Kuikufuru Siku

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Ayubu 3 & 7)
Swahili
Year: 
2016
Quarter: 
4
Lesson Number: 
5

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Je, unakumbuka katika Ayubu 2:9 mkewe Ayubu alimshauri kuwa “amkufuru Mungu, akafe?” Ayubu alikataa. Badala yake, juma hili tunajifunza kuwa Ayubu aliulaani uwepo wake mwenyewe. Je, unamfahamu mtu aliyejiua? Nilipokuwa kijana mdogo, mama yangu alikuwa na wasiwasi kwamba ningeweza kujiua kwa sababu ya kuachana na rafiki wangu wa kike. Sikumbuki nilichokuwa nikikiwaza wakati huo, lakini sidhani kama mama yangu alikuwa na sababu yoyote ya kuwa na wasiwasi. Ninaposikia habari za mtu kumwua mwenzi wake, huwa ninatafakari, “kwa nini wasipeane talaka?” Mtazamo wangu ni huo huo juu ya suala la mtu kujiua, kwa nini tu nisibadili mwelekeo wa maisha yangu? Ikiwa unafanana nami na huyaelewi mawazo ya aina hiyo, Ayubu anatuelekeza kwenye fikra za watu waliokata tamaa (fikra zisizo na matumaini), watu walio kwenye lindi la msongo mkubwa wa mawazo. Hebu tuchimbue somo letu la Biblia ili tujifunze zaidi!

  1. Kuikufuru Siku

    1. Soma Ayubu 3:1-3. Ayubu anatamani nini? (Kwamba kamwe asingezaliwa.)

      1. Kwa nini anafikia hitimisho hilo? (Maisha yake yalikuwa mazuri sana (au angalao inaonekana kuwa yalikuwa hivyo) kabla Shetani hajamshambulia. Kwa nini asitamani kufa sasa hivi badala ya kutamani kuwa heri asingezaliwa? (Haileti mantiki yoyote, lakini haya ni baadhi ya mapendekezo. Wakati mwingine tunapopata mateso makubwa, huwa tunaonyesha hisia zisizo na mantiki. Pili, Ayubu amechanganyikiwa na kukasirika kwa namna “haki” isivyotendeka maishani mwake. Ikiwa haelewi jinsi maisha yalivyo, huenda ingekuwa bora zaidi endapo kamwe asingekuwa sehemu ya hayo maisha.)
    2. Soma Ayubu 3:4-6. Ayubu anatamani jambo gani jingine kuhusu siku yake ya kuzaliwa? (Kwamba Mungu aisahau kabisa. Anataka kumbukumbu zote rasmi za siku ya kuzaliwa kwake zifutiliwe mbali.)

      1. Linganisha matamanio ya Ayubu na uhalisia wa hali aliyonayo. Je, hicho ndicho Mungu anachokitaka? (Mungu anataka kinyume chake. Ayubu ni mpiganaji wa Mungu, chombo chake cha muhimu sana kilichotumika kumkaripia Shetani. Ayubu ni shujaa machoni mwa Mungu.)

      2. Hii inatufundisha nini kuhusu uelewa wa kile ambacho Mungu anakifikiria juu yetu?

    3. Soma Ayubu 3:7-9. Ayubu anatamani jambo gani jingine kuhusu siku yake ya kuzaliwa? (Mtu yeyote asiifurahie. Badala yake, siku yake ya kuzaliwa inapaswa kulaaniwa.)

  2. Pumziko la Kifo

    1. Soma Ayubu 3:10-13. Ayubu anatamani kwamba ingekuwa heri kama kamwe asingezaliwa, au kwamba heri angekufa wakati wa kuzaliwa kwake, na kwamba Mungu angesahau siku ya kuzaliwa kwake na kwamba wanadamu wangeilaani badala ya kuibariki hiyo siku. Je, mafungu haya yanatuambia nini juu ya sababu ya matamanio ya Ayubu yasiyo ya kawaida? (Ayubu anasema kuwa endapo kamwe asingezaliwa, au endapo angefariki wakati wa kuzaliwa kwake, angefurahia amani ya mauti yake (angelala usingizi na kupata kupumzika).)

      1. Ikiwa hilo ndilo lengo la Ayubu, kwa nini basi asijiue? Kwa nini asimwambie mkewe mwaminifu, “Unataka nife, unaonaje ukiniua?” (Miongoni mwa mawazo ya Ayubu ya kutisha na ya kukatisha tamaa, kujiua si miongoni mwa mawazo hayo. Lazima Ayubu aliamini kuwa kujiua si njia ambayo Mungu ataipuuzia.)
    2. Soma Ayubu 3:13-15. Mustakabali wa Ayubu unafananaje na wa watawala wanaojenga makasri na majumba makubwa, waliokuwa matajiri wakimiliki dhahabu na fedha? (Ayubu ameangamizwa. Unapokuwa umefariki haijalishi kama kasri lako limeangamizwa au dhahabu yako imepotea. Ayubu anataka afe ili uharibifu wa maisha yake usahaulike kabisa.)

    3. Soma Ayubu 3:16-19. Ayubu ana mtazamo gani juu ya asili/chanzo cha kifo? (Anakichukulia kifo kama jambo linalomuweka mtu huru dhidi ya matatizo. Hawaoni waovu wakiungua au wenye haki wakifurahia raha ya mbinguni.)

      1. Unadhani hii inalenga kutufundisha jambo fulani kuhusu maisha yajayo baada ya haya ya sasa? (Agano la Kale halielezei vizuri suala la kifo kuliko Agano Jipya. Kimsingi Sulemani alisema vivyo hivyo katika Mhubiri 9:9-10, kwamba kaburi ndio mwisho wa maisha na hakuna mustakabali wowote. Kwa upande mwingine, Agano Jipya limejaa rejea zinazohusu maisha yajayo, hususani kwa wale wanaomtumaini Mungu.)

      2. Kutokana na uelewa wa Ayubu kuhusu habari za kifo, je, unaweza kufikiria uchungu aliokuwa nao kutokana na kuwapoteza watoto wake?

  3. Asili (Chanzo) ya Maisha

    1. Soma Ayubu 7:1-3. Kutokana na jinsi unavyomfahamu Ayubu, je, maneno haya yana mantiki yoyote? (Hapana! Alikuwa mtu “mkuu sana upande wa Mashariki,” Ayubu 1:3. Sina wasiwasi kwamba alifanya kazi kwa bidii, angalao katika jambo moja, lakini kujilinganisha na “mtumwa” au “mwajiriwa,” ni jambo la kimzaha.)

      1. Hebu subiri kidogo! Je, Ayubu anayazungumzia maisha yake ya zamani? (Ayubu anaposema, “ni vivyo nami nimepewa miezi ya ubatili,” inaonekana anazungumzia tu kuhusu maisha yake baada ya shambulio la Shetani.)
    2. Soma Ayubu 7:4-5. Ayubu hawezi kulala. Je, huo ndio “uajiriwa wake (kazi yake ngumu)” (Ayubu 7:1?) (Nadhani uelewa sahihi ni kwamba Ayubu anayazungumzia maisha yake ya sasa na sio maisha yake ya zamani. Ayubu anabainisha kuwa waajiriwa wanatazamia nyakati za jioni kwa ajili ya ujira wa siku. Anatamani usiku wake wa mateso upite kwa sababu hajisikii vizuri na hawezi (anashindwa) kulala.)

    3. Soma Ayubu 7:6-8. Je, Ayubu anasema kuwa nyakati za usiku huwa ndefu, lakini nyakati za mchana zinapita upesi? (Sidhani. Anasema kuwa maisha yake mazuri yamekwisha. Sasa maisha bora yamekwisha na hana matumaini.)

      1. Fikiria kauli ya Ayubu kuhusu maisha. Je, huo ndio ukweli juu ya maisha yako? Wakati fulani utasema, “maisha mazuri yamekwisha, na sasa nina matumaini tu ya kufa?” (Kwa watu wengi huu ndio ukweli. Ni hoja nzuri sana kuhusu kuzingatia ulaji wako na kuweka mwili katika hali njema kiafya, ili uongeze uwezekano kwamba utakapokuwa mzee bado uendelee kuyafurahia maisha.)
  4. Malalamiko

    1. Soma Ayubu 7:11. Je, mtazamo wa Ayubu umebadilika? (Ndiyo. Anasema kuwa maisha yake bora yamekwisha, anatumainia kifo, kwa hiyo atalalamika kwa sababu ana uchungu.)

      1. Soma Ayubu 2:4-5. Je, Shetani ameshinda? (Hapana! Ayubu hamkufuru Mungu, anamwendea Mungu akiwa na malalamiko yake.)
    2. Soma Ayubu 7:12-16. Malalamiko ya Ayubu ni yapi? (Mungu amemwacha kwenye hali ya kutisha sana kiasi kwamba anatamani kufa. Anataka Mungu “aachane naye.”)

      1. Unadhani kweli hiki ndicho anachokitaka Ayubu, au haya ni mazungumzo yake yanayotokana na msongo wa mawazo tu? (Kutokana na Ayubu kufikia hatua ya kudhani kuwa Mungu amemletea matatizo, angependa kuachwa peke yake.)
    3. Soma Ayubu 7:17-18. Ayubu anafikiria kuwa Mungu anamtendea jambo gani? (Anamchunguza, anamjaribu.)

      1. Hapo awali niliandika kuwa kamwe Ayubu, katika kipindi cha miaka elfu moja, hawezi kufahamu sababu ya mateso yake. Lakini, hapa tunaona kwamba inawezekana siko sahihi. Ayubu anahisi kwamba anajaribiwa.)

        1. Je, Mungu anamjaribu? (Hili ni wazo la Shetani.)
    4. Soma Ayubu 7:20. Ayubu anageukia sababu nyingine ya mateso yake, je, ni sababu gani hiyo? (Kwamba ametenda dhambi, na Mungu anamfanya kuwa “shabaha” kutokana na dhambi hiyo.)

      1. Je, bado Ayubu anamtumaini Mungu? (Ayubu anadhani kuwa lazima Mungu atakuwa anamjaribu au anamlenga kutokana na dhambi zake. Anamtaka Mungu “aache kumwangalia” (Ayubu 7:19). Lakini, pamoja na sababu yoyote ya kweli iliyosababisha mateso yake, bado Ayubu anamgeukia Mungu ili kupata suluhisho la matatizo yake.)
    5. Soma Ayubu 7:21. Ayubu anafikiria nini kuhusu neema? (Amaanini katika neema. Anamwomba Mungu amsamehe dhambi zake kwa kuwa ana uhakika atakufa hivi karibuni.)

      1. Soma tena Ayubu 7:19 na ulinganishe fungu hilo na sehemu ya mwisho ya Ayubu 7:21. Je, kauli hizi mbili zinakinzana? (Ndiyo. Kwa upande mmoja Ayubu anasema kuwa Mungu anamwangalia wakati wote. Kwa upande mwingine anasema kuwa Mungu atamtafuta.)

        1. Jambo hilo linatufundisha nini? (Tunapokuwa na marafiki au familia ambazo, kama ilivyo kwa Ayubu, zinateseka, tunaweza kutarajia kwamba si mara zote watakuwa wakifikiri vizuri. Tuliona jambo hilo hapo awali kwenye somo hili na tunaliona tena sasa hivi.)

        2. Wajibu wetu ni upi katika mazingira kama hayo? (Soma Ayubu 1:11-13. Nadhani njia hii ina faida nyingi. Kadri tunavyoendelea kujifunza kitabu cha Ayubu tutaona jinsi marafiki wa Ayubu walivyojaribu kusahihisha mitazamo yake. Lakini, hilo halikuonekana kusaidia.)

    6. Rafiki, bado Ayubu anasalia kuwa hamasa kwetu pale tunapoteseka. Ayubu analalamika, wakati mwingine fikra yake inachanganyikiwa, na ana msongo wa mawazo. Licha ya yote hayo anamgeukia Mungu ili kupata jibu. Je, utadhamiria kumwangalia Mungu wakati wote kwa ajili ya kupata majibu ya matatizo yako maishani mwako?

  5. Juma lijalo: Kukufuru Bila Sababu?