Kristo, Sheria na Injil
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Bila kujali kama mtu amekuambia siri, au kama una maarifa au ujuzi wa pekee, unajisikia kuwa mtu wa pekee sana pale unapokuwa unafahamu mambo ambayo watu wengine hawayafahamu. Baadhi ya siri hazipaswi kusemwa, lakini kushiriki maarifa au ujuzi wako na watu wengine ni mojawapo ya mibaraka mikubwa sana maishani. Unakuwa na uwezo wa kuboresha maisha ya watu wengine kwa kuwafundisha mambo ya muhimu wasiyoyafahamu. Injili inafanishwa hivyo. Mungu anakupatia ujumbe wake. Baraka iliyoje kushiriki na watu wengine habari za uzima wa milele! Baadhi ya ujumbe unaeleweka bila ya msaada wako kuhitajika, lakini watu wengine wanategemea ufafanuzi wako. Hebu tupitie somo letu la Biblia ili tujifunze zaidi juu ya kushiriki watu wengine na masuala ya sheria na injili!
- Kufundisha Sheria za Asili na Sheria sza Maadili
- Soma Warumi 1:16-17. Kwa nini suala la kuionea haya injili lilijitokeza mawazoni mwa Paulo? Kwa nini anaona hitaji la kupinga kwamba injili si jambo la kuonea haya? (Mungu wetu alikuja duniani na kuishi kama mwanadamu. Alikufa kama mhalifu mikononi mwa serikali. Mungu wetu alijitoa mwenyewe ili sisi tuweze kuishi. Kwa mungu, jambo hili linahitaji ufafanuzi ili kuweza kuwasaidia watu wengine waweze kuelewa.)
- Kuna jambo gani jingine lisilo la kawaida kuhusu imani yetu? (Kuhesabiwa kwetu haki kunatokana na imani, sio matendo. Siwezi kuzungumzia juu ya tamaduni zote, lakini utamaduni wa eneo langu unaamini kwamba kufanya kazi ni muhimu kwa ajili ya kupata mafanikio. Baba yangu alinifundisha kufanya kazi kwa bidii na kwa ubora wa hali ya juu kuliko watu wanaonizunguka. Kwa hiyo, kazi ni sehemu ya mtazamo wangu wa msingi maishani.)
- Tunaweza kuhitimisha nini kutokana na mawazo mawili tuliyoyajadili? (Tuna imani za dini zisizo za kawaida. Mungu wetu ni mwenye kujitoa nafsi. Kuhesabiwa kwetu haki hakubadili juhudi zetu katika kazi (matendo). Mambo haya ni kinyume kabisa na matarajio yetu.)
- Soma Warumi 1:18-20. Je, mafungu haya yanasema nini kuhusu mantiki, hisia za Mungu wetu? (Jambo hili linabainisha kwamba uwezo na asili ya Mungu vinaweza kuonekana kwa wazi katika mambo yanayowazunguka wanadamu. Wanadamu hawana kisingizio cha kumpuuzia Mungu.)
- Hebu tuangalie kidogo hizi dhana mbili. Paulo anasema kuwa uwezo na asili ya Mungu viko wazi na vinaeleweka kwa watu wote. Kwa upande mwingine, vipengele vingine vya namna ambayo Mungu anatenda kazi haviko wazi sana na havieleweki. Je, hii inazungumzia nini juu ya uhusiano kati ya sheria ya asili na sheria ya maadili? (Sehemu kubwa ya sheria ya asili inaweza kueleweka. Tunaiona ikitenda kazi kila siku. Lakini, uhusiano wa sheria ya asili na sheria yote ya maadili unaweza usiwe wazi sana.)
- Hebu tusome tena Warumi 1:16. Je, rejea ya “Myahudi” kwanza ikifuatiwa na “Mataifa” inaashiria nini? (Muktadha unahusu kuuamini ujumbe wa wokovu wetu. Wayahudi walikuwa wa kwanza kupewa huu ujumbe na sasa Mataifa wamepewa ujumbe huu.)
- Soma tena Warumi 1:18. Nani mwingine tena aliyepo? (Waipingao kweli.)
- Je, hii inaashiria nini kuhusu maisha yako? (Unaweza kuwa mpinga kweli badala ya kuwa mfundisha kweli.)
- Soma Kumbukumbu la Torati 30:15-18. Je, kuna chaguzi gani maishani? (Uzima na usitawi au kifo na aungamivu.)
- Soma Mathayo 7:24-27. Je, utii unaleta tofauti gani kwa namna ambayo maisha yako yanabadilika? (Kwa mara nyingine, hii ni ahadi na onyo. Kufuata sheria ya Mungu ya maadili huleta maisha bora.)
- Je, sisi sasa (Mataifa) ndio chanzo cha ujumbe wa Mungu kuhusu injili yake ulimwenguni? Je, umewekwa kuwa mwalimu wa kuifundisha kweli tofauti na kuwa mpingaji wa hiyo kweli?
- Ikiwa umesema, “Ndiyo, nitakuwa mwalimu wa ile kweli,” je, utaanzaje? (Nitaanza kwa jambo lililo wazi – uwezo na asili ya Mungu. Kisha nitaingia kwenye jambo lisilo wazi sana, Mungu aliyejitoa mwenyewe tunayemtumikia ambaye anatuokoa kwa neema yake.)
- Hebu tujadili maswali yanayotokea maishani kivitendo. Nakumbuka vikao vya kanisa ambapo swali lilikuwa ni kwamba “Kanisa letu linawezaje kushiriki kweli na majirani zetu?” Wengine walisema, “Hebu tushiriki nao kijitabu kinachohusu Sabato.” Wengine walitaka tuwapatie kitabu kikubwa kinachozungumzia historia ya pambano kati ya wema na uovu.” Bado wengine walitaka tuwapatie kitabu kinachohusu upendo wa Mungu. Angalia tena Mathayo 7:24-27 na Kumbukumbu la Torati 30:15. Je, mafungu haya yanashauri nini kuhusu njia zetu tutakazozitumia? (Mungu anatuajia kwa kusema kuwa anayo siri ya maisha bora. Anayo siri ya kuyajenga maisha yatakayokabiliana na dhoruba. Nadhani tunapaswa kutumia njia hiyo hiyo.)
- Soma Warumi 1:16-17. Kwa nini suala la kuionea haya injili lilijitokeza mawazoni mwa Paulo? Kwa nini anaona hitaji la kupinga kwamba injili si jambo la kuonea haya? (Mungu wetu alikuja duniani na kuishi kama mwanadamu. Alikufa kama mhalifu mikononi mwa serikali. Mungu wetu alijitoa mwenyewe ili sisi tuweze kuishi. Kwa mungu, jambo hili linahitaji ufafanuzi ili kuweza kuwasaidia watu wengine waweze kuelewa.)
- Mfano wa Yohana
- Soma Yohana 1:1-5. Yohana anaanzaje maelekezo yake kumhusu Yesu? (Anaanza na jambo la asili. Unauona uumbaji? Yesu ndiye aliyeufanya huo uumbaji.)
- Soma Yohana 1:10-11. Jambo gani lisilo wazi sana kumhusu Yesu? (Ulimwengu haukumtambua Yesu kama Muumba! “Walio wake,” yaani Wayahudi, hawakumpokea. Hawakuukubali ujumbe wake.)
- Soma Yohana 1:12-13. Yesu aliwaendea watu gani baada ya hapo? (“Wote waliompokea.”)
- Kuna siri gani ya pekee kuhusu kumpokea Yesu kama Muumba na Mwokozi? (Tunafanyika kuwa watoto wa Mungu!)
- Fikiria juu ya watoto wako. Je, unayafahamu matamanio makuu ya mtoto wako mawazoni mwako? (Ndiyo! Kwa kawaida kama wewe ni mzazi, basi ungependa kuwa mbaraka mkubwa kwa watoto wako. Huo ndio mtazamo wa Mungu dhidi yetu! Sifa kwake!)
- Soma Yohana 1:14. Je, hapa imani ya msingi ni ipi? (Mungu alifanyika mwanadamu na akakaa pamoja nasi.)
- Inamaanisha nini kusema kuwa Yesu alijaa “neema na kweli?” (Kimsingi, neema inairejea injili – kwamba Yesu aliishi, akafa na kufufuka tena ili kutuokoa kutoka dhambini na kutupatia ahadi ya uzima wa milele.)
- Je, sehemu ya “kweli” ya Yesu ni ipi? (Yesu alibainisha asili ya kweli ya Mungu.)
- Unaweza kuona kwamba Yohana anafuata mkondo ule ule tulioujadili hapo kabla? Unapotaka kushiriki ujumbe na watu wengine, anza na mambo yanayofahamika na watu wote, mambo yale yanayoakisi masuala ya asili na sheria ya asili. Kisha ingia kwenye mafundisho ambayo yako wazi kidogo, Mungu alifanyika kuwa mwanadamu na kufa ili kutupatia uzima wa milele.)
- Soma Yohana 1:16-17. Kwa nini mafungu yanasema kuwa torati ilitolewa “kwa mkono” wa Musa? (Mungu alimpatia Musa Amri Kumi. Kutoka 24:12. Hili halikuwa wazo la Musa.)
- Hebu turejee kwenye dhana zinazopatikana katika Kumbukumbu la Torati 30 na Mathayo 7. Mafungu haya yanaelezea jinsi utii unavyoyaboresha maisha yako. Je, hii ni sehemu ya kipengele cha “asili” cha ujumbe wa injili? Je, jambo hili linapaswa kuwa wazi kwa watu wote? (Ndiyo. Inapaswa kuwa wazi kwamba ukiepuka kufanya mauaji na wizi maisha yako yatakuwa bora.)
- Ikiwa Mungu ndiye Mwandishi wa Amri Kumi, nazo ni sehemu ya jambo lililo “wazi,” kinachofuata ni kwamba kuendana nazo kutaendana na huu mpango. Kwa mfano, ni kwa jinsi gani utaendana na Sabato (amri ya nne)? (Sitaanza kwa kusema kuwa “hivi ndivyo asemavyo Mungu,” badala yake nitasema kuwa “Je, maisha yako yatakuwa bora zaidi ikiwa utaacha kufanya kazi na kutenga siku moja ya juma kuwa na familia yako?” “Vipi kama haya ndio mapenzi ya Mungu kwa ajili yako kiasi kwamba kamwe hujisikii hatia kwa kutokufanya kazi siku ya Sabato?”)
- Mfano wa Paulo
- Soma Waefeso 2:1-3. Paulo anaanzaje hoja yake? (Anafanya jambo lile lile. Anaanza na jambo la asili. Badala ya kushikilia ahadi za mibaraka, Paulo anasema, “Maisha yenu yalikuwa ya ovyo (mabaya), sawa? Mlikuwa mkijikuta mnasigana na sheria ya asili na halikuwa jambo la kufurahisha.”)
- Soma Waefeso 2:4-7. Hoja ya Paulo inayofuata ni ipi? (Jambo linalofuata anaelezea jinsi Yesu alivyotupenda, alivyotuokoa, na kutupatia ahadi ya mbinguni. Hii ni sehemu ambayo haiko wazi. Hii ndio siri ambayo tunatakiwa kuwaambia watu wengine.)
- Hebu tupitie tena Yohana 1:17. Neema na kweli zilikuja “kwa mkono” wa Yesu. Torati ilitolewa kwa mkono wa Musa na neema na kweli kwa mkono wa Yesu. Kwa nini Yohana anasema kauli za “kwa mkono” mbili kwa njia hii? (Huu ni muhtasari wa ujumbe wetu wa injili. Mungu alitupatia sheria – na sheria hiyo inaleta mantiki kwa werevu na wale ambao tayari wamevikita vichwa vyao kwenye sheria ya asili. Na, Mungu alitupatia kisicho wazi sana, zawadi ya pekee ya Yesu inayotuonesha neema na upendo wa Mungu. Hatuwezi kuishika sheria. Hatuwezi kufanya kazi ili kuupata wokovu. Lakini, tunaweza kuiamini neema ya Yesu, na tunaweza kuonesha umahiri kwa kuishi maisha yanayoendana na sheria ya Mungu.)
- Rafiki, je, utaonyesha busara katika kushiriki injili na watu wengine? Kwa nini usianze na mambo yaliyo wazi, na kisha ushiriki nao siri ya upendo na wokovu wa Mungu wetu Mkuu?
- Juma lijalo: Kristo, Sheria na Maagano.