Somo la 13: Taswira za Mwisho (Tamathali za Semi za Ule Mwisho

Yona 3, Ufunuo 14, Danieli 5
Swahili
Year: 
2025
Quarter: 
2
Lesson Number: 
13

Somo la 13: Taswira za Mwisho (Tamathali za Semi za Ule Mwisho

 

(Yona 3, Ufunuo 14, Danieli 5)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2025, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Watu wengi wanaamini kuwa “Ujumbe wa Malaika Watatu” wa Ufunuo 14:6-13 ni ujumbe wa mwisho kabla ya ujio wa Yesu Mara ya Pili. Ufunuo inataarifu kuwa malaika walipeleka ujumbe wakati wakiwa wanaruka angani. Hilo linatendekaje? Je, ni sawa na ndege ndogo inayokwenda kwa mwendo wa pole ambayo ina bango lenye ujumbe? Mara zote nimekuwa nikiamini kuwa “malaika” ni sisi – wale wanaopeleka habari njema juu ya ujio wa Yesu Mara ya Pili. Lakini je, hilo ni sahihi? Ikiwa malaika si wanadamu halisi, bali wanadamu, je, kuna aina kadhaa za wanadamu wanaohusika katika kazi? Na kwa nini hatuwajumuishi malaika halisi? Visa vya Agano la Kale vinatufundisha nini kuhusu jinsi Mungu anavyotekeleza kazi yake ya kutoa maonyo hapa duniani? Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tujifunze zaidi!

  1.    Malaika ni Wanadamu?
    1.    Soma Wagalatia 4:12-14. Paulo anakumbuka jinsi Wagalatia walivyomjibu mara ya kwanza. Je, walimchukulia kuwa ni malaika? Je, walimchukulia kuwa ni Yesu? (Paulo hajiiti Yesu wala malaika, bali analinganisha ujumbe wake wa injili na kazi ya malaika.)
    1.    Soma Ufunuo 14:6. Ukipitia kamusi ya Strong kuangalia msamiati wa “angel” anasema kuwa kwa lugha ya Kiyunani unamaanisha “mjumbe” na linaashiria “mchungaji.” Maoni ya B. W. Johnson yanatetea kwamba “wakala yeyote anayetenda kazi ya Mungu au kupeleka ujumbe wake anaweza kuwa malaika.” Una maoni gani? (Kwa hakika sitatupilia mbali maana halisi ya malaika wa Ufunuo 14, ikizingatiwa kwamba hata rejea nyingine za malaika katika kitabu cha Ufunuo zinaonekana kuwarejelea malaika halisi. Wakati huo huo, kitabu cha Ufunuo kimejawa ishara.)
      1.    Je, kuna umuhimu wowote wa malaika “akiruka katikati ya mbingu?” Je, hiyo inaweza kuwa rejea ya kutumia mawasiliano ya satilaiti? Intaneti?
      1.    Baadhi ya watu wanaashiria kuwa kuruka “katikati ya mbingu” na kunena kwa “sauti kuu” (Ufunuo 14:7) kunarejelea udharura wa ujumbe. Ikiwa hilo ni kweli, kwa nini ujumbe unaitwa “injili ya milele?”
  1.   Malaika Wasio Wakamilifu?
    1.    Soma Yona 3:1-3. Je, unakumbuka mtazamo wa Yona ulikuwaje kuhusu kwenda Ninawi ili kuuonya juu ya uangamivu? (Hatutaingia kwenye historia iliyomo katika kitabu cha Yona 1, lakini Yona alikuwa anajaribu, kwa kutumia kila njia, kuepuka kuwapelekea ujumbe watu wa Ninawi.)
    1.    Soma Yona 3:4-5. Je, hayo ni mafanikio makubwa isivyo kifani? Mgeni huyu anajitokeza, anawaambia watubu, na mji ambao ni mkubwa sana kiasi cha kuhitajika siku tatu kuutembea wanatubu. Je, hayo ni matokeo ya Yona, au unadhani Roho Mtakatifu alikuwa akitenda kazi na Yona?
      1.    Una maoni gani juu ya kauli kwamba Yona alitembea kwa siku moja tu katika mji uliohitaji siku tatu kuutembea wote? (Huenda alisimama katikati ya mji. Huenda bado anasitasita.)
    1.    Soma Yona 3:10. Mungu ana mwitiko gani kwenye kazi ya mafanikio ya Yona? (Anaamua kutouangamiza mji.)
    1.    Soma Yona 4:1-3 na Yona 4:5. Kwa nini Yona anasubiri kuona “mji ule utakuwaje” Mungu alipoamua kutouangamiza? (Anatumaini kwamba Mungu alishawishika na ombi lake la kuuangamiza mji na kuithibitisha hadhi yake.)
    1.    Soma Yona 4:10-11. Yona ni mtu wa namna gani? Yeye ni shuhuda wa Mungu wa namna gani? (Ni mtu wa ajabu (terrible). Anataka kuona vifo vya watu wengi.)
      1.    Hebu tulijadili hili. Je, Yona anafanana na malaika? Je, yeye ni mjumbe wa Mungu (Ndiyo.)
        1.    Kwa nini Mungu alimchagua?
      1.    Hii inatufundisha nini kuhusu kupeleka ujumbe wa malaika watatu wa Ufunuo? (Una sifa zinazostahili!)
  1.      Mjumbe Asiye na Mikono
    1.    Soma Danieli 5:1-2. Kwa nini mfalme anatumia vikombe vya kunywea kutoka katika hekalu la Yerusalemu? (Inawezekana anajaribu kuonesha ubora (superiority) wake kwa Mungu wa kweli.)
    1.    Soma Danieli 5:4-6. Kuitumaini miungu ya dhahabu na shaba kunamwendeaje Belshaza? (Anaogopa, anafadhaika, hawezi kusimama, na magoti yake yanagongana. Kinyume na hapo, mambo yako vizuri.)
    1.    Soma Danieli 5:10-11. Je, Danieli amepoteza mvuto katika nyumba ya mfalme? (Ndiyo. Malkia anamkumbuka Danieli tangu siku za Mfalme Nebukadreza. “Baba” ni neno la jumla, kuna uwezekano mkubwa kwamba Nebukadreza alikuwa babu wake Belshaza kwa mujibu wa maoni ya watu wengi ambao nimewasoma.)
    1.    Danieli anaitwa ili kusoma maandishi yaliyoandikwa kwa vidole vya mkono ukutani. Soma Danieli 5:23-28. Mustakabali wa mfalme unaonekanaje? Kwa nini umepinda kona mbaya na kugeuka kiasi hicho?
    1.    Soma Danieli 5:30-31. Ujumbe huu wa hukumu unaletwa kwa vidole! Je, inawezekana hawa ni malaika watatu wa Ufunuo 14? Je, hii ni ishara kwamba tangazo la Ujumbe wa Malaika Watatu pia utakuwa wa kimwujiza (supernatural)?
    1.    Linganisha Danieli 5:29 na Danieli 6:1-3. Danieli anahamaje kutoka kuwa afisa wa ngazi ya juu katika ufalme ulioshindwa hadi kuwa afisa wa ngazi ya juu katika ufalme mpya? (Kwa sababu “roho bora ilikuwa ndani yake.”)
      1.    Kama umejawa Roho Mtakatifu, je, unaweza kutoka katika giza (obscurity) na kuwa wa kwanza kwenye nafasi ya uongozi serikalini? Yatafakari maisha ya Danieli. Alichukuliwa kama mtumwa alipokuwa kijana mdogo, licha ya hayo alifikia kilele cha hadhi ya juu katika falme za Babeli na Umedi na Uajemi.)
        1.    Danieli alikuwa na umri gani alipopandishwa cheo katika kitabu chake cha Danieli 6? (Anaaminika kuwa na umri wa zaidi ya miaka themanini. Huenda hata 90.)
  1.   Wajumbe wa Kipagani
    1.    Hebu tuangalie historia ya matukio tuliyojifunza hivi punde. Soma 2 Mambo ya Nyakati 36:18-21. Je, hii inafafanua jinsi vikombe vya hekaluni na Danieli walivyokuja Babeli? (Ndiyo. Haya ni maelezo ya kihistoria.)
    1.    Soma Yeremia 51:57-58 na Isaya 45:2. Je, anguko la Belshaza ni sehemu ya unabii? (Ndiyo! Zingatia ufafanuzi wa kina.)
    1.    Soma Isaya 44:28. Kitu gani kinatabiriwa kuhusu Koreshi? (Kwamba atajenga upya hekalu katika Yerusalemu.)
    1.    Katika Daniel 5:31 tunaambiwa kuwa “Dario, Mmedi” alimshinda Belshaza. Soma Danieli 6:28. Je, Dario na Koreshi ni mtu mmoja? (Baadhi ya watu wanadhani kuwa wawili hao ni mtu mmoja, ingawa kifungu hiki kinaashiria kuwa ni watu wawili tofauti. Cha msingi kwa ajili ya mjadala wetu ni kwamba mtawala wa ufalme mpya – Wamedi na Waajemi – anampendelea Danieli na kwamba anaamrisha ujenzi upya wa hekalu la Yerusalemu lililoangamizwa na Wababeli.)
    1.    Soma 2 Mambo ya Nyakati 36:22-23. Hapa mjumbe wa Mungu ni nani? Nani anayeamrisha ujenzi upya wa nyumba ya Mungu duniani? (Mfalme huyu wa kipagani! Inawezekana pia kwamba alishawishiwa na Danieli.)
      1.    Hetu tusome hili huko nyuma katika uelewa wetu wa Ufunuo 14. Je, inaleta mantiki kuamini kwamba ujumbe wa kimalaika unapelekwa na afisa wa serikali? Au kwamba afisa wa serikali anasaidia katika kusambaza ujumbe?
        1.    Je, kuna kanuni ya jumla ya kujifunza kutokana na kile tulichojifunza kuhusu Mungu kuwatumia watu gani kama wajumbe wake? (Angalia tena 2 Kumbukumbu la Torati 36:23. Kwa umahsusi mfalme Koreshi anamhusisha Mungu katika “amri” ya “kumjengea [Mungu] nyumba Yerusalemu.” Kanuni ni kwamba Roho wa Mungu anatumia kila njia kutangaza ujumbe wake.)
      1.    Kisa cha Mungu kumhamasisha Mfalme Koreshi kujenga upya hekalu la Mungu Yerusalemu kinasema nini kuhusu suala la fedha zinazotokana na kodi kutangaza dini?
    1.    Rafiki, Mungu anaweza kutumia njia nyingi za kupeleka ujumbe. Njia mojawapo ni kukutumia wewe! Kwa nini usimwombe Roho Mtakatifu, sasa hivi, akujaze ili uweze kuitangaza injili ya Mungu?
  1.    Juma lijalo tunaanza somo jipya juu ya kitabu cha Kutoka.