Bwana wa Mataifa Yote (Amosi)

(Amosi 1-2)
Swahili
Year: 
2013
Quarter: 
2
Lesson Number: 
4

Utangulizi: Wanangu walipokuwa wadogo sana nilikuwa nikicheza nao mchezo ulioitwa “Unguruma.” Nilikuwa nikijificha na kisha niliunguruma kama simba. (Kwa kiasi fulani hivi niliunguruma kama simba.) Kisha watoto walijaribu kubaini mahali nilipokuwa nimejificha. Kwa kuwa uwezo wao wa kutambua uelekeo wa sauti haukuwa mzuri sana, matokeo yake yalikuwa yanachekesha sana. Nilikuwa karibu nao sana, halafu nikawa naunguruma, na wao walikuwa wakikimbia upande tofauti na ule ambao sauti ilikuwa ikitokea. Somo letu juma hili linahusu Mungu “kuungurumisha” ujumbe wake kwa wapagani na wafuasi wake. Je, sisi ni kama watoto, tusioelewa uelekeo wa Mungu? Je, tunashindwa kufuata maelekezo yake maishani mwetu? Je, sisi ni “viziwi wa sauti” ya muungurumo wa Mungu? Hebu tukimbilie kwenye somo letu la kitabu cha Amosi na tuone kile tunachoweza kujifunza!

  1. Muungurumo wa Kwanza
    1. Soma Amosi 1:1-2. Utangulizi fulani ni wa msingi sana hapa. Taifa kubwa lililojengwa na Mfalme Daudi na Mfalme Sulemani linagawanyika. Kati ya makabila kumi na mawili, makabila kumi ya kaskazini yanajitenga na taifa kwa sababu ya utozaji mkubwa sana wa kodi uliopita kiasi. Ufalme wa Kaskazini uliitwa Israeli na mataifa mawili yaliyosalia yalikuwa ni ya Yuda. Yerusalemu ilikuwa ndani ya utawala wa Yuda, kwa hiyo ilisalia kuwa kiini cha ibada. Hili lilikuwa ni tatizo kwa Israeli, kwa hiyo ilitenga vituo vyake viwili kwa ajili ya ibada. Amosi ni mchungaji anayeishi Yuda.
      1. Je, Amosi anafikisha ujumbe wa Mungu kwa nani? (Kwa Israeli.)
        1. Je, jambo hilo linaibua mambo gani akilini mwako? (“Mgeni” anatuambia cha kufanya! Tumechoka kwa ufalme wa kusini kutuambia mambo ya kufanya kuhusiana na kodi. Sasa wanamtuma mchungaji ili atuambia cha kufanya!)
      2. Je, Mungu anaunguruma na kutoa radi kutokea wapi? (Kutoka Yerusalemu.)
        1. Je, suala hilo linaibua jambo gani akilini mwako? (Hii inaashiria kwamba maeneo yetu mbadala kwa ajili ya ibada hayakubaliki. Hili ni shambulio jingine kwenye uamuzi wetu.)
      3. Je, ukweli kwamba ujumbe wa Mungu unalinganishwa na muungurumo na radi inaashiria nini? (Mungu anaonekana kutofurahia. Anataka ujumbe huu upenye na kuwafikia watu.)
    2. Soma Amosi 1:3-4. Je, kuna kitu gani cha kushangaza katika huu ujumbe wa kwanza? Je, Dameski iko upande gani? (Dameski inapatikana Syria. Ujumbe huu hauihusu Israeli.)
      1. Gileadi ilikuwa ni nchi ya watu wa Mungu. Je, unadhani Mungu anamaanisha nini kwa kusema “kuipura Gileadi kwa vyombo vya kupuria vya chuma?” (Maneno ya Kiingereza “sled” (au sleji kwa Kiswahili) – likimaanisha sleji inayokokotwa na farasi na “Sleigh” (pia sleji kwa Kiswahili) – likimaanisha kitoroli cha kuteleza juu ya theluji, yote mawili yanafananishwa na neno “sledge.” Hicho ni kifaa kisicho na magurudumu kinachovutwa ardhini. Taswira ninayoipata ni kifaa cha chuma kinachonata chini kwenye jukwaa la mbao. Fikiria kuvuta kifaa hicho kwenye miili ya watu.)
        1. Je, unaweza kuelezeaje jambo hilo kwa kutumia maneno ya siku hizi? (Kwa hakika alinichana chana sana! Inamaanisha unyanyasaji wa hali ya juu.)
      2. Je, kuna somo gani hapa la kujifunza? (Mungu anajali jinsi watu wake wanavyotendewa. Mungu atalipiza.)
      3. Unafikiria nini kuhusu aina hiyo ya “muungurumo?” (Ni habari njema!)
  2. Muungurumo wa Pili
    1. Soma Amosi 1:6-7. Je, Gaza ni kitu gani? (Ni nchi ya Wafilisti.)
      1. Hapo kabla hatukutoa maoni kwenye maneno “kwa makosa matatu…naam hata makosa manne.” Je, hiyo inamaanisha nini? (Mungu haadhibu dhambi moja au mbili. Watu hawa wanarudiarudia dhambi iliyotajwa.)
      2. Je, ni dhambi gani inayohusika hapa? (Bishara ya kusafirisha watu. Utumwa. Wafilisti waliwachukua watu wa Mungu na kuwauza Edomu. Maoni ya Jamieson, Fausset na Brown yaliwaita Waedomu kuwa ni “maaduni hatari sana wa Yuda.”)
      3. Je, tunapata somo gani hapo hivi leo? (Biashara ya usafirishaji wa watu ni suala linalosumbua sana hivi leo. Zaidi ya biashara ya kusafirisha watu, suala hili litakemea kutomtendea vibaya mtu yeyote, kukiuka matakwa yao huru.)
      4. Je, watu wa Mungu wanauchukuliaje huu muungurumo? (Wanaufurahia. Ni muungurumo mzuri!)
  3. . Muungurumo wa Ndani kwa Ndani
    1. Tumeangalia miungurumo miwili ya kwanza. Kuna miungurumo mingine mitano, kwa ujumla ipo saba, inayoelekezwa dhidi ya dhambi za mataifa ya kipagani yalioyoishi karibu na watu wa Mungu. Miungurumo hii kwa kawaida ilikabiliana na dhambi zilizojipenyeza dhidi ya watu wa Mungu. Soma Amosi 2:4-5. Je, muungurumo huu unaelekezwa kwa nani? (Yuda! Watu wa Mungu. Watu wa Amosi.)
      1. Je, dhambi zao ni zipi? (Kuikataa sheria ya Mungu na kuifuata miungu ya uongo.)
      2. Kwa miaka mingi nimekuwa nikishangaa “ibada ya sanamu.” Hakuna mtu niliyemfahamu aliabudu sanamu. Ni kwa jinsi gani kampeni ya Shetani yenye historia ya mafanikio ipotee kirahisi namna hiyo?
        1. Watu walisema kwamba kuwa na gari zuri au nyumba nzuri ni “kuabudu sanamu,” lakini nilifahamu kwamba kauli hiyo haina maana kwa sababu hakuna aliyefikiria kwamba gari au nyumba yake ilikuwa ni mungu. Je, wewe unafikirije?
      3. Je, kiini cha ibada ya sanamu kinachomfanya Mungu kutokuwa na furaha ni kipi? (Kukitegemea kitu tulichokitengeneza badala ya kumtegemea yeye.)
        1. Yaangalie maisha yako. Je, ni kitu gani unachokitegemea (au unachoweza kukitegemea) badala ya kumtegemea Mungu? (Upendeleo wa bosi wako, umahiri wako, elimu yako, fedha zako, nafasi yako, mwonekano wako mzuri, haiba yako. Biblia inatufundisha kuwa waajiriwa wazuri, sio kuwakosoa mabosi wetu, kuwa wenye busara, wataratibu na kuwa na ustadi/umahiri wa kazi. Tatizo ni pale tunapoyategemea mambo haya
          1. Je, maisha yako yangebadilikaje kama kweli kwa dhati kabisa ungemtumainia Mungu? (Ni ukombozi!)
  4. Muungurumo wa Israeli
    1. Soma Amosi 2:6. Je, mlengwa wa huu muungurumo ni nani? (Israeli! Hebu ngoja nikupe chimbuko zaidi. Makabila kumi ya kaskazini yaliyoijumuisha Israeli yamefanya vizuri sana. Yamelipanua taifa hadi karibia na siku za Mfalme Daudi na Sulemani. Wamefanikiwa na kuridhika na mfumo wao mbadala wa kidini.)
      1. Je, ni nani anayeuzwa? (Wenye haki na wahitaji.)
      2. Hili ni kundi la ajabu sana. Unadhani kuwauza wenye haki inamaanisha nini? (Hii inaonekana kama rushwa. Mtu asiye na haki anamlipa hakimu ili kununua hukumu ya upendeleo dhidi ya mtu mwenye haki.)
      3. Vipi kuhusu kuwauza wahitaji? Je, hiyo inamaanisha nini? (Soma Mambo ya Walawi 25:39-41. Inamaanisha kwamba watu wanajiuza kwa ujira mdogo kuliko inavyostahili.)
        1. Je, utatumiaje maishani jambo hilo hivi leo? (Usiwachukulie wahitaji kwa manufaa yako.)
    2. Soma Amosi 2:7. Je, “kutweta mavumbi yaliyo juu ya vichwa” vya maskini inamaanisha nini? Je, unadhani kuwa kimsingi wanatembea juu ya vichwa vyao? (Rejea hii ya kuikana haki na “vichwa” inaashiria kwamba maskini wanakatishwa tamaa kwa haki wanayoikosa kabisa au wanayoipata lakini kidogo sana. Badala ya kutiwa moyo kwamba wanaweza kufanya vizuri zaidi, maskini wanafanywa kuamini kwamba watakuwa masikini milele.)
      1. Kwa nini Mungu anasema kwamba jina lake takatifu linatiwa unajisi kwa uchafu wa ngono? (Mungu ni mtakatifu. Anaichukulia sheria yake kwa makini sana kwa sababu inaakisi tabia yake. Kwa hiyo, dhambi ni kosa mbele zake.)
      2. Maoni ya J.A. Motyer’s kuhusu kauli ya “baba na mwana kumwendea mwanamke mmoja,” ni kwamba Amosi hajadili kuhusu upotovu wa familia, badala yake anaelezea mfumo wa makahaba wa hekaluni. Israeli, kama majirani zake wa kipagani, ilijumuisha ngono kama sehemu ya huduma yake ya ibada. “Kuabudu” kwa kufanya ngono na hawa “wanawake watakatifu” kulikiuka amri za wazi kabisa za Mungu kwa watu wake.
    3. Soma Amosi 2:8. Je, dhambi hii inafanyikia wapi? (Kwenye sehemu ya ibada.)
      1. Soma Kumbukumbu la Torati 24:12-13 na Kutoka 22:25-27. Je, hawa wakopeshaji wanapaswa kulalia mavazi yaliyowekwa rehani? (Hapana. Mungu anasema rejesha mavazi kwa wakopeshwaji kabla ya jioni.)
      2. Je, hili ni suala tu la kushindwa kufuata kanuni za Mungu kuhusu mikopo? Je, huku ni kushindwa kufuata taratibu? Au, je, kuna jambo la dhati zaidi linahusika? (Hii ni neema. Watu wanakwenda hekaluni kupokea msamaha wa dhambi. Wazo asilia la makabila kumi kutenga eneo lao kwa ajili ya ibada ilikuwa ni kumwabudu Mungu wa kweli. Dhambi ilisamehewa hekaluni. Neema ilitolewa. Watu hawa sasa wanalala hekaluni kwenye mavazi yasiyoonesha neema kwa watu wengine.)
        1. Je, jambo hilo linatumikaje maishani mwetu hivi leo?
    4. Rafiki, tunafurahia tunapowaona watu wengine “wanapata kile wanachostahili.” Je, umeyachunguza maisha yako kwa dhati kabisa? Je, umefikiria jinsi dhambi yako inavyomchukiza/inavyomkosea Mungu? Je, umeangalia kwamba hukumu sio kwa watu wengine tu? Yesu anatupatia wokovu kwa njia ya neema pekee. Je, utadhamiria hivi leo kuiheshimu sheria ya Mungu na kuonesha neema kwa watu wengine kama vile Mungu anavyoonesha neema kwako?
  5. Juma lijalo: Mtafute Bwana ili Uishi! (Amosi)