Kristo na Sabato
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Sabato ni muda wa pekee sana. Nilipokuwa mdogo sana, Sabato ilikuwa ni siku ambayo familia ilikuwa pamoja. Ndio maana kuna nyakati ambazo nilitamani Sabato iishe mapema kwa sababu wazazi wangu walikuwa wakiniamualia mambo ya kufanya na kutokufanya siku ya Sabato. Nilipokuwa chuoni, Sabato ilikuwa ni siku ya pekee kwani nilitumia siku hiyo kuwa na rafiki yangu wa kike na wala sikuwa nikisoma siku hiyo. Katika shule ya sheria na baadaye maishani, Sabato ilikuwa ni muda wa pekee wa kupumzika bila kujisikia hatia. Kwa kawaida huwa nina mambo mengi ya kufanya yenye ukomo wa tarehe wa kuwasilisha kazi hizo. Lakini, kwa kuwa ninaamini kuwa kufanya kazi siku ya Sabato ni dhambi, lilikuwa ni pumziko lisilo na hatia. Je, msingi wa Biblia juu ya kuichukulia Sabato kwa umakini ni upi? Je, tunapaswa kuichukuliaje Sabato? Hebu tuzame kwenye Biblia zetu ili tubaini zaidi!
- Uumbaji wa Sabato
- Soma Mwanzo 2:1-2. Unadhani kwa nini Mungu alitumia siku sita kuumba “mbingu na nchi… na jeshi lake lote?” (Kutokana na maelezo yaliyopo katika Mwanzo 1, inaonekana kwamba Mungu angeweza kuyafanya mambo yote mara moja. Lakini, alikuwa na jambo akilini mwake. Ninahisi jambo lenyewe lilikuwa ni kuwapatia wanadamu mpangilio wa kufanya kazi na kupumzika.)
- Soma Mwanzo 2:3. Sote tunaweza kufahamu hitaji la pumziko baada ya Mungu kukamilisha mambo yote, lakini kwa nini “aliibariki” siku ya saba na “kuitakasa?” (Inaonekana Mungu alihitaji muda wa pekee wa kufurahia kazi yake ya uumbaji.)
- Soma 1 Samweli 7:12-13. Samweli alikumbuka ushindi wa Waisraeli dhidi ya Wafilisti kwa kusimamisha jiwe la Eben-ezeri. Kwa nini? (Watu watakuwa wakikumbuka ushindi ambao Mungu aliwapatia.)
- Je, jiwe la Eben-ezeri ni sawa na Sabato? (Nadhani ni kitu sawa kabisa chenye kufanana na Sabato.)
- Soma Kutoka 20:8-10. Je, wanyama wanaweza kukumbuka Uumbaji? Kwa nini Mungu anawajumuisha? (Mungu anatutaka tuwapumzishe wale wote walio ndani ya udhibiti wetu. Sabato haiutegemei utajiri, uwezo au ushawishi. Sabato ni kwa ajili ya vitu vyote.)
- Soma Kutoka 20:11. Hiki ni kipindi cha maelfu ya miaka baada ya Uumbaji. Je, hii inaashiria nini kuihusu Sabato? (Ni jambo la kudumu katika kumbukizi ya Uumbaji.)
- Soma Kumbukumbu la Torati 5:12-15. Kwa nini hii kauli ya Amri ya Nne inatupatia sababu tofauti ya kuwepo kwa Sabato? (Hapa sababu ni kwamba Mungu aliwakomboa watu wake kutoka utumwani Misri. Hii inaashiria kuwa Sabato ni kumbikizi ya mambo yote yaliyofanywa na Mungu kwa ajili ya watu wake – aliumba ulimwengu mkamilifu kwa ajili yao na kuwakomboa kutoka utumwani.)
- Soma Mathayo 27:50-52. Siku chache zilizopita tulisherehekea kipindi cha Pasaka. Tunatambua kwamba fungu hili linatuelezea juu ya mateso ya Yesu kwa ajili yetu. Je, fungu hili linatuambia kuwa jambo gani lilitokea wakati Yesu alipokuwa akielekea kufa? (Pamoja na mambo mengine, watu wengi walifufuliwa.)
- Chukulia kwamba Yesu alikuwa mwanao, na mwanao aliumizwa kwa kuchubuliwa vibaya na hatimaye kuuawa. Chukulia kwamba katika kipindi hicho hicho mwanao alishinda kikombe kwenye Mashindamo Maarufu ulimwenguni. Endapo ungekuwa Mungu, je, ungemfufua Yesu wakati bado akiwa msalabani – kama ilivyokuwa kwa hawa wengine waliofufuliwa – na kumkaribisha mbinguni kwa utukufu? (Ndiyo, kwa hakika tungefanya hivyo.)
- Kwa nini Mungu alisubiri hadi Jumapili? (Huu ni mwelekeo ule ule tuliouona hapo kabla kuhusu Sabato – Yesu alipumzika kaburini siku ya Sabato ili kukumbuka kazi yake kubwa inayofuata – akituokoa kutoka dhambini na mautini. Alipumzika siku ya Sabato ili kukumbuka Uumbaji. Alipumzika siku ya Sabato ili kukumbuka uhuru kutoka utumwani Misri. Alipumzika siku ya Sabato kukumbuka ukombozi wetu kutoka katika utumwa wa dhambi na uhusiano wetu mpya na Mungu!)
- Chukulia kwamba Yesu alikuwa mwanao, na mwanao aliumizwa kwa kuchubuliwa vibaya na hatimaye kuuawa. Chukulia kwamba katika kipindi hicho hicho mwanao alishinda kikombe kwenye Mashindamo Maarufu ulimwenguni. Endapo ungekuwa Mungu, je, ungemfufua Yesu wakati bado akiwa msalabani – kama ilivyokuwa kwa hawa wengine waliofufuliwa – na kumkaribisha mbinguni kwa utukufu? (Ndiyo, kwa hakika tungefanya hivyo.)
- Soma Isaya 66:22-23. Je, tutaacha kuitunza Sabato lini? (Kamwe hatupaswi kuacha! Mungu anatuambia kuwa utunzaji wa Sabato utaendelea katika dunia itakayofanywa upya.)
- Unadhani Sabato itasimama kwa ajili ya nini? (Soma Isaya 66:24. Hii inaashiria kuwa tunashangilia ushindi mkuu wa Mungu dhidi ya uasi. Ushindi juu ya dhambi, magonjwa na kifo.)
- Sabato na Sheria ya Asili
- Hapo kabla tuliafikiana kwamba sheria ya maadili (ambayo inajumuisha ibada ya Sabato) ni ramani ya kutusaidia kuepuka kujitumbukiza kwenye matatizo kwa kuzikiuka sheria za asili za ulimwengu. Je, Sabato inakubalianaje na huo mfumo wenye mantiki?
- Soma Marko 2:23-24. Je, msingi wa mashtaka ya Mafarisayo ni upi? (Bila shaka ni kufanya kazi siku ya Sabato.)
- Soma Marko 2:25-26. Majuma mawili yaliyopita tulimsikia Yesu akitoa jibu kama hilo. Viongozi wa dini wanasema kuwa wanafunzi wake wanakiuka sheria na Yesu anawajibu kuwa “nanyi mnakiuka sheria.” Je, makosa mawili yanafanya jambo kuwa sahihi?
- Unadhani Yesu anamaanisha nini hapa? (Yesu ni mwerevu sana kiasi cha kujibu kuwa, “Nanyi pia mnafanya hivyo.” Lazima atakuwa anasema kuwa ilikuwa sahihi kwa Mfalme Daudi na washirika wake kula mikate ya Wonyesho walipokuwa na njaa. Kwa hiyo, wanafunzi wa Yesu wakiwa na njaa wanaweza kula katika siku iliyowekwa wakfu.)
- Ikiwa njaa inapiku kitu kichowekwa wakfu, je, hiyo inatufundisha nini juu ya Sabato na ulaji?
- Unadhani Yesu anamaanisha nini hapa? (Yesu ni mwerevu sana kiasi cha kujibu kuwa, “Nanyi pia mnafanya hivyo.” Lazima atakuwa anasema kuwa ilikuwa sahihi kwa Mfalme Daudi na washirika wake kula mikate ya Wonyesho walipokuwa na njaa. Kwa hiyo, wanafunzi wa Yesu wakiwa na njaa wanaweza kula katika siku iliyowekwa wakfu.)
- Soma Marko 2:27-28. Je, Yesu anamaanisha nini anaposema, “Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu?” (Sabato haipaswi kuwa siku yenye kuleta maumivu, bali inapaswa kuwa siku ya furaha. Sabato ilifanywa ili kutupatia pumziko katika majukumu yetu ya kila siku.)
- Je, Yesu anamaanisha nini anaposema kuwa Yeye (“Mwana wa Adamu”) ni “Bwana wa Sabato pia?” (Yesu aliiumba Sabato (Yohana 1:1-3), na kwa hiyo kwa mamlaka aliyo nayo anaelezea malengo yake na namna inavyopaswa kutunzwa.)
- Je, ni kwa namna gani kauli ya Yesu inaendana na uelewa wetu wa sheria ya asili? (Inatuambia kuwa kila mtu anahitaji pumziko la Sabato. Ulaji ni sehemu ya hilo pumziko.)
- Sabato na Uponyaji
- Soma Marko 3:1-2. Kwa nini viongozi wa dini wanadhani kuwa Yesu atafanya uponyaji siku ya Sabato? (Lazima atakuwa aliwahi kufanya hivyo hapo kabla. Au, kwa kiwango kidogo kabisa, walikuwa wanaanza kuuelewa mtazamo wa Yesu juu ya utunzaji wa Sabato.)
- Soma Marko 3:3-4. Kwa nini Yesu anauliza hili swali? (Anadhamiria kufundisha. Anadhani kuwa jambo hili ni la muhimu.)
- Soma Marko 3:5. Je, ilikuwa lazima kuponya mkono wa huyu mtu siku ya Sabato? (Hapana, hata kidogo. Halikuwa jambo la dharura.)
- Kwa nini Yesu alikasirika? (Alikuwa amefadhaika kwa kuwa uelewa wao wa Sabato ulikuwa umepotoka sana.)
- Je, ni jambo gani kuhusu Sabato tunalopaswa kujifunza kutokana na mfululizo huu? (Kwamba kutenda jambo jema kwa watu wengine katika siku ya Sabato kunaendana na lengo la kuwepo kwa Sabato.)
- Je, hii inasema nini kuhusu Yesu na viwango vya utunzaji wa Sabato? Je, vimepitwa na wakati (vimekoma)? (Kisa hiki kinafundisha kinyume chake. Yesu anawataka wanadamu waelewe viwango sahihi vya utunzaji wa Sabato. Kama angekuwa hajali, asingetumia muda wake kuelezea suala hili.)
- Soma Marko 3:6 na upitie tena Marko 3:4. Je, jambo hili linaelezea kiwango gani cha hasira ya Yesu? (Yesu alifahamu kuwa walikuwa radhi kutumia muda wao wa Sabato kupanga kifo chake. Kwa upande mwingine, Yesu alikuwa akitoa uzima wa kutosha.)
- Soma Yohana 5:5-6 na Yohana 5:8-11. Kwa dhahiri uponyaji huu haukuwa na udharura. Kubeba godoro haikuwa sehemu ya lazima ya uponyaji. Je, Yesu anatufundisha jambo gani?
- Soma Yohana 5:14 na Yohana 5:16-17. Tuna sehemu kadhaa hapa katika kisa hiki. Uponyaji siku ya Sabato usio wa dharura. Amri ya kubeba godoro siku ya Sabato na kuacha kutenda dhambi. Kauli inayosema kuwa Yesu anafanya kazi siku ya Sabato. Unawezaje kuziunganisha sehemu hizi ili zilete mantiki kuhusu utunzaji wa Sabato? (Kwanza, Yesu hafanyi uasi dhidi ya sheria kwa sababu anasema, “Usitende dhambi tena.” Pili, uponyaji, ubebaji wa godoro, na kazi fulani fulani vinapazwa kuendana na Sabato.)
- Je, aina gani ya kazi inaendana na Sabato? (Kuwasaidia watu wengine. Kuwainua watu wengine.)
- Vipi kuhusu kubeba godoro? (Kuwa na uwezo wa kubeba godoro lake ilikuwa ni sehemu ya muujiza wa kufanyiwa urejeshaji.)
- Rafiki, je, somo hili linakupatia ndoto ya lengo la Mungu kwa ajili ya Sabato yake? Sabato ni siku ya kushangilia kile ambacho Mungu amekitenda kwa ajili yetu ni siku ya kupumzika na kuacha kutenda shughuli zetu za kila siku. Ni siku ya kuwafanyia watu wengine urejeshaji. Je, utadhamiria kuitunza Sabato kwa usahihi?
- Juma lijalo: Kifo cha Kristo na Sheria.