Petro na Watu wa Mataifa

(Matendo 2 and 10)
Swahili
Year: 
2015
Quarter: 
3
Lesson Number: 
9

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: "Petro na Watu wa Mataifa" inaonekana kuwa kama kikundi cha uimbaji! Tayari Petro amekwishapangilia sauti, lakini ilikuwa ni sauti ya injili kwa Watu wa Mataifa. Petro, chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu, alivunjavunja vizingiti vya kimbari na kidini ili kupanua wigo wa kazi ya Mungu. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia ili tuone kile tunachoweza kujifunza kutokana na kazi ya Petro ya kiinjilisti itakayotuongoza katika juhudi zetu kwenye kazi za kimisionari leo!

6. Soma Matendo 10:20 na Matendo 10:28. Je, maono yanahusu ulaji wa nyama isiyo safi? (Hapana. Maoni yanalenga kumfanya Petro aziangalie kanuni zinazowafanya Wayahudi wasishikamane na watu wa Mataifa. Tatizo lililopo ni kwamba katika hali ya kawaida Petro atasita kwenda na watu wa Mataifa waliotumwa na Kornelio.)

7. Soma Matendo 10:22-26 naMatendo 10:29. Kwa nini Kornelio alimwangukia Petro miguuni mwake? Kwa nini Petro hakuchukulia kitendo hicho kama fursa ya kufanya kazi ya kimisionari? Kwa nini Petro aliuliza tu kwamba, "Kwa nini mlitumwa kwangu?" (Hii inaonesha kuwba si Kornelio wala Petro aliyeelewa mapenzi ya Mungu kwa ukamilifu katika jambo hili.)

8. Soma Matendo 10:30-33. Unaweza kutafsiri vipi jibu la Kornelio kwa kutumia msamiati wa leo? (Petro anauliza, "Kwa nini ulituma watu wanifuate?" Kornelio anajibu, "Sifahamu, Mungu aliniambia nifanye hivyo." Konelio sio mpumbavu, anaendelea kusema kuwa lazima Petro ana ujumbe kwa ajili yao.)

9. Soma Matendo 10:34-35. Kisha Petro anaendelea na injili ya Yesu. Soma Matendo 10:44-46. Tunajifunza mambo gani ya kazi za kimisionari hapa? (Kwanza, tuweke kando chuki zetu. Pili, kuutafuta uongozi wa Roho Mtakatifu.)

10. Angalia tena Matendo 10:45-46. Tuliposoma Matendo 2:4 hapo awali, kwa dhahiri hii ilikuwa ni karama ya kunena kwa lugha (au ya kueleweka) kwa kutumia lugha ya kigeni. Tunaona karama gani hapa? (Hapa hakuna wageni. Hakuna haja ya kuamini kuwa hii ni lugha ya kigeni.)

11. Soma Matendo 10:47-48. Kuna jambo gani la muhimu katika swali la Petro? (Inaonesha kwamba anaukubali kabisa uongozi wa Mungu. Alianza kwa kufikiri kwamba hapaswi hata kuingia kwenye nyumba ya mtu wa Mataifa. Sasa anaukubali ujumbe aliouona kwenye maono, uthibitisho wa kumwagwa kwa Roho Mtakatifu, na anamalizia kwa kuhitimisha kwamba wanapaswa kubatizwa.)

12. Soma Matendo 11:1-3. Je, tunaweza kutarajia ukosolewaji katika kazi yetu ya kimisionari?

13. Rafiki, Petro aliasisi kazi ya kimisionari kwa watu wa Mataifa. Tumeona kwamba kiini cha kazi ya Petro ni kujihusisha na uongozi wa Roho Mtakatifu, hata kama unakinzana na mambo tuliyokuwa tuyaamini hapo kabla. Je, u radhi kujitoa kwa ajili ya kuongozwa na Roho Mtakatifu? Ikiwa sivyo, kwa nini usijitoe sasa hivi kwenda mahali ambapo Roho Mtakatifu anakuongoza!

  1. Pentekoste
  2. Majuma mawili yaliyopita tulijifunza Matendo 1:6, iliyotuonesha kuwa bado wanafunzi hawakuwa wameuelewa ujumbe wa injili kwa ukamilifu. Wakati ule tulijadili hali iliyosababisha tukio lile. Hebu tusome Matendo 2:1-4. Nini kimewasili? (Roho Mtakatifu!)
  3. Tunajuaje? (Sauti, moto, na ndimi.)
  4. Soma Matendo 2:5. Unaizungumziaje hadhira? (Hadhira ni ya watu wanaomcha Mungu na wanatoka "kila taifa chini ya mbingu.")
  5. Kwa nini walikuwepo Yerusalemu? (Kisa kifupi: Sehemu ya shinikizo la Mungu kwa Farao kuwaachia watu wake kutoka utumwani Misri ilikuwa ni pigo la kifo kwa wazaliwa wote wa kiume wa kwanza. Hata hivyo, Mungu aliwakinga watu wake dhidi ya kifo hiki. Kumbukumbu ya ulinzi huu ni "Pasaka" (Kutoka 12:3-14). Siku hamsini ("majuma saba") baada ya Pasaka, Wayahudi walitakiwa kusherehekea "Sikukuu ya Majuma " (2 Mambo ya Nyakati 8:13; Mambo ya Walawi 23:4-16). Sikukuu hii pia iliitwa "Pentekoste" kutokana na kipindi cha siku hamsini. Baadhi ya maoni yanaongezea kwamba Pentekoste ilisherehekewa kwa sehemu fulani kwa sababu Mungu alitoa torati yake katika Mlima wa Sinai siku hamsini baada ya Pasaka. Watu walikuwa Yerusalemu kwa ajili ya Sikukuu ya Majuma/Pentekoste.)
  6. Soma Matendo 2:6-12. Tunaweza kupata vidokezo gani vya kimisionari kutokana na kile tulichojifunza hadi sasa? (Watu walio tayari kupokea neno la Mungu ni mahali pazuri pa kuanzia kazi za kimisionari. Roho Mtakatifu anatoa zana za ushuhudiaji makinifu.)
  7. Soma Matendo 2:13-15. Petro anaanzaje utetezi wake wa ushuhuda? (Anatumia mantiki! Ni asubuhi mno kwa mtu kulewa.)
  8. Unaweza kuongezea mantiki gani? (Unadhani sauti na moto vimefikaje hapa? Je, ni kwa sababu ya unywaji?)
  9. Soma Matendo 2:16-18. Mbinu ya Petro inayofuatia katika ushuhudiaji ni ipi? (Unakumbuka kwamba watu hawa "wanamcha Mungu?" Petro anatoa hoja ya kivitendo lakini papo hapo anageukia Biblia kwa kuinukuu. Anayachukulia matukio wanayoyaona na kuyahusianisha na Maandiko wanayoyafahamu.)
  10. Unaichukuliaje njia ya kimisionari?
  11. Unawezaje kufanya hivyo leo?
  12. Tumejadili jinsi tunavyopaswa kutumia akili ya kawaida/mantiki (Mathayo 10:16) katika kazi zetu za kimisionari. Je, werevu na mbinu za Roho Mtakatifu kutumia akili ya kawaida katika tukio hili kwa Petro ni zipi? (Wageni wamchao Mungu kutoka sehemu mbalimbali wapo mjini. Roho Mtakatifu anapata usikivu wao, na Petro anaielezea injili. Kitendo hiki kinaruhusu injili kupelekwa kwenye nchi za wageni, yaani, kule walikotoka.)
  13. Unawezaje kutumia mkakati huu leo? (Tuuangalie mtandao wa intaneti. Watu wanaomjali Mungu wanaweza kuangalia jambo linalomhusu Mungu kwenye mtandao. Mtandao unalifikia kila taifa.)
  14. Tutaruka ujumbe mkuu uliowasilishwa na Petro. Hebu tusome Matendo 2:36-37. Watu waliuitikiaje ujumbe wa Petro? (Walishawishiwa na ukweli wa kile alichokisema.)
  15. Tunawezaje kurudufu kitendo hicho leo? (Tunatakiwa kutumia akili ya kawaida/mantiki katika kupeleka ujumbe unaowataka watu kuenenda kivitendo. Hata hivyo, uongoaji ni kazi ya Roho Mtakatifu.)
  16. Soma Matendo 2:38-39. Je, ni mara ngapi unasikia wito wa kutubu? Je, ni mara ngapi unatoa wito kwa watu kutubu?
  17. Soma Matendo 2:40-41. Angalia jinsi jambo hili linavyoandikwa. "Kizazi" "chenye ukaidi" na maneno ya Petro "kuonya" na "kusihi." Je, leo tunaogopa kuiita dhambi kwa jina lake kamili tunapotaka kuwaleta watu kanisani? Je, tunaogopa kuwaudhi watu kwa kuwaita waifikilie toba?
  18. Katika Matendo 2:2-4 tuliona mambo ya kushangaza yaliyotendwa na Roho Mtakatifu. Tukiongezea na miujiza, na ikiwa jambo kama hilo litatokea katika kanisa mahalia leo, waongofu wengi watakuja kanisani. Je, umejiuliza kuwa, "Kwa nini jambo hilo halitokei leo?" Je, inawezekana kwamba halitokei leo kwa sababu hatutawaita watu ili waifikilie toba?
  19. Kornelio
  20. Soma Matendo 10:1-2. Angalia maelezo ya huyu akida. Je, watu wanaweza kusema hivyo kukuhusu?
  21. Soma Matendo 10:3-6. Malaika wa Mungu anamwambia Kornelio kuwa Mungu amebaini jambo gani? (Maombi yake na utoaji wake.)
  22. Soma Matendo 10:9-14. Kuna tatizo gani katika ulaji wa Petro? (Wanyama sio safi. Hii ni rejea ya kanuni za ulaji zilizopo katika kitabu cha Mambo ya Walawi 11.)
  23. Soma Matendo 10:15. Je, kanuni zilizopo katika kitabu cha Mambo ya Walawi 11 kuhusu wanyama safi na wasio safi zimebatilishwa?
  24. Je, kanuni hizi za ulaji zilitoka kwa Musa? (Soma Mwanzo 7:8-9. Hii inatuonesha kuwa tofauti kati ya nyama safi na isiyo safi haikutoka kwa Musa wala kwenye mfumo wa hekalu. Kanuni hizo zilikuwepo tangu nyakati za zamani kabisa, hata kabla wanadamu hawajaruhusiwa (Mwanzo 9:1-3) kula nyama.)
  25. Soma Matendo 10:17-19. Kwa nini Petro anayafikiria maono? (Inaonekana kuwa ni jambo baya sana kula wanyama wasio safi.)
    1. Kwa nini Wayahudi walihusianisha kunena kwa lugha na kupewa karama ya Roho Mtakatifu?
      1. Kunena kwa lugha ni jambo linaloleta mtafaruku katika baadhi ya madhehebu. Kuna umuhimu gani kuhusu kuwa na uelewa sahihi wa hii mada? (Soma Mathayo 12:22-24 na Mathayo 12:31-32. Ikiwa utasoma muktadha kamili wa mafungu haya katika Mathayo 12, Yesu anatuonya kwamba kuiita kazi ya Roho Mtakatifu kuwa ni kazi ya Shetani ni dhambi isiyosameheka. Jambo hili ni la hatari sana.)
        1. Juma lijalo: Filipo Kama Mmisionari.