Somo la 8: Ukuu wa Kristo Katika Yote
Somo la 8: Ukuu wa Kristo Katika Yote
(Wakolosai 1:13-19)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2025, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani.
Utangulizi: Vaa “kofia yako ya kumbukumbu” ili ukumbuke masomo yetu mawili ya awali katika mfululizo wa masomo haya. Tulijifunza utangulizi wa vitabu vyote viwili vya Wafilipi na Wakolosai. Utakumbuka kwamba Paulo alianza barua yake kwa Wafilipi kwa kusema kwa unyenyekevu kuwa alikuwa mtumwa. Alionekana tofauti kabisa kwa Wakolosai kwa kujielezea kama mtume. Tukaamua kwamba, tofauti na barua yake kwa Wafilipi, Paulo alitaka kujionesha kwa Wakolosai kama mtu mwenye mamlaka. Kwa nini? Alikuwa na maelekezo madhubuti kwa ajili yao kuhusu nuru na giza. Maelekezo haya yanahusiana na asili ya Yesu. Hebu tuendelee na somo letu la Wakolosai ili tujifunze zaidi kuhusu habari za Yesu!
- Yesu Mzaliwa wa Kwanza
-
- Soma Wakolosai 1:13-14. Paulo anaandika kuhusu Baba wetu Mungu na anabainisha kuwa Baba alituokoa kutoka gizani na kutuhamisha katika Ufalme wa Yesu. Je, hilo linaonekana jambo la ajabu kwako? Je, haikuwa Yesu ambaye alituokoa kutoka gizani na kuturuhusu kuingia mbinguni? (Zilikuwa juhudi za “kundi.” Utatu wote ulihusika kwenye wokovu wetu.)
-
-
- Tafakari kipindi alichokilenga Paulo. Anaandika kana kwamba kuhamishwa kwetu kwenda katika Ufalme wa Yesu tayari kumeshatokea? Je, hiyo ingebadili namna ambavyo ungeishi kama ungedhani kuwa kwa sasa wewe ni raia wa Ufalme wa Yesu?
-
-
- Soma Wakolosai 1:15. Je, Yesu ni mwanadamu aliyeumbwa? Je, anafanana zaidi na malaika kuliko kufanana na Mungu?
-
-
- Paulo anapoandika kuwa Yesu ni “mfano” wa Mungu ambao hauonekani kama yeye ni Mungu, inaonekana kama anafanana zaidi na mmoja wetu. Soma Mwanzo 1:26-27. Tafakari maswali mawili:
-
-
-
-
- Ikiwa Yesu aliumbwa na si Mungu, nani ambaye ni “wetu” katika Mwanzo 1:26.
-
-
-
-
-
- Je, kweli Yesu alifanywa kwa mfano wa wanadamu?
-
-
-
- Soma Yohana 1:1-3 na Yohana 1:14. Neno ni nani? (Hii inabainisha kuwa “Neno” ni Yesu.)
-
-
- Neno amefanya nini? (Neno ni Mungu Muumbaji ambaye alikuwapo na Mungu Baba hapo mwanzo. Na pia ni Mungu “aliyefanyika mwili” ikimaanisha kuwa alizaliwa kama mwanadamu. Wanadamu wameumbwa kwa “mfano” wa Mungu. Yohana 1 inatatua fumbo la kwa nini Paulo anaandika kuwa Yesu “alizaliwa” na yu mfano wa Mungu.)
-
-
-
- Ikiwa tuko sahihi kwenye jibu la awali, una maoni gani kwamba Yesu alikuwa “mzaliwa wa kwanza?” Mariamu, mamaye, alipomzaa Yesu hakuwa mzaliwa wa kwanza, je, hakuwa mzaliwa wa kwanza wa vyote vilivyoumbwa?
-
-
- Soma Zaburi 89:27 na Ufunuo 1:5. Vifungu hivi vinashughulikaje na dhana ya “mzaliwa wa kwanza?” (Hii inatupatia mitizamo miwili tofauti. Kwanza, Ufunuo inahusisha lugha ya “mzaliwa wa kwanza” na ufufuo wa Yesu. Yeye ni mzaliwa wa kwanza wa wafu. Pili, zaburi inatumia neno “mzaliwa wa kwanza” kuashiria umuhimu. Hakuna chochote kati ya haya kinachotufundisha kwamba kiuasilia Yesu alikuwa mwanadamu aliyeumbwa kama malaika au sisi.)
-
-
- Yuda 9 na Mathayo 17:1-3 zinatufunulia kwamba Musa alifufuliwa kutoka katika wafu na hii ilikuwa kabla ya ufufuo wa Yesu. Tunaielezeaje kauli ya ”mzaliwa wa kwanza” wa Ufufuo? (Ninaamini kuwa kigezo cha ufufuo wa Musa kilijengwa juu ya ufufuo wa Yesu. Yesu alikuwa mzaliwa wa kwanza wa kweli wa wafu.)
-
- Yesu Muumbaji
-
- Soma Wakolosai 1:16-17. Hii inaendanaje na hoja kwamba Yesu alikuwa mwanadamu aliyeumbwa kama ilivyo kwa malaika? (Haiendani kabisa. Kinyume chake, inatuambia kuwa Yesu si tu kwamba aliumba ulimwengu (inayoendana na Yohana 1), bali yeye pia ni Muumbaji wa kila kiumbe aliyeumbwa aliyepo mbinguni.)
-
-
- Kuna maneno ambayo tunatakiwa kuyachunguza zaidi. Tunaambiwa kuwa “vitu vyote” viliumbwa “kwa ajili yake,” ikimaanisha “kwa ajili ya Yesu.” Hii inatoa umaizi (insight) gani kwenye sababu ya Yesu kujitoa ili kutupatia uzima wa milele? (Hakutaka zawadi aliyoitoa mwenyewe kwa njia ya uumbaji wetu iharibiwe. Waebrania 12:2 inatuambia kuwa ilikuwa ni kwa ajili ya “furaha” kwamba Yesu alijitoa. Furaha hiyo inahusu kutupatia zawadi ya kuja tena kwenye uhusiano sahihi na Yesu.)
-
-
-
- Hii inafunua nini kuhusu hamasa ya Shetani ya kuwaingiza Adamu na Eva dhambini? (Kwa sehemu fulani hizi zilikuwa juhudi za kumdhuru Yesu. Shetani alikuwa anamwonea wivu Yesu. Alitaka kuharibu zawadi ya uumbaji.)
-
-
-
- Maneno mengine ambayo tunatakiwa kuyachunguza ni kwamba “vitu vyote hushikamana” katika Yesu. Unadhani mambo gani yanashikamana katika Yesu? (Wokovu wetu, na hatimaye kuangamizwa kwa uovu, “vinashikamana” katika kazi ya Yesu. Mtu anayeelewa fizikia ya hali yabisi na kimiminika (condensed-matter physics) anafahamu kuwa atomu zinajongea, lakini zimeungana, hivyo vitu vinaonekana machoni mwetu kuwa thabiti. Mtu anayeelewa astrofizikia (astrophysics) anaelewa kuwa ulimwengu wetu ungeparanganyika kama isingekuwepo nguvu inayodhibiti utanukaji wake. Yote haya yanatokana na uwezo wa Yesu.)
-
-
- Soma Wakolosai 1:18. Kwa mara nyingine tunaweza kuona maneno “mzaliwa wa kwanza katika wafu,” inayounga mkono dhana ya kwamba Yesu hakuwa mwanadamu aliyeumbwa na Mungu. Tunamfanyaje Yesu kuwa “mkuu katika yote” maishani mwetu?
- Yesu na Mgogoro
-
- Soma Wakolosai 1:19. Paulo anapoandika kuwa “utimilifu wa Mungu” unakaa kwa Yesu, hiyo inakufundisha nini kuhusu mgogoro wa dhahiri kati ya Agano la Kale na Agano Jipya? Ninawafahamu Wakristo ambao wanajikita kwenye Agano Jipya pekee kwa sababu Agano la Kale halionekani kuwa la muhimu na kwa baadhi ya maeneo lina makosa. (Kila tunachotaka kukijua kumhusu Mungu Baba, tunaweza kukipata kwa Yesu.)
-
-
- Kwa kuwa tunajua kwamba Yesu alikuwa Muumbaji aliyerejelewa katika kitabu cha Mwanzo, kinachoonekana ni kwamba mwingiliano kati ya Mungu na wanadamu katika Agano la Kale ulikuwa pamoja na Yesu. Je, lazima tumwone Yesu katika kile kilichotokea katika Agano la Kale? (Sidhani kama tunaweza kulitenga Agano la Kale tunapojaribu kumwelewa Mungu. Sidhani kama tunaweza kuhitimisha kuwa tunachojifunza kuhusu habari za Yesu alipotembea duniani kinatupatia uelewa kamili wa Yesu. Tunahitaji taswira pana ya Mungu.)
-
-
- Soma Wakolosai 1:20. Je, tuko vitani na Mungu bila kile ambacho Yesu alitufanyia? (Yesu anatumia maneno ya utatuzi wa mgogoro, “kuvipatanisha,” na “kufanya amani.” Bila Yesu tungekuwa vitani na Mungu.)
-
-
- Je, wale wasiomkubali Yesu wako vitani na Mungu?
-
-
-
- Ninaamini ninaona ongezeko la ushetani siku hizi. Tunakiri kuongezeka kwa ugonjwa wa afya ya akili. Sijawahi kusikia ufafanuzi wa kuridhisha wa jinsi mambo yalivyofafanuliwa kama kupagawa pepo katika Agano Jipya katika zama za leo ni magonjwa ya afya ya akili tu. Je, unadhani tumehama kutoka kwenye kupagawa pepo na kuingia kwenye ugonjwa wa akili? Ikiwa ndivyo, hilo limetokeaje? (Sikubaliani na jibu kwamba siku hizi tumestaarabika na kuwa wa kisasa zaidi. Matatizo mengine ya wanadamu ambayo Yesu aliyaponya yalisemwa kuwa ni ugonjwa. Watu walioishi wakati wa Yesu waliainisha baadhi ya maradhi kama magonjwa na mengine kama kupagawa pepo.)
-
-
-
- Ni kwa nini katika Dunia ya Magharibi pekee, nje ya sinema, tunaonekana kudhani kuwa kupagawa pepo hakupo tena?
-
-
- Hebu tuangalie tena asili ya upatanisho ambao Yesu aliushinda kwa ajili yetu. Paulo anasema Yesu alifanya hivi “kwa damu ya msalaba wake.” Unadhani kwa nini ilimpasa Yesu kufa kifo cha vurugu, chenye mateso makali?
-
-
- Kama umejibu, “Kwa sababu Shetani alitaka kumdhuru Yesu na kumfanya akate tamaa,” je, huo ndio ufafanuzi kamili?
-
-
-
- Je, kifo cha Yesu cha vurugu na mateso makali kwa namna fulani kinahusiana na vurugu katika Agano la Kale? (Silielewi hili, lakini ninaona uhusiano kati ya namna mapenzi ya Mungu yalivyotimizwa kwa vurugu katika Agano la Kale na vurugu iliyohusika kwa Yesu kupokea adhabu kwa ajili ya dhambi zetu.)
-
-
-
-
- Unapolitafakari hili, utalinganishaje kwenye jibu lako kwamba Mungu alimuahidi Yoshua (kiongozi wa kijeshi katika kuishinda Kaanani), kwamba Mungu atatanguliza mavu mbele ya Yoshua ili kuwaondoa wapagani? Angalia Yoshua 24:12, Kutoka 23:28, na Kumbukumbu la Torati 7:20. (Yesu mwenye upendo tunayemwona katika Agano Jipya anaakisi namna ambavyo Mungu anapendea kushughulika na wanadamu. Isivyo bahati, katika Agano la Kale, na katika siku zijazo, Mungu atatumia vurugu kukomesha uovu.)
-
-
-
- Rafiki, Je, utamchagua Yesu na si giza? Yeye ni Muumbaji na Mkombozi wetu na anastahili utii wetu. Kwa nini usifanye uchaguzi huo sasa hivi?
- Juma lijalo: Upatanisho na Tumaini.
