki” katika Luka 14:26 ni neno hilo hilo alilolitumia Yesu kuelezea mtazamo wa ulimwengu dhidi yetu. Je, hiyo inaandaaje mtazamo wetu dhidi ya ulimwengu? (“Chuki” inaweza tu kuwa ni upendeleo wa kitu kingine.)
      2. Je, nini kinachobainisha tabia za watu wengi tunaokutana nao? (Wao ni kondoo wasio na msaada. Huenda tusiwavutie, lakini tunahitajika kuwahurumia.)
      3. Je, uwepo wa mwovu na wasaidizi wake unatusaidiaje kuwa na mtazamo sahihi juu ya ushuhudiaji na chuki ya kipagani? (Wakati ambapo kwa hakika kabisa wapo watu waovu, mapambano yetu kwa ujumla sio dhidi ya watu, bali dhidi ya mwovu. Hii inamaanisha kuwa chuki sio suala la binafsi kati yako na wapagani. Badala yake, ni suala binafsi kati ya Mungu na Shetani. Wewe ni sehemu tu ya taswira pana. Mara nyingi unakuwa unakabiliana na watu waliochanganyikiwa ambao wana vipaumbele vingine.)
    6. Soma Yohana 13:34-35. Tunapokuwa tunasimama kama kiungo kati ya ulimwengu wa kipagani na uzima wa milele, je, tunapaswa kuwa na mtazamo gani?
      1. Angalao katika hili fungu, amri ya upendo inaelekezwa kwa waumini wenzetu. Je, tunapaswa kuhusianaje na waumini wenzetu wanaoungana nasi kama walinzi kwenye daraja linaloelekea kwenye uzima wa milele? (Tutakabiliana na chuki kutoka ulimwenguni kwenye kazi yetu ya darajani, lakini tunapaswa kupata upendo (na kuwapenda) kutoka kwa wafanyakazi wenzetu.)
    7. Hebu tupitie upya tena. -Kama washuhudiaji na wainjilisti, tu walinzi katika daraja kati ya dunia na maisha ya milele. Jukumu letu ni kuleta utukufu kwa Bwana. Tunafanya hivi kwa kusaidia watu kumjua Mungu. Ingawa kazi yetu inafanyika katikati ya uwanja wa vita, mahali ambapo nguvu za giza upande wa pili unatuchukia, mkakati wetu ni kwa ajili ya watu ambao sio wapinzani haswa bali waliochanganyikiwa.
  2. Somo la Utume
    1. Soma Marko 5:1-5. Unafikiri ni kwa jinsi gani mtu huyu aliathiri bei ya bidhaa za mazingira hayo? (Kwa namna hasi. Je, ungependa kuishi mazingira ambayo mwendawazimu anaranda huru? Fikiria kumsikia akilia usiku. Luke 8:27 inaongeza kuwa mtu huyu alikuwa havai nguo.)
    2. Soma Marko 5:6-7. Je, unafikiri ni kwa namna gani mitume walimchukulia huyu mwendawazimu, aliyekuwa mtupu mwenye uwezo wa kukata minyororo vipande viwili, akiwa anawakimbilia? (Nahisi walikuwa wakikimbia uelekeo tofauti. Shingo zao hazikuwa imara kama minyororo. Kwa kuongezea, je, ni kwa kiasi gani wangeweza kustahili? Katika sura iliyotangulia (Marko 4) walinusurika kuzama. Habari hii ya huduma ilipelekea maisha yaliyojawa na matukio!)
      1. Umewahi kuona bandiko la gari lililoandikwa “chuki sio adili la kifamilia?” Je, ni kitu ganihaswa kinachomaanishwa? (Hili ni zao la ushawishi wa wanaharakati wa ushoga. Pendekezo ni kwamba kama unaamini ushoga sio sahihi, wewe ni mtu mwenye ni chuki.)
      2. Tuhuma gani za uongo ambazo mwendawazimu yule alimrushia Yesu? (Kwamba Yesu alikuwa mtesi. Yesu alikuwa katili.)
    3. Soma Marko 5:8. Kwa nini mwendawazimu alisema hivi? (Ilikuwa ni pepo ndani yake. Yesu alimwambia pepo kutoka. Yesu alitofautisha mdhambi na dhambi. Ingawaje, pepo mchafu aliona kama ni kitu kimoja na kwa uongo akamwita Yesu kuwa ni mtu mwenye chuki sana kiasi cha kutesa mtu. Usishangae ukiitwa majina na pepo wachafu.)
    4. Soma Marko 5:9-13. Je, mapepo yana fikra gani juu ya maisha yako? (Yanataka kukuzamisha.)
      1. Je, wanaweza? (Sio bila ruhusa.)
    5. Soma Marko 5:14-17. Watu wa mji walimwambia nini Yesu, wale ambao mali zao ndio punde zimepanda thamani? (Ondoka!)
      1. Kwa nini? (Kwa sababu thamani ya nguruwe wao imeporomoka.)
        1. Hii huonyesha nini kuwahusu na juu ya huduma yako? (Ya kwamba watu wanathamini vitu vyao kuliko wokovu wa wengine.)
      2. Utabaini kuwa mafungu haya yanasema watu walikuwa wanaogopa. Kwa nini? Yesu ameondoa tishio moja lilikokuwa bayana kabisa! (Fikira tukio la asili lisilo la kawaida ambalo limetokea hivi karibuni. Hii ilikuwa ni vita kubwa kati ya Mungu na nguvu za giza. Katika hali ya uhalisia watu waliogopa.)
  3. . Uinjilisti Ng’ang’anizi - Barua
    1. Soma 2 Wakorintho 3:2 na Marko 5:18-19. Aliyekuwa mwendawazimu ni nani sasa? (Yeye ni “barua” kutoka kwa Mungu.)
      1. Je, yule mtu mwendawazimu hakuwa mwenye upungufu wa mafunzo ya teolojia? Je, asingeweza kutumia mizunguko michache ndani ya chombo na Yesu kabla ya kutumwa kwenye utume huu? (Alikuwa shahidi. Alikuwa akisimulia habari yake mwenyewe. Hakuhitaji mafunzo ya kiinjilisti kwa hili, kwa kuwa alifahamu habari yake vizuri kuliko mtu mwingine yeyote. Unafahamu habari yako kuliko mtu mwingine yeyote.)
    2. Soma Marko 5:20. Je, mtu huyu alikuwa shuhuda thabiti? (Watu walishangaa.)
    3. Soma 2 Wakorintho 3:3. Ni mara nyingi kiasi gani barua yetu “hutumwa?” (Mfululizo. Wajibu wetu ni kudumu kusimama kama walinzi katika daraja lililo kiungo kati ya ulimwengu wa kipagani na uzima wa milele. Chochote tukifanyacho kinapaswa “kinga'anganize” uzima wa milele.)
      1. Je, ni nani anayekupa maelekezo ya kila siku ya namna gani ung'ang'anize? Je, ni nani aliye wa msingi kwenye ujumbe wa barua ya maisha yako? (“Roho wa Bwana aliye Hai.” Hatuwezi kuhudumu kwa dhati bila Roho Mtakatifu kuandika barua ya maisha yetu.)
    4. Rafiki, utajitoa katika kila kitu kuwa mlinzi wa daraja, kuwa barua, iunganishayo na yenye kuarifu ulimwengu wa kipagani juu ya uzima wa milele. Ni kwa utukufu wa Mungu!
  4. Juma lijalo: Kuufuatilia Uinjilisti na Ushuhudiaji.