Wokovu: Suluhisho Pekee
(Mwanzo 4, Mambo ya Walawi 1 & 6, Wagalatia 3, Warumi 3)
Swahili
Year:
2012
Quarter:
4
Lesson Number:
4
Utangulizi: Hivi karibuni mke wangu alihudhuria mkutano la watenda kazi na walimu wa shule wa kanisa. Kupitia uchawi wa teknolojia ya kisasa, katika kipindi kimoja hadhira iliweza kutoa mrejesho kwa njia ya elektroniki ambao ulikokotolewa mara moja na kuonyeshwa kwenye skrini mbele. Swali lililoulizwa kwa hadhira lilikuwa endapo walikuwa wanajiamini na wokovu wao. Jibu chanya lilikuwa ni la kukatisha tamaa. Kama umefanya maamuzi yako kwa ajili ya kristo, lakini huna uhakika na wokovu wako, lazima hii teolojia ya “taswira pana”uipate kwa usahihi. Jiunge nami katika safari hii muhimu katika biblia katika kujifunza maana halisi ya neema.
- Neema Katika Agano la Kale
- Soma Mwanzo 4:2-5.Kwanini sadaka ya Habili inakubaliwa zaidi kuliko ya Kaini? Je huu ni ubaguzi wa shughuli?
- Soma Mwanzo 4:6-7. Mambo gani yenye kufanana ambayo watoto wote waliyafanya? (Wote walifanya kazi shambani. Wote walichagua vilivyo bora (mazao ya kwanza) kwa Mungu. Wote walileta sadaka kwa Bwana.)
- Sasa ni nini Mungu anachomaanisha anaposema Kaini “usipotenda vyema?” Kaini na Habili walifanya kimsingi kitu kinachofanana! (Si kwamba mmoja alifanya na mwingine hakufanya. Ni kwamba mmoja alifuata maagizo ya Mungu ya sadaka.)
- Nini dhumuni la sadaka?
- Soma Mambo ya Walawi 1:1-2. Nini kinajadiliwa hapa? (Sadaka ya wanyama – mada sawa na ile ya kwenye simulizi ya Kaini na Habili.)
- Soma Mambo ya Walawi 1:3-4. Jambo gani lilitakiwa katika mfumo wa Agano la Kale kwa mtu kufanya upatanisho na Mungu? (Hakukuwa na tendo lililohitajika kwa mtu kupata msamaha wa dhambi. Utakaso ulipatikana kwa njia ya mnyama kufa badala ya mwanadamu pekee. Zingatia, hatahivyo, Mungu anajali haki ya umiliki, na katika Mambo ya Walawi 6:1-7 inataka mali iliyoibiwa kurudishwa na adhabu ya 20%. Hatahivyo, hii inaakisi kujali kwa Mungu kwa haki ya kumiliki baina ya watu, mwizi hamlipi Mungu kwa dhambi yake.)
- Ni nini tunachojifunza katika safari yetu fupi katika Mambo ya Walawi kuhusu kwanini sadaka ya Kaini haikukubalika? (Soma Mwanzo 3:2-4. Adhabu ya dhambi ni kifo. Kifo cha mnyama kilileta utakaso wa dhambi. “Kifo” cha tunda hakifanyi hivyo. Damu siyo juisi ya matunda iletayo utakaso wa dhambi.)
- Chini ya mfumo wa Agano la Kale, je bidii kubwa katika matendo inaweza kuleta uhusiano mzuri na Mungu? (Muulize Kaini. Kiburi cha Kaini na hasira yake kwa kutokuwa sahihi katika ukweli huu kulimfanya amuue kaka yake.)
- Je umewahi kufikiri mfumo wa neema katika Agano la Kale wa kusamehe dhambi? Soma Tito 1:1-3. Ni kwa muda gani Mungu amekuwa na mpango wa neema ukitenda kazi? (Uliahidiwa “tangu milele!” Inaleta mantiki kamilifu ya kuwa mfumo wa hema ungekuwa ni kielelezo cha rehema.)
- Shida ya Kaini leo
- Muda wowote nifundishapo juu ya neema, Napata ujumbe kutoka kwa wasomaji kupinga kwamba tunaokolewa “kutoka kwenye dhambi zetu, siyo katika dhambi zetu.” Unafikiri hii inamaanisha nini? Je, hii humaanisha kuwa tukiwa na dhambi hatuwezi kuokolewa? Kama ndivyo, ni nani asiye na dhambi? Na, nini hasa humaanishwa na “dhambi?”
- Soma Jeremia 17:9, Warumi 5:14, Isaya 64:6 na Warumi 3:9-12. Kulingana na mafungu haya, kama hatuwezi kukolewa “katika dhambi zetu,” ni nani awezaye kuokolewa? (Hakuna.)
- Shida gani inawakabili wale waaminio, kama Kaini, ya kwamba bidii yao kwenye matendo (sadaka zao) zitawafanya kukubalika kwa Mungu? (Wamepotea. Hakuna aliye na haki. Endapo unafikiri kuwa tabia yako inakuokoa kwa namna yoyote, upo kama Kaini. Si tu kwamba Kaini anamkasirikia kaka yake Habili, lakini alikataliwa na Mungu kwa kushindwa kufuata njia pekee ya wokovu.)
- Hebu na turudi kwenye utambulisho. Kama mkristo ametoa moyo wake kwa Mungu, na hana uhakika na wokovu wake, hiyo inamaanisha nini? (Inamaanisha kuwa mkristo anaamini kuwa matendo yake kwa namna fulani yamemfanya apoteze wokovu wake. Hizi ni fikra za Kaini. Imani hiyo, zaidi ya dhambi katika maisha, inaleta hatari kubwa katika wokovu. Sadaka ya matendo ya Kaini haikukubalika mbele ya Mungu.)
- Je, hii humaanisha kuwa pindi mtu aokolewapo basi ameokolewa kwa wakati wote? (Hapana! Suala ni kwamba endapo umechagua kuwa Habili, kuchagua kuwa upande wa Mungu, na kukubali mpango wake wa wokovu. Unaweza ukageuka mbali na Mungu daima,unaweza kuvunja uhusiano na yeye, na unaweza kuchagua kuisho maisha nje ya mapenzi ya Mungu.
- . Uthibitisho wa wokovu kupitia neema pekee
- Soma Wagalatia 3:6-9. Ni nani Paulo anamwelekeza kama mfano wa haki kwa njia ya imani? (Abraham, shujaa wa Agano la Kale.)
- Soma Wagalatia 3:10-14. Ni ipi hatari ya kuwa na mtazamo wa Kaini ya kuwa matendo yetu yanabainisha nafasi yetu mbele ya Mungu? (“Wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana.” Kujaribu kutunza sheria ni hali isiyokuwa na ushindi.)
- Soma Warumi 3:21-23. Paulo anaposema “hakuna tofauti” ni tofauti gani anayozungumzia? (Hakuna tofauti baina yetu wadhambi, tumetenda dhambi wote. Wengine wanatenda dhambi sana, wengine kidogo, lakini kwakuwa wote tu wadhambi, hakuna tofauti machoni pa Mungu.)
- Soma Warumi 3:24-26. Ni njia ipi pekee ya wokovu. (Neema! Tunahesabiwa haki kwa neema.)
- Kama mtu hana uhakika na wokovu wake, ni nini itakuwa sababu ya hilo? (Watakuwa wanafikiria mapungufu katika maisha yao. Jambo ambalo wanapaswa kulishughulikia.)
- Ni nini kauli hii ya “hakuna tofauti” inasema kwa mtu ambaye anasumbuliwa na “kuwa ndani ya dhambi?” (Huna “dhambi ndogo” katika maisha yako. Kwa kadiri imuhusuvyo Mungu “hakuna tofauti” baina yako na muuaji wa mfululizo! “Wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.” Warumi 3:23. Endapo utapungua, ni unapungua tu iwe ni kwa inchi moja au kwa maili mia moja. Neema ni zawadi, haitegemei matendo yako.)
- Kama mtu hana uhakika na wokovu wake, ni nini itakuwa sababu ya hilo? (Watakuwa wanafikiria mapungufu katika maisha yao. Jambo ambalo wanapaswa kulishughulikia.)
- Soma Warumi 3:27-30. Paulo anasema “hakuna kujisifu.” Kwanini? (Kwa sababu matendo yetu hayahusiki kwenye neema.)
- Nini kinyume cha kujisifu? (Hisia za unyonge au kupungua.)
- Endapo kama kujisifia hakupo, je hisia za kujihisi kupungua hazipo? (Ndiyo! Bwana asifiwe ya kuwa hazina mantiki kama ilvyo kujisifu. Kukosa kujiamini katika neema ya Mungu, si zaidi ya kujisifu kwetu kuhusu jukumu letu katika zawadi ya Mungu ya neema.)
- Nini kinyume cha kujisifu? (Hisia za unyonge au kupungua.)
- Soma Warumu 4:4-5. Ni lipi jukumu letu ijapo neema? (Kumwamini Mungu.)
- Kamahatuna uhakika na wokovu wetu, je tunamwamini Mungu? (Hapana. Tunazingatia endapo kama tuna “salio” la kutosha kutokana na matendo yetu.)
- Njia ya wokovu
- Soma Warumi 3:31. Namna gani uelewa sahihi wa neema tusiyostahili unaathiri dhana ya sheria? (Hauko kinyume na sheria. Unainua sheria.)
- Soma Wagalatia 5:13-18. Pindi tutakapokuwa na uthibitisho wote na kamili wa wokovu kwa neema pekee, tutaishi vipi? (Tupo huru! Hatuhitajiki kutii sheria kuendelea kuwa kwenye neema. Lakini Paulo anasema “uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili.”)
- kwanini itakuwa jambo lisilo la asili kwa sisi kuufuata mwili? (Mungu alikufa kwa dhambi zangu. Alitoa maisha yake kwa ajili ya dhambi zako. Dhambi imeleta mafuriko ya uchungu kwa Mungu na wanadamu pia. Kama Mungu alikupenda kiasi hicho, ni kwa vipi utashindwa kuishi maisha ya kupenda wengine? Msingi wa sheria ni upendo.)
- soma tena Wagalatia 5:16-18. Nini Msingi wa kuishi maisha ya upendo, maisha ya kumpendeza Mungu? (Ishi kwa uweza wa Roho Mtakatifu!)
- soma Wagalatia 5:19-25. Je, tunaitwa kuishi maisha matakatifu? (Ndiyo. Bila shaka.)
- Je, kuishi maisha matakatifu, na kujizuia kuishi maisha ya dhambi, inatuokoa? (Hapana! Bado tunaokolewa kwa neema pekee. Ni zawadi.)
- Tukiwa tumehakikishiwa wokovu wetu, nini lengo la maisha yetu? (Kumwaacha Roho Mtakatifu asulubu asili yetu ya dhambi na “mawazo na tamaa” zake.)
- Ndugu rafiki, kubali zawadi ya Mungu ya wokovu kwa neema pekee kwa furaha na kujiamini! Kama ukichagua kutubu dhami, na kukubali kafara ya Yesu kwa niaba yako, umeokolewa. Haupaswi kuwa na shaka ya wokovu wako. Kwa upande mwingine, kama unaamini kuwa wokovu wako unaamsha haki ya matendo, unamfuata Kaini na uko chini ya laana. Je, utachukua zawadi leo na si laana?
- Juma lijalo: Kukua Katika Kristo