Walimu wa Uongo

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(2 Petro 2:1-22)
Swahili
Year: 
2017
Quarter: 
2
Lesson Number: 
11

 

 

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Unajuaje, katika suala la kumjua Mungu, kwamba mtu fulani anakupotosha? Unajuaje kama ninakuelekeza kwenye njia ya uongo katika masomo haya? Katika kujitetea kwangu ninasema kwamba: maswali yangu yanaanza kwa kukutaka usome Biblia. Ni vigumu kuwa mbali sana kwa kuiacha njia wakati rejea yako kuu ni Biblia! Petro anaionya hadhira yake kwamba kihistoria walimu wa uongo wamekuwa ni tatizo kubwa na wataendelea kuwa tatizo katika siku zijazo. Hebu tuchimbue somo letu la Biblia na tuone kile tunachoweza kujifunza ili kujikinga dhidi ya mafundisho ya uongo!

 

  1. Walimu wa Uongo

 

    1. Soma Kumbukumbu la Torati 13:1-3. Vigezo gani vinatumika kutambua kama nabii ni wa uongo? (Kisicho kigezo ni endapo unabii huo unakuwa wa kweli. Kilicho kigezo ni endapo nabii anapendekeza kuwa uifuate miungu mingine.)

 

    1. Soma Kumbukumbu la Torati 18:22. Hii inanoaje bongo zetu endapo anachokisema nabii kinatokea kweli? (Katika hili nabii ananena kwa jina la Mungu wa kweli. Lakini, unabii hautimii katika kweli. Tunatakiwa kuwa makini na manabii kama hao.)

 

    1. Soma Yeremia 23:30-31. Ikiwa nabii anatoa sifa kwa Mungu wa kweli wa mbinguni, je, huo ni uthibitisho kwamba yeye ni nabii wa kweli? (Hapana. Mtu anaweza kutunga unabii wake mwenyewe, au kuuazima kutoka kwa mtu mwingine, na bado akauhusianisha na Mungu wa kweli. Lakini, hiyo haimhalalishi mtu huyo kuwa ni nabii.)

 

      1. Angalia tena sehemu ya mwisho ya Kumbukumbu la Torati 18:22. Kwa mara nyingine, huu ni unabii ambao Mungu hakuutoa. Je, huyu ni nabii wa uongo? (Kifungu kinasema kuwa “kwa kujikinai amelinena huyo nabii.” Ikiwa adhabu ni “usimwogope,” basi angalao huyu ni nabii asiyeaminika.)

 

    1. Je, unazifahamu “barabara zinazoruhusu magari kupita kwa uelekeo mmoja pekee?” Ikiwa nabii anatabiri mambo yajayo kwa usahihi au anampa sifa Mungu wa kweli, hiyo haimhalalishi nabii huyo. Hata hivyo, ikiwa nabii anakosea kutabiri mambo yajayo au anawaelekeza watu kwa miungu ya uongo, basi huyo ni nabii wa uongo.)

 

    1. Soma Maombolezo 2:14. Ni onyo (ishara) gani jingine tunalopaswa kuliangalia kwa nabii wa uongo? (Hawaizungumzii dhambi ili tusiingie matatizoni.)

 

    1. Soma 2 Petro 2:1. Ni kwa jinsi gani walimu wa uongo wanafanana na manabii wa uongo wa Agano la Kale? (Wanamkana Yesu kwamba si Bwana. Wanaanzisha uzushi.)

 

 

      1. Nini kinawatokea hawa walimu wa uongo? (Wanajiletea “uharibifu usiokawia.”)

 

    1. Soma 2 Petro 2:2-3. Matokeo gani mengine yanatokana na mafundisho ya uongo? (Yanaufanya ukweli “utukanwe.”)

 

      1. Tunaona mambo gani ya kufanana kwa manabii wa uongo? (Walimu wa uongo wanatunga habari, kama manabii wa uongo walivyotunga unabii.)

 

      1. Ikiwa una mwalimu fidhuli (linganisha Kumbukumbu la Torati 18:22), ambaye anafundisha jambo lisilotoka kwa Mungu, je, huyo naye ni mwalimu wa uongo? (Kanuni ile ile ya “usimwogope” inapaswa kutumika.)

 

    1. Soma Marko 9:38-40. Ni jambo gani lisilo sehemu ya kuwa nabii wa uongo au mwalimu wa uongo? (Kwa kuwa tu wewe si sehemu ya “kundi” (kanisa lako au madhehebu yako) haimaanishi kuwa wewe ni nabii wa uongo au mwalimu wa uongo. Utaona kwamba mtu huyu anatenda miujiza na anafanya hivyo kwa jina la Yesu.)

 

  1. Adhabu kwa Walimu wa Uongo

 

    1. Soma 2 Petro 2:4-6. Tutasimama kabla Petro hajamalizia sentensi yake. Hii inaashiria nini juu ya hatima ya manabii wa uongo na walimu wa uongo? (Mungu anajua jinsi ya kuwaadhibu wale wanaotenda makosa na jinsi ya kuwalinda wale wanaoenenda vyema.)

 

    1. Soma 2 Petro 2:7-9. Nilikatisha sentensi hii kwa sababu nilitaka kujikita kwa Lutu. Je, Lutu alikuwa na maamuzi sahihi? (Kwa nini Lutu hakuondoka? Ikiwa aliteseka na kuumizwa kwa uovu uliomzunguka, kwa nini hakuondoka? Kwa nini amwache mkewe na familia yake wavutiwe uovuni?)

 

      1. Kwa nini vifungu vinasema kuwa Mungu alimwokoa Lutu?

 

    1. Soma 2 Petro 2:10 (sehemu ya kwanza). Sifa mbili za uovu za watu ambao “hususani” wanastahili hukumu (2 Petro 2:9) ni zipi? (Wanaifuata asili yao ya dhambi, na ni waasi dhidi ya mamlaka.)

 

    1. Soma 2 Petro 2:10-12. Tafakari jambo hili. Je, watu unaowafahamu “wanawakashifu” wale wanaoishi mbinguni? (Nimewasikia watu wanaomdhihaki Mungu.)

 

      1. Je, kukana kwamba Mungu si Muumba ambaye alitamka na ulimwengu ukapata kuwepo ni “kashfa?” (Ikiwa niliuumba ulimwengu kwa siku sita kwa kutamka, na mtu mwingine anasema kuwa huo ni uongo, na kwamba kila kitu kiliibuka na kuwepo kwa bahati na kwa nguvu ya asili, nitaichukulia hiyo kuwa ni kashfa.)

 

  1. Kosa la Jinai na Adhabu

 

    1. Soma 2 Petro 2:13-14. Petro anaandika kuwa hawa walimu wa uongo “wanafanya anasa ya ulevi wakati wa mchana.” Je, dosari za kitabia za hawa walimu wa uongo ni jambo ambalo ni gumu kulitambua? (Hapana! Petro anaandika kwa uwazi ili tuweze kuona. Kumbuka kwamba katika 2 Petro 2:10 aliwaita “shupavu na fidhuli.” Huu si uzushi wa siri.)

 

 

      1. Petro anapoandika kuwa “macho” yao “yamejaa uzinzi” je, unadhani kwamba anazungumzia dhambi ya uzinzi? (Soma Mathayo 12:39, Hosea 1:2, na Ufunuo 17:1-2. Dhambi ya ngono inaweza kujumuishwa, lakini nadhani Petro anaandika juu ya kutokuwa waaminifu kwa Mungu. Hii inaturejesha kwenye mjadala wetu wa awali kuhusu manabii wa uongo kutuelekeza kwenye miungu mingine.)

 

    1. Soma 2 Petro 2:15. Unafahamu nini kumhusu Balaamu? (Soma Hesabu 22:10-12. Mfalme wa Moabu alimtaka Balaamu awalaani watu wa Mungu wakati walipokuwa kwenye safari yao kutoka Misri.)

 

    1. Soma 2 Petro 2:16. Je, Balaamu alisema, “sitafikiria kuwalaani watu maalum wa Mungu?” (Soma Hesabu 22:32-33. Kisa chote kinahusu jinsi Balaamu anavyojaribu kwa kadri inavyowezekana kupata upendeleo (na fedha) wa mfalme wa Moabu. Ulikuwa ni uzembe wa hali ya juu, na Balaamu aliokolewa na punda wake.)

 

      1. Je, wewe ni bubu zaidi ya punda? Petro anamaanisha nini? (Walimu wa uongo wanataka kuwa sehemu ya kile “malipo” ya uovu yanachokilipa. Wanataka “thawabu” za ulimwengu. Wanakwenda mbali sana kiasi kwamba hata punda anaweza kuona tatizo.)

 

    1. Soma 2 Petro 2:17-18. Unawafahamu walimu kama hawa? (Miaka mingi iliyopita, niliwatembelea wanadoa na waliniuliza kama nimesoma vitabu vya mwandishi fulani wa kidini. Jibu langu lilikuwa “hapana,” lakini nilikaa chini na kusoma sehemu ya kitabu. Kitabu kiliandikwa kwa maneno yaliyoonekana kuwa ya kidini, lakini kilihamasisha mambo ambayo kwa asili moyo ungependa kuyasikia, na si viwango vya Biblia. Mawazoni mwangu kitabu kile kilikuwa ni upuuzi wa dhahiri. Wazo lililonijia kwanza ni kwamba ninaweza kuandika vitabu kama hicho nilichokisoma na kujipatia fedha nyingi. Wazo lililofuata ni kwamba ingekuwa vigumu kutafakari dhambi kubwa zaidi ya hiyo! Nadhani hiki ndicho Petro anachokizungumzia.)

 

    1. Soma 2 Petro 2:19-20. Petro anasema ahadi ya hawa walimu wa uongo ni “uhuru.” Ni uhuru wa namna gani anaoumaanisha? (Petro anatumia maneno haya: “watumwa wa uharibifu,” “wakinaswa tena” na “ufidhuli.” Dhambi za ulimwengu ni zipi? Ni dhambi zilizokunasa kabla hujaongolewa? Hawa walimu wa uongo wanajenga hoja kwamba unaweza kuufurahia uhuru wa dhambi ambayo hapo kabla iliyazonga maisha yako wakati ukingali Mkristo.)

 

      1. Wale ambao mnasoma masomo haya mara kwa mara mnafahamu kuwa mimi ni mtetezi mkubwa wa neema. Hata hivyo, neema si leseni ya kutenda dhambi. Nakumbuka mtu aliyekuwa anazungumzia dhambi mbaya sana na kusema, “Mungu atanisamehe.” Mungu anasamehe dhambi, lakini Mungu pia alikufa ili kuonesha kuwa sheria ni ya haki. Tunanufaika kwa kuishika sheria.

 

      1. Ngoja nikupatieni mifano miwili. Mtu anaendesha pikipiki bila kufaa kofia ngumu kwa sababu anauamini utaalamu wa watu wanaofanya kazi kwenye hospitali iliyopo karibu na eneo lake. Mtu hazingatii mlo kamili na mazoezi kwa sababu ya uwezo wa madaktari wa upasuaji kuweza kufanya upasuaji wa moyo kwa mafanikio makubwa. Je, hii inaleta mantiki yoyote?

 

    1. Angalia tena sehemu ya mwisho ya 2 Petro 2:20. Kwa nini hali ya watu hawa imekuwa mbaya zaidi? (Sasa wanaona kuwa ni halali katika matendo yao ya uharibifu na ufidhuli. Wanawezaje kuyageukia mambo sahihi wakati wanaamini kuwa Mungu anaruhusu uovu?

 

 

    1. Soma 2 Petro 2:21-22. Kama mbwa ameyarudia matapishi yake na nguruwe amerudi kwenye matope, kwa nini ingekuwa bora zaidi kutoijua kamwe “njia ya haki?” (Kwa sababu ya mfano wao kwa watu wengine. Kuyarudia matapishi na kuwa matopeni ndio jambo linalojengewa hoja sasa kwamba ni sahihi.)

 

    1. Rafiki, Petro anatuambia kuwa mafundisho ya uongo ni jambo la dhahiri. Kama mwalimu anamdhoofisha Mungu wa kweli au anakurejesha kwenye maisha ya dhambi, basi unatakiwa kuwa bubu zaidi ya punda ili kushindwa kuliona tatizo. Je, hutafumba macho yako na kuifanya akili yako kuwa makini unaposikia fundisho jipya?

 

  1. Juma lijalo: Siku ya Bwana.