Mambo Yote Yatakapokuwa Mapya
(Ufunuo 19-22)
Swahili
Year:
2012
Quarter:
4
Lesson Number:
13
Utangulizi: Hebu tuendelee na upembuzi wetu wa juma lililopita kuhusu “kustaafu” mbinguni – mahali palipo na utukufu ambapo tuna muda na rasilimali nyingi zisizo na mpaka. Tunayo tiketi yetu na tunaelewa kwamba tunapaswa kuwa makini ili kuepuka kwenda kwenye tukio lisilostahili. Tunaishi maisha yanayoakisi upendo wa Mungu kwetu na hivyo tunayatarajia maisha yetu ya mbinguni. Kisha Yesu anakuja! Hebu tuzame kwenye Biblia yetu tujifunze zaidi kuhusu kile kitakachofuatia!
- Ufufuo!
- Soma 1 Wathesalonike 4:16-18. Je, ni kitu gani kinachoelezewa hapa? (Ujio wa Yesu Mara ya Pili.)
- Fungu hili haliwataji watu wasiokwenda mbinguni. Je, kila mtu atakwenda mbinguni?
- Soma Ufunuo 20:5. Je, kuna ufufuo wa aina ngapi? (Zaidi ya mmoja! Mafungu haya yanatuambia kwamba kuna ufufuo wa aina mbili. Ujio wa Yesu Mara ya Pili unawakilisha ufufuo wa mara ya kwanza – ule wa wenye haki. Ufufuo wa pili ni wa waovu. Kidokezo: Utahitaji kuwa sehemu ya ufufuo wa kwanza!)
- Soma Ufunuo 19:11-16, Ufunuo 14:14-20 na Ufunuo 6:15-17. Je, hiki ndicho unachokisubiria? Juma lililopita tulijadili kuhusu uzoefu wa furaha kuu tunaponyakuliwa mawinguni ili kumlaki Yesu. Je, kwenye mafungu haya tunasoma nini kuhusiana na jambo hili? (Katika ujio wa Mara ya Pili, Yesu anawakusanya wenye haki, waliokufa na walio hai, na kisha anawaangamiza waovu walio hai.)
- Soma Ufunuo 19:17-21. Je, nini kitawatokea maadui wa Mungu wakati wa ujio wa Mara ya Pili? (Huu ni uthibitisho zaidi kwamba wataangamizwa.)
- Je, unafurahia unapoyaona mambo haya? (Je, ni vitabu vingapi na sinema ngapi tulizozitazama ambapo “watu wazuri” wanaandamwa na kutishiwa na “watu wabaya,” na ghafla shujaa anawasili kuwaokoa watu wazuri na kuwaondosha watu wabaya? Hii inaashiria kwamba wenye haki watakuwa kwenye matatizo makubwa kabla tu ya ujio wa Mara ya Pili. Yesu, Shujaa wetu, anakuja na Kalwari kisha anatuokoa! Furaha ya ajabu namna gani! Afueni nzuri ajabu!)
- Wakati huo huo, suala hili linaonekana kuwa la ajabu kidogo. Kama Yesu anakuja kama mwivi wakati wa usiku (1 Wathesalonike 5:2, 2 Petro 3:10), ni kwa vipi kwamba Yesu ana jeshi la adui linalosubiri kumshambulia? (Vipi kama jeshi hili kiukweli limekusanyika ili kuwaangamiza watakatifu wa duniani, na Bwana wetu anakuja kutuokoa? Tatizo ni kwamba kifungu kinasema kuwa “wamekusanyika kufanya vita dhidi ya [Yesu].” Ufunuo 12:17 inatuambia kwamba joka linafanya vita dhidi ya watakatifu. Kufanya vita kwa wafuasi wa Mungu inaweza kuchukuliwa kama kufanya vita na Yesu.)
- Soma 1 Wathesalonike 4:16-18. Je, ni kitu gani kinachoelezewa hapa? (Ujio wa Yesu Mara ya Pili.)
- Kituo cha Kwanza: Mbingu
- Soma Ufunuo 20:1-3. Je, hukumu ya Shetani ni ipi? (Miaka elfu moja!)
- Je, Shetani atamdanganya nani? (Hana wa kumdanganya. Waovu wote watakuwa wamekufa.)
- Soma Ufunuo 20:4-5. Je, wenye haki wamekwenda wapi? (Wamekwenda mbinguni. Hapa tunayo “taswira pana” kwamba katika ujio wa Mara ya Pili, wenye haki watachukuliwa mbinguni, na waovu watauawa.)
- Soma Ufunuo 20:11-14. Je, msingi wa hukumu ni upi? Je, unategemea kama umeokolewa au hujaokolewa? (Jambo hili ni la muhimu sana. Wale waliopotea wanahukumiwa kwa matendo yao. Wale waliookolewa majina yao yameandikwa kwenye Kitabu cha Uzima. Hii ni neema! Unapotubu na kumtegemea Yesu, jina lako linaandikwa kwenye Kitabu cha Uzima. Ukiyategemea matendo yako mwenyewe kwa ajili ya kupata wokovu, utahukumiwa kwa matendo hayo!)
- Je, wenye haki wanafanya nini mbinguni? (Soma 1 Wakorintho 6:2. Mafungu katika kitabu cha Ufunuo yakiunganishwa na kauli ya Paulo hapa, yanaashiria kwamba wenye haki angalao watatumia sehemu ya miaka yao elfu moja wakiiangalia hukumu iliyofanywa kwa waliopotea.)
- Kwa nini Mungu awaruhusu wafanye hivyo? (Mungu ni muwazi kwenye hukumu zake. Mungu anataka tuufurahie uamuzi wake. Anataka tufahamu ya kwamba yeye ni zaidi ya mwenye haki. Fikiria kama mmojawapo wa wapendwa wetu amepotea. Mungu anataka tukubaliane naye kwenye hukumu.)
- Je, ni sababu gani nyingine unazoweza kuzifikiria kwa Mungu kuturuhusu kuthibitisha hukumu yake? (Uzima wa milele unahitaji kutokuwa na dhambi. Milele zote tunahitajika kushawishika kuhusu kosa la dhambi.)
- Kwa nini Mungu awaruhusu wafanye hivyo? (Mungu ni muwazi kwenye hukumu zake. Mungu anataka tuufurahie uamuzi wake. Anataka tufahamu ya kwamba yeye ni zaidi ya mwenye haki. Fikiria kama mmojawapo wa wapendwa wetu amepotea. Mungu anataka tukubaliane naye kwenye hukumu.)
- Je, wenye haki wanafanya nini mbinguni? (Soma 1 Wakorintho 6:2. Mafungu katika kitabu cha Ufunuo yakiunganishwa na kauli ya Paulo hapa, yanaashiria kwamba wenye haki angalao watatumia sehemu ya miaka yao elfu moja wakiiangalia hukumu iliyofanywa kwa waliopotea.)
- Soma Ufunuo 20:1-3. Je, hukumu ya Shetani ni ipi? (Miaka elfu moja!)
- Kituo cha Pili: Dunia Iliyofanywa Upya
- Soma Ufunuo 21:1-4. Baada ya miaka elfu, je, watakatifu wanaelekea wapi? (Yerusalemu mpya inashuka duniani. Huu unapaswa kuwa uhamishwaji mwepesi, kwa sababu wakati huo huo wanahamisha majengo ya Mji wangu Mpya wa Yerusalemu! Sipaswi kufungasha mizigo yangu, lakini huenda nitapaswa kuhamisha picha zilizopo ukutani.)
- Soma Ufunuo 20:5 na Ufunuo 20:7-9. Angalia kwa makini Ufunuo 20:9. Je, huu ni mji gani? Je, hii inaashiria nini? (Ufufuo wa pili wa waovu hutokea baada ya miaka elfu moja. Waovu wanafufuliwa. Shetani anafunguliwa. Wanaizunguka Yerusalumu Mpya mara ya mwisho wakiwa na tamaa ya kushinda pambano kati ya wema na uovu.)
- Hebu tutafakari jambo hili kwa dhati. Kwanza, je, hii inatuambia nini kuhusu Shetani? Alikuwa na miaka elfu moja ya kutafakari dhambi zake. Je, angepaswa kuhitimisha jambo gani? (Hii inaonyesha kwamba Shetani ni mgumu sana. Yeye ni mpinzani mkali sana wa Yesu.)
- Waovu tayari wamekwishakufa. Kwa nini Yesu awafufue ili wauawe tena? (Angalia tena watakatifu walio na marafiki na wanafamilia ambao hawakuokolewa. Awali tuliona kwamba Yesu anawaruhusu watakatifu kupitia kumbukumbu, na kisha kuwa na hitimisho lao wenyewe kuhusu hukumu yake. Fikiria jinsi ambavyo hukumu hiyo inavyokaziwa ambavyo marafiki na wanafamilia waliopotea wanavyojaribu kuishambulia Yerusalemu? Wanajaribu kuwashambulia watakatifu.)
- Je, hii inasema nini kuhusu waliopotea? Je, hii inasema nini kuhusu Bwana wetu? (Inatuonyesha kwamba Bwana wetu ni zaidi ya mwenye haki. Anajali mawazo yetu kuhusu hukumu yake.)
- Soma Ufunuo 20:10. Je, hatma ya mwisho ya Shetani ni ipi?
- Je, uasi ulioelezewa katika Ufunuo 10:9 unatendaje kazi kwa waovu? (Moto unashuka kutoka mbinguni na kuwaangamiza.)
- Soma Ufunuo 21:1. Je, kuna sifa gani ya msingi kwa nchi iliyofanywa upya? (Haina bahari.)
- Kwa nini bahari inaondolewa? (Bahari inachukua asilimia 71 ya uso wa dunia. Nadhani mabara yatapanuka ili kuchukua nafasi iliyochukuliwa na bahari. Hii itaruhusu nafasi ya watu wengi zaidi.)
- Soma Ufunuo 21:2-3. Kwa nini tupelekwe kwenye hii dunia ya kale (mpya)? Kwa nini Mungu anahamishia ufalme wake hapa? (Hili ni tukio la ushindi mkuu wa Mungu dhidi ya dhambi. Hiki ndicho kiini cha pambano.)
- Je, tutatambua sehemu mbalimbali hapa duniani? (Nadhani. Kama Mungu atabadili kila kitu, kwa nini aonyeshe hatma ya bahari tu? Kwa nini aiite “nchi mpya” – kwa kutumia sehemu ya jina la zamani? Kama vile tutakavyokuwa wapya tena tulioboreshwa lakini bado tukiendelea kutambulika (angalia Mathayo 8:11, 1 Wakorintho 13:12), nadhani dunia itakuwa mpya, iliyoboreshwa na bado ikiendelea kutambulika.)
- Soma Ufunuo 21:3-4. Je, Mungu anatutendea nini? (Anafuta kila chozi!)
- Mambo mabaya yanapotutokea duniani, je, Mungu anajali? (Mchezo wake wa mwisho ni kuyachukua maombolezo, vilio na maumivu yote! Hilo ndilo lengo la Mungu.)
- Soma Ufunuo 22:1-5. Je, hii inaashiria nini kuhusu maisha katika dunia itakayofanywa upya? (Mwanzo 1:26 inatuambia kwamba tuliumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Hitimisho lenye mantiki ni kwamba miili yetu mipya katika nchi mpya inafanana “kwa sura na mfano” wa miili yetu ya sasa katika dunia ya zamani. Tutaona miti, mito, mazao, matunda, matawi na mwanga katika Yerusalemu Mpya. Fikiria jinsi ambavyo simu za kwanza za ajabu tena zisizo imara zinavyofanana na simu zetu za kisasa za siku hizi. Mtumiaji wa simu ya zamani atashangazwa na simu ya kisasa, lakini haitamchukua muda mrefu kufahamu jinsi zinavyofanana. Nadhani kwa namna isiyo nzuri sana hii inaelezea asili ya nchi mpya.)
- Rafiki, vipi kuhusu wewe? Je, ungependa kuutumia umilele katika dunia iliyoboreshwa kwa mapana yake? Je, ungependa kuwa huru dhidi ya wasiwasi wote kuhusu wanafamilia na marafiki? Nadhani uchaguzi uko wazi. Tunaye adui ambaye, hata baada ya miaka elfu moja ya kutafakari, anataka kumwangamiza Mungu na kutuangamiza sisi. Wale wanaomfuata Shetani wana lengo moja pamoja naye. Uchaguzi uko wazi. Kwa nini usiufanye uchaguzi huo sasa hivi?
- Juma lijalo: Tutaanza somo kuhusu umuhimu wa imani yetu katika Uumbaji. Hili ni somo la muhimu sana, kwa hiyo tafadhali tufuatane pamoja!
