Paulo: Mtume kwa Mataifa
Utangulizi: Kuna msemo wa zamani unaosema kwamba tunahitajika kujiweka kwenye nafasi ya mtu mwingine kabla hatujaelewa kwa dhati kabisa hali anayopitia mtu huyo. Nilipokuwa kijana mdogo, nilikuwa nikitumia muda wa majira ya kiangazi kwa kujenga miji (nyumba) na fleti (vyumba vya kuishi) pamoja na kaka wangu. Asubuhi moja tukiwa kwenye safari ndefu ya kuelekea kazini, gari la kaka wangu liliharibika na akaamua kwamba tunapaswa tu kutembea na kuona kama mtu fulani anaweza kutupatia “lifti.” Hatukuwa tumevaa kwa unadhifu, na tulikuwa tumebeba vifaa. Haikuwa taswira nzuri ya kumfanya mtu afikirie kutupa “lifti.” Kwa kawaida nilipokuwa nikiendesha gari, sikuwa nikiwabeba wale waliokuwa wakijaribu kuomba “lifti” – hiyo ilikuwa hatari! Lakini sasa, nilikuwa nikisubiri kwa matumaini makubwa na kutamani kuona mtu fulani aonyeshe moyo wa huruma kwetu! Ili kuweza kuelewa vizuri barua iliyoandikwa kwa Wagalatia, tutajaribu kujiweka sisi wenyewe kwenye nafasi ya mwandishi wake, Paulo. (Kwa wale wasiojua, aliyekuwa “Sauli” ndiye baadaye aliitwa “Paulo.” Nitamwita tu kuwa “Paulo” katika somo hili.) Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na kuona kile Biblia inachotufundisha kuhusu maisha yake. Hebu tuone itakuwaje tukiwa kama Paulo!
- Paulo: Utangulizi
- Soma Matendo 21:26-28. Paulo anatiwa kizuizini/mbaroni kwa mashtaka gani? (Kwa sababu anakiuka sheria ya Kiyahudi na kufundisha kinyume kwa watu wa Kiyahudi.)
- Hebu turuke mafungu kadhaa na kusoma utetezi wa Paulo. Soma Matendo 22:2-3. Je, huu ni wasifu wa aina gani? (Paulo anasema yeye ni Myahudi, sio adui wa WayahudAlilelewa Yerusalemu, kituo cha utamaduni wa Kiyahudi.)
- Kama ilivyo kwa mashtaka kwamba Paulo yu kinyume na sheria, anasema kwamba alifundishwa na GamalielJe, Gamalieli ni nani? (“Commentary” ya Adam Clarke inatuambia kuwa Gamalieli alikuwa mjukuu wa Hillel (mmojawapo wa walimu maarufu wa Kiyahudi), alikuwa rais wa baraza la Sanhedrin, na mpokeaji wa 35 wa tamadun“Commentary” ya Fausset inaongezea kwamba alifurahiwa kama “utukufu wa sheria,” na alikuwa mteuzi wa kwanza kuitwa Raban “bwana wetu.”)
- Kwa kutumia maneno ya siku hizi, je, Paulo anasema nini? (Kwamba alifundishwa na mamlaka ya juu kabisa ya sheria dunianAna uzoefu/maarifa/ujuzi mkubwa sana wa sheria kuliko wale wanaomshtaki.)
- Kama ilivyo kwa mashtaka kwamba Paulo yu kinyume na sheria, anasema kwamba alifundishwa na GamalielJe, Gamalieli ni nani? (“Commentary” ya Adam Clarke inatuambia kuwa Gamalieli alikuwa mjukuu wa Hillel (mmojawapo wa walimu maarufu wa Kiyahudi), alikuwa rais wa baraza la Sanhedrin, na mpokeaji wa 35 wa tamadun“Commentary” ya Fausset inaongezea kwamba alifurahiwa kama “utukufu wa sheria,” na alikuwa mteuzi wa kwanza kuitwa Raban “bwana wetu.”)
- Soma Matendo 22:4-5. Je, ni kwa namna gani hii inahusika na mashtaka dhidi ya Paulo? (Unasema kwamba niko radhi kukiuka sheria? Nimekuwa nikiwaua watu waliopingana na sheria!)
- Je, unaweza kuelezeaje kwa ufupi utetezi wa Paulo hadi hatua hii tuliyofikia? (Ana elimu bora zaidi ya sheria kuliko washtaki wake, na ana ari kubwa ya sheria kuliko washtaki wake. Hakanushi mashtaka, ila anasema tu kuwa “Ninyi ni akina nani hadi mnishtaki?”)
- Umemsikia Paulo. Hebu jiweke kwenye nafasi yake. Je, ni mtazamo wa namna gani ambao ungetarajia awe nao? Je, mtazamo wa aina gani unaakisiwa kwenye utetezi wake hadi hapo tulipofikia? (Angejisikia kuwa mtu wa hali ya juu sana. Na, yeye ni mtu wa hali ya juu kwa mujibu wa elimu yake.)
- Soma Matendo 22:6-10. Hebu tuzungumze kuhusu hilPaulo anaweka wasifu wake mkubwa kabisa kupita maelezo, na kisha anasema “Mungu alinichagua.” Kwa nini Mungu alimchagua?
- Soma Waamuzi 7:2-3, 1 Wakorintho 1:20-21 na 1 Wakorintho 1:26-29. Biblia ina habari inayojirudiarudia kuhusu Mungu kutenda kupitia kwenye udhaifu wa wanadamu. Kuwa mwerevu na mwenye elimu ya kutosha ni tatizo kwa sababu watu wa aina hiyo wana tabia ya kudai utukufu unaompasa Mungu. Je, Mungu amebadili njia yake?
Tatizo jingine la kuwa na akili nyingi, elimu na uwezo ni kwamba tuna kawaida ya kuvitegemea badala ya kumtegemea Mungu. Pamoja na yote haya, kwa nini Mungu amchague mtu (Paulo) mwenye mtazamo wa kujiona kuwa ni mtu wa hali ya juu? (Sina uhakika. Lakini, hii ni habari njema kwa watu werevu, wenye elimu ya kutosha. Mungu hakumtumia Paulo kwa namna kubwa tu, bali pia alimtumia Danieli na Musa. Mungu anawatumia watu wenye vipaji/vipawa, wenye elimu ya kutosha na anawatumia wale wanaopungukiwa hivi vipawa/vipajBwana asifiwe kwa sababu sisi sote tuna fursa ya kumtumikia Mungu.)

- Paulo: Maelekezo
- Angalia tena sentesi ya kwanza ya matendo 22:10. Kama ungekuwa na elimu kama ya Paulo, ari yake kwa sheria ya Mungu, na hati yake ya mamlaka kutoka baraza la Sanhedrin kuwaangamiza Wakristo, je, ungekuwa unauliza hili swali? (Maisha yako yote yamepinduliwa juu chini! Ulidhani kwamba ulikuwa ukimtii Mungu. Ulidhani kwamba Yesu alikuwa mlaghai/mdanganyifu. Sasa unabaini kwamba Yesu ni Mungu! Kwa kweli kabisa hutajua nini cha kufanya.)
- Je, Mungu anatoa jibu la aina gani? (Kwanza, fuata maelekezo rahisi, kisha nitakupa maelekezo zaidi.)
- Soma Matendo 22:12 na Matendo 9:10-15. Je, Anania ni mtu wa namna gani? (Mwenye kuamini! Lakini, anataka kuwa na uhakika kuwa Mungu anafahamu kweli zote kuhusu huyu mtu ambaye amekuwa akiwaua Wakristo! Utabaini kwamba Paulo anamwita Anania “mtauwa kwa kuifuata sheria.” Hiyo ilimpa kitu fulani kinachofanana na cha Paulo. Na kwa kuongezea, mtu huyu aliwaheshimu majirani zake wa Kiyahudi.)
- Soma Matendo 22:13. Je, kitendo hiki kinamwashiria nini Paulo? (Mtu huyu anaweza kutenda miujiza. Anaweza kufanya zaidi ya kile alichofanya Mungu! Kwa hiyo, lazima atakuwa amepewa uwezo wa Mungu. Mara moja nitakuwa na mtazamo wa imani kubwa na shukrani mbele zake.)
- Tunapata habari zaidi za hili tukio katika Matendo 9. Hebu tusome Matendo 9:17-19. Utabaini kwamba Anania ananukuu matendo ya Yesu na Roho Mtakatifu kwenye hili tukio. Je, hii inapendekeza kitu gani?
- Paulo alipofushwa na mwanga. Kwa nini “magamba” yaanguke kutoka machoni mwake? (Undani wa habari hii unakifanya kisa hiki kiwe cha kuaminika – kitu chenye sura ya kuonekana kilibadili kile ulichoweza kuona. Haionekani kwamba magamba yalifanyika ikiwa ni matokeo ya mwanga mkali, lakini Mungu alitaka kuonyesha badiliko lenye sura ya kuonekana.)
- Soma Matendo 22:14. Hebu tuvunjevunje hili kwenye sehemu kadhaa. Nilidhani kuwa Paulo alikuwa mjuzi zaidi kwenye sheria – akiwa amefundishwa na GamalielJe, lugha ya “amekuchagua wewe upate kujua mapenzi yake” inapendekeza kitu gani? (Kwamba Paulo anahitaji elimu zaidHuenda elimu tofauti.)
- Je, ni nani “Mwenye Haki?” (Hii lazima imaanishe kuwa ni Yesu. Angalia Zaburi 16:10.)
- Kama inamaanisha Yesu, je, hii inawezekanaje? (Hii inatupatia mwangaza wa kufurahisha. Paulo anaahidiwa kwamba Yesu mwenyewe atamfundisha. Kwa vile Matendo 1:3 inaandika kwamba Yesu aliwafundisha mitume wengine baada ya ufufuo wake, hii inaleta mantiki.)
- Soma Wagalatia 1:11-12 na Wagalatia 1:15-17. Je, ni madai gani yale yale anayoyadai Paulo kuhusu maelekezo yake katika injili? (Kwamba aliyapokea moja kwa moja kutoka kwa Yesu!)
- Je, ni nani “Mwenye Haki?” (Hii lazima imaanishe kuwa ni Yesu. Angalia Zaburi 16:10.)
- Soma Matendo 22:15-16. Je, Paulo anamshuhudia nani? (Watu wote.)
- Je, hii iliathiri vipi uelewa wake wa awali kuhusu maisha? (Lengo lake lilikuwa ni kuwafundisha Wayahudi na kuendeleza uelewa wa sheria. Sasa ana ujumbe wa juu zaidi ya watu wake mwenyewe.)
- Kwa nini Paulo alipaswa kubatizwa? (Huu ni ukubali/uelewa kwamba mafundisho yake ya awali kuhusu maisha, kile alichodhani kuwa ni Ufalme wa Mungu, badala yake kilikuwa ni dhambi.)
- Je, ni vigumu kiasi gani kwa mtu mwenye akili nyingi, elimu kubwa na mtazamo wa hali ya juu, kugeuka kwa nyuzi 180? (Kwa hakika hii ilikuwa ni vigumu sana.)
- Soma Matendo 22:17-20. Je, Paulo anakubali maelekezo ya Mungu bila kusita? (Hapana! Mungu anamwambia Paulo aondoke kwa sababu hataweza kuwashawishi watu hawa. Paulo anasema, “Bila shaka! Watu hawa wanajua kuwa nilikuwa mtetezi mwenye ari ya juu wa mawazo yao! Kwa hakika, watanichukulia kwa dhati kabisa!)
- Soma Matendo 22:21. Je, maelekezo ya Mungu kwa ajili ya maisha ya Paulo ni yapi? (Kuwafundisha watu wa mataifa.)
- Unadhani ni kwa nini Paulo anaandika hoja yake dhidi ya maelekezo ya Mungu? Je, anawaambia nini wasikilizaji wake pamoja na sisi? (Anasisitiza sehemu ya Mungu kwenye kazi yake. Anampa Mungu sifa. Paulo anasema nilikuwa na elimu bora, nilikuwa mwerevu, nilikuwa mwenye hamasa kubwa na mchapa kazNiliungwa mkono na viongozi wa dini wa taifa langu. Lakini, Mungu aliyabadili hayo yote. Alibadili kila kitu na kunipa utume ambao sikuuchagua.)
- Hebu jiweke kwenye nafasi ya Paulo. Je, ungejisikiaje?
- Unadhani ni kwa nini Paulo anaandika hoja yake dhidi ya maelekezo ya Mungu? Je, anawaambia nini wasikilizaji wake pamoja na sisi? (Anasisitiza sehemu ya Mungu kwenye kazi yake. Anampa Mungu sifa. Paulo anasema nilikuwa na elimu bora, nilikuwa mwerevu, nilikuwa mwenye hamasa kubwa na mchapa kazNiliungwa mkono na viongozi wa dini wa taifa langu. Lakini, Mungu aliyabadili hayo yote. Alibadili kila kitu na kunipa utume ambao sikuuchagua.)
- Soma Matendo 22:22. Je, Paulo alikuwa anaelezea kisa maarufu? (Hapana!)
- Je, unadhani kwamba Paulo angeweza kutarajia hili? (Ndiyo. Hii inafanya kile alichokisema kiwe cha kuaminika. Watu wanasema uongo ili kuepuka matatizo. Watu wanaosema mambo yanayowaingiza kwenye matatizo kwa kiasi kikubwa sana wanaweza kuwa wanasema ukwelWanasheria wanaita hili kuwa ni “tamko dhidi ya maslahi binafsi.”)
- Kama wewe ungekuwa Paulo, ukayaangalia maisha yako ya zamani, je, ungefikiria nini kuhusu jinsi ambavyo Mungu amekuongoza?
- Je, ilikuwa ni upotezaji wa muda kwa Paulo kufundishwa na Gamalieli? (Hapana. Ilikuwa ni muhimu kwamba Paulo alikuwa ni mwanafunzi mzuri, na kwamba alikuwa na mwalimu bora kabisa, na kwamba alijawa na msukumo. Alichohitaji sasa kilikuwa ni kuelewa mapenzi ya Mungu kwa ajili ya maisha yake kwa uzuri zaidi.)
- Rafiki, je, vipi kukuhusu wewe? Je, unapambana kwa ajili ya kupata mafanikio katika yote uyafanyayo? Je, Mungu amekupatia talanta ambazo unazitumia kuuendeleza ufalme wake? Je, u wazi ili uweze kuongozwa na Roho Mtakatifu katika njia ambazo hukuzitarajia?
- Angalia tena sentesi ya kwanza ya matendo 22:10. Kama ungekuwa na elimu kama ya Paulo, ari yake kwa sheria ya Mungu, na hati yake ya mamlaka kutoka baraza la Sanhedrin kuwaangamiza Wakristo, je, ungekuwa unauliza hili swali? (Maisha yako yote yamepinduliwa juu chini! Ulidhani kwamba ulikuwa ukimtii Mungu. Ulidhani kwamba Yesu alikuwa mlaghai/mdanganyifu. Sasa unabaini kwamba Yesu ni Mungu! Kwa kweli kabisa hutajua nini cha kufanya.)
- Juma lijalo: Mamlaka ya Paulo na Injili.