Yesu, Roho Mtakatifu na Maombi
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Maisha yako kimaombi yakoje? Je, unatumia nguvu nyingi kufanya maombi? Kwa kuwa tayari Mungu anafahamu mahitaji yako, huenda huhitaji nguvu nyingi kiasi hicho. Ama kwa hakika, kwa nini urudie kuomba kile ambacho tayari Mungu anakifahamu? Juma hili tunajifunza mambo ya kufurahisha kuhusu maombi, Roho Mtakatifu, na kuomba kwa ujasiri. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia!
6. Soma Matendo 4:32. Je, haya ni matokeo makubwa?
- Sala ya Bwana
- Soma Luka 11:1. Ungejibuje swali hilo? Je, ungesema kuwa “Kunja mikono yako, fumba macho yako” na kisha utoe majibu ya “aina nyingine?” Unadhani mwanafunzi huyu alikuwa anauliza jambo gani hasa?
- Je, unahitaji msaada katika maombi yako?
- Utabiri wangu ni kwamba maombi yako huwa ni yale yale kila mara uombapo. Mawazo yako hayapo hai kwa kadri itakikanavyo, kwa sababu unarudia mambo yale yale. Je, ni kweli?
- Soma Luka 11:2-4. Ikiwa kurudia maombi yale yale ni tatizo, je, hili ndilo suluhisho?
- Soma Mathayo 6:7-8. Mafungu haya yanabainisha toleo la Mathayo la Sala ya Bwana. Je, tunaonywa dhidi ya jambo gani? (Kubwabwaja!)
- Hilo linaashiria nini kuhusu maombi ya mfano ya Yesu? (Kwamba lengo sio kurudiarudia pasipo kutafakari!)
- Soma Mathayo 6:7-8. Mafungu haya yanabainisha toleo la Mathayo la Sala ya Bwana. Je, tunaonywa dhidi ya jambo gani? (Kubwabwaja!)
- Pamoja na wazo la kutorudiarudia pasipo kutafakari kutakiwa kuepukwa, hebu tuangalie kwa kina ombi la Yesu lililopendekezwa. Soma Luka 11:2. Ikiwa huu ndio mwongozo, na si mswada unaotakiwa kukaririwa, kila ombi linapaswa kuanzaje? (Kwa kumsifu Mungu!)
- Soma tena Luka 11:2. Jambo gani linafuatia? (Ombi la ufalme wa Mungu kuja.)
- Je, ombi hili ni kwa ajili ya ujio wa Yesu Mara ya Pili? (Ndiyo.)
- Soma Mathayo 6:10. Fungu hili linaelezeaje zaidi juu ya ufalme wa Yesu? (Hatupaswi kusoma Luka 11:2 kwa mawazo mafinyu kwamba inamaanisha ujio wa Mara ya Pili pekee. Hili ni ombi kwa ajili ya Ufalme wa Mungu kuja hapa duniani sasa hivi.)
- Una wajibu gani katika jambo hilo? (Kila siku tunayo sehemu ya kufanya katika kusaidia Ufalme wa Mungu kuwajia wale tunaokutana nao.)
- Je, unapenda mapenzi ya Mungu yatimie maishani mwako? (Ufalme wa Mbinguni unaanza sasa, kila siku, kwako na kwangu!)
- Soma Luka 11:3. Hapa mada ni ipi? (Mahitaji yako! Unataka Mungu akutendee jambo gani.)
- Soma Luka 11:4. Unapopangilia maombi yako binafsi, unaanza na jambo gani kwanza? (Mara zote huwa ninakimbilia kuomba msamaha wa dhambi zangu. Wazo langu huwa ni kutakaswa na Mungu Mtakatifu kabla hatujaingia kwenye mambo mengine.)
- Kwa nini Yesu anatuambia tuombe mahitaji yetu kabla hatujaomba msamaha wa dhambi zetu? (Hii inazungumzia jambo fulani juu ya vipaumbele vya Mungu. Anatupenda, anataka kutusaidia, na hilo hutokea kabla ya kushughulika na tatizo letu la dhambi.)
- Je, hilo ndilo tunalojifunza hapa kwa ajili ya kushughulika na wanadamu wenzetu?
- Je, msamaha wa dhambi una masharti? (Soma Mathayo 6:14-15. Haya ndio mandishi ya Mathayo yanayohusu maneno ya Yesu kuhusu jinsi tunavyopaswa kuomba. Hii inaweka wazi kwamba kuwasamehe watu wengine ni jambo la muhimu sana. Tunatakiwa kuwa na mtazamo wa kusamehe, vinginevyo Mungu hatatusamehe. Hili ni onyo la muhimu na la kutisha.)
- Kwa nini Yesu anatuambia tuombe mahitaji yetu kabla hatujaomba msamaha wa dhambi zetu? (Hii inazungumzia jambo fulani juu ya vipaumbele vya Mungu. Anatupenda, anataka kutusaidia, na hilo hutokea kabla ya kushughulika na tatizo letu la dhambi.)
- Soma tena sehemu ya mwisho ya Luka 11:4. Je, Mungu anatutia majaribuni?
- Soma Yakobo 1:13. Yakobo anasema nini juu ya jambo hilo?
- Tulipojifunza kitabu cha Yakobo, mara nyingine kauli zake zilinichoma moyo. Yakobo alionekana kuandika mambo yaliyokinzana na Paulo, na hivyo tulichimbua zaidi ili kujaribu kuelewa. Je, tunapaswa kuangalia kwa kina zaidi hapa, au maana ya dhahiri iko sahihi?
- Soma uwiano wa kile anachokisema Yakobo: Yakobo 1:14-15. Yakobo anasema kuwa ni nani anayetujaribu? (Tunajaribiwa kwa tamaa zetu wenyewe ovu.)
- Soma 1 Wakorintho 7:5. Paulo anasema kuwa jambo gani linalotutia majaribuni? (Shetani. Lakini, Paulo anaashiria kwamba hizi ni juhudi shirikishi kati ya Shetani na sisi kutokana na kushindwa kwetu kujidhibiti. Angalia pia Mathayo 4:3.)
- Soma Mathayo 6:13. Je, maandiko ya Mathayo yanatupatia mwanga gani zaidi? (Niko pamoja na Yakobo katika kutafakari kwamba kamwe Mungu hatuingizi majaribuni. Kwa kuzingatia muktadha wa Mathayo, uelewa wangu bora zaidi wa jambo hili ni kwamba Yesu anamwomba Mungu atusaidie kuyaepuka majaribu.)
- Soma Yakobo 1:13. Yakobo anasema nini juu ya jambo hilo?
- Soma Luka 11:1. Ungejibuje swali hilo? Je, ungesema kuwa “Kunja mikono yako, fumba macho yako” na kisha utoe majibu ya “aina nyingine?” Unadhani mwanafunzi huyu alikuwa anauliza jambo gani hasa?
- Rafiki Aliyelala
- Soma Luka 11:5-6. Hii inaelezea hali halisi? (Marafiki watatu. Mmoja ana nyumba, mwingine ana mkate, na mmoja anasafiri kumtembelea yule mwenye nyumba lakini hana mkate.)
- Soma Luka 11:7-8. Je, urafiki ni mkubwa sana kiasi cha wewe kuweza kupata mkate? (Hapana. Ujasiri wakati wa usiku na Maanan (manane) ndio unaokupatia mkate.)
- Je, utakubaliana kwamba kisa hiki ni cha ajabu? Hebu niambie kwa nini unadhani kisa hiki kinafuatia mara baada ya Yesu kuelezea jinsi tunavyopaswa kuomba?
- Je, Mungu atajibu maombi ya ujasiri ambayo vinginevyo asingeyajibu kutokana na urafiki na upendo uliopo? (Hilo hitimisho kali linaonekana kutokubalika.)
- Soma Luka 11:9-10. Angalia kile tulichokwishajifunza hadi sasa katika Luka 11. Je, Yesu anatufundisha nini? (Yesu anatufundisha kwamba sehemu ya muhimu sana ya maombi yanayojibiwa ni kuomba kwa ujasiri! Sishangai!)
- Soma tena Mathayo 6:7-8. Ikiwa Mungu anafahamu kile tunachokihitaji, na kwamba hatutakiwi kupayuka-payuka (jambo tuliloliangalia hapo kabla), je, ni jambo gani jingine analotufundisha Yesu kuhusu maombi? (Hatuna haja ya kuelezea tatizo kwa Mungu. Hatuna haja ya kuendelea kurudiarudia jambo lile lile. Lakini, (angalia Luka 18:1-8), hata hivyo, tunatakiwa kuomba!)
- Je, unaona haya (aibu) kuhusu kuomba kwa “ujasiri” kwa ajili ya jambo fulani? (Tunatakiwa kuwa na nguvu kimatendo na kivitendo katika kumwomba Mungu! Tunatakiwa kuwa majasiri! Haya ndio maelekezo ya Mungu kwetu! Hiki sio kiburi wala ufidhuli.)
- Soma Luka 11:11-13. Je, kuna mtu aliyesema kwamba Mungu atatupatia kitu kinachoweza kutudhuru au kutuua? (Hadi sasa hakuna kitu kama hicho kwenye mafungu hayo.)
- Ikiwa Yesu anatufundisha kwamba maombi ya “ujasiri” ndio ufunguo – kwamba ikiwa tunataka jambo fulani, tunatakiwa tu kuomba, kwa nini uwe na wasiwasi? (Mtu mwenye busara atajali sana kuomba na kupokea jambo fulani litakalokuwa na madhara. Sasa tunaelewa mantiki ya jambo hili. Mungu anasema, “Omba kwa ujasiri nami nitakupatia – lakini sitakupatia kitu kitakachokudhuru vibaya sana.)
- Roho Mtakatifu
- Soma tena Luka 11:13. Je, hii ni kinyume na jinsi hali ilivyo? Je, huku ni kuangushwa? Baada ya mjadala wote huo kuhusu kuomba kwa ujasiri, mambo yanabadilika na kwamba hatupati gari jipya aina ya Merecedes, bali tunapata Roho Mtakatifu?
- Umejifunza nini kuhusu uwezo wa Roho Mtakatifu kutenda mambo makuu?
- Soma Matendo 2:1-4 na Matendo 2:41. Je, haya ni matokeo makubwa?
- Soma Matendo 5:15-16. Je, haya ni matokeo makubwa?
- Soma Matendo 4:31. Je, haya ni matokeo makubwa?
- Soma Matendo 9:40-41. Je, haya ni matokeo makubwa?
- Unaelewaje kile alichokisema Yesu hadi kufikia hapa? Tukiomba kwa ujasiri, je, Mungu atatupatia uwezo, kwa njia ya Roho Mtakatifu, kutenda miujiza, kuwabadili watu imani zao, kutatusaidia kuelewa mapenzi ya Mungu na kuleta upatanifu/amani kanisani?
- Tukishindwa kuomba, je, Mungu anatupatia vitu hivi hata kama anafahamu kwamba tunavihitaji? (Lazima tuombe. Mfano wa rafiki unatuambia kwamba bila kuomba hatutapata/hatutapokea.)
- Rafiki, je, unaona uwezekano mkubwa sana uliowekwa mbele yako? Mungu anatupatia mambo makuu, na anatuahidi hatatupatia vitu vitakavyokuwa vibaya kwetu. Je, utamwomba Mungu kwa ujasiri akupatie mambo makuu, kwa njia ya Roho Mtakatifu, ili kuuendeleza Ufalme wa Mungu?
- Unaelewaje kile alichokisema Yesu hadi kufikia hapa? Tukiomba kwa ujasiri, je, Mungu atatupatia uwezo, kwa njia ya Roho Mtakatifu, kutenda miujiza, kuwabadili watu imani zao, kutatusaidia kuelewa mapenzi ya Mungu na kuleta upatanifu/amani kanisani?
- Juma lijalo: Utume wa Yesu.
- Soma tena Luka 11:13. Je, hii ni kinyume na jinsi hali ilivyo? Je, huku ni kuangushwa? Baada ya mjadala wote huo kuhusu kuomba kwa ujasiri, mambo yanabadilika na kwamba hatupati gari jipya aina ya Merecedes, bali tunapata Roho Mtakatifu?