Safari ya Tatu ya Kimisionari

Swahili
(Matendo 18-20)
Year: 
2018
Quarter: 
3
Lesson Number: 
10

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Katika somo letu la Matendo tunasoma kwamba kuna nyakati Paulo alizuiliwa na Roho Mtakatifu asiingie Asia. Hatujui sababu, kwa kuwa Asia ipo kwenye mpango (ramani) wa Mungu kwa ajili ya kazi ya Paulo ya Kiinjilisti. Tunajua hilo ni kweli kwa sababu juma hili somo letu linajikita kwenye kazi ya Paulo katika Efeso, uliokuwa mji mkuu wa Jimbo la Asia. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tujifunze zaidi!

 1.    Efeso na Apolo

  1.    Soma Matendo 18:23. Mji wa Antiokia unaonekana kuwa “kitovu” cha Paulo. Hata hivyo, anaondoka na kusafiri tena (angalia Matendo 18:19-22) kuelekea Efeso. Mwelekeo wa kazi ya Paulo unatufundisha jambo fulani kuhusu waumini wapya, unadhani ni jambo gani hilo? (Unatakiwa kuwafuatilia. Unatakiwa kuwaimarisha. Hupaswi tu kuwaongoa na kuwaacha wenyewe.)

  1.    Soma Matendo 18:24. Kuna jambo lolote linaloonekana kuwa la kushangaza kwa Apolo? (Mambo mengi yanaonekana kuwa ya kushangaza. Biblia inatuambia kuwa yeye ni Myahudi, lakini alizaliwa Misri na jina lake linatokana na mungu wa Kiyunani, Apolo. Yumkini wazazi wake walikuwa waongofu wa Kiyahudi.)

  1.    Soma Matendo 18:25. Apolo aliwezaje kufundisha kwa usahihi habari za Yesu, lakini alijua ubatizo wa Yohana pekee? (Hii inaonesha kuwa lazima itakuwa alikuwa mwongofu wa mwanzoni kabisa. Anafahamu habari za Yohana Mbatizaji na Yesu, lakini hakuijua Pentekoste.)

  1.    Soma Matendo 18:26-28. Kama wewe ni wakili mkubwa wa Yesu, lakini humwelewi Roho Mtakatifu, je, elimu yako ina upungufu? (Ndiyo. Prisila na Akila “walimwelezea [Apolo] njia ya Bwana kwa usahihi zaidi.”)

  1.    Soma Matendo 19:1-3. Kuna tatizo gani ikiwa wewe ni mwinjilisti na bado hujapokea ubatizo wa Roho Mtakatifu? (Ingawa kitabu cha Matendo hakizungumzii jambo hili moja kwa moja, inaonekana kwamba hawa ni Wakristo walioongolewa na Apolo. Kwa kuwa hakumjua Roho Mtakatifu, wao pia hawakumjua.)

  1.    Soma Matendo 19:4-7. Tunajuaje kwamba Roho Mtakatifu amewajia? (“Walinena kwa lugha na kutabiri.”)

   1.    Soma Matendo 2:4, Matendo 10:45-46 na 1 Wakorintho 12:7-10. Kwa nini kunena kwa lugha na unabii ni uthibitisho wa Roho Mtakatifu? (Sio tu kwammba kunena kwa lugha na unabii vilitumika hapo awali kama uthibitisho, bali pia vinabainishwa wazi wazi kama karama zinazotolewa na Roho Mtakatifu.)

    1.    Kama bado hujanena kwa lugha wala kutabiri, je, unapaswa kuwa na wasiwasi kwamba unaweza kuwa kama Apolo au wanafunzi kumi na wawili?

 1.   Efeso na Miujiza

  1.    Soma Matendo 19:8-9. Je, unao marafiki ambao umewashirikisha injili na wakaishia kuikataa imani yako? Jambo jema la kufanya hapa ni lipi? (Ondoka. Umepeleka injili. Yaliyosalia ni kazi ya Roho Mtakatifu na huyo mtu.)

   1.    Kuna tofauti gani ikiwa wataamini? (Badala ya kuondoka tu, Paulo anawaendea tena ili kuwaimarisha wale walioamini.)

  1.    Soma Matendo 19:10-12. Unazizungumziaje lezo na nguo za “uponyaji” zilizotoka mwilini mwa Paulo?

   1.    Fikiria taswira ya jambo hili kichwani mwako. Inaonekana kwamba watu wanamwendea Paulo, wakimgusa kwa vipande vya nguo, na kisha wanaondoka haraka haraka kwenda kuwagusa wagonjwa. Kisha mgonjwa anapona. Imani ya nani inahusika kwenye huu mchakato? (Mtu anayeshughulika na kipande cha nguo ndiye ambaye matendo yake yanaakisi imani zaidi.)

   1.    Utaona kwamba Biblia inaiita hii miujiza kuwa ni “miujiza ya kupita kawaida.” Bila shaka si ya kawaida, lakini ninadhani kila muujiza si wa kawaida. Tunapaswa kujifunza nini kwa kuiita miujiza hii kuwa “si ya kawaida?” (Huenda dhana ni kwamba hii si njia ambayo Mungu anatenda kazi kwa njia ya kawaida.)

  1.    Soma Matendo 19:13. Je, waliondoa pepo wachafu hapo kabla? (Inaonekana kuwa walifanya hivi siku za nyuma, au angalao walijifanya kufanya hivyo.)

   1.    Soma Mathayo 12:27. Hii inaashiria nini kuhusu haya matendo ya baadhi ya viongozi wa dini ya Kiyahudi? (Hii inaashiria kuwa waliweza kuondoa pepo kwa uwezo wa Mungu.)

   1.    Soma Luka 9:49-50. Je, wanafunzi wanatilia shaka kwamba huyu mtu “asiyefuatana nasi” anatoa pepo? (Hawalalamiki kwamba anafanya mambo bandia, wanalalamika kwamba wanafanya hivi ingawa si miongoni mwa wanafunzi kumi na wawili.)

  1.    Soma Matendo 19:14-16. Tunajifunza nini? Kwamba baadhi ya pepo ni wagumu kuliko wengine? Wengine wanaipa mamlaka changamoto?

   1.    Je, kipigo hiki kinapaswa kututia wasiwasi ikiwa tunatumia jina la Yesu kuondoa pepo? (Hiki ni kisa cha kufurahisha sana. Inaonekana kwamba hii ilifanya kazi kwa baadhi ya pepo, hivyo kwa dhahiri baadhi ya pepo wana woga zaidi kuliko wengine. Hata hivyo, hakuna uthibitisho kwamba hawa wana wa Skewa walikuwa waongofu wa Kikristo. Walikuwa tu wanatumia majina ya Yesu na Paulo.)

  1.    Soma Matendo 19:17-20. Jambo gani jema linatokana na hiki kipigo? (Inabainisha kuwa Yesu ndio nguvu ya kutenda mambo mema na pepo wana uwezo wa kutenda mambo mabaya. Jambo zuri zaidi ni kwamba, Yesu anaoneshwa kuwa na nguvu zaidi, na kwamba kumkubali kikamilifu ndiko kunakotakiwa ili kuushinda uwezo wa dhambi.)

 1. Efeso na Artemi

  1.    Soma Matendo 19:23-26. Malalamiko ya Demetrio yana asili gani? (Mapato yanayotokana na biashara yanaporomoka kwa sababu ya Paulo.)

  1.    Soma Matendo 19:27. Hoja ya pili ya Demetrio ni ipi? (Mungu mke, Artemi atashushwa hadhi. Hoja yake ya kiteolojia ni ya pili.)

  1.    Soma Matendo 19:28-31. Ikiwa suala la kiteolojia ni jambo dogo (la pili) kwa nini wanapiga kelele kuwa “Artemi wa Efeso ni mkuu?” (Isingekuwa na wito ule ule ikiwa wangepiga kelele kuwa “Ifanye akaunti yangu ya benki iwe nono!”

  1.    Soma Matendo 19:32-33. Je, asili ya kundi la watu wenye fujo imebadilika baada ya miaka mingi? Hii inabainisha kuwa watu wengi hawakujua sababu ya kuwepo kwao pale!

  1.    Soma Matendo 19:34. Kwa nini baada ya kutambua kuwa Iskanda ni Myahudi iliwafanya watu waendelee kupiga kelele? (Wayahudi wanaamini jambo lile lile wanaloliamini Wakristo kuhusu ibada ya sanamu.)

  1.    Soma Matendo 19:35-41. Una maoni gani juu ya ubora wa uhalali kisheria wa maelekezo ya karani wa mji? Hii inalinganishwaje na hatua nyingine za kisheria alizokabiliwa nazo Paulo? (Huu ni mfano wa hatua stahiki. Zamani kabla ya hapo, hatua iliyokuwepo ilikuwa ni kumfunga au kumpiga Paulo na kisha kuuliza maswali baadaye. Katika Efeso, Mahakama, na si vipigo, ndizo njia sahihi za kutanzua migogoro.)

 1.   Troa na Eutiko

  1.    Soma Matendo 20:6-7. Hii ni siku gani ya juma? (Kumbuka kwamba kwa hesabu za Kiyahudi, siku moja inaisha na siku nyingine inaanza nyakati za kuzama kwa jua. Hiyo inamaanisha kuwa huenda hii ni Jumamosi jioni.)

   1.    Kwa nini siku hii imechaguliwa ili “kumega mkate?” (Paulo alikuwa anaondoka siku inayofuata. Biblia haitoa sababu ya kidini ya kukutana kwao, bali sababu ya kivitendo.)

    1.    Je, unaweza kuona sababu ya kidini katika jambo hili? (Paulo hatasafiri siku ya Sabato. Hivyo, anaondoka Jumapili asubuhi.)

  1.    Soma Matendo 20:8-9. Je, Paulo ana mahubiri mafupi yaliyo hai? (Kwa dhahiri hapana. Kifungu kinasema “Paulo alipoendelea sana kuhubiri,” na angalao mtu mmoja alizidiwa usingizi na kulala. Baadaye tunasoma kuwa aliendelea kunena hadi alfajiri.)

  1.    Soma Matendo 20:10-12. Ninaamini hii ni mara pekee ambapo kumbukumbu inaandikwa kuwa Paulo alimfufua mtu. Je, njia aliyoitumia Paulo inatofautianaje na ile ya Petro? (Soma Matendo 9:39-40. Paulo hatendi jambo hili kifichoni. Kimsingi, anapunguza asili ya huu muujiza usio wa kawaida kwa kwaambia watu wasifanye ghasia na kwamba Eutiko yu hai. Mtu anaweza kupotoka na kusahau kwamba kimsingi Eutiko alikuwa amekufa.)

   1.    Sipendi mahubiri marefu. Kwa ujumla, mahubiri marefu yanaakisi kutojipanga na kutojiandaa kwa mzungumzaji. Inahitaji maandalizi marefu ili kuweza kuzungumza kwa kifupi na kwa ufasaha, kama ambavyo inahitaji muda mrefu ili kuweza kuandika kwa ufupi na kwa ufasaha. Ingawa ninajihangaisha na kitendo cha Paulo kuzungumza usiku kucha, Paulo haruhusu kitendo cha kumfufua mtu kiingilie hubiri lake la usiku kucha. Hii inaashiria nini kuhusu ujumbe wa Paulo? (Yumkini Paulo alidhani kuwa hatarejea Troa. Kwa dhahiri, alitaka kusema kila alichoweza kukisema ili kiwasaidie katika siku zijazo, na hakutaka “jambo dogo” kama la ufufuo liingilie kati hubiri lake.)

  1.    Rafiki, je, umempokea Roho Mtakatifu? Je, uko radhi kumruhusu Roho Mtakatifu ayaongoze maisha yako? Kwa nini usimwombe Roho Mtakatifu ayaongoze maisha yako sasa hivi?

 1.    Juma lijalo: Kukamatwa Yerusalemu.

 2.    Efeso na Apolo
 3.  

  1.    Soma Matendo 18:23. Mji wa Antiokia unaonekana kuwa “kitovu” cha Paulo. Hata hivyo, anaondoka na kusafiri tena (angalia Matendo 18:19-22) kuelekea Efeso. Mwelekeo wa kazi ya Paulo unatufundisha jambo fulani kuhusu waumini wapya, unadhani ni jambo gani hilo? (Unatakiwa kuwafuatilia. Unatakiwa kuwaimarisha. Hupaswi tu kuwaongoa na kuwaacha wenyewe.)
 4.  

  1.    Soma Matendo 18:24. Kuna jambo lolote linaloonekana kuwa la kushangaza kwa Apolo? (Mambo mengi yanaonekana kuwa ya kushangaza. Biblia inatuambia kuwa yeye ni Myahudi, lakini alizaliwa Misri na jina lake linatokana na mungu wa Kiyunani, Apolo. Yumkini wazazi wake walikuwa waongofu wa Kiyahudi.)
 5.  

  1.    Soma Matendo 18:25. Apolo aliwezaje kufundisha kwa usahihi habari za Yesu, lakini alijua ubatizo wa Yohana pekee? (Hii inaonesha kuwa lazima itakuwa alikuwa mwongofu wa mwanzoni kabisa. Anafahamu habari za Yohana Mbatizaji na Yesu, lakini hakuijua Pentekoste.)
 6.  

  1.    Soma Matendo 18:26-28. Kama wewe ni wakili mkubwa wa Yesu, lakini humwelewi Roho Mtakatifu, je, elimu yako ina upungufu? (Ndiyo. Prisila na Akila “walimwelezea [Apolo] njia ya Bwana kwa usahihi zaidi.”)
 7.  

  1.    Soma Matendo 19:1-3. Kuna tatizo gani ikiwa wewe ni mwinjilisti na bado hujapokea ubatizo wa Roho Mtakatifu? (Ingawa kitabu cha Matendo hakizungumzii jambo hili moja kwa moja, inaonekana kwamba hawa ni Wakristo walioongolewa na Apolo. Kwa kuwa hakumjua Roho Mtakatifu, wao pia hawakumjua.)
 8.  

  1.    Soma Matendo 19:4-7. Tunajuaje kwamba Roho Mtakatifu amewajia? (“Walinena kwa lugha na kutabiri.”)
 9.  

   1.    Soma Matendo 2:4, Matendo 10:45-46 na 1 Wakorintho 12:7-10. Kwa nini kunena kwa lugha na unabii ni uthibitisho wa Roho Mtakatifu? (Sio tu kwammba kunena kwa lugha na unabii vilitumika hapo awali kama uthibitisho, bali pia vinabainishwa wazi wazi kama karama zinazotolewa na Roho Mtakatifu.)
 10.  

    1.    Kama bado hujanena kwa lugha wala kutabiri, je, unapaswa kuwa na wasiwasi kwamba unaweza kuwa kama Apolo au wanafunzi kumi na wawili?
 11.  

 12.   Efeso na Miujiza
 13.  

  1.    Soma Matendo 19:8-9. Je, unao marafiki ambao umewashirikisha injili na wakaishia kuikataa imani yako? Jambo jema la kufanya hapa ni lipi? (Ondoka. Umepeleka injili. Yaliyosalia ni kazi ya Roho Mtakatifu na huyo mtu.)
 14.  

   1.    Kuna tofauti gani ikiwa wataamini? (Badala ya kuondoka tu, Paulo anawaendea tena ili kuwaimarisha wale walioamini.)
 15.  

  1.    Soma Matendo 19:10-12. Unazizungumziaje lezo na nguo za “uponyaji” zilizotoka mwilini mwa Paulo?
 16.  

   1.    Fikiria taswira ya jambo hili kichwani mwako. Inaonekana kwamba watu wanamwendea Paulo, wakimgusa kwa vipande vya nguo, na kisha wanaondoka haraka haraka kwenda kuwagusa wagonjwa. Kisha mgonjwa anapona. Imani ya nani inahusika kwenye huu mchakato? (Mtu anayeshughulika na kipande cha nguo ndiye ambaye matendo yake yanaakisi imani zaidi.)
 17.  

   1.    Utaona kwamba Biblia inaiita hii miujiza kuwa ni “miujiza ya kupita kawaida.” Bila shaka si ya kawaida, lakini ninadhani kila muujiza si wa kawaida. Tunapaswa kujifunza nini kwa kuiita miujiza hii kuwa “si ya kawaida?” (Huenda dhana ni kwamba hii si njia ambayo Mungu anatenda kazi kwa njia ya kawaida.)
 18.  

  1.    Soma Matendo 19:13. Je, waliondoa pepo wachafu hapo kabla? (Inaonekana kuwa walifanya hivi siku za nyuma, au angalao walijifanya kufanya hivyo.)
 19.  

   1.    Soma Mathayo 12:27. Hii inaashiria nini kuhusu haya matendo ya baadhi ya viongozi wa dini ya Kiyahudi? (Hii inaashiria kuwa waliweza kuondoa pepo kwa uwezo wa Mungu.)
 20.  

   1.    Soma Luka 9:49-50. Je, wanafunzi wanatilia shaka kwamba huyu mtu “asiyefuatana nasi” anatoa pepo? (Hawalalamiki kwamba anafanya mambo bandia, wanalalamika kwamba wanafanya hivi ingawa si miongoni mwa wanafunzi kumi na wawili.)
 21.  

  1.    Soma Matendo 19:14-16. Tunajifunza nini? Kwamba baadhi ya pepo ni wagumu kuliko wengine? Wengine wanaipa mamlaka changamoto?
 22.  

   1.    Je, kipigo hiki kinapaswa kututia wasiwasi ikiwa tunatumia jina la Yesu kuondoa pepo? (Hiki ni kisa cha kufurahisha sana. Inaonekana kwamba hii ilifanya kazi kwa baadhi ya pepo, hivyo kwa dhahiri baadhi ya pepo wana woga zaidi kuliko wengine. Hata hivyo, hakuna uthibitisho kwamba hawa wana wa Skewa walikuwa waongofu wa Kikristo. Walikuwa tu wanatumia majina ya Yesu na Paulo.)
 23.  

  1.    Soma Matendo 19:17-20. Jambo gani jema linatokana na hiki kipigo? (Inabainisha kuwa Yesu ndio nguvu ya kutenda mambo mema na pepo wana uwezo wa kutenda mambo mabaya. Jambo zuri zaidi ni kwamba, Yesu anaoneshwa kuwa na nguvu zaidi, na kwamba kumkubali kikamilifu ndiko kunakotakiwa ili kuushinda uwezo wa dhambi.)
 24.  

 25. Efeso na Artemi
 26.  

  1.    Soma Matendo 19:23-26. Malalamiko ya Demetrio yana asili gani? (Mapato yanayotokana na biashara yanaporomoka kwa sababu ya Paulo.)
 27.  

  1.    Soma Matendo 19:27. Hoja ya pili ya Demetrio ni ipi? (Mungu mke, Artemi atashushwa hadhi. Hoja yake ya kiteolojia ni ya pili.)
 28.  

  1.    Soma Matendo 19:28-31. Ikiwa suala la kiteolojia ni jambo dogo (la pili) kwa nini wanapiga kelele kuwa “Artemi wa Efeso ni mkuu?” (Isingekuwa na wito ule ule ikiwa wangepiga kelele kuwa “Ifanye akaunti yangu ya benki iwe nono!”
 29.  

  1.    Soma Matendo 19:32-33. Je, asili ya kundi la watu wenye fujo imebadilika baada ya miaka mingi? Hii inabainisha kuwa watu wengi hawakujua sababu ya kuwepo kwao pale!
 30.  

  1.    Soma Matendo 19:34. Kwa nini baada ya kutambua kuwa Iskanda ni Myahudi iliwafanya watu waendelee kupiga kelele? (Wayahudi wanaamini jambo lile lile wanaloliamini Wakristo kuhusu ibada ya sanamu.)
 31.  

  1.    Soma Matendo 19:35-41. Una maoni gani juu ya ubora wa uhalali kisheria wa maelekezo ya karani wa mji? Hii inalinganishwaje na hatua nyingine za kisheria alizokabiliwa nazo Paulo? (Huu ni mfano wa hatua stahiki. Zamani kabla ya hapo, hatua iliyokuwepo ilikuwa ni kumfunga au kumpiga Paulo na kisha kuuliza maswali baadaye. Katika Efeso, Mahakama, na si vipigo, ndizo njia sahihi za kutanzua migogoro.)
 32.  

 33.   Troa na Eutiko
 34.  

  1.    Soma Matendo 20:6-7. Hii ni siku gani ya juma? (Kumbuka kwamba kwa hesabu za Kiyahudi, siku moja inaisha na siku nyingine inaanza nyakati za kuzama kwa jua. Hiyo inamaanisha kuwa huenda hii ni Jumamosi jioni.)
 35.  

   1.    Kwa nini siku hii imechaguliwa ili “kumega mkate?” (Paulo alikuwa anaondoka siku inayofuata. Biblia haitoa sababu ya kidini ya kukutana kwao, bali sababu ya kivitendo.)
 36.  

    1.    Je, unaweza kuona sababu ya kidini katika jambo hili? (Paulo hatasafiri siku ya Sabato. Hivyo, anaondoka Jumapili asubuhi.)
 37.  

  1.    Soma Matendo 20:8-9. Je, Paulo ana mahubiri mafupi yaliyo hai? (Kwa dhahiri hapana. Kifungu kinasema “Paulo alipoendelea sana kuhubiri,” na angalao mtu mmoja alizidiwa usingizi na kulala. Baadaye tunasoma kuwa aliendelea kunena hadi alfajiri.)
 38.  

  1.    Soma Matendo 20:10-12. Ninaamini hii ni mara pekee ambapo kumbukumbu inaandikwa kuwa Paulo alimfufua mtu. Je, njia aliyoitumia Paulo inatofautianaje na ile ya Petro? (Soma Matendo 9:39-40. Paulo hatendi jambo hili kifichoni. Kimsingi, anapunguza asili ya huu muujiza usio wa kawaida kwa kwaambia watu wasifanye ghasia na kwamba Eutiko yu hai. Mtu anaweza kupotoka na kusahau kwamba kimsingi Eutiko alikuwa amekufa.)
 39.  

   1.    Sipendi mahubiri marefu. Kwa ujumla, mahubiri marefu yanaakisi kutojipanga na kutojiandaa kwa mzungumzaji. Inahitaji maandalizi marefu ili kuweza kuzungumza kwa kifupi na kwa ufasaha, kama ambavyo inahitaji muda mrefu ili kuweza kuandika kwa ufupi na kwa ufasaha. Ingawa ninajihangaisha na kitendo cha Paulo kuzungumza usiku kucha, Paulo haruhusu kitendo cha kumfufua mtu kiingilie hubiri lake la usiku kucha. Hii inaashiria nini kuhusu ujumbe wa Paulo? (Yumkini Paulo alidhani kuwa hatarejea Troa. Kwa dhahiri, alitaka kusema kila alichoweza kukisema ili kiwasaidie katika siku zijazo, na hakutaka “jambo dogo” kama la ufufuo liingilie kati hubiri lake.)
 40.  

  1.    Rafiki, je, umempokea Roho Mtakatifu? Je, uko radhi kumruhusu Roho Mtakatifu ayaongoze maisha yako? Kwa nini usimwombe Roho Mtakatifu ayaongoze maisha yako sasa hivi?
 41.  

 42.    Juma lijalo: Kukamatwa Yerusalemu.