Umoja Katika Injili

(Wagalatia 2:1-14)
Swahili
Year: 
2011
Quarter: 
4
Lesson Number: 
3

Utangulizi: Juma lililopita tulijifunza kwamba Paulo alikuwa na madai ya kushangaza kuhusiana na chanzo cha ujumbe wake. Alidai kwamba Yesu mwenyewe ndiye aliyemfundisha, na kwamba hakuna mtu mwingine yeyote yule aliyewajibika kwa ujumbe aliokuwa akiutangaza. Tulipochunguza suala hili, tulijifunza kwamba Luka na Petro waliyaamini madai na fikra za Paulo kwamba Paulo alikuwa anashiriki nao ujumbe alioujifunza moja kwa moja kutoka kwa Mungu. Juma hili tunaendeleza mjadala kuhusu kama Paulo ana ujumbe unaotofautiana na ule wa viongozi wengine wa kanisa la awali. Je, umoja ni muhimu? Je, suala la kutokukubaliana kanisani ni jambo jema? Je, tunapaswa kuwa na “Wakristo” na “akina Paulo?” Au, je, injili ya haki kwa imani ni ujumbe unaounganishwa wa kanisa la Mungu? Hebu tuzame kwenye somo letu la Wagalatia na kujifunza zaidi!

  1. Safari ya Kurejea/Kurudi
    1. Soma Wagalatia 2:1-2. Kumbuka kwamba katika sura ya kwanza ya Wagalatia Paulo anasema kwamba alikwenda Yerusalemu kuwatembelea Petro na Yakobo. Paulo sasa anarejea. Kwa nini? (Mungu alimwambia arudi. Anasema ilikuwa ni “jibu la kufunuliwa.”)
      1. Je, unadhani lengo la Mungu lilikuwa ni lipi kwa kumtaka Paulo arejee kwenye “ofisi ya nyumbani?” (Utagundua kuwa Paulo anasema kwamba “aliwaeleza injili ile aihubiriyo katika Mataifa.” Lazima Mungu atakuwa alijihusisha na injili ile ile iliyofundishwa kwa Wayahudi na watu wa Mataifa.)
      2. Paulo anasema kwamba ana uwoga, na kwa sababu hiyo aliongea kwa faragha na uongozi. Je, ni woga upi ambao yumkini Paulo anauzungumzia?
        1. Je, woga wa Paulo ni kwamba amekosea kwenye teolojia yake?
        2. Je, ni woga ambao viongozi katika Yerusalemu hawatakubaliana naye? (Mwelekeo wote wa Wagalatia hadi hivi sasa ni kwamba Paulo alipokea ujumbe wake kutoka kwa Yesu. Hana yeyote wa kumshukuru kwa ajili ya ujumbe wake katika ofisi yake ya kule nyumbani. Kwa hiyo, haionekani kama anaogopa kwamba amekosea. Vile vile haonekani kujali sana kuhusiana na uongozi katika ofisi ya nyumbani pia. Lazima iwe kwamba anajihusisha sana kuhusiana na umoja wa kanisa.)
      3. Ni kwa jinsi gani Paulo aogope kwamba amekuwa akipiga mbio kwa muda wa miaka kumi na minne ya kazi bure? (Kumbuka kwamba Paulo anapambana dhidi ya injili ya uongo katika kanisa la Galatia. Kama hana uungwaji mkono kutoka kwenye ofisi ya nyumbani, je, anawezaje kutarajia kuwashawishi Wagalatia kwamba yuko sahihi? Isipokuwa tu kama kuna umoja katika ujumbe, wakashifikaji wake watadai kwamba Paulo hayuko sahihi (amekosea).)
      4. Kwa nini Paulo aombe mkutano wa faragha? (Kwa hakika kabisa alikuwa na wapinzani Yurusalemu na Galatia. Mara nyingi mikutano mikubwa huwa inayumbishwa na hisia kali, badala ya kutafakari sababu za msingi. Kwa kukutana na uongozi wa juu, angeweza kuelezea kile alichokuwa akikifanya na kukifundisha kwa uhakika, na sababu za kufanya hivyo.)
        1. Je, hii inatufundisha nini kuhusu demokrasia kanisani?
    2. Soma Wagalatia 2:3. Je, Paulo alifanikiwa? (Utakumbuka kwamba mojawapo ya jambo kubwa lilikuwa ni tohara. Uongozi haukupendekeza kwamba mmojawapo wa wasaidizi wa msingi wa Paulo alipaswa kutahiriwa.)
    3. Soma Wagalatia 2:4-5. Elezea jinsi ambavyo unafikiria hiki kitendo cha “upelelezi” kilifanya kazi? (Paulo hakuwa akifanya kazi katika nyakati za simu, barua pepe na televisheni. Je, viongozi wa kanisa kule Yerusalemu wangewezaje kujua kwamba alikuwa akifundisha isipokuwa kama yeye (au watu wengine) alitoa taarifa ya kile alichokuwa akikifanya? Pendekezo ni kwamba maadui wa kiteolojia wa Paulo walikuwa wakipeleka taarifa za uongo kwa viongozi kule Yerusalemu. Mungu alimfunulia Paulo kwamba alipaswa kufanya safari kuelekea kwenye ofisi ya nyumbani ili kuwaelezea ukweli.)
      1. Je, Paulo anazungumza na nani anaposema “hatukujitia chini yao hata saa moja?” (Paulo anazungumza na washiriki wa kanisa la Galatia na anawarejea wapinzani wake wa kiteolojia.)
        1. Je, nia ya Paulo kusema jambo hili ni ipi? Hebu jiweke kwenye nafasi ya mshiriki wa kanisa la Galatia unapojibu swali hili. (Kama vile ambavyo viongozi katika ofisi ya nyumbani hawakujua kile ambacho Paulo alikuwa akiwafundisha watu wa Mataifa, vivyo hivyo washiriki wa kanisa la Galatia hawakujua kile ambacho Paulo alikuwa akikisema kwenye taarifa yake kwa ofisi ya nyumbani. Angeweza kusema kwa kila kundi kile tu ambacho walitaka kukisikia. Paulo anawahakikishia Wagalatia kwamba hafanyi kitu kama hicho. Ana ujumbe ule ule bila kujali kama hadhira yake ni Wayahudi katika ofisi ya nyumbani au makanisa ya Mataifa.)
    4. Soma Wagalatia 2:6-9. Je, viongozi muhimu ni wapi? (Paulo anawataja: Yakobo, Petro na Yohana.)
      1. Je, Paulo anaonekana kuwa kama mwasi hapa? (Ndiyo. Je, umewahi kubaini kwamba mtu fulani “atalipa zaidi” kwa sababu ya msingi wa matatizo flani flani? Nimewahi kuona hili – kanisa linalojizatiti kwenye tatizo linajikita zaidi katika eneo hilo. Paulo hahitaji kuwa na mashaka kwa umuhimu wa Yakobo, Petro na Yohana ili azidishe/aongezee mamlaka yake mwenyewe. Lakini, hivyo ndivyo ninavyoelewa kauli zake zinazoonekana kupunguza umuhimu wa uongozi katika ofisi ya nyumbani.)
      2. Je, inaonekana kuwa jambo la ajabu kwamba Paulo alikuwa na dosari binafsi? (Muda, utamaduni, muktadha na tafsiri vinafanya hitimisho langu kuhusu mtazamo wa Paulo kuwa usioeleweka. Lakini, kama niko sahihi basi inaibua tu umuhimu wa neema!)
    5. Hapo awali nilikuuliza kuhusu demokrasia kanisani. Paulo anasema kwamba alipokea ujumbe wake moja kwa moja kutoka kwa Yesu (Wagalatia 1:1), na kwamba alishiriki ujumbe huo na uongozi wa juu kwanza. Inaonekana wazi kwamba Paulo haangalii kura za watu wachache miongoni mwa watu ili athibitishe mawazo yake. Anaonekana kuangalia uthibitisho wa mawazo yake kutoka kwa viongozi katika ofisi ya nyumbani, badala ya kuwa radhi kupokea maelekezo kutoka kwa viongozi. Je, ni aina gani ya uongozi wa kanisa utakaopatikana kutokana na mitazamo ya aina hii? (Njia pekee ya kuoanisha kauli na mwenendo wa Paulo hapa na uongozi wa kanisa ni kuamini kwamba Paulo alikuwa na uhakika kwamba ujumbe wake ulitoka kwa Mungu, na kwamba Mungu atayafanya mapenzi yake kwa uwazi kabisa kwa uongozi.)
  2. Masikini
    1. Soma Wagalatia 2:10 na Matendo 2:44-47. Je, umaskini uliotajwa kwenye Wagalatia ni matokeo ya maamuzi ya kiuchumi ya kanisa la awali? (Kihistoria, unapoondoa kichocheo cha kufanya kazi kwa ajili ya kupata faida, kinachofuatia ni umaskini. (Angalia Mithali 16:26 & Mithali 14:23.) Hata hivyo, Matendo 11:27-29 inapendekeza kuwa njaa kubwa inaweza kuwa sehemu ya tatizo. Utabaini kwamba hii njaa kubwa inaukabili ufalme wote wa Rumi.)
      1. Kati ya mahitaji yote ya kiteolojia ambayo viongozi wa kanisa wangeweza kuyaweka kwa Paulo, hili pekee ndilo. Je, hiyo inapendekeza nini kuhusu umuhimu wa kuwasaidia maskini? Au, je, hii inafundisha kwamba kuwasaidia maskini ni pendekezo tu?
      2. Utabaini kwamba watu wa Mataifa hawakuombwa kuenenda kwa mujibu wa Matendo 2:44-47. Kwa nini hivyo? (Hebu subiri. Matendo 2:45 inasema kwamba waumini walipewa kile walichokuwa na haja nacho. Pendekezo kwa watu wa Mataifa katika Wagalatia 2:10 ni kuwasaidia maskini – wale walio wahitaji.)
  3. . Petro Dhidi ya Paulo
    1. Soma Wagalatia 2:11-14. Hebu tujadili hili kwa undani zaidi. Paulo anamkabili Petro hadharani, kiongozi mahiri wa kanisa. Je, tunapaswa kuwakabili viongozi wetu wa kanisa hadharani pale tunapodhani kuwa wamekosea?
      1. Kama jibu ni, “ndiyo,” je, nani anayepaswa kufanya hivi? Mtu yeyote, au viongozi wengine tu kama Paulo?
      2. Je, nini asili ya tatizo lililoanzishwa na Petro? (Tatizo ni hadhara. Sio tu kwamba Petro anafanya mwafaka kwenye suala muhimu, lenye teolojia iliyokuwepo kwa kipindi hicho, bali pia watu wa Mataifa wanadhalilishwa kwa kufikirishwa kuwa wao ni Wakristo wa daraja la pili. Sidhani kwamba viongozi wanapaswa kukabiliwa hadharani kuhusiana na matatizo binafsi, yanapaswa kuwa matatizo ya hadhara.)
        1. Vipi kuhusu swali la nani anayepaswa kumkabili kiongozi? (Paulo alipokea ujumbe wake kutoka kwa Yesu. Ujumbe wake ulithibitishwa na viongozi wa kanisa. Kweli hizo mbili ni za muhimu sana kwenye suala la kuwakabili viongozi wa kanisa.)
      3. Angalia fungu hilo kwa undani zaidi na baini tofauti kati ya kile Paulo anachokifikiria na kile anachokisema. Je, kuna tofauti gani kati ya vitu hivyo viwili? (Mawazo yake ni makali, lakini kile anachokisema ni kauli ya ukweli usiopingika ukifuatiwa na swali.)
        1. Je, sababu ni ipi ya kwa nini Paulo atumie swali kukabiliana na Petro? (Alimtaka Petro ajibu swali kwa njia ambayo ilimtia Petro hatiani kosa lake. Linganisha 2 Samweli 12:1-10 ambapo Nathani anaomba ushauri wa Mfalme Daudi. Swali linawasilishwa kama kisa, na jibu la Daudi linamtia hatiani kutokana na dhambi yake.)
        2. Je, hili ni somo kwa jinsi ambavyo sisi (au viongozi wa kanisa) tunapaswa kuukabili uongozi wa kanisa? (Huu unaonekana kuwa mfano mzuri. Fanya makabiliano ya hadhara kwa masuala ya hadhara tu. Makabiliano hayapaswi kuwa makali, badala yake yanapaswa kutafuta namna ya kumtia hatiani kiongozi kuhusu tatizo la dhambi. Ni bora zaidi kwa viongozi kuwakabili viongozi wengine. Makabiliano hayatakiwi kuwepo bila uungwaji mkono wa uongozi wa kanisa kwenye mada husika na uongozi wa Roho Mtakatifu.)
      4. Rafiki, Mungu anajihusisha sana na umoja wa kanisa lake. Je, utaomba na kufanya bidii kwa ajili ya kanisa lenye umoja?
    2. Juma lijalo: Haki kwa Imani Pekee.