Mavuno na Wavunaji
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Katika Mathayo 9:37, Yesu aliwaambia wanafunzi wake, “Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache.” Kwa kuwa Yesu anazungumzia juu ya uvunaji wa roho kwa ajili ya Ufalme wa Mungu, ninaongezea kuwa, “na watendakazi wenye ujuzi ni wachache zaidi.” Ninao mkono wa mundu wa zamani kwenye gereji yangu. Mundu ni zana za mkono za kuvunia ngano. Mundu zina mkono mrefu uliojikunja, na ubapa mrefu mwembamba uliochomekwa sehemu ya mwisho ya mkono. Ninafahamu jinsi mundu inavyofanya kazi, lakini nitahitaji kufundishwa kivitendo ili niweze kutumia mundu vizuri. Vipi kuhusu uvunaji wa roho? Je, tunakuwaje watendakazi wenye ujuzi kwenye hiyo kazi ya msingi? Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia ili tuone kile tunachoweza kujifunza!
- Zoezi la Majaribio
- Soma Marko 6:7. Wangapi kati yenu mlifanya kazi za majaribio kwa ajili ya kazi yako ya sasa? Je, hicho ndicho tunachokiona hapa, yaani, mafunzo kazini? (Ndiyo. Yesu anafanya uamuzi kwamba kabla hajarejea mbinguni, atawapa wanafunzi jaribio, au mazoezi kazini, kwa ajili ya kazi iliyo mbele yao ya uvunaji.)
- Angali mambo mawili ya kwanza ambayo Yesu anayafanya. Kwa nini Yesu aliwatuma wawili wawili?
- Unadhani kwa nini jambo la pili alilolifanya ni kuwapatia mamlaka juu ya pepo wachafu?
- Soma Waefeso 6:12. Katika kazi yetu ya uinjilisti leo, je, hatutilii maanani umuhimu wa vita vya kiroho?
- Soma Marko 6:8-9. Watoto walipokuwa wadogo, tulikuwa tukichukua likizo na kwenda na magari yetu makwetu. Niliamini katika kuchukua vifaa vya akiba pamoja na vipuri. Niliamini kuwa haya ni maandalizi ya busara. Je, wanafunzi hawajajiandaa? Kwa nini hawana hata vitu vya msingi – kama vile chakula na fedha?
- Je, wazo lililopo ni kuwafundisha imani ya kweli na utegemezi? (Soma Mathayo 10:10. Tafsiri ya Mathayo juu ya hili tukio inampatia Yesu sababu – na habainishi ongezeko la imani. Badala yake, Yesu anasema kuwa wale wanaonufaika na kazi ya utume wanapaswa kuitegemeza.)
- Katika siku za nyuma, idara kadhaa ziliniomba kuchangia kwenye mfuko wao ili waweze kukusanya fedha za kutosha na “kuzindua” kazi ya umisionari. Hivi karibuni zaidi, idara iliniomba kuchangia kwenye kazi ya marafiki wa karibu. Je, njia hii ina dosari? Je, wale wanaonufaika moja kwa moja na kazi ya utume ndio wanaopaswa kuichangia? (Soma 1 Wakorintho 9:6, 12 na 15. Kanuni iliyopo ni kwamba wale wanaonufaika ndio wanaopaswa kulipia, lakini sio uadilifu kuwaambia walipe.)
- Soma Marko 6:10. Kwa nini tusiangalie malazi bora zaidi? (Ukiyaangalia kwa makini maelekezo yote ya Yesu, yanaonekana kuelezea njia isiyo ngumu – usihangaishwe na mambo ya ziada na usitafute sehemu nyingine za kukaa. Jikite kwenye kazi ya kushiriki injili na watu wengine.)
- Soma Marko 6:11. Je, kuna jambo gani la kujifunza hapa litakalotusaidia kwenye juhudi zetu za sasa katika uinjilisti? (Tunapaswa kujikita kwa wale wanaotaka kusikia kile tunachokisema.)
- Wale waliosoma masomo yangu kwa miaka mingi wanaweza kukumbuka masumbufu niliyokuwa kwa majirani wangu watu wazima. Niliwafanyia “kazi” za aina nyingi, lakini yule mwanaume hakutaka kujadiliana nami suala la wokovu, na kuna wakati fulani mkewe alionekana kuwa na uhasama na mimi. Walipokuwa na matatizo, waliniita ili kuwaombea, lakini kamwe sikumwongoa hata mmoja wao. Nilidhani kwamba kushindwa huko kulikuwa ni suala langu binafsi. Je, fungu hili linaashiria nini? (Kama baadhi ya watu wanaipinga injili, endelea kwa mtu mwingine).
- Soma Marko 6:7. Wangapi kati yenu mlifanya kazi za majaribio kwa ajili ya kazi yako ya sasa? Je, hicho ndicho tunachokiona hapa, yaani, mafunzo kazini? (Ndiyo. Yesu anafanya uamuzi kwamba kabla hajarejea mbinguni, atawapa wanafunzi jaribio, au mazoezi kazini, kwa ajili ya kazi iliyo mbele yao ya uvunaji.)
- Ujumbe
- Soma Marko 6:12. Angalia ujumbe wa wanafunzi. Je, huo ndio unaopaswa kuwa ujumbe wetu leo?
- Soma Mathayo 3:1-2. Yesu alihubiri juu ya toba kwa kuwa Yesu alikuwa anakuja. Yesu alipokuja aliwatuma wanafunzi na wakaihubiri toba. Je, unajumuishaje ujumbe wa toba dhidi ya kuwa na mtazamo wa kuwakaribisha wadhambi?
- Soma Luka 5:29-30. Mafarisayo walitaka wadhambi wabadilike kabla hawajala pamoja nao, lakini Yesu anakula na wadhambi. Unadhani jambo la kwanza ambalo Yesu aliwaambia wadhambi ni lipi? (Nina mashaka kama jambo hilo lilikuwa “tubuni.” Yumkini zaidi, huenda aliwaambia, “Kwa nini tusile pamoja?”)
- Soma Luka 5:31-32. Je, ujumbe wa Yesu ni upi? (Tubuni!)
- Kivitendo, unadhani jambo hili linamaanisha nini? Je, tunapaswa kuwaambia nini watu wanaokuja kanisani kwetu kuutafuta ukweli?
- Tunapoona jambo ambalo wageni wanalitenda au wanachovaa au wanachokula ambacho hakiendani na mtazamo wetu wa jambo lililo sahihi, je, tunapaswa kuwaambia watubu kutokana na kile walichokitenda, walichokivaa au walichokula?
- Kivitendo, unadhani jambo hili linamaanisha nini? Je, tunapaswa kuwaambia nini watu wanaokuja kanisani kwetu kuutafuta ukweli?
- Soma Mathayo 21:23 na Mathayo 21:32. Je, Yesu anazungumza na watu gani? (Viongozi wakuu wa dini. Hawa ni watu wanaomwamini Mungu na wanaonekana kuzingatia matakwa ya utendaji, kuvaa na kula kwa usahihi kabisa.)
- Katika huu muktadha, je, Yesu anawaambia kuwa wafanye nini katika Mathayo 21:32? (Watubu juu ya kushindwa kwao kumwamini. Yohana pia alikuwa akihubiri juu ya kumwamini Yesu.)
- Walipokataa “kutubu” na kuikubali “njia ya haki,” je, walikuwa wamekataa jambo gani? (Neema! Kuhesabiwa haki kwa njia ya imani katika Yesu.)
- Sasa, ngoja nikuulize tena, je, ni jambo gani ambalo tunapaswa kuwaambia wageni wetu kuhusu toba? (Wanapaswa kutubu dhambi, wanapaswa kutubu kutokana na kuamini juu ya kuhesabiwa haki kwa njia ya matendo yao, wanapaswa kukubali kuhesabiwa haki kwa njia ya imani katika Yesu!)
- Ikiwa tutawaambia wageni wanaoutafuta ukweli kwamba wanatakiwa kuacha kutenda, kuvaa au kula kitu fulani ili waweze kuokolewa, je, nani anayetakiwa kutubu? (Mtu anayependekeza kwamba wokovu unapatikana kwa njia ya matendo, uvaaji na kwa njia ya chakula!)
- Soma Mathayo 21:28-30. Hiki ndicho kisa kilichotupeleka kwenye mafungu tuliyoyajadili muda mfupi uliopita. Je, mwana yupi aliyatenda mapenzi ya babaye? (Soma Mathayo 21:31. Si yule aliyesema tu mambo sahihi, bali ni yule aliyetenda jambo sahihi.)
- Hebu tujadili jambo hili. Kwa mujibu wa mafungu yanayofungamana na hiki kisa, nimependekeza kwamba watu wa kanisani wanaowaambia wageni kwamba lazima waache kutenda, kuvaa au kula kitu wanatakiwa kutubu. Kisa hiki kinasema kuwa mwana anayetenda jambo sahihi ni yule anayetenda mapenzi ya babaye. Je, pendekezo langu halikuwa sahihi? (Natumaini hapana. Badala yake, nadhani jambo hili linatuonesha pande mbili za kosa. Upande mmoja wa kosa unaangukia kwenye shimo la matendo – kwamba lazima utende au usitende jambo fulani ili uweze kuupata wokovu. Upande mwingine wa kosa unaangukia kwenye shimo la kusema kuwa dhambi ni njema. Hutakiwi kubadili chochote. Njia ya ukweli ni kwamba unakubali kumpokea Yesu kama chanzo chako pekee cha wokovu na kuyageuza maisha yako na mapenzi yako kwa Yesu.)
- Soma Luka 24:46-49. Je, mafungu haya yanatuambia kuwa ujumbe wetu kwa ulimwengu ni upi? (Tubuni na kuutafuta msamaha wa dhambi, nawe utahesabiwa haki kwa njia ya maisha, kifo na ufufuo wa Yesu.)
- Wanao ujumbe. Kwa nini wasubiri? (Uwezo, na maarifa vimeahidiwa. Tutaligeukia jambo hilo katika sehemu inayofuata.)
- Soma Marko 6:12. Angalia ujumbe wa wanafunzi. Je, huo ndio unaopaswa kuwa ujumbe wetu leo?
- Uwezo
- Soma Matendo 16:6. Kama lengo letu ni kushiriki habari njema za Yesu, kwa nini Roho Mtakatifu anatukataza tusitende kazi njema? (Roho Mtakatifu hakuwa akiwakataza kuhubiri, alikuwa tu akiwaongoza mahali wasipotakiwa kwenda.)
- Soma Matendo 16:7-10. Je, umewahi kupigwa butwaa endapo unapaswa kushiriki injili na mtu fulani? Je, tunaweza kutarajia msaada wa aina gani kutoka kwa Roho Mtakatifu? (Kisa hiki kinatufundisha kuwa Roho Mtakatifu atatuongoza kwa watu wanaotaka kuisikia injili.)
- Soma Matendo 2:1-3. Kwa nini upepo, uvumi na ndimi za moto? (Soma Matendo 2:4-6. Vilivuta usikivu wa kundi la watu. Angalia jinsi kanisa lako linavyojaribu kuwaleta watafutaji wa ukweli kanisani.)
- Soma Matendo 2:7-12. Endapo mlikuwa na kikao cha kanisa, na mkataka kushiriki injili na watu wanaozungumza lugha 15 tofauti, je, mngetimizaje jambo hilo? (Utakumbuka kwamba nilikuwa ninajilaumu kwa kutokuwa na “sauti” bora ya injili kwa majirani zangu watu wazima. Jukumu ambalo wanafunzi walikuwa wanakabiliana nalo lilikuwa haliwezekani – lugha 15 tofauti (zihesabu). Lakini Roho Mtakatifu alitatua jambo hilo.)
- Je, hilo linatufundisha nini juu ya jinsi tunavyopaswa kuwasilisha ujumbe wa injili? (Inaniambia kwamba kupata “msaada” sahihi ndilo jambo la msingi zaidi.)
- Rafiki, endapo hushiriki ujumbe wa injili na watu wengine, je, utaanza leo? Je, utashiriki ujumbe huo na wale wanaotaka kuusikia? Je, utashiriki habari za toba na wokovu kwa njia ya neema pekee? Je, utaomba ili Roho Mtakatifu akuwezeshe kupata fursa, maneno na matendo sahihi?
- Juma lijalo: Gharama ya Uanafunzi.