Somo la 6: Mashujaa wa Maombi
Somo la 6: Mashujaa wa Maombi
(Mathayo 6, Danieli 6, Luka 11, Zaburi 139)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2026, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani.
Utangulizi: Ikiwa maombi yanapaswa kuwa mazungumzo baina ya mtu na Mungu, basi lazima Mungu atadhani kuwa kweli mimi ni mzungumzaji wa hovyo (mbaya). Nina tabia ya kurudiarudia bila kujali maneno kama, “Tafadhali, Bwana, nisaidie.” Au, “Asante, Bwana.” Sehemu ya tatizo langu ni kwamba Yesu alisema, “Basi ninyi salini hivi” na akatupatia Sala ya Bwana. Angalia Mathayo 6:9-13. Kama Yesu anatupatia mfano wa sala, je, hiyo inamaanisha maombi yanapaswa kufuata mpangilio fulani? Ikiwa ndivyo, tunayafanyaje maombi yasiwe ya kujirudiarudia bila kujali? Tunaepukaje mazungumzo yasiyovutia na Mungu? Mungu anataka nini tunapomwomba? Je, anatafuta kuwa na mazungumzo ya kuvutia? Au je, anatafuta jambo jingine? Somo la juma hili na juma lijalo linahusu maombi. Juma lijalo tutajikita kwenye Sala ya Bwana. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tuanze safari yetu ya kutafuta kile tunachoweza kujifunza kuhusu maombi!
- Mshirika Wetu wa Maombi
-
- Soma Mathayo 6:5-6. Kuna uwezekano mkubwa wa kutokea tatizo gani kwa maombi ya hadharani? (Mtu anayeomba hazungumzi na Mungu, bali anazungumza na wale wanaosikiliza.)
-
-
- Ni nini thawabu kwa wale wanaokusudia kuwafurahisha wengine kwa maombi yao? (Thawabu yao ni kwamba tu wanawafurahisha watu wengine. Mungu hatoi thawabu kwa maombi ya namna hiyo.)
-
-
-
- Mshirika wa maombi wa mtu huyu ni nani? (Sio Mungu. Ni wasikilizaji.)
-
-
-
- Mara ngapi unajikuta unaomba hadharani?
-
-
-
-
- Je, kwa ujumla hili ni wazo lako, au umeombwa kusali? (Mfano alioutoa Yesu ni wa wale wanaojitolea kusali hadharani.)
-
-
-
-
- Unadhani kwa nini Yesu anatuambia kumwomba kwa siri? (Mungu anataka maombi yetu yaelekezwe kwake, si kwa watu wengine. Yeye ni mshirika wetu wa maombi.)
-
-
-
-
- Je, unadhani kuwa Yesu anatuambia kuwa na mahali maalumu pa kufanyia maombi? (Baadhi ya wanamaoni wanadhani hivyo, lakini mimi sidhani hivyo kwa sababu Yesu anasema “ingia katika chumba chako cha ndani,” ikimaanisha mahali pa faragha kinyume na sehemu maalumu.)
-
-
-
-
-
- Ni nini faida ya kumwomba Mungu kwa umahsusi? (Kama Mshirika wetu wa maombi, Mungu “atatuona” na kutujazi.)
-
-
-
- Soma Mathayo 6:7-8. Kundi lipi lina mfano mbaya wa maombi? (Wapagani. Yesu amehama kutoka kuwakosoa wanafiki wa kidini na kwenda kukosoa maombi ya kipagani.)
-
-
- Ni nini tatizo mahsusi la maombi ya kipagani? (Wanadhani kuwa uwingi ni wa muhimu. Wanatumia maneno mengi na maneno hayo hayana cha ziada kwa kile kinachosemwa.)
-
-
- Angalia tena Mathayo 6:8. Kwa nini Mungu hahitaji au hataki maneno mengi matupu? (Mungu anajua tunachohitaji kabla hatujakiomba.)
-
-
- Whoa! Je, Yesu anasema kuwa hatuhitaji kufafanua mahitaji yetu kwake tunaposali? Tayari anayajua mahitaji yetu? (Hicho ndicho hasa anachokisema Yesu.)
-
-
-
- Hebu tuchimbue hili kwa kina zaidi. Kama unazungumza na rafiki, na tayari rafiki anafahamu taarifa zote za awali, hiyo inakuruhusu ufanye nini? (Kwanza, kutopoteza muda. Pili, inaruhusu mazungumzo yaende moja kwa moja kwenye kiini cha tatizo.)
-
- Kile ambacho Mshirika Wetu wa Maombi Asicho
-
- Soma Luka 11:5-7. Je, rafiki huyu amepata mkate aliouomba? (Ndiyo. Rafiki hatoi madai yaliyo kinyume na hili.)
-
-
- Yesu anauliza swali katika vifungu hivi. Unadhani jibu linalotarajiwa ni lipi? (Rafiki ataamka na kumkopesha mkate. Rafiki wako atafanya hivyo, si ndio?)
-
-
- Soma Luka 11:8. Tafsiri ya ESV inaiitaje sababu ambayo hatimaye rafiki anatoa msaada? (“Ufidhuli (Impudence.)” Tafsiri nyingine zinatumia dhana kama vile king’ang’anizi au uthubutu wa haya (soni). Kinachomaanishwa ni kwamba hata rafiki wa kibinaadamu mwenye kusitasita hatimaye anaweza kujibu.)
-
-
- Je, Yesu anasema kuwa Mungu anasitasita na lazima achoke? (Hapana. Rafiki anayesita anatofautishwa na Mungu. Hata rafiki kama huyo anajibu, ni zaidi kiasi gani basi tunapaswa kumtumaini Mungu katika kutusikiliza.)
-
-
- Soma Luka 11:9-10. Nani anayejibu maombi hapa? (Soma Luka 11:1. Kisa hiki kinafuatia Yesu kutoa sehemu moja ya Sala ya Bwana. Mtu anayeombwa ni Mungu.)
-
-
- Yesu anamaanisha nini? Je, ni kwamba tunapaswa kumchagiza Mungu? (Hapana. “Rafiki” huyu anatofautishwa na Mungu. Mungu hahitaji kuchagizwa.)
-
-
-
- Dhana ya kwamba tayari Mungu anajua mahitaji yetu inaendanaje hapa?
-
-
- Soma 1 Wathesalonike 5:16-18. Je, maneno “ombeni bila kukoma” yanaashiria kumchagiza Mungu? (Maneno hayo hayasemi tunapaswa kuomba bila kukoma kuhusiana na mada hiyo hiyo. Yanamaanisha tunapaswa kuwa na mtazamo wa kumtegemea Mungu kila mara.)
- Maombi ya Danieli
-
- Soma Danieli 6:5-7. Je, hii ni njama ya kumwangamiza Danieli kutokana na imani zake za kidini?
-
- Soma Danieli 6:10-11. Je, Danieli anakataa kutia matatani (compromise) imani zake za kidini?
-
- Hebu turejee kwenye Mathayo 6:6. Yesu alikuwa bado hajanena maneno haya wakati Danieli alipokabiliana na changamoto yake. Je, Danieli anatenda jambo lisilo sahihi? Je, inakubalika kuacha madirisha yako wazi kama utafunga mlango?
-
-
- Tulikubaliana kwamba dhambi kuu katika Mathayo 6:5 ni ipi? (Majivuno.)
-
-
-
-
- Je, dhambi hiyo inahusika katika mazingira ya Danieli? (Hapana. Kuonwa na watu ilikuwa tatizo kwa Danieli. Danieli alikuwa anakataa kuacha kuomba kwa sababu watu walikataza.)
-
-
-
- Somo letu lina kichwa cha habari, “Mashuja wa Maombi. Tunapata fundisho gani la shujaa wa maombi kutoka kwenye maneno ya Yesu katika Mathayo 6 na matendo ya Danieli katika Danieli 6? (Jambo linalofanana katika vitabu vyote viwili vya Mathayo 6 na Danieli 6 ni kwamba tunapozungumza na Mungu katika maombi, hatupaswi kudhibitiwa na kile kinachofikiriwa na watu wengine. Hatupaswi kujaribu kuwafurahisha, na hatupaswi kuwaogopa tunamwomba Mungu!)
-
- Hebu tuangalie kipengele kingine cha Danieli 6:10. Hii inabainisha kuwa Danieli alipiga magoti na kuomba mara tatu kwa siku. Je, hii inaonekana kuendana na dhana ya maombi kuwa mazungumzo na Mungu? (Je, unatenga muda kumpigia mtu simu? Kama mtu fulani ni wa muhimu, au mtu fulani anadhani wewe ni wa muhimu, ni jambo la kawaida kuweka miadi.)
-
-
- Utaona kwamba maombi ya Danieli yalihusisha kutoa shukurani mbele za Mungu. Jiweke kwenye nafasi ya Danieli. Kwa kutambua kile alichokifanya, je, mada ya maombi yako itakuwa ni kumshukuru Mungu au kuomba (angalia Danieli 6:7) kwamba usije kuwa chakula cha simba?
-
-
- Soma Mathayo 6:8. Je, unadhani kwamba inawezekana Danieli hakubainisha suala la hatari ya kifo kwa sababu tayari Mungu alijua kile alichokihitaji?
-
- Soma Danieli 2:17-18. Hii inatufundisha nini kuhusu dhana ya kwamba tayari Mungu anajua kile tunachohitaji? (Danieli na marafiki wake kwa umahsusi wanapeleka mgogoro (hatari inayowakabili) mbele ya Mungu. Hii inaonesha kuwa kauli ya Yesu kwamba tayari Mungu anajua mahitaji yetu imedhamiriwa kutupatia faraja, si kuweka ukomo wa maudhui ya maombi yetu.
- Maombi na Uwepo wa Mungu
-
- Soma Zaburi 139:1-3. Mungu anafahamu mambo yetu kwa kiasi gani? (Anajua hadi mawazo yetu “tokea mbali.”)
-
- Soma Zaburi 139:4. Hii inaendana na Mathayo 6:8. Kama tayari Mungu anajua hali yetu, na anajua kile tutakachokisema, hiyo inaathirije jinsi unavyoomba? (Hii inaashiria kwamba maombi ni mawazo yetu yakizungumza na Roho wa Mungu. Hiyo inafafanua kwa upana dhana ya kutenga muda wa kuomba. Badala yake, tunaweza kumwomba Mungu kila wakati. Sisemi kwamba kutenga muda maalumu si jambo sahihi, bali tu kwamba hatuna ukomo wa muda maalumu uliotengwa.)
-
- Soma Kutoka 33:13-15. Huyu ni Musa akizungumza na Mungu. Mungu anamuahidi nini Musa kuhusu uwepo wake? (Anasema kuwa atakuwa pamoja na Musa.)
-
-
- Ni muhimu kiasi gani kuwa na uwepo wa Mungu maishani mwetu ili tuweze kuzungumza naye? (Musa anasema kuwa hawezi kusonga mbele na jukumu alilopewa na Mungu bila uwepo wa Mungu. Mungu anasema kuwa uwepo wake utampa Musa “raha.”)
-
-
- Rafiki, Mungu anatutaka tuwe na uhusiano wa maombi na Yeye. Maombi yetu si kama mazungumzo yetu na mtu mwingine, kwa sababu tayari Mungu anajua mahitaji yetu na hata anajua kile tunachokusudia kukisema. Hana haja ya kuchagizwa (pestered), kwa sababu anatupenda na anajua vipaumbele vyetu. Je, utaingia kwenye ubia wa maombi na Mungu leo? Kwa nini usifanye uamuzi sasa hivi?
- Juma lijalo: Maombi Halisi.
