Kuishi kwa Ajili ya Mungu
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Juma lililopita Petro alituambia jinsi tunavyopaswa kuhusiana na serikali, waajiri wetu na wenzi wetu. Juma hili anaendelea kutupatia ushauri katika mahusiano yetu mengine. Ninaposema “mahusiano” sizungumzii tu kuhusu kuchangamana na watu wengine. Petro anatupatia ushauri wa namna bora ya kuutangaza Ufalme wa Mungu. Je, unahisi kwamba mahusiano yako na watu wengine yanaweza kuboresheka? Je, huduma yako inaweza kuboresheka? Ikiwa ndivyo, hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia ili tuone kile tunachoweza kujifunza katika kuboresha maisha yetu na huduma yetu!
- Upatanifu/Amani/Mwafaka
-
- Soma 1 Petro 3:8-9. Hapa hadhira ni ipi? Je, ujumbe huu unawasilishwa kwa washiriki wa kanisa katika mahusiano yao na washiriki wengine wa kanisa? (Nadhani hivyo kwa sababu Petro anasema, “kupendana kidugu.”)
-
-
- Matokeo ya kujibu matusi kwa baraka ni yapi? (Tunabarikiwa.)
-
-
- Soma 1 Petro 3:10-12. Kuna thawabu gani mahsusi zinazotokana na kuwa mwaminifu na kuepuka uovu? (Utaweza kuyafurahia maisha. Utaziona “siku za fanaka.” Kwa kuwa Mungu ndiye mshirika wako, utayafurahia maisha zaidi, wakati Mungu anapowapa kisogo watu watendao uovu.)
-
- Soma 1 Petro 3:13. Nchini Marekani ni kinyume cha sheria kuwabagua waajiriwa (wafanyakazi) kutokana na imani zao za kidini. Hii inawafundisha nini wafuasi wa Mungu zaidi ya ulinzi wa kisheria tu? (Kama wewe ni mfanyakazi mzuri, waajiri watataka kuendelea kuwa nawe. Ulinzi bora kabisa maishani sio sheria, bali ni mjibizo (reaction) wa wale wanaomwona Yesu akiakisiwa ndani yako.)
- Mtazamo Sahihi
-
- Soma 1 Petro 3:14. Je, mara zote ni kweli kwamba kama una hamu ya kutenda mema, basi watu wengine watakufurahia? (Angalia kilichomtokea Yesu. Kuna uovu ulimwenguni, na uovu unataka kuudhuru wema. Hivyo, kuna jambo la pekee (lisilofuata kawaida) katika kanuni ya jumla.)
-
- Angalia tena 1 Petro 3:14. Kwa nini Petro anaongezea “msiogope kile wanachokiogopa?” (Kwa sababu, ikiwa tunatenda mema, Mungu atatuangalia kwa upekee.)
-
- Soma 1 Petro 3:15-17. Tumejadili mtazamo tunaopaswa kuwa nao kwa washiriki wenzetu wa kanisa. Tunapaswa kuwa na mtazamo wa namna gani kwa wapagani? (Tunapaswa kujiandaa kukabiliana nao. Tunapaswa kuwa na jibu kwa ajili ya imani yetu kwa Yesu. Tunapaswa kuwasilisha hoja zetu kwa “upole na heshima.”)
-
-
- Je, upole na heshima ni jambo rahisi? (Hii ni dhambi ninayoikiri. Nje ya masomo haya ya Biblia, nimeandika makala za kuwadhihaki watu wanaoshambulia vikali imani yangu. Ucheshi ni silaha yenye nguvu sana, na nina umahiri (ustadi) katika eneo hili, lakini nina mashaka kama nimeshawahi kumshawishi mtu akubaliane na mtazamo wangu kwa kumdhihaki mtu huyo. Petro anasema “Usifanye hivyo.”)
-
-
- Petro anajenga hoja yake juu ya jambo gani, kwamba tunapaswa kutenda mema kuwa wapole na kuwaheshimu watu wanaotenda uovu? (Soma 1 Petro 3:18. Mtazamo wa kujitoa nafsi ndivyo jinsi ambavyo Yesu alituokoa. Ni mkazo wa injili – Yesu aliwafia wale ambao ni waovu, na hiyo inakujumuisha wewe pamoja na mimi. Kutumia ucheshi dhidi ya wapagani ni kusema, “Mimi ni mwerevu zaidi yako na nitakuaibisha kutokana na hoja zako zisizo na mashiko. Ni kujitumikia wewe mwenyewe, sio kutokuwa na ubinafsi.)
-
- Soma 1 Petro 3:19-21. Je, Yesu alikwenda toharani au kuzimu ili kuwahubiri wale ambao hawakumsikiliza Nuhu?
-
-
- Ikiwa ndivyo, kwa nini awahubiri wale tu waliompuuzia Nuhu? Je, kuna sehemu maalum kuzimu kwa wale waliompuuzia Nuhu? (Kwa kuuliza maswali haya pekee kunaonesha kuwa maoni ya Petro hayakomei kwa hadhira ya Nuhu. Petro anasema tu kwamba Yesu alipokufa kwa ajili ya wasio na haki, alikufa kwa wasio na haki wa nyakati zote – wakiwemo wale walioishi na kufa kabla Yesu hajafufuka kutoka kaburini.)
-
-
-
- Kwa nini kwa mahsusi kabisa hadhira ya Nuhu inatajwa? (Soma Mwanzo 6:3. Hii inaelezea kwamba Roho Mtakatifu alikuwa akishindana na wanadamu katika kipindi cha miaka 120 ambayo Nuhu alikuwa akihubiri na kujenga safina.)
-
-
-
- Kwa nini anabainisha maji ya gharika? (Petro anamtumia Nuhu kama mfano wa vitu viwili. Kwanza, kwamba Roho Mtakatifu amekuwa akifanyia kazi mioyo ya wanadamu kabla Yesu hajaja kukaa nasi. Pili, gharika ni mfano wa uoshaji wa dhambi. Gharika liliwafutilia mbali watu wadhambi. Ubatizo unaosha maisha yako ya kale ya dhambi. Kwa njia ya ufufuo wa Yesu, unazaliwa mara ya pili katika uzima wa milele.)
-
-
- Soma 1 Petro 3:22. Nini matokeo ya mtazamo wa unyenyekevu wa Yesu alipokuwa hapa duniani? (Sasa yupo mkono wa kuume wa Mungu na wengine wote (malaika na enzi na nguvu) wanajitiisha kwake.)
-
-
- Je, jambo hilo litakuwa la kweli hapa? Ikiwa unajinyenyekeza kwa Mungu na kwa mamlaka, je, utapewa mamlaka?
-
-
- Soma 1 Petro 4:1-2. Je, ungependa “kuachana na dhambi?” Vinfungu hivi vinapendekeza njia gani tunayoweza kuachana na dhambi? (Yesu aliteseka kwa sababu ya dhambi zetu. Tunateseka kutokana na dhambi zetu. Ikiwa tutaangalia kwa makini uhusiano kati ya mateso na dhambi, tutajua kwamba tamaa ya wanadamu waovu ndio njia ya kuelekea matatizoni, bali kuyashikilia mapenzi ya Mungu ni njia inayotuelekeza kwenye siku za fanaka na maisha ya furaha.)
-
- Soma 1 Petro 4:3-4. Ikiwa maelezo haya yanaelezea maisha yako ya zamani, je, unaweza kuthibitisha kwamba marafiki wako wa zamani wanashangaa kwa nini umeuacha mtindo wao wa maisha? Je, wamekughasi baada ya kugeuka na kuachana na maisha yako ya zamani?
-
- Soma 1 Petro 4:5-6. Marafiki wako waliomkataa Mungu watakabiliana na nini? (Hukumu.)
-
-
- Je, injili inahubiriwa kwa wafu? (Angalia tena 1 Petro 3:19-20. Nadhani Petro anazungumzia jambo lile lile – anasema kuwa injili ilihubiriwa kwa wale walioishi kabla Yesu hajaja duniani, watu waliokufa zamani sana. Ikiwa walimkiri Mungu, majina yao yanaandikwa kwenye kitabu cha uzima. Ikiwa hawakumkiri, wanahukumiwa kwa matendo yao. Angalia Warumi 20:11-15.)
-
- Mwisho U Karibu
-
- Soma 1 Petro 4:7. Hii ni mara ya tatu Petro anazungumzia kuhusu kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya maombi yetu. Hapo awali alibainisha jambo hili katika 1 Petro 3:7 na 1 Petro 3:12. Kwa nini uwezo wa “kujidhibiti” na kuwa na “mawazo sahihi” vinatusaidia katika maombi? (Hatupendi kuvurugwa mawazo. Tunataka kuwa na mawazo bayana. Tunataka tuwe na uwezo wa kutambua kile ambacho Roho Mtakatifu anatuambia majibu ya maombi yetu yanapojibiwa.)
-
- Soma 1 Petro 4:8. Je, wewe ni mtu mwenye mwelekeo wa kutenda makosa na kuwakebehi na kuwajeruhi watu wengine? Njia bora ni ipi kwa watu walio na “dhambi nyingi sana” za kuficha? (Kuwa na upendo. Kudhihirisha upendo kunarekebisha kasoro nyingi.)
-
- Soma 1 Petro 4:9-10. Kukaribishana, kutendeana wema na kuhudumiana kunahusianaje na upendo? (Hii inawaonesha watu wengine neema ambayo Mungu ametuonesha.)
-
- Soma 1 Petro 4:11. Mojawapo ya kazi zangu ni kuwashauri waajiriwa walio na vipingamizi vya kidini katika kushiriki kwenye vyama vya wafanyakazi. Hii inamhitaji mwajiriwa akifahamishe chama cha wafanyakazi kuhusu imani zake za kidini. Kwa miongo kadhaa, nimekuwa na waajiriwa kadhaa waliokiandikia chama cha wafanyakazi ujumbe kwa kutumia lugha unayoweza kuipata kutoka kwenye tafriri ya Biblia ya Mfalme Yakobo (KJV). Hizia zangu ni kwamba waajiriwa hawa hawakuwa waaminifu (wanyofu) kwenye imani zao za dini. Walidhani kuwa wataonekana kuwa ni watu wa dini sana kwa kuandika kwa namna hii. Je, hiki ndicho anachokimaanisha Petro anapotuambia kuwa tunapaswa “kusema kama mausia ya Mungu?” (Ukipitia vifungu vilivyotangulia, Petro anatuambia kuhusu kuwahudumia wengine. Petro anatushauri, “Tafakari jinsi ambavyo Yesu angeshughulikia jambo hili.” Kauli maarufu ni, “Je, Yesu angefanya nini?”)
-
-
- Unavunaje “nguvu ambayo Mungu anaitoa?” (Mwombe Mungu. Habari njema ni kwamba huna haja ya kutenda mambo haya kwa kutumia nguvu zako.)
-
-
-
- Mungu anatusihi tufanye nini? (Anatafuta ubora, jitihada [bidii] na uadilifu katika kazi yetu ya injili. Uwezo wake usio na mipaka upo kwa ajili yetu!)
-
-
-
-
- Ni mara ngapi umeona kazi ya kanisa inayofanywa kihobelahobela (kiholelaholela) na kwa namna isiyo ya kitaalam? Je, umewahi kuwaona washiriki wa kanisa wakifanya uamuzi katika dakika ya mwisho kabisa kwamba nani afanye nini katika huduma ya kanisa (ibada)? Je, umewaona wachungaji wanaotumia muda mchache sana kuandaa mahubiri na matokeo yake wanahubiri mahubiri marefu yasiyo na mpangilio? (Mifano hii inakiuka kanuni za ubora, uaminifu na uadilifu.)
-
-
-
-
- Angalia sehemu ya mwisho ya 1 Petro 4:11. Petro anasema kuwa lengo la huduma bora ni lipi? (Kumpa Mungu utukufu! Jiulize kama kazi yako inampa Mungu utukufu?)
-
-
- Rafiki, chunguza mahusiano yako na huduma yako kwa Mungu. Je, vinahitaji maboresho? Kwa nini usimwombe Roho Mtakatifu ayaongoze upya mahusiano yako na kuboresha huduma yako?
Juma lijalo: Kuteseka kwa Ajili ya Kristo.