Sheria na Injili
Utangulizi: Unazionaje Amri Kumi za Mungu? Je, unaweza kuona ulinganifu wenye mantiki kati ya amri hizo na mara ya mwisho ulipoona taa za kuongozea magari barabarani kwa kutumia kioo cha nyuma cha gari lako? Yesu hakusaidia kutatua tatizo hili alipoelezea kwamba amri ya uzinzi na mauaji zilijumuisha tatizo la kawaida la tamaa na hasira. Je, ni watu wangapi , pale wanaposikia kuhusu neema, wanafurahi kwa sababu wanadhani hawana haja tena ya kuwa na wasiwasi kuhusu hizo amri zenye usumbufu, zinazochukiza na kutaabisha? Wino mwingi sana umekwishatumika kuhusu mada ya sheria na neema, lakini nadhani tutaielewa neema vizuri zaidi kama tukiielewa vizuri asili ya sheria. Tunadai kuwa kama tunaokolewa kwa neema, basi tutahitajika kumtii Mungu. Lakini, hilo haliendani na kulinganisha suala la amri na suala la kujisikia kama askari polisi anataka kututia kizuizini! Kwa hiyo, hebu tuzame kwenye Biblia ili tuelewe vizuri zaidi kile inachokisema kuhusu sheria!
- Sheria ya Mungu na Faida
- Soma Zaburi 19:7. Ninaweza kuelewa kwamba ni kwa nini Roho Mtakatifu alimvuvia Daudi kusema kwamba sheria ya Mungu ni kamilifu. Lakini je, ni kwa namna gani sheria “inaburudisha nafsi?”
- Unaweza kutafakari kauli hii, ya kwamba polisi anakuambia kuwa, “hapa mwendo wa gari unaotakiwa umedhibitiwa kikamilifu – na udhibiti wa mwendo utakufurahisha!” (Ninapenda utaratibu na ninachukia suala la kutokuwa na utaratibu. Mahali ninapofanyia kazi na mahali ninapioshi pamepangiliwa, kiasi kwamba ni nadra sana kwangu mimi kujaribu kutafuta kitu fulani. Ninaelewa kwamba utaratibu unaboresha maisha yangu. Watu wanapokuwa na tofauti ya mwendokasi wa maili 20 kwa saa barabarani, hii inasababisha vurugu/usumbufu. Magari yaliyopo mbele yangu yanapokuwa yanasimama, na ninakuwa sijagundua hilo, mke wangu huwa anasikitika/hafurahii.)
- Zaburi 19:7 pia inatuambia kuwa sheria inawafanya watu wajinga kuwa werevu, na sababu ni kwamba sheria ni aminifu. Hakuna hata moja kati ya masuala haya inaleta mantiki. Je, unaweza kulielezeaje suala hili?
- Unapokuwa unaomba ushauri, kwa sababu wewe sio mwerevu vya kutosha (au hujaelimika vya kutosha) kutafakari mambo peke yako, je, ni ushauri gani unaokuwa unautaka? (Ushauri unaoweza kuuamini.)
- Kwa nini unataka ushauri wenye kuaminika? (Tatizo ni kwamba hujiamini wewe mwenyewe kuwa unaweza kuwa na suluhisho sahihi. Kitu kimoja kinachowatofautisha watu werevu na wapumbavu ni kwamba watu werevu wanajua nini cha kufanya ili waweze kuishi vizuri. Fungu hili linaashiria kwamba sheria ya Mungu inawapa watu wapumbavu ushauri wanaoweza kuuamini ili waishi maisha bora.)
- Soma Zaburi 19:8. Tumeona namna ambavyo mara nyingine sheria inaonekana kuwa kama polisi. Ni kwa namna gani sheria inatufurahisha? (Polisi anatusimamisha kwa sababu tunakuwa tumekiuka sheria. Tukiishika sheria, tunaepuka matatizo. Hii ndio sababu ya furaha.)
- Zaburi 19:8 inatuambia kuwa sheria ni kama nuru. Je, ni kwa namna gani sheria inafananishwa na nuru? (Hii inafanana na lile suala la kuwafanya watu wajinga kuwa werevu. Sheria inadhihirisha siri (au angalao basi ukweli) kuhusu tabia. Tukifuata kile ambacho sheria inakisema kuhusu tabia nzuri, tutakuwa werevu.)
- Je, umewahi kujisikia kwamba kama ungekuwa mwerevu maisha yako yangekuwa bora? Kama ndivyo, ni kwa nini? (Ungefanya maamuzi mazuri zaidi ambayo yangeimarisha ubora wa maisha yako.)
- Fikiria siku ambayo ulijisikia kuwa na hatia zaidi. Je, ulijisikia vibaya kwa sababu ulikiuka sheria, au kwa sababu ulihatarisha mahusiano yako na watu wengine? (Tunaweza kuona moja kwa moja kwamba hii inaongelea ubora wa maisha.)
- Soma Zaburi 19:9-11. Je, hapa kuna kaulimbiu kuhusu sheria? (Ndiyo! Sheria ya Mungu inatupatia ushauri mzuri wa namna ya kuishi. Tukiufuata, ushauri huo ni bora kuliko kuwa na utajiri – maisha yetu yanakuwa matamu. Tunaonywa mambo ya kuepuka, na tunazawadiwa kwa kutenda yaliyo sahihi.)
- Soma Zaburi 19:7. Ninaweza kuelewa kwamba ni kwa nini Roho Mtakatifu alimvuvia Daudi kusema kwamba sheria ya Mungu ni kamilifu. Lakini je, ni kwa namna gani sheria “inaburudisha nafsi?”
- Faida na Kujikana Nafsi
- Watu wanapotuambia kuwa kama tunaokolewa kwa neema, tutaitii sheria kwa sababu tunampenda Mungu, je, hiyo inaonekana kuwa kauli yenye uaminifu wote kabisa? Je, ni ukweli wote kabisa? (Mafungu ya Biblia ambayo tumekuwa tukiyasoma yanaashiria kuwa tunaishika sheria kwa sababu tunamtumaini Mungu na tunajipenda!)
- Je, kaulimbiu tuliyokuwa tukiiendeleza inakutaabisha? Amri Kumi za Mungu ni “kitabu cha mtu kujisaidia yeye mwenyewe” ambacho mtu yeyote mwenye akili sahihi atakifuata? Kwa hiyo, kuzishika amri ni rahisi kwa sababu hicho ndicho tunachokifanya ili kuwa na maisha bora?
- Ama kwa hakika, sio sheria zote za Mungu zina faida kwako na kwangu, sawa? Kwa mfano, Yesu anasema kwamba (Mathayo 22:37-40) kumpenda jirani yangu kama nafsi yangu ndio nguzo ya sheria. Jirani yangu amegonga sehemu ya kifaa cha gari langu na kukitenganisha vipande viwili! Je, baadhi ya sheria ni sawa na maumivu shingoni? Tutaliona hilo katika sehemu inayofuata.
- . Sabato na Kujikana Nafsi
- Soma Kutoka 20:8-11. Mwajiri wako anapokupa likizo yenye malipo, je, unalalamika? Je, Mungu ametupa likizo ya kila juma kutokana na hii amri?
- Je, ni nani mwingine ambaye Mungu amempa likizo? (Waajiriwa wetu na wanyama wetu.)
- Je, hiyo ni sawa kwako – kuwapatia wafanyakazi wako siku ya kupumzika kila juma? (Hapana. Hii ni fedha kutoka mfukoni mwangu. Ninaweza kuwa ninaipata kutokana na kazi yao.)
- Je, ni nani mwingine ambaye Mungu amempa likizo? (Waajiriwa wetu na wanyama wetu.)
- Kama Amri Kumi ni fungu la kanuni zinazomwongoza mtu kujisaidia mwenyewe, je, tunaielezeaje amri ya Sabato katika kuwapatia wafanyakazi wetu siku ya kupumzika?
- Kwa sababu hiyo, tunazielezeaje amri dhidi ya mauaji, wizi, uzinzi, kushuhudia uongo na kutamani? (Je, unaweza kuiona kaulimbiu hapa? Sheria ya Mungu hairuhusu mtu kuwa jeuri. Unaweza kulipenda gari, nyumba, mke, kazi au kipato cha jirani yako zaidi kuliko vyako. Lakini, huruhusiwi kuvichukua. Ama kwa hakika, huruhusiwi hata kufikiria namna unavyopendelea vitu hivyo, kwani huko ni kutamani.)
- Soma Warumi 7:7-9. Je, hii inasema nini pale asili yetu ya uanadamu inapokabiliwa na kanuni? (Haturidhiki kwa kuwa na maisha bora tu. Haturidhiki kwa kuwa na maboresho ya kawaida tu. Tunaridhika pale tunapokuwa tumeimarika zaidi kuliko watu wanaotuzunguka. Tunataka pumziko la Sabato, lakini hatutaki pumziko hilo kwa wafanyakazi wetu. Kama jirani yetu ana gari zuri, tunalitaka, naye anaweza kuchukua gari letu lenye hadhi ya chini.)
- Soma Kutoka 20:8-11. Mwajiri wako anapokupa likizo yenye malipo, je, unalalamika? Je, Mungu ametupa likizo ya kila juma kutokana na hii amri?
- Sabato na Asili ya Mwanadamu
- Soma Kutoka 20:11 kwa mara nyingine tena. Je, sababu ya kuitunza Sabato ni ipi – kuwa na likizo? (Hapana. Sabato imebarikiwa na ni takatifu kwa sababu inatukumbusha kwamba Mungu ni Muumba wetu.)
- Soma Kumbukumbu la Torati 5:15. Je, hii inatoa sababu gani ya kuitunza Sabato? (Kwamba Mungu aliwakomboa Wayahudi kutoka utumwani Misri.)
- Soma Mathayo 27:62-63 na Mathayo 28:1-4. Mafungu haya yanabainisha kuwa Yesu alikuwa kaburini siku ya Sabato na akafufuka katika siku ya kwanza ya juma (Jumapili). Unadhani ni kwa nini alifanya hivi? (Hapa tunaona kwamba Sabato imedhamiriwa kutukumbusha si tu kwamba Yesu ni Muumba wetu, bali pia alitukomboa kutoka katika utumwa wa dhambi. Yesu alipumzika ili kufanya ukumbusho (kukumbukia) ushindi wake dhidi ya dhambi. Vinginevyo, kuchelewa kwake hakuna mantiki yoyote.)
- Soma Wakolosai 1:16-22. Tunapomjumuisha, kama anavyofanya Paulo hapa, Yesu kama Muumba na Mkombozi, je, hilo linatusaidiaje kukabiliana na asili yetu ya uanadamu? (Mambo mawili. Kwanza, inaanzisha mtazamo wa upendo na shukrani kwa Yesu. Pili, inaunda mtazamo wetu dhidi ya watu wengine. Tuliumbwa na Mungu na kukombolewa na Mungu. Watu wote wamo ndani ya chombo kimoja. Je, kwa nini tunadhani kwamba kutokuwa na jeuri ni jambo sahihi?)
- Soma 1 Yohana 2:3-6. Yohana anasema jambo la kufurahisha sana hapa. Hasemi kwamba “Tunajua kwamba tunaokolewa kama tunatii amri za Mungu.” Badala yake, anasema kuwa “tunamjua Mungu” kama tukitii. Kwa nini kumjua Mungu kunakuza utii? (Amri Kumi zinaboresha maisha yetu. Amri hizo ni namna ya kutuwekea nafasi kwa ajili ya kuishi maisha bora. Tunaingia matatizoni kutokana na amri, hata hivyo, hapo ni pale tunapokuwa na jeuri binafsi. Kulijua somo linalohusu Sabato, ya kwamba Mungu alituumba na kutukomboa kwa kujitoa kwa ajili yetu, kunatufundisha kudhibiti matakwa yetu binafsi. Inatufundisha kutaka kutazamia kuwaangalia watu wengine.
- Rafiki, je, utamwomba Roho Mtakatifu akusaidie kumjua Yesu anayetuhamasisha kuishi maisha ya kudhibiti matamanio yetu binafsi? Maisha yenye furaha ndani ya sheria, ikiwemo Sabato inayotukumbusha kile ambacho Mungu amekitenda kwa ajili yetu na kwenye mtazamo wetu sahihi dhidi ya watu wengine?
- Juma lijalo: Maisha ya Mkristo.