Adhabu ya Kupatiliza

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Ayubu 8-9, 11-12)
Swahili
Year: 
2016
Quarter: 
4
Lesson Number: 
7

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Ninapenda sana mantiki! Bildadi, mmojawapo wa marafiki wa Ayubu pia anapenda mantiki. Bildadi anaijua teolojia yake, anaijua mantiki yake, na anahitimisha kwamba watoto wa Ayubu walistahili kufa. Ungeweza kuiita hiyo “Adhabu ya Kupatiliza” iliyo halisi. Wakati mwingine mantiki inatuangusha. Wakati mwingine mtazamo wetu wa jinsi Mungu anavyotenda kazi huwa hauko sahihi, na hivyo hitimisho letu enye mantiki pia linakuwa si sahihi (lina makosa). Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia ili tujifunze zaidi juu ya upendo, mantiki na adhabu ya kupatiliza!

 

1)      Upepo Mkuu

 

a)      Soma Ayubu 8:1-3. Bildadi, mmojawapo wa marafiki wa Ayubu, anajitokeza. Lengo lake ni nini? (Sio kumfariji Ayubu. Badala yake, anataka kumthibitisha Mungu.)

 

i)        Hebu turejee nyuma kidogo ili tuone Bildadi anafikiria nini juu ya “upepo mkuu.” Soma Ayubu 7:19-20. Ayubu anasema nini? (Kwamba hastahili kuwa “shabaha” ya adhabu ya Mungu. Ikiwa ametenda dhambi, basi dhambi hiyo haikumdhuru Mungu.)

 

ii)      Kwa nini Bildadi amefadhaika sana kuhusu jambo hilo? (Inamfanya Mungu aonekane kuwa hatendi haki. Bildadi anadhani kuwa Ayubu anafahamu alichokifanya, anakataa tu kukikiri.)

 

iii)    Kwa nini Bildadi ana uhakika kabisa kuwa Ayubu ametenda dhambi? (Kwa sababu ana mtazamo sawa na ule uliopo kwenye Kumbukumbu la Torati 28 ambao tuliujadili katika masomo ya awali – ikiwa wewe ni mtiifu utasitawi, ikiwa hutakuwa mtii utadhuriwa.)

 

b)      Soma Ayubu 8:4. Hili ni pigo kubwa kiasi gani kwa Ayubu? (Soma Ayubu 1:4-5 na Ayubu 1:18-19. Hili ni jambo baya kabisa ambalo Bildadi alilisema kwa sababu liliakisi fikra ya Ayubu. Huenda Ayubu alijitambua na kuijua dhambi yake, lakini hakujua na hakuwa na uhakika kuhusu watoto wake – hususani baada ya karamu.)

 

i)        Kuna kasoro gani kwenye kauli ya Bildadi kuhusu watoto wa Ayubu? (Bildadi anajenga hoja kwa mujibu wa uelewa wake wa teolojia. Hatoi kauli kwa mujibu wa uelewa wake halisi wa dhambi. Ikiwa teolojia ya Bildadi sio sahihi (kwa ujumla iko sahihi), au haihusiki kwenye mazingira yote (ambalo ndilo jambo lililopo hapa), basi Bildadi ameyaongezea mateso ya Ayubu.)

 

c)      Soma Ayubu 8:5-7. Unadhani Bildadi anaamini kwamba maneno haya ni ya kutia moyo?

 

i)        Ungeonesha hisia gani kama ungekuwa Ayubu?

 

d)     Soma Ayubu 8:8-10. Bildadi anaamini kuwa tunapaswa kuyaelewaje matendo ya Mungu leo? (Kwa kuiangalia historia.)

 

i)        Je, unakubaliana na jambo hilo? (Ndiyo.)


 

ii)      Je, hii ndio sababu iliyomfanya Mungu ajumuishe kitabu cha Ayubu kwenye Biblia? (Ndiyo!)

 

e)      Soma Ayubu 8:20-22. Je, Mungu ni mtu wa kawaida na mwenye kutabirika kama adaivyo Bildadi?

 

f)       Soma Ayubu 9:1-4. Ayubu anajibuje mtazamo wa Bildadi juu ya Mungu katika historia? (Anakiri kuwa kanuni ya jumla ni kwamba watu wema wanasitawi na watu wabaya wanapata mateso, lakini Ayubu anamwona Mungu kama mtu asiyeelezeka kwa urahisi. “Yeye ni mwenye hekima moyoni, na mwenye uwezo katika nguvu.” Kwa kutabiri atakachokifanya Mungu katika hali zote, Bildadi anajifananisha na Mungu. Kosa baya kiasi gani!)

 

2)      Majibu ya Sofari

 

a)      Sasa tunamsikia Sofari, “rafiki” mwingine. Soma Ayubu 11:4-6. Je, Sofari yuko sahihi kwamba mara zote kuna pande mbili za kisa?

 

i)        Ni “upande” gani ambao Sofari anadhani kuwa unatakiwa kuelezewa? (Uongo wa Ayubu kuhusu kuwa “safi” unatakiwa kubainishwa. Ayubu ni mdhambi sana kiasi kwamba “hata Mungu amesahau baadhi ya dhambi zake.”)

 

b)      Hebu turejee nyuma ili tuone kwa nini Sofari anajisikia hivi. Soma Ayubu 11:1-3. Lengo la Sofari ni lipi? (Anaamini anapaswa kumkemea Ayubu.)

 

i)        Kwa nini? (Wote wawili, yaani Bildadi na Sofari wanajisikia kuwa na wajibu wa kuithibitisha tabia ya Mungu. Wanadhani kuwa Ayubu anamtuhumu Mungu kwa uongo – yaani Mungu kukiuka kanuni zake mwenyewe.)

 

ii)      Je, kweli kuna “pande mbili” kwenye hiki kisa? (Sofari anasema kuwa kuna pande mbili, lakini haamini kabisa kwamba upande wa Ayubu ni halali.)

 

c)      Soma Ayubu 11:7-9. Sofari ana mtazamo gani juu ya akili na maarifa ya Mungu? (Haina kipimo.)

 

d)     Soma Ayubu 11:11-12. Sofari ana mtazamo gani juu ya Ayubu? (Anapendekeza kwamba Ayubu ni “mpumbavu.” Kwa dhahiri, hatuzioni “pande mbili” mawazoni mwa Sofari.)

 

i)        Sofari anatufundisha kuwa njia mbaya ya kuziendea aina hizi za mijadala juu ya mapenzi ya Mungu ni ipi? (Kudhani kwamba upande mwingine ni upumbavu, na kuweza kusema hivyo tu.)

 

3)      Jibu la Ayubu

 

a)      Soma Ayubu 12:1-3. Ayubu anajibuje tuhuma kwamba yeye ni mpumbavu? (Ayubu anasema kuwa yeye ni mwerevu kama Sofari. Na kwa kuongezea, pia anazifahamu kanuni za ulimwengu ambazo Sofari na Bildadi wamekuwa wakizisema.)

 

b)      Soma Ayubu 12:4-5. Ayubu anashikilia msimamo kwamba yeye ni “mwenye haki na asiye na mawaa.” Kwa nini anasema kwamba Sofari na Bildadi hawalioni hili? (“Watu walio na raha huidharau taabu.”)

 

i)        Hebu tuangalie kama anachokisema Ayubu ni kweli. Je, watu wasio na matatizo kama yako wanadhani kuwa matatizo yako yanatokana na makosa yako?

 

(1)   Je, kwa ujumla ni kweli kwamba matatizo yetu yanatokana na makosa yetu?


 

c)      Soma Ayubu 12:6. Je, “wanyang’anyi” ni watu wabaya? (Naam.)

 

i)        Ayubu anasema nini? Kwamba si mara zote kanuni zinatumika kwa usawa?

 

(1)   Ikiwa kweli Ayubu anasema hivyo, basi anaikana haki. Haki inatolewa kwa usawa. Je, una maelezo tofauti juu ya wanyang’anyi kuwa na maisha mazuri?

 

4)      Adhabu

 

a)      Soma Hesabu 16:1-3. Je, unakubaliana kwamba baadhi ya viongozi walijiweka juu ya viongozi wengine wote katika jamii?

 

b)      Soma Hesabu 16:4-7. Musa ndiye kiongozi ambaye Kora pamoja na Walawi walikuwa wanamtia msukosuko. Musa anajibu nini juu ya huu uasi? (Kwa unyenyekevu anamgeukia Mungu. Anasema “Mungu atachagua.”)

 

c)      Soma Hesabu 16:28-33. Je, Sofari na Bildadi wangeweza kutabiri hivi?

 

i)        Je, ungeweza kutabiri matokeo haya kwa Kora na washirika wake?

 

ii)      Hapo awali tulijadili kanuni za Mungu za ulimwengu za “moja kwa moja,” lakini hapa tunamwona Mungu akiingilia kati papo hapo kuadhibu uasi. Unadhani kiasi gani cha hukumu hiyo kinatokea sasa hivi?

 

5)      Tunapaswa kuhitimishaje?

 

a)      Hebu tuangalie jinsi mambo yote tuliyojifunza yanavyoweza kutumika kwetu. Kwa dhahiri, tutakuwa na mjadala juu ya mambo tunayodhani kuwa ni mapenzi ya Mungu. Ninaweza kufikiria mjadala mkubwa unaoendelea kanisani kwangu sasa hivi. Kora alidhani kuwa Musa hayuko sahihi. Bildadi na Sofari walidhani kuwa Ayubu ana makosa. Swali la kwanza tunalopaswa kuuliza katika mazingira kama haya ni lipi? (Je, kweli tunadhani kuwa tuna uelewa makinifu wa kanuni na mapenzi ya Mungu? Je, tunadhani kweli kwamba sisi ni werevu zaidi au ni waaminifu zaidi kuliko wale tusiokubaliana nao?

 

i)        Tunajifunza nini kutokana na njia aliyoitumia Musa? (Musa hakusema, “Mimi ni mwerevu au mimi ni kiongozi.” Badala yake, kwa unyenyekevu alimgeukia Mungu na kusema, “Mungu ataamua.”)

 

(1)   Je, bado hilo linafanya kazi leo?

 

ii)      Maswali gani mengine ni sahihi sisi kuuliza tunapokuwa na mjadala/mzozo? (Je, kweli tuna uhakika kwamba haya ni mapenzi ya Mungu katika jambo na hali kama hii? Tunaweza kuzifahamu kanuni za jumla za Mungu, lakini je, inawezekana kwamba hazitumiki hapa?)

 

(1)   Tutajuaje kwamba suala la “mteka nyara/mnyang’anyi” (Ayubu 12:6) halihusiki? (Sidhani kama wanyang’anyi hawakushughulikiwa na kanuni za Mungu, nadhani kanuni hizo zinatuonesha kwamba Mungu anatenda mambo kwa wakati wake.)

 


b)      Angalia tena Ayubu 8:4. Unadhani kanuni gani ingetumika hapa? (Soma 1 Wakorintho 16:14. Bildadi haoneshi upendo kwa Ayubu kwa sababu hakuna ambacho Ayubu angeweza kukifanya kubadili kifo cha watoto wake.)

 

c)      Rafiki, unapoingia kwenye mjadala juu ya mipango ya Mungu au matendo yake ulimwenguni, je, kwanza utamgeukia Mungu kwa njia ya maombi? Je, utajihoji kama wewe ni mwerevu, endapo una uhakika juu ya kanuni kwenye jambo hili, na endapo unaonesha upendo? Kwa nini, kama ilivyokuwa kwa Musa, usimwache Mungu ajithibitishe mwenyewe?

 

6)Juma lijalo: Damu Isiyo na Hatia.