Somo la 4: Astahili Mwana-Kondoo

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Ufunuo 4:4 & 5)
Swahili
Year: 
2019
Quarter: 
1
Lesson Number: 
4

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Je, umewahi kutembelea nyumba nzuri na kukuta mlango ukiwa umefunguliwa kidogo? Je, ulitaka kuchungulia ndani? Nini kilikuzuia usichungulie? Hivyo ndivyo somo letu la Ufunuo linavyoanza juma hili! Tutakachokiona ndani kinastaajabisha! Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tuone kile ambacho Mungu anatufundisha!

 

  1.     Mlango

 

    1.     Soma Ufunuo 4:1. Fikiria kwamba wewe ndiye uliyesimama mbele ya mlango ulio wazi. Una sababu gani za kukufanya utake kuingia? (Udadisi! Sio tu kwamba nitataka kuona kilichopo nyuma ya mlango, ningependa pia kusikia “kitakachofuata baada ya hapo.” Kimsingi, Yohana pia alikaribishwa ndani!)

 

      1.     Nani anazungumza na Yohana? (Tulijifunza kwenye somo letu la Ufunuo sura ya 1 kwamba “sauti kuu kama sauti ya baragumu” (Ufunuo 1:10) ni Yesu (Ufunuo 1:12-13).)

 

      1.     “Huku” ni wapi (“Panda hata huku”) palipo nyuma ya mlango? (Tutajifunza katika sehemu inayofuata kwamba hiki ni kiti cha enzi cha Mungu.)

 

    1.     Soma Ufunuo 4:2-4. Tunaona nini baada ya kuingia mlangoni na kuingia kwenye chumba cha kiti cha enzi? (Tunaona kiti cha enzi na viti vingine ishirini na vinne.)

 

      1.     Nani ameketi kwenye kiti cha enzi? (Hatujaambiwa nani aliyepo kwenye kiti cha enzi, lakini kimantiki atakuwa Yesu au Mungu Baba kwa sababau kipo kwenye nafasi ya mamlaka ya juu kabisa.)

 

        1.     Kitu gani kinakizunguka hiki kiti cha enzi? (Upinde wa mvua.)

 

          1.   Unadhani kwa nini vuguvugu la haki za wasenge linatumia upinde wa mvua kama ishara yao?

 

      1.     Akina nani wamekaa kwenye viti ishirini na vinne? (“Wazee.”)

 

        1.     Je, tunawafahamu? (Hatujaambiwa hapa. Utakumbuka kwamba walikuwepo mitume kumi na wawili na makabila kumi na mawili kule Israeli. Hii inaweza kuwakilisha viongozi wa watu wa Mungu katika Agano la Kale na mitume katika Agano Jipya.)

 

    1.     Soma Ufunuo 4:5. Mara zote huwa nina mvuto kwenye maelezo ya kiti cha enzi cha Mungu yanayotupatia utambuzi wa kihalisia. Je, umeme (mwanga), sauti na ngurumo vinaashiria nini juu ya hiki kiti cha enzi? (Ni chanzo cha mamlaka. Yohana anaelezea jinsi mambo yanavyotiwa nguvu katika siku zijazo.)

 

      1.     Taa ni nini? (Tulijadili jambo hili hapo awali. Haya yanaelekea kuwa ni maelezo ya Roho Mtakatifu.)

 

    1.     Soma Ufunuo 4:6-8. Kuna kitu kati ya kiti cha enzi na viti ishirini na vinne. Ni vitu gani hivyo? (Viumbe hai.)

 

      1.     Hawa viumbe hai wamefunikwa na macho. Unadhani hiyo inamaanisha nini? (Lazima hii itakuwa ni ishara ya maarifa.)

 

      1.     Soma Ezekieli 10:12-15. Hii ni dondoo kutoka kwenye njozi ya Ezekieli. “Viumbe” hawa ni akina nani? (Ni malaika – makerubi. Kuwaita “viumbe” inamaanisha kuwa wanaweza kuwa kitu chochote. Kwa isivyo bahati, nadhani “kiumbe” inamaanisha mtazamo hasi. Kimsingi, ninaamini hawa ni malaika maalumu wenye tabia zinazoakisiwa kwenye nyuso zao. Wanachangamana na Mungu mara kwa mara.)

 

    1.     Soma Ufunuo 4:9-10 na ulinganishe na Ufunuo 4:8. Mke wangu anasema kuwa asingependa kuwa mmoja wa “viumbe” hawa kwa sababu itakuwa kazi ya uchoshi sana duniani kila mara kurudia rudia kutamka “Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu” milele zote. Je, unadhani hicho ndicho kinachoelezewa? (Sidhani kama hivyo ndivyo jinsi jambo hili linavyopaswa kueleweka. Endapo ingekuwa hivyo, basi wazee ishirini na wanne watakuwa wanaanguka kila mara na kuinuka. Hiyo haina mantiki. Badala yake, nadhani kauli ya “kamwe hawataacha kusema” inamaanisha kwamba mara zote watasalia kuwa waaminifu kwa Mungu. Mara zote watakuwa na mtazamo wa kumtukuza Mungu. Kimsingi wanapomtukuza Mungu, Wazee wanaungana nao na kuanguka mbele za Mungu. Ninahisi viumbe hawa wana kazi bora kabisa hapa ulimwenguni!)

 

    1.     Soma Ufunuo 4:11. Msingi wa kumpa Mungu utukufu ni upi? (Yeye ni Muumbaji wetu.)

 

      1.     Hii inazungumzia nini juu ya nadharia ya uibukaji? (Ni shambulio kuu kwenye sababu halisi ya Mungu kupewa utukufu mbinguni. Je, hiyo inatupatia utambuzi mkubwa zaidi kwenye ushawishi wa wasenge kutumia upinde wa mvua kama ishara yao?

 

      1.     Je, hii inabainisha ni nani aliyepo kwenye hiki kiti cha enzi? (Soma Yohana 1:1-3. “Neno” endapo utaendelea kusoma sura hii, ni rejea ya Yesu. Hivyo, hapa Yohana anasema kwamba “vitu vyote vilifanywa” na Yesu. Lakini, uelewa wa kwamba Yesu anakaa kwenye hiki kiti unaingia kwenya matatizo tutakapoingia kwenye sura inayofuata.)

 

 

  1.   Kitabu

 

    1.     Soma Ufunuo 5:1. Je, mbinguni wanajali uhifadhi wa mazingira? (Utaona kwamba kitabu kimeandikwa ndani na nyuma (pande zote).)

 

      1.     Kwa ujumla ninafanya utani kuhusu “uhifadhi” mbinguni, lakini unadhani kwa nini Yohana anaandika taarifa hii? (Huu ni uthibitisho zaidi juu ya usahihi wa njozi yake. Anaangalia mambo madogo madogo ya ndani zaidi.)

 

      1.     Kwa nini kuna “mihuri saba?” (Saba ni namba kamili, hivyo hili limepigwa mhuri kikamilifu.)

 

    1.     Soma Ufunuo 5:2-5. Nani awezaye kufungua kitabu? (Yesu. Watoa maoni kadhaa niliosoma maoni yao wanakubaliana kwamba huyu ni Yesu – kama itakavyothibitishwa kadri tunavyoendelea kusoma.)

 

      1.     Unaelezeaje suala la ustahili? Ikiwa Mungu Baba anakaa kwenye kiti cha enzi na anashikilia kitabu hiki, inawezekanaje “asistahili?” (Liweke jambo hili akilini mwako. Tutaendelea kulifunua.)

 

    1.     Soma Ufunuo 5:6. Mwana-Kondoo ni nani? (Kwa dhahiri huyu ni Yesu.)

 

      1.     “Unasimamaje” katikati ya “kiti cha enzi?” Tayari pameshaelezewa kama mahali pa kukaa! (Tunatakiwa kurekebisha kidogo mtazamo wetu juu ya hiki kiti cha enzi. Kuna angalao watu wawili kwenye hiki kiti cha enzi. Mmoja amekaa na Mwingine amesimama. Wote wawili ni Mungu. Aliyesimama, Yesu, yupo katikati. Tuna wakati mgumu kuuelewa Utatu Mtakatifu. Pendekezo langu ni kuangalia zaidi kipengele hiki kimoja cha Utatu Mtakatifu.)

 

      1.     Je, sasa Yesu ana pembe saba na macho saba? Anawezaje kuonekana kama mwanadamu na awe na sifa hizi? (Tunaambiwa kwamba macho saba ya Yesu ni ya kiishara. Hao ni Roho Mtakatifu. Saba, kwa mara nyingine, inakuwa ni ishara ya ukamilifu. Yumkini hii inamaanisha kwamba pembe saba pia ni za kiishara.)

 

        1.     Fikiria viumbe wanne wa Ufunuo 4:6-7 wenye macho yote. Je, macho haya pia ni ya kiishara? Je, maelezo yote haya ni ya kiishara? Ikimaanisha kwamba, kimsingi hawajafunikwa kwa macho na kimsingi hawana sura zinazofanana na simba, maksai, mwanadamu au tai? (Nadhani wote hawa ni ishara.)

 

        1.     Pembe hizi zinawakilisha nini? (Tuchukulie kwamba jambo hili si gumu sana kufahamuika. Pembe ya kifaru, pembe za mbuzi, au pembe za mbawala (paa) zote zinatumika kama silaha. Hii inatuambia kuwa Yesu ana uwezo (mamlaka) kamili. Linganisha na Mathhayo 28:18.)

 

    1.     Soma Ufunuo 5:7-9. Unakumbuka nilikuomba uweke akilini mwako suala la “ustahili?” Inawezekanaje Mungu Baba asistahili? Vifungu hivi vinajibuje swali hilo? (Yesu astahili kwa sababu aliishinda dhambi. Alitupatia fursa tusiyostahili ya uzima wa milele!)

 

      1.     Fikiria juu ya kitabu hiki katika muktadha wa nani anayestahili kukifungua. Tutajifunza zaidi miktadha ya kitabu kwenye sura inayofuata, lakini unadhani kitabu kinajihusisha na nini? (Tunao mustakabali mpya uliofunguliwa kwetu. Badala ya mauti ya milele, Yesu alifungua mustakabali wa uzima wa milele kwa ajili yetu. Hiyo inamaanisha kuishinda dhambi na kifo. Kimantiki, kitabu kinahusu mustakabali wetu wenye utukufu na ushindi. Sasa tunaona kwa nini Yesu ndiye pekee “anayestahili” kukifungua, kwa sababu alikifungua kwa ajili yetu.)

 

    1.     Soma Ufunuo 5:10. Ni kwa namna gani nyingine tumenufaishwa na Yesu? (Sisi sote ni makuhani. Huu ni ushindi mkubwa katika msimamo wetu wa kiroho, na usawa wetu wa pamoja kwa kila mmoja wetu.)

 

 

  1. Astahili Mwana-Kondoo

 

    1.     Soma Ufunuo 5:11-14. Nani anayemtukuza Yesu? (Kila mtu! Utaona kwamba pia wanamtukuza Mungu Baba.)

 

      1.     Kwa nini Yesu astahili? (Alishinda pambano kubwa sana hapa ulimwenguni. Aliishinda dhambi kwa kuishi maisha yasiyo na dhambi kwa ajili (niaba) yetu. Alikufa kwa ajili yetu na kufufuka kwenye uzima wa milele kwa ajili yetu. Alifaulu pale ambapo Adamu na Hawa walishindwa. Sifa kwake!)

 

    1.     Rafiki, tafakari juu ya sifa tulizozijadili. Je, unapuuzia kile ambacho Yesu amekitenda kwa ajili (niaba) yako? Je, umemkataa Yesu? Au, je, umeamini kwamba matendo yako yatakuokoa – ambayo ni namna nyingine wa kukataa kile ambacho Yesu ametutendea? Kwa nini usikubali na kupokea hii zawadi ya pekee na uungane na sifa za milele kwa Mungu wetu Mkuu!

 

  1.   Juma lijalo: Mihuri Saba.