Uhai wa Kanisa
(1 Wathesalonike 5 :12 - 28)
Swahili
Year:
2012
Quarter:
3
Lesson Number:
10
Utangulizi: Ninakumbuka jinsi wazazi wangu walivyokuwa wakienda likizo na kuniacha mimi na kaka yangu nyumbani. Tulikuwa chuoni, lakini walipokuwa wakijiandaa kuondoka mama yangu alikuwa akitupa mafundisho mafupi kuhusu lishe bora, afya na usalama. Hizo ndizo hisia nilizonazo tunapoelekea mwishoni mwa barua ya kwanza ya Paulo kwa Wathesalonike. Anawapatia “nukuu muhimu” kuhusu uhai wa kanisa na maisha ya Kikristo (kuishi Kikristo). Kwa hakika kabisa Paulo aliwachukulia kuwa wao ni watu muhimu, vivyo hivyo nasi ni wa muhimu. Hebu tuzame kwenye somo letu ili tuone kile tunachoweza kujifunza kutokana na kile Paulo anachokisema wakati watu wanapoachana!
- Kazi
- Soma 1 Wathesalonike 5:12. Je, ni watu gani tunaopaswa kuwaheshimu? (Wale wanaojibidiisha kwa ajili ya kanisa, wale walio “juu” yetu, na wale wanaotukemea.)
- Huu ni mjumuisho mzuri: bidii ya kazi, uongozi na heshima. Vipi kama tunaye kiongozi wa kanisa ambaye ni mvivu? Au, Yule anayefanya kazi kwa bidii, lakini sio kwa ajili ya kanisa? (Kiongozi huyo hastahili heshima.)
- Waprotestanti wana tatizo dogo kuhusu wazo la mamlaka ya kanisa. Je, Paulo anapendekeza nini kuhusu mamlaka ya kanisa kwenye hiki kifungu? (Kanisa lina mamlaka (“wale wanaowasimamia ninyi katika Bwana”), na mamlaka hayo yanajumuisha haki ya kutuonya.)
- Soma 1 Petro 2:9. Kama sisi sote ni makuhani, je, ni kwa jinsi gani basi mtu mwingine anaweza kuwa na mamlaka juu yetu?
- Soma 1 Petro 2:13-14 na Matendo 5:27-29. Je, unalinganishaje hizi kauli mbili za Petro?
- Utabaini ukweli kwamba Baraza la Sanhedrin lilijumuisha watu waliokuwa na mchanganyiko wa mamlaka za kidini na kiserikali. Je, tunapaswa kuelewaje rejea ya Paulo kwa wale walio “juu” yetu “katika Bwana?” (Mungu anaamini katika utaratibu/mfumo, muundo na mamlaka. Ndio maana Petro aliyasifia mamlaka ya kiserikali. Paulo anaunga mkono mamlaka ya kanisa. Lakini, hatma ya utii wetu ni kwa Mungu, sio kwa wanadamu. Hata mamlaka ya kidini yanaweza kukosea. Wanapokosea wanakuwa hawapo “katika Bwana.”)
- Je, tunapaswa kuyachukulia mamlaka ya kanisa kwa udhati gani tunapokuwa hatukubaliani nayo? (Katika miaka yangu mingi ya kukabiliana na kesi za uhuru wa dini, nimebaini kwamba watu wenye matatizo ya mara kwa mara na mamlaka ya kanisa, watu ambao hawawezi kuishi ndani ya mipaka ya kanisa, ni wale ambao kwa ujumla sio waaminifu kwenye imani zao.)
- Soma 1 Wathesalonike 5:13. Je, sababu ya kuyapenda mamlaka ya kanisa ni ipi? (Hapa Paulo haandiki kuhusu neema. Anasema “muwapende kutokana na kazi/majukumu wanayoyafanya.”)
- Je, upendo unawezaje kutokana na kazi? (Ninafanya hivi pamoja na wachungaji, walimu na viongozi kanisani kwangu. Ninapoona jambo ambalo ninaona kuwa ni la kipumbavu, katika mashaka yangu huwa ninampa faida mtu huyo kwa sababu amejitolea maisha yake kuiendeleza injili.)
- Soma 1 Wathesalonike 5:14. Je, kazi ni muhumu kiasi gani kwa Paulo? (Anasema kuwa waonyeni wale wanaokaa bila kufanya kazi (wasio na utaratibu), na kuwaheshimu na kuwapenda wale wanaofanya kazi kwa bidii.)
- Katika nchi ya Marekani (na kwingineko duniani pote) tuna uibukaji wa kundi la watu wanaoishi maisha yaliyo tegemezi wa serikali au ndugu. Je, Paulo anasema nini kuhusu jambo hilo? (Hatupaswi kuuhamasisha uzembe, badala yake tunapaswa tuupige vita.)
- Je, unadhani Paulo anamaanisha nini anaposema, “muwaonye wasiokaa kwa utaratibu?” Muwaonye kuhusu jambo gani? (Katika 2 Wathesalonike 3:10, Paulo anasema kuwa wale wasiotaka kufanya kazi, basi wasile chakula.)
- Linganisha mtazamo wa Paulo dhidi ya watu wavivu na mtazamo wake dhidi ya watu waoga, wanyonge na wenye maudhi? (Paulo anadokeza kwamba tunapaswa kuwasaidia watu wenye matatizo haya. Kimantiki hii inadokeza kwamba mtazamo “mzito” wa Paulo dhidi ya watu wavivu ni jambo ambalo linadhamiria kuwasaidia – na sio kuwaadhibu.)
- Katika nchi ya Marekani (na kwingineko duniani pote) tuna uibukaji wa kundi la watu wanaoishi maisha yaliyo tegemezi wa serikali au ndugu. Je, Paulo anasema nini kuhusu jambo hilo? (Hatupaswi kuuhamasisha uzembe, badala yake tunapaswa tuupige vita.)
- Soma 1 Wathesalonike 5:12. Je, ni watu gani tunaopaswa kuwaheshimu? (Wale wanaojibidiisha kwa ajili ya kanisa, wale walio “juu” yetu, na wale wanaotukemea.)
- Mtazamo
- Soma 1 Wathesalonike 5:15. Je, tunapaswa kuwa wema kwa watu gani, je, ni kwa wale walio kanisani tu? (Tunapaswa kuwa wema kwa wale waliotukosea, wale walio kanisani, na “kila mtu mwingine yeyote yule.”)
- Soma 1 Wathesalonike 5:16-18. Je, umewahi kujaribu “kufurahi siku zote?” Je, matokeo yake yalikuwaje?
- Je, mapendekezo haya matatu yanatofautiana (furaha, kuomba na kushukuru), au yote kwa pamoja yanaunganishwa kimantiki? (Haiwezekani kusema “nitakuwa mwenye furaha sasa hivi” na kisha kuwa na furaha. Badala yake, maombi na shukrani vinatusaidia kutupatia furaha. Maombi yanatuelekeza kwenye mapenzi ya Mungu. Shukrani inaielekeza mioyo yetu kwa ajili ya thawabu kubwa za Mungu. Maombi na shukrani ndio njia ikuelekezayo kwenye furaha zaidi maishani mwako.)
- . Roho Mtakatifu
- Soma 1 Wathesalonike 5:19-22. Je, mafungu haya manne yanaunganishwa kimantiki? Je, Paulo anabainisha “mambo muhimu” katika mada moja? (Nadhani.)
- Soma Yoeli 2:28-29. Je, “baada ya hapo” tunaahidiwa nini? (Kumiminwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu katika unabii.)
- Je, “baada ya hapo” ni lini? (Soma Matendo 2:15-17. Baada ya hapo inamaanisha baada ya ufufuo wa Yesu!)
- Soma tena 1 Wathesalonike 5:19-21 kwa muktadha wa Yoeli 2. Je, tunapaswa kutarajia watu walio kanisani (wanaume na wanawake, vijana na wazee) kuonyesha karama ya unabii? (Ndiyo!)
- Je, mtazamo wetu dhidi ya hao manabii unapaswa kuwaje? (Hatupaswi kuwatendea mambo kwa dharau/kuwabeza. Tunahitajika kuuchukulia ujumbe kwa umakini. Lakini, tunahitajika “kuyajaribu” mambo yote.)
- Je, tunamjaribu nabii au unabii? (Kwa kuwa karama ya unabii imeenea sana, na kwa kuzingatia jinsi mafungu yalivyoandikwa, inaonekana wazi kabisa kwamba tunaujaribu unabii na sio kumjaribu nabii.)
- Soma Kumbukumbu la torati 18:18-22. Je, adhabu iliyotolewa katika Agano la Kale kwa unabii wa uongo ni ipi? (Kifo.)
- Je, huku ni kumjaribu nabii au kuujaribu unabii? (Maelekezo ya kumwua nabii wa uongo, au “kutomwogopa,” yanaelekezwa kwa nabii mwenyewe, badala ya kuelekezwa kwenye ujumbe mahsusi. Kamwe hatuwezi kumtegemea nabii “mbaya” kwa yeye kutoa ujumbe wa kweli.)
- Je, karama ya unabii inatendewa vingine katika Agano Jipya tofauti na vile inavyotendewa katika Agano la Kale? (Ndiyo. Angalau kwa sasa hivyo ndivyo ninavyofikiria. Katika kipindi ambacho wafuasi wa Mungu hawakuwa na maandiko yake yaliyoandikwa, Mungu alizungumza nao kupitia kwa manabii wachache. Usahihi wa ujumbe kutoka kwa nabii haukuweza kuhakikiwa kwa urahisi, na kwa hiyo kauli zisizo sahihi zilikuwa na madhara makubwa. Katika Agano Jipya, karama ya unabii ilienea, tunayo Biblia kama zana ya kujaribia, na tunaujaribu ujumbe, sio manabii. Kwa hiyo, manabii wa leo wanaweza “kukosea” na sio tatizo kubwa. Nabii huyo anaweza kutoa ujumbe wa kweli baadaye. Hakuna anayeuawa. Ujumbe wote lazima uendane na kuthibitishwa na Biblia.)
- “Tunapolishika lililo jema” katika 1 Wathesalonike 5:21, je, ni jambo gani hicho tunalolishikilia? (Unabii tulioujaribu na kuuona kuwa mzuri.)
- Je, mtazamo wetu dhidi ya hao manabii unapaswa kuwaje? (Hatupaswi kuwatendea mambo kwa dharau/kuwabeza. Tunahitajika kuuchukulia ujumbe kwa umakini. Lakini, tunahitajika “kuyajaribu” mambo yote.)
- Soma tena 1 Wathesalonike 5:22. Katika muktadha wa manabii wa leo, je, ni uovu gani tunaojitenga nao? (Ingawaje ninadhani Paulo anazungumza kuhusu unabii badala ya manabii, kwa dhahiri kabisa wapo manabii wa uongo ambao kamwe hawaliendelezi neno la Mungu. Wale walio waovu wanapaswa kuepukwa kabisa.)
- Mwenendo
- Soma 1 Wathesalonike 5:23-24. Utakumbuka kuwa katika 1 Wathesalonike 4:1 Paulo aliwaambia Wathesalonike kwamba “kimsingi” walikuwa wakiishi ili “kumpendeza Mungu.” Lakini baadaye tulijifunza katika 1 Wathesalonike 4:3-5 kwamba walikuwa na tatizo la uzinzi na uasherati. Je, uelewa wetu wa msingi wao unatusaidiaje kuelewa 1 Wathesalonike 5:23-24? (Mungu anatutakasa. Anatusafisha, “tena na tena.” Tuna uhakika wa wokovu wetu wakati Mungu akitusafisha.)
- Kama Mugu anatusafisha, kwa nini Paulo anawaandikia Wathesalonike kuhusu habari hiyo? (Lazima tuonyeshe ushirikiano. Tunaokolewa kwa neema pekee, lakini linapokuja suala la usafishaji, sisi tu watendakazi pamoja na Mungu na tunashirikiana naye. Lengo letu ni kuufikia utakatifu!)
- Soma 1 Wathesalonike 5:25-28. Kwa nini Paulo anasisitiza maombi yao? (Sote tunahitaji mtu wa kutuombea. Tunahitaji kuwaona watu wengine wakitupokea kwenye mahusiano na kuchangamana kwetu. Tunahitaji neema ya Bwana wetu Yesu.)
- Rafiki, je, upo kwenye njia inayouelekea utakatifu? Paulo anatuambia kuwa tufanye kazi kwa bidii, tuwe na mtazamo chanya, tuwaheshimu viongozi wa kanisa, tufungue mioyo yetu kwa ajili ya kupokea ujumbe wa Roho Mtakatifu, na kuwa wema kwa watu wengine. Je, upo kwenye uelekeo unaoelekea kwenye hayo mambo yote? Kama sivyo, kwa nini usijizatiti na kudhamiria kuanza hivi leo?
- Soma 1 Wathesalonike 5:23-24. Utakumbuka kuwa katika 1 Wathesalonike 4:1 Paulo aliwaambia Wathesalonike kwamba “kimsingi” walikuwa wakiishi ili “kumpendeza Mungu.” Lakini baadaye tulijifunza katika 1 Wathesalonike 4:3-5 kwamba walikuwa na tatizo la uzinzi na uasherati. Je, uelewa wetu wa msingi wao unatusaidiaje kuelewa 1 Wathesalonike 5:23-24? (Mungu anatutakasa. Anatusafisha, “tena na tena.” Tuna uhakika wa wokovu wetu wakati Mungu akitusafisha.)
- Juma lijalo: Ahadi kwa Wateswaji.