Huduma Endelevu

(Hesabu 8, Luka 12, Mathayo 5 & 10)
Swahili
Year: 
2012
Quarter: 
2
Lesson Number: 
13

Utangulizi: Kwa kuwa sasa tumefika katika somo la mwisho la kujifunza kwetu kuhusu ushuhudiaji na uinjilisti, tunapaswa tujiulize, “Lini tunaanza?” Ingawaje, inaonekana kana kwamba tunajiuliza “Lini tunaacha?” Je, “huduma endelevu” inamaanisha kwamba hatukomi kamwe? Tabia yangu, kila asubuhi niwapo katika ufukwe wa Virginia, ni kutembea ufukweni. Mtu mwingine nimwonaye mara kwa mara kwenye matembezi yangu ni mstaafu. Hutumia vizuri kila muda wake wa mchana kukaa na mke wake katika ufukwe. Je, ungependa hivyo? Binafsi sikuweza kustahimili. Je, Biblia inafundisha nini juu ya kustaafu kutoka kwenye huduma? Tufanye nini juu ya wale waliostaafu kutoka kwenye huduma kwa sababu hawana furaha? Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia ili tuone kile tunachoweza kujifunza!

  1. Kustaafu
    1. Je, umewahi kusikia mtu akisema kuwa kustaafu si fundisho la ki-Biblia? Hatupaswi kustaafu kwa sababu Biblia haizungumzii jambo hilo? Soma Hesabu 8:23-36. Biblia inapendekeza nini kuhusu kustaafu? (Walawi walistaafu katika huduma za kawaida katika umri wa miaka hamsini!)
      1. Je, walirudi nyumbani na kutazama luninga? (Waliruhusiwa kusaidia, lakini haionekani kuhitajika.)
      2. Tunasikia kwamba umri wa kustaafu unapaswa kuongezwa kwa sababu ya umri mrefu wa kuishi. Soma Kumbukumbu la Torati 34:7 na Yoshua 24:29. Hii, hupendekeza nini juu ya urefu wa maisha ya watu kipindi cha akina Musa? (Inaonekana kwamba watu waliishi miaka 100.)
      3. Hebu tuchukulie kuwa ilikuwa ni kawaida watu kuishi miaka 100 kipindi cha Musa. Je, tufikie hitimisho gani juu ya umri wa miaka 50 ya kustaafu ya Walawi? Je, hivi leo unapaswa kuwa na uwezo wa kustaafu katika umri wa miaka 40?
    2. Soma Luka 12:13-15. Katika mafungu yaliyotangulia katika Luka sura ya 12, Yesu alifundisha kuhusu unafiki na kumcha Mungu. Huyu mtu alitaka kubadilisha mjadala kuzungumzia jambo ambalo alidhani lilikuwa muafaka zaidi kwa maisha yake. Ni kwa namna gani Yesu alijibu swali hili? Alipingana naye. Kisha akapendekeza kwa mtu yule kuzingatia zaidi mada ambayoYesu alikuwa akiizungumzia, kuliko mada ya fedha.)
    3. Soma Luka 12:16-17. Chukulia kwamba unakabiliwa na “tatizo” hili. Je, ungefanya nini?
    4. Soma Luka 12:18-19. Je, hili ni suluhisho lenye mantiki kwa tatizo hili?
      1. Kama ungejibu,“Ningeuza mazao yangu na kuwekeza fedha kwa ajili ya siku za usoni,” je, suluhisho la mkulima ni tofauti kwa namna yoyote na la kwako?
    5. Soma Luka 12:20. Kwa nini mtu huyu ni mpumbavu? Kwa sababu amewekeza kwa siku za usoni? Kwa sababu amestaafu? Kwa sababu hakuweka bima ya maisha? Kwa sababu alikosa mali yake ya mwaka mzima?
      1. Soma Luka 12:21. Yesu anatoa dondoo gani ya kumwita mtu huyu mpumbavu? (Aliandaa maisha yake ya baadaye akilenga raha yake binafsi tu.)
    6. Fikiri kidogo kuhusu kustaafu kwa Walawi na mkulima aliyefariki. Biblia inatufundisha nini kuhusu “huduma endelevu?” (Upande mmoja hatutarajiwi kufanya kazi muda wote kwenye huduma (ama kingine chochote) maisha yetu yote. Kwa upande mwingine, hatupaswi kufikia hatua ya kulenga raha yetu tu. Inatupasa kubakia “matajiri kwa Mungu” maishani mwetu mwote.)
  2. Wastaafu wa Kale (Awali)
    1. Wote tunafahamu watu waondokao kanisani kwa sababu hawana furaha kanisani, waliochoshwa na kanisa, au kutukanwa na washiriki wa kanisa. Je, tunapaswa tuwafuate hawa watu “wanaowahi kustaafu?”
    2. Soma 2 Wakorintho 5:18-19. Kazi gani tumepewa? (Ujumbe wa “upatanisho.”)
      1. Ujumbe huo ni upi? (Kwamba Mungu hahesabu makosa yetu kama tupo ndani ya Yesu.)
    3. Soma Mathayo 10:5-6. Yesu anapozungumzia “kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli,” je, anazungumzia wale waliokwishasikia ujumbe wa upatanisho? (Wakati huduma ya dhabihu hekaluni ilikuwa ni ujumbe wa upatanisho, walikuwa hawajasikia kuhusu Yesu, na namna alivyotimiza huduma ya hekaluni.)
    4. Soma Mathayo 10:11-15. Bidii gani inapaswa ifanyike kwa wale wanaoikataa injili? (Kama ujumbe ukikataliwa, unaondoka.)
      1. Je, hii inatufundisha nini kuhusu kushughulika na “wastaafu” – wale walioacha kanisa kwa sababu mbalimbali? (Inatufundisha kwamba jitihada zetu zielekezwe kwa wale ambao hawajawahi kusikia injili, sio wale ambao wameshawahi kuisikia na kuikataa.)
    5. Hilo linaonekana kuwa hitimisho kali. Je, kuna sababu zozote zinazofanya hitimisho hilo liwe hivyo?
      1. Hebu turejee suala la “kondoo waliopotea wa nyumbani ya Israeli.” Je, hawakuwa wakimfahamu Mungu (Hapana. Isipokuwa tu hawakuwa wamepata ujumbe wa injili.)
        1. Je, kuna washiriki wa zamani wa kanisa lako ambao hawajapokea injili? (Kihistoria, kumekuwa na tatizo la uwasilishaji sahihi wa injili katika baadhi ya makanisa. Watu wengi niliowafahamu ujanani wapo nje ya kanisa sasa, na inaonekana wako nje kwa kuwa hawakuwa wamepata vizuri ujumbe wa upatanisho – Mungu hashikilii dhambi dhidi ya wale walio katika Kristo.)
          1. Maagizo ya “kondoo waliopotea” yanapendekeza nini kwetu kuhusu wale washiriki wa zamani? (Kama hawakuwasilishiwa vizuri injili ya rehema, tunahitajika kujaribu kuwaelimisha kuhusu hili, kuliko kukung’uta mavumbi ya viatu vyetu.)
      2. Soma Mathayo 5:23-24. Jukumu letu ni lipi kwa wale washiriki wa zamani “wenye neno juu yetu?” (Kupatanishwa nao.)
        1. Je, yatupasa sisi kuwa ndio wakosaji ili fungu hili lizewe kutumika? (Endapo kama tu wakosaji, kwa hakika tunapaswa kufanya upatanisho. Lakini, fungu hili linawahusu pia wale wanaofikiri hawana “hatia” ya kutenda kosa. Miaka kadhaa, fungu hili lilinisukuma kujaribu kutaka kufanya upatanisho na mshiriki wa zamani aliyeonekana kunichukia, ingawaje nilifikiri nilikuwa sina hatia. Jitihada zangu za kupatana zilifanya hasira zake kuwa butu, lakini hazikumrudisha kanisani. Ingawaje, watoto wake waliona nilichokifanya na hivyo kuleta upatanisho baina yangu na wao.)
      3. Soma Mathayo 5:44. Tunapaswa kufanya nini kwa adui zetu? (Kuwaombea.)
        1. Je, tunapaswa kufanya chini ya hapo kwa washiriki wetu wa zamani?
    6. Soma 2 Timotheo 2:1-4. Kwa nini mwanajeshi hajihusishi na mambo ya raia? (Hayo sio madhumuni ya jeshi. Watu wataogopa au kulikataa jeshi kama litajihusisha na masua yaya raia.)
      1. Timotheo hayupo katika jeshi. Kwa nini Paulo anaandika hili kwake? (Kwa kiasi fulani, Paulo anamtaka kujikita kwenye shughuli na ujumbe wake sahihi.)
      2. Ni mara ngapi kanisani watu wanakwazwa na mambo ambayo sio ya msingi kwa kazi ya kanisa?
      3. Nina misimamo mikali ya kisiasa. Wakati misimamo yangu inatokana na imani yangu ya dini. Nawafahamu Wakristo wasio na misimamo sawa na mimi ya kisiasa. Ni nini wajibu wangu kwenye misimamo ya kisiasa na kukwaza watu kanisani?
    7. Hivi karibuni tulisoma hili fungu, lakini hebu tulisome tena: 1 Wakorintho 9:20-23. Paulo anafundisha nini kuhusu hatua tunayoweza kwenda kuepuka kukwaza kwenye masuala yasiyo ya msingi kwenye injili?
    8. Rafiki, Biblia inatufundisha kwamba tutapungua kasi kadri umri uongezekavyo, lakini hatupaswa kujigeukia na kutafuta kujifurahisha binafsi. Yatupasa mara zote kuwa matajiri kumwelekea Mungu kwa kushiriki ujumbe wake wa upatanisho. Wakati hatupaswi kupoteza muda mara kwa mara kufuatilia washiriki wa zamani, tunapaswa kutoleta “washirika wa zamani” kwa kukwaza. Kama watu wameondoka kwa sababu ya kukwazwa, au kotofundishwa kwa usahihi, yatupasa kujaribu kurekebisha dosari hizo. Je, utajitolea hivi leo kwa “huduma ya kudumu” ya akili?
  3. . Juma lijalo: Tunaanza somo jipya la Barua kwa Wathesalonike.