Roho na Neno
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Kati ya mafundisho ya muhimu katika Biblia, mojawapo ya fundisho la muhimu kabisa ni juu ya uelewa wa kazi ya Roho Mtakatifu. Katika Matendo 8:14-17 tunasoma kisa cha waumini wapya waliobatizwa katika jina la Yesu, lakini bado wana upungufu mkubwa sana; kwamba bado “hawajampokea Roho Mtakatifu.” Petro na Yohana “wakaweka mikono yao juu yao, nao wakampokea Roho Mtakatifu.” Je, unao upungufu katika maisha yako ya Kikristo? Je, unafanana na jinsi Wakristo wale walivyokuwa, wakabatizwa, lakini hawakuwa na Roho Mtakatifu? Kiwango cha tatizo kinakuwa wazi zaidi tunapotafakari jinsi Roho Mtakatifu anavyotenda kazi maishani mwetu. Hebu tuanze safari yetu ya kujifunza Biblia ili tuone jinsi Roho Mtakatifu alivyo wa muhimu kupindukia maishani mwetu!
I. Roho Mtakatifu na Ufahamu [Uelewa] Juu ya Mungu
A. Soma 1 Wakorintho 2:13. Kuna tatizo gani kwenye hekima ya mwanadamu? (Ina upungufu. Hata hekima ya kibinadamu itakuambia kuwa hekima ya Mungu inapaswa kuwa kubwa kuliko hekima ya viumbe walioumbwa na Mungu.)
B. Soma 1 Wakorintho 2:14. Wakristo tunakabiliwa na tatizo gani kubwa ikiwa hatutakuwa na Roho Mtakatifu? (Hatuwezi kuyaelewa mambo ya Mungu.)
1. Kuna wachekeshaji wengi maarufu pamoja na watu wanaojiita wasomi wanaoudhihaki Ukristo. Kila ninaposikia hii dhihaka huwa ninakasirika. Je, ninapaswa kukasirika? Au, je, ninatakiwa tu kuwa na hisia nyinginezo? (Kifungu hiki kinafundisha kwamba ni jambo la kawaida kwa mwanadamu kudhani kuwa Ukristo ni “upumbavu” ikiwa mtu huyo hana Roho Mtakatifu. Ingawa ninadhani baadhi ya wadhihaki hawa wamejawa ushawishi wa pepo, jambo la kawaida kwa hekima ya mwanadamu ni kushindwa kuyaelewa mambo ya Mungu.)
C. Soma 1 Wakorintho 2:15. Inamaanisha nini kusema kwamba “hatutambuliwi na mtu” kwa muktadha wa kile ambacho tumekuwa tukijifunza? (Watu ambao hawaongozwi na Roho Mtakatifu watadhani kuwa sisi ni wapumbavu, lakini hatutakiwi kuwasikiliza wala kuwazingatia kwa sababu hatuko chini yao. Hawana uwezo wa kuwa na uamuzi sahihi juu yetu.)
II. Roho Mtakatifu na Neno la Mungu
A. Soma 2 Petro 1:19-21. Tunaona tofauti gani hapa kati ya hekima ya mwanadamu na fikra ya mwanadamu inayoongozwa na Roho Mtakatifu? (Hakuna unabii wa Biblia ambao asili yake ni hekima ya mwanadamu. Badala yake, wanadamu walinena maelezo [matukio] ya siku zijazo yaliyotoka kwa Mungu “wakiongozwa” na Roho Mtakatifu.)
B. Soma Zaburi 95:7-9 na ulinganishe na Waebrania 3:7-9. Nini chanzo cha hii sehemu ya kitabu cha Zaburi? (Roho Mtakatifu! Tunaona kwamba Roho Mtakatifu ndio msingi wa uandikwaji wa Biblia.)
III. Roho Mtakatifu na Utatuzi wa Tatizo
A. Soma Danieli 2:1-3. Chukulia kwamba ulikuwa miongoni mwa wanajimu wa Mfalme, je, ungemwuliza swali gani?
B. Soma Danieli 2:4-5. Kama ilivyotarajiwa ni kwamba wanajimu wana swali lile lile kama tulilonalo, “Tuambie ndoto yako.” Unadhani kwa nini mfalme alichukua hatua ngumu kiasi hicho kwa wanajimu? (Lazima itakuwa mfalme alikuwa na mawazo ya aina mbili. Kwanza, hii ni ndoto ya muhimu sana ambayo anataka aielewe kwa usahihi. Pili, hakuwaamini washauri wake. Angeweza kuwajaribu endapo walikuwa wanasema ukweli kwa kuthibitisha kuwa wangeweza kuirudia ile ndoto kwa usahihi.)
C. Soma Danieli 2:11-12. Unaichukuliaje afya ya akili ya mfalme? Je, mfalme ana wazimu, au hizi ni hisia za kawaida kwa kundi hili la “wenye hekima” ambao mfalme amekuwa akiwawezesha kifedha?
D. Soma Danieli 2:13-15. Sasa jiweke kwenye nafasi ya Danieli. Je, hili ndilo swali ambalo ungeuliza?
E. Soma Danieli 2:16. Ombi la Danieli lina nadharia gani ndani yake? (Kwamba anaweza kutoa tafsiri ya ndoto.)
1. Tafakari hatari ya kumwendea mfalme. Mlinzi wa mfalme anawatafuta wenye hekima ili awaue!
F. Soma Danieli 2:17-18. Linganisha maelezo ya Danieli na kauli ya wenye hekima – miungu pekee ndio wanaojua jibu. Hii inatuambia nini? (Danieli pamoja na wale wengine wenye hekima walikubaliana – kwamba hili ni suala la miungu. Tofauti iliyopo ni kwamba Danieli anaamini kuwa anaweza kumfikia Mungu, na Mungu atamsaidia.)
1. Je, umewahi kupita uzoefu wa jambo la kutisha lililojaa msongo zaidi ya hili – kwamba serikali imeamua kukukata vipande vipande na kuangamiza nyumba [familia] yako ikiwa utashindwa kutoa majibu sahihi?
G. Soma tena Danieli 2:11. Utaona wenye hekima wanasema kuwa miungu hawana kikao na wenye mwili. Je, hii ni kweli kwa mujibu wa Mungu wako? (Soma Yohana 14:17, Warumi 8:11 na 1 Wakorintho 6:19. Vifungu hivi vinatuambia kuwa Roho Mtakatifu anakaa ndani yetu! Hivyo, zaidi ya miungu kukaa “miongoni” mwa wanadamu ni kwamba Mungu anakaa “ndani” yetu!)
1. Ikiwa, kama ilivyokuwa kwa Danieli, ulikuwa na tatizo la taarifa, na maisha yako yalikuwa hatarini, je, ungekuwa na uelewa wa Mungu kwa kuwa tu Roho wa Mungu anakaa ndani yako?
H. Soma tena Danieli 2:18. Je, msaada wa Roho Mtakatifu ni wa moja kwa moja pasipo kufanya jambo lolote? (Kwa dhahiri unatakiwa kuuomba. Danieli na marafiki wake watatu “waliomba rehema” ili kwamba Mungu awapatie jibu.)
I. Soma Danieli 2:19. Kwa nini jibu lilimjia Danieli wakati wa usiku? Kwa nini halikumjia mara moja? (Soma Danieli 2:22-23. Roho Mtakatifu akaaye ndani yako hakujazi maarifa yote ya Mungu moja kwa moja. Badala yake, tunamwomba Mungu atupatie uwezo [taarifa] wa kutatua matatizo naye anatupatia taarifa tulizomwomba.)
1. Zamani nilikuwa ninadhani kwamba Roho Mtakatifu alikuwa “anakaa ndani yangu” ili kunisaidia kwenye masuala ya kiroho pekee. Angalia Yohana 16:8. Je, hiyo ni kweli? (Si kwa mujibu wa kisa hiki. Roho Mtakatifu alimsaidia Danieli kwa matatizo yaliyohusiana na kazi yake.)
IV. Roho Mtakatifu na Mpango Mkakati
A. Soma Yohana 16:12-13. Tumejadili wazo hili, kwamba Roho Mtakatifu akikaa ndani yetu anaweza kujaza akili zetu maarifa yote ya Mungu. Yesu anatoa sababu gani za jambo hilo kutotendeka? (Tusingeweza kustahimili. Kuna aina fulani hivi ya kipimo cha Mungu ambacho kinashiriki nasi maarifa ambayo tunaweza kuyastahimili. Kimsingi Yesu anasema “Siwezi kuwaambia sasa hivi kwa sababu hamwezi kustahimili, lakini siku zijazo Roho Mtakatifu atayaongoza mawazo yenu kuwa na maarifa makubwa zaidi.)
1. Yesu anaposema kuwa Roho Mtatatifu “atatuongoza kwenye kweli yoye,” je, hiyo inamaanisha kuwa hatimaye tutafahamu kile anachokijua Mungu?
B. Soma Yohana 16:13-15. Hii inaashiria nini kuhusu maarifa ya Roho Mtakatifu? Je, maarifa yake ni pungufu ya maarifa ya Mungu Baba? Roho Mtakatifu anachukua tu mambo ambayo anayasikia kwa mbali, na hayo ndio yanayoletwa kwetu?
C. Soma 1 Wakorintho 2:10-11. Hii inatufundisha nini kuhusu undani wa maarifa ya Roho Mtakatifu? (Vifungu hivi vinatuambia kuwa hakuna kitu chochote ulimwenguni kinachoyafahamu mawazo ya Mungu vizuri zaidi ya Roho Mtakatifu! Kwa dhahiri, Roho Mtakatifu “hachukui [haokotiokoti] tu mambo.”)
D. Soma 2 Wakorintho 3:17-18. Hii inatufundisha nini kuhusu asili ya msingi ya Mungu? (Kwamba Bwana “ni Roho.” Kama sehemu ya Utatu Mtakatifu, Roho Mtakatifu ni Mungu kamili. Ni dhana potofu kudhani kuwa Roho Mtakatifu hajui kile ambacho Mungu Baba anakijua. Badala yake, nadhani tunapaswa kuelewa jambo hili la “yote atakayoyasikia” kumaanisha kwamba Utatu Mtakatifu hujadili na kuamua ukweli wote tunaotakiwa kuujua. Inahusiana na upungufu wetu, sio upungufu wa Roho Mtakatifu.)
1. Tunaposoma kwamba Roho Mtakatifu “atatuongoza” kwenye “kweli yote,” je, hiyo inaashiria wajibu gani kwetu? (Sio kukaa tu! Kama Danieli na marafiki wake walivyomwomba Mungu awadhihirishie ndoto ya ajabu [ya kimiujiza], vivyo hivyo nasi tunatakiwa kuungana na Roho Mtakatifu katika kuitafuta “kweli yote.”)
2. Utaona kwamba 2 Wakorintho 3:17-18 pia inarejea “uhuru” na “nyuso zisizotiwa utaji.” Unadhani hii inaashiria nini juu ya kazi ya Roho Mtakatifu? (Roho Mtakatifu anavyotusaidia kuelewa vizuri zaidi mapenzi ya Mungu kwa ajili ya maisha yetu, hii hutuweka huru dhidi ya kutoelewa torati ya Mungu.)
E. Rafiki, je, unaye Roho Mtakatifu maishani mwako? Ikiwa huna uhakika, kwa nini usimwombe Roho Mtakatifu akae ndani yako. Na jambo jema zaidi ni kwamba, kwa nini usimwombe mchungaji wako akuwekee mikono na kukupatia hii zawadi ya muhimu kutoka kwa Mungu?
V. Juma lijalo: Roho Mtakatifu: Kazi Itendwayo Nyuma ya Pazia [Jukwaa].Introducción: De todas las grandes enseñanzas de la Biblia, una de las más importantes es la comprensión de la obra del Espíritu Santo. En Hechos 8:14-17 leemos la historia de los nuevos creyentes que han sido bautizados en el nombre de Jesús, pero todavía tienen un déficit muy serio; todavía no han "recibido el Espíritu Santo". Pedro y Juan "pusieron sus manos sobre ellos, y recibieron el Espíritu Santo". ¿Tienes un déficit en tu vida cristiana? ¿Eres como los cristianos solían ser, bautizados, pero carentes del Espíritu Santo? El alcance del problema potencial se vuelve más claro cuando consideramos cómo opera el Espíritu Santo en nuestra vida. Comencemos nuestro viaje en la Biblia para aprender cómo el Espíritu Santo es crítico para nuestra vida.
- El Espíritu Santo y la Comprensión de Dios
- Lee 1 Corintios 2:13. ¿Qué tiene de malo la sabiduría humana? Incluso la sabiduría humana les diría que la sabiduría de Dios tiene que ser mayor que la de Su creación.
- Lee 1 Corintios 2:14. ¿Qué grave problema enfrentamos como cristianos si nos falta el Espíritu Santo? (No podemos entender las cosas de Dios.)
- Hay algunos cómicos bien conocidos y los llamados intelectuales que se burlan del cristianismo. Cada vez que oigo esta burla me pone enojado. ¿Debería estar enojado? O, ¿debo tener una reacción emocional diferente? (Este texto enseña que es natural para un humano pensar que el cristianismo es una "tontería" si esa persona carece del Espíritu Santo. Aunque creo que algunos de estos burladores están bajo influencias demoníacas, el defecto de la sabiduría humana es no entender las cosas de Dios.)
- Lee 1 Corintios 2:15.¿Qué significa que no estamos "sujetos al juicio de nadie" en el contexto de lo que estudiamos? (Las personas que no son guiadas por el Espíritu Santo piensan que somos necios, pero no debemos prestarles atención porque no estamos sujetos a su juicio, son incapaces de llegar a un juicio correcto acerca de nosotros).
- El Espíritu Santo y la Palabra de Dios
- Lee 2 Pedro 1:19-21. ¿Qué distinción encontramos entre la sabiduría humana y el pensamiento humano dirigido por el Espíritu Santo? (Ninguna profecía bíblica encuentra su origen en la sabiduría humana, sino que el Espíritu Santo "lleva" descripciones humanas del futuro).
- Compara Salmos 95:7-9 con Hebreos 3:7-9. ¿Cuál es la fuente de esta parte de Salmos? (¡El Espíritu Santo! Vemos que el Espíritu Santo es central para la creación de la Biblia).
- El Espíritu Santo y la Solución de Problemas
- Lee Daniel 2:1-3. Supónque eres uno de los astrólogos del rey, ¿qué pregunta te gustaría tener para él?
- Lee Daniel 2:4-5. Resulta que los astrólogos tienen la misma pregunta: "Cuéntanos el sueño". ¿Por qué crees que el rey tuvo tal línea dura con los astrólogos? (El rey debe haber tenido dos pensamientos: en primer lugar, este es un sueño tan importante que quiere hacerlo bien. En segundo lugar, no confiaba en sus asesores. Podía probar si decían la verdad al confirmar que podían recitar correctamente su sueño.)
- Lee Daniel 2:11-12. ¿Qué piensas de la salud mental del rey? ¿Es un maníaco, o es una reacción razonable a este grupo de "sabios" a quienes el rey ha apoyado financieramente?
- Lee Daniel 2:13-15.Ahora ponte en el lugar de Daniel. ¿Es esta la pregunta que harías?
- Lee Daniel 2:16. ¿Qué asume la petición de Daniel? (Que él puede interpretar el sueño.)
- Considera el peligro de ir al rey. ¡La guardia del rey está buscando hombres sabios para que puedan matarlos!
- Lee Daniel 2:17-18. Compara la explicación de Daniel con la declaración de los sabios: sólo los dioses saben la respuesta. ¿Qué nos dice esto? (Daniel y los otros sabios estuvieron de acuerdo, esto es asunto de los dioses, la diferencia es que Daniel cree que tiene acceso a Dios, y que Dios lo ayudará).
- ¿Has tenido una experiencia más aterradora y llena de presión que esta: que el gobierno ha decidido cortarte en pequeñas piezas y destruir tu casa si no se producen las respuestas correctas?
- Relee Daniel 2:11. Nota que los sabios dicen que los dioses no viven entre los hombres. ¿Es esto cierto con respecto a tu Dios? (Lee Juan 14:17, Romanos 8:11 y 1 Corintios 6:19 ¡Estos textos nos dicen que el Espíritu Santo vive en nosotros! Por lo tanto, ¡mejor que los dioses que viven entre los hombres es que Dios vive en nosotros!)
- Si, como Daniel, tuvieras un problema de información y tu vida en juego, ¿tendrías el conocimiento de Dios simplemente porque el Espíritu de Dios vive dentro de ti?
- Relee Daniel 2:18. ¿Es la ayuda del Espíritu Santo automática? (Al parecer, tienes que pedir a Daniel y a sus tres amigos "imploren misericordia" que Dios les dé la respuesta.)
- Lee Daniel 2:19. ¿Por qué la respuesta vino a Daniel por la noche? ¿Por qué no enseguida? (Lee Daniel 2:22-23) El Espíritu Santo que vive en ti no te infunde automáticamente todo el conocimiento de Dios, sino que le pedimos a Dios información para resolver problemas y Él nos da la información requerida).
- En el pasado he pensado que el Espíritu Santo sólo estaba "viviendo en mí" para ayudarme con asuntos espirituales. Véase Juan 16:8. ¿Es eso cierto? (No según esta historia. El Espíritu Santo ayudó a Daniel con sus problemas relacionados con el trabajo.)
- El Espíritu Santo y la Planificación Estratégica
- Lee Juan 16:12-13. Discutimos esta idea de que tener el Espíritu Santo viviendo en nosotros podría infundir nuestras mentes con todo el conocimiento de Dios. ¿Por qué dice Jesús que no sucede? (No podríamos soportarlo.) Hay una especie de medición divina que nos comparte el conocimiento como somos capaces de soportarlo. Jesús esencialmente dice: "No puedo decirte ahora porque no puedes soportarlo, pero el Espíritu Santo en el futuro guiará tu mente hacia un mayor conocimiento.)
- Cuando Jesús dice que el Espíritu Santo nos "guiará" a toda la verdad, ¿significa eso que finalmente sabremos lo que Dios sabe?
- Lee Juan 16:13-15. ¿Qué sugiere esto acerca del conocimiento del Espíritu Santo? ¿Es menor que la de Dios el Padre? ¿El Espíritu Santo sólo recoge cosas que El oye, y eso es lo que nos pasa a nosotros?
- Lee 1 Corintios 2:10-11.¿Qué nos enseña esto acerca de la profundidad del conocimiento del Espíritu Santo? (¡Este texto nos dice que nada en el universo conoce mejor la mente de Dios que el Espíritu Santo! Es evidente que el Espíritu Santo no está simplemente "recogiendo cosas").
- Lee 2 Corintios 3:17-18. ¿Qué nos enseña esto acerca de la naturaleza esencial de Dios? Como parte de la Trinidad, el Espíritu Santo es completamente Dios, es una falsa idea pensar que el Espíritu Santo no sabe lo que Dios Padre sabe, sino que debemos entender esto "sólo lo que Él oye" significa que la Trinidad trata y decide todo el alcance de la verdad que necesitamos saber, que tiene que ver con nuestras limitaciones, no con las limitaciones del Espíritu Santo.)
- Cuando leemos que el Espíritu Santo nos "guiará" a "toda la verdad", ¿qué papel nos sugiere? (¡No es un papel pasivo! Al igual que Daniel y sus amigos le pidieron a Dios que le revelara el misterioso sueño, así necesitamos unirnos con el Espíritu Santo en una exploración de "toda la verdad").
- Note que 2 Corintios 3:17-18 también se refiere a "libertad" y "caras descubiertas". ¿Qué crees que esto sugiere acerca de la obra del Espíritu Santo? (Como el Espíritu Santo nos ayuda a entender mejor la voluntad de Dios para nuestra vida, nos libera de los malentendidos sobre la ley de Dios.)
- Amigo, ¿tienes el Espíritu Santo en tu vida? Si no estás seguro, ¿por qué no pedirle al Espíritu Santo que habite en ti? Mejor aún, ¿por qué no pedirle a tu pastor que ponga las manos sobre ti para darte este importante regalo de Dios?
- Lee Juan 16:12-13. Discutimos esta idea de que tener el Espíritu Santo viviendo en nosotros podría infundir nuestras mentes con todo el conocimiento de Dios. ¿Por qué dice Jesús que no sucede? (No podríamos soportarlo.) Hay una especie de medición divina que nos comparte el conocimiento como somos capaces de soportarlo. Jesús esencialmente dice: "No puedo decirte ahora porque no puedes soportarlo, pero el Espíritu Santo en el futuro guiará tu mente hacia un mayor conocimiento.)
- La próxima semana: El Espíritu Santo: Trabajando Detrás de la Escena.