Matengenezo: Kuwa na Fikra Mpya

(Warumi 12, 1 Wakorintho 10)
Swahili
Year: 
2013
Quarter: 
3
Lesson Number: 
11

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: “Takataka ziingiazo ndizo takataka zitokazo,” ndicho wakisemacho watu katika dunia ya teknolojia. Je, kauli hiyo ni ya kweli pia linapokuja suala la akili (mawazo) zetu? Dunia iliyojaa uburudishaji inapima kile kinachostahili kuingia akilini mwetu kwa kuangalia umri. Dhana yake ni kwamba umri huleta tofauti; akili zilizozeeka sio rahisi sana kushawishiwa kuingia kwenye ushawishi mbaya. Je, hiyo ni kweli? Kusema kweli, nadhani kauli ya takataka ziingiazo ndizo takataka zitokazo inahusika katika umri wowote kwa sababu watu wa rika zote hupata ushawishi kutoka kwa wale wanaowazunguka. Hebu jiulize, je, unatumia ishara ambazo marafiki wako wanazitumia? Ninaye rafiki wa siku nyingi ambaye hurejea mambo yote madogo madogo kama “featurette” (yaani sinema fupi). Kutokana na maneno hayo ya rafiki wangu, mimi pamoja na mke wangu huwa tunairejea “sinema fupi” mara kwa mara. Hebu tuzame kwenye somo letu ili tuone kile Biblia inachofundisha kuhusumawazo (akili) yetu!

  1.  Ibada Hekaluni
    
    1. Soma Warumi 12:1-2. Je, unakumbuka kuwa majuma mawili yaliyopita tulijifunza (kutoka 1 Wakorintho 3:16) kwamba miili yetu ni hekalu ambamo Roho Mtakatifu anaishi? Je, Warumi 12 inasema nini kuhusu miili yetu? (Inasema kuwa miili yetu ni dhabihu iliyo hai.)
      1. Ninapoifikiria “dhabihu” huwa ninafikiria kitu kinachounguzwa au kinachotolewa. Je, unadhani ni dhabihu gani ya mwili inayomaanishwa hapa? (Nikimruhusu mtu mwingine aishi kwenye nyumba yangu, ninaweza kusema kwamba nimeitoa nyumba yangu sadaka. Wazo lililopo ni kuwa tunaitoa miili yetu kwa Mungu.)
      2. Utabaini kwamba hii inaitwa “tendo la kiroho la ibada.” Ibada hii ikoje? (Tunapoabudu, tunampa Mungu utukufu. Dhana iliyopo ni kwamba kwa kuitoa miili yetu kwa Mungu tunampa utukufu.)
      3. Je, ni sehemu gani mahsusi ya mwili inayotajwa? (Akili [ubongo].)
        1. Kwa nini sehemu hii inabainishwa, na si sehemu nyinginezo? (Hili ni wazo la hekalu tulilolijadili majuma mawili yaliyopita. Kumjua Mungu ni kumruhusu Roho wake Mtakatifu aishi ndani yetu.)
      4. Je, lengo la kumpa Mungu mawazo (akili) yetu ni lipi? (Badiliko. Kumpa Mungu mamlaka juu ya mawazo yetu kutayafanya mawazo kuwa mapya ili tuweze kubadilishwa na kuachana na fikra za kidunia.)
        1. Je, kuna ukomo wa umri katika jambo hili? (Haukubainishwa!)
      5. Je, badiliko la mawazo yetu litatufanyia jambo gani? (Tutaweza kuyapima kwa usahihi kabisa mapenzi ya Mungu kwa ajili yetu.)
        1. Je, hii inaashiria nini juu ya kutokuwa na Roho Mtakatifu ayafanyaye upya mawazo yetu? (Hatuwezi kuyaelewa mapenzi ya Mungu.)
    2. Hebu tujaribu hili wazo kwamba Roho Mtakatifu huleta badiliko mawazoni mwetu linalotusaidia kuyajua mapenzi ya Mungu. Kwenye suala la dhambi, je, mara nyingine huwa huna uhakika? Je, unao huu mjadala mawazoni mwako kuhusu kama jambo fulani ni dhambi, ni wazo baya tu, au jambo lisilo na maana yoyote?
      1. Je, umewahi kuwa kwenye kikao cha kanisa, au ukijifunza Biblia, au kwa namna fulani ukijihusisha kwenye jambo ambalo yumkini Roho Mtakatifu yupo kwa uwezo mkuu, na mara ukawa na mguso madhubuti kuhusu mjadala mawazoni mwako juu ya dhambi?
        1. Je, mguso madhubuti unapotea unapokuwa kwenye jaribu?
      2. Maswali haya yanaakisi kile kinachonitokea. Kama unao uzoefu kama huo, nadhani tunaweza kuanza kuona umuhimu wa kuyatoa mawazo yetu (hekalu letu) kwa Mungu ili tuweze kuwa na hili badiliko na kuyafahamu mapenzi ya Mungu vizuri zaidi.
  2. “The Offer”
    1. Hilo bado linatuacha na swali la jinsi ambavyo hii “offer” ya kuyatoa mawazo yetu kuwa dhambihu inavyofanya kazi kivitendo. Kwa kiwango cha chini kabisa, inaonekana kuwa mara kwa mara tunahitajika kumkaribisha Roho Mtakatifu kuongoza fikra zetu ili tuweze kufanya maamuzo sahihi kuhusu dhambi. Je, inaweza kumaanisha nini kingine tofauti na hivyo?
    2. Soma 1 Wakorintho 10:1. Je, inamaanisha nini kwamba watu walikuwa “chini ya wingu” na “wakapita kati ya bahari?” (Wote walifuata maelekezo ya Mungu alipowaelekeza kwenda, na wote walinufaika na ulinzi wa Mungu. Walikuwa sehemu ya “kundi la Mungu.”)
    3. Soma 1 Wakorintho 10:2. Je, inamaanisha nini “kubatizwa wawe wa Musa?” (Nadhani inamaanisha kuwa walijitoa kwa Musa. Musa aliwaongoza kupita baharini (Kutoka 14). Alizungumza na Mungu mawinguni (Kutoka 34:29). Alikuwa kiungo kati ya watu na Mungu.)
    4. Soma 1 Wakorintho 10:3-4. Je, ni kwa jinsi gani chakula na kinywaji chao kilikuwa cha “kiroho?” (Kilitolewa na Mungu. Mana ilishuka kimaajabu (Kutoka 16), kama ilivyokuwa kwa maji kutoka mwambani (Kutoka 17).)
    5. Soma 1 Wakorintho 10:5. Je, Paulo anajenga dhana gani kwa kauli ya “maana (hata hivyo)?” (Uzoefu huu kati ya Mungu na watu haukuwapatanisha na Mungu. Hawakuwa “offer” ya mawazo.)
      1. Je, unayatumiaje mafungu haya maishani mwako? (Kuendana na watu wa Mungu, kuwa na kiongozi wa Kimungu, kula na kunnywa vitu sahihi, vyote hivyo sio kanuni ya kumpendeza Mungu. Vyote hivyo sio “offer.”
    6. Soma 1 Wakorintho 10:6. Je, kanuni ya kumpendeza Mungu ni ipi? (Kuiweka mioyo/mawazo yetu kwa Mungu na sio kuyaweka juu ya mambo maovu.)
      1. Paulo anaporejea jambo hili kuwa “mfano,” je, anamaanisha nini? (Somo hilo ni kwa ajili yetu!)
      2. Tukichukulia kile tulichokisoma, je, kitu gani kilicho cha muhimu na kisicho cha muhimu linapokuja suala la kutoa dhabihu zetu “zilizo hai?” (Unaweza kujivika kwa mambo ya nje – kanisa, matendo yako, chakula chako, lakini hicho sicho cha msingi kwa Mungu. Anachokijali Mungu ni mtazamo wa mioyo na mawazo yetu.)
    7. Hebu tuchimbue zaidi hapa, kwa sababu tunataka kuwa na uhakika kuwa tunalielewa jambo hili kwa usahihi. Soma 1 Wakorintho 10:7. Je, ni uovu gani wa kwanza ambao watu hawa wameiweka mioyo yao juu yake? (Kutomtumaini Mungu. Walitengeneza ndama wa dhahabu na wakaihusianisha na uwezo wa Mungu. (Kutoka 32).)
      1. Hapo kabla tuliona kuwa “kufuata maelekezo ya Mungu” haikuwa mojawapo ya mambo ya msingi. Je, unatofautishaje jambo hilo na hili? (Watu walifuata maelekezo ya jumla ya wingu, kinyume na kumtegemea Mungu. Kama kweli ulidhani kuwa Mungu mkuu wa Mbinguni alikuwa akiyaongoza mapito yako, kwa nini uabudu kitu ulichokitengeneza?)
    8. Soma 1 Wakorintho 10:8. Je, uasherati unaendanaje na orodha ya “dhabihu?” (Hauonekani kuendana na dhabihu. Hadi kufikia hapa, tumeonekana kutofautisha kati ya matendo yetu na imani yetu.)
      1. Hebu tuchambue kisa hiki. Soma Hesabu 25:1-3. Je, kiini cha hii dhambi ni kipi? (Uabudu wa miungu ndio ulikuwa mzizi wa tatizo.)
      2. Hata hivyo, hatuwezi kupuuzia kwamba Paulo kwa mahsusi kabisa anataja dhambi ya zinaa. Je, dhambi za uzinzi zipo kwenye kundi maalum? (Soma 1 Wakorintho 6:18-20. Paulo anatuambia kuwa dhambi za zinaa zipo kwenye kundi maalum kwa sababu zinaushambulia mwili, ambao ni hekalu la Roho Mtakatifu.)
    9. Soma 1 Wakorintho 10:9-10. Rejea ya “nyoka” inarejea Hesabu 21 ambapo watu “walizungumza kinyume na Mungu.” Hapa tatizo ni kumnung’unikia na kumlalamikia Mungu. Je, mtazamo huo unaendana na kuyatoa mawazo yetu dhabihu kwa Mungu? (Ndiyo na hapana. Hapana, kwa sababu Paulo anatuonya kuhusu huu mtazamo. Lakini, kumlalamikia Mungu bado kunamweka Mungu katika kiti chake cha enzi kama Yeye aliye mtawala na anaweza kubadili mambo. Nadhani Mungu anachukulia malalamiko dhidi yake kuwa kitu cha juu kuliko uabuduji wa sanamu – ambapo tunampuuzia Mungu. Kama unatilia shaka jambo hili, fikiria kisa cha Ayubu.)
  3. . Ushauri kwa Vitendo
    1. Hebu turuke mafungu kadhaa na tusome 1 Wakorintho 10:18-20. Je, hapa tatizo ni lipi? (Kushirikiana na mashetani.)
      1. Hatuna dhabihu za mashetani katika eneo ninaloishi. Je, bado huu ushauri ni wa muhimu?
    2. Soma 1 Wakorintho 10:21. Je, tunaweza kuweka mguu mmoja katika kambi ya Mungu na mguu mwingine katika kambi ya mwovu? (Hapana.)
      1. Je, inamaanisha nini “kukinywea kikombe cha mashetani” leo? (Shetani anazipatia akili zetu mambo mengi ili tuweze kushirikiana naye. Sehemu ya msingi ya kuyatoa mawazo yetu dhabihu kwa Mungu ni kuepuka kukinywea kikombe cha Shetani. Nadhani tunakinywea kikombe cha Shetani kila tunapoziweka akilini mwetu njia zake – bila kujalisha umri wetu.)
    3. Rafiki, je, unayatoa mawazo yako yawe dhabihu kwa Yesu? Au, je, unakunywa kutoka kwenye maburudisho na falsafa za Shetani? Pambano lipo akilini. Jiulize kama unatumia muda mwingi kunywa kutoka kwenye chemchemi ya Roho Mtakatifu au chemchimi ya dhambi? Kwa nini usidhamirie leo kuyaweka mawazo yako kwenye mambo ambayo Roho Mtakatifu anayatamania?
  4. Juma lijalo: Matengenezo: Kuponya Mahusiano Yaliyovunjika.