Somo la 13: Kuishi Kikristo

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Warumi 14)
Swahili
Year: 
2017
Quarter: 
4
Lesson Number: 
13

Somo la 13: Kuishi Kikristo

 

(Warumi 14)

 

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Tunafikia mwisho wa somo letu kwenye mfululizo wa masomo kutoka katika kitabu cha Warumi. Kitabu hiki ni Baraka! Katika suala la kujifunza kivitendo, tutamalizia na Warumi 14 na hatutaweza kupitia sura mbili za mwisho za kitabu cha Warumi. Mojawapo ya sura ya vitabu vya Biblia ninazozipenda sana ni Warumi 14. Huenda ni kwa sababu kinaturuhusu kuwa “wanafiki watakatifu” – katika mazingira fulani. Jambo kubwa kuhusu sura hii ni kwamba Paulo anatufundisha juu ya kile kilicho cha muhimu maishani mwetu kwa ajili ya Kristo. Hebu tuchimbue somo letu la Biblia na tujifunze zaidi!

 

  1. Mboga za Majani

 

    1. Soma Warumi 14:1-2. Kwa nini ulaji wa mbogamboga (na kuachana na ulaji wa nyama) uhusianishwe na imani dhaifu? (Soma 1 Wakorintho 10:18-22. Suala ilikuwa ni endapo nyama iliyokuwa inauzwa sokoni ilikuwa imetolewa sadaka kwa sanamu. Nani angeweza kubainisha hilo? Tunaweza kuona sababu iliyowafanya baadhi ya Wakristo kuwa makini kuhusu kula nyama ambayo yumkini ilikuwa imetolewa sadaka kwa sanamu.)

 

      1. Soma 1 Wakorintho 10:23-26. Paulo anasema kuwa suluhisho kamili juu ya suala hili ni lipi? (Songa mbele na kula nyama. Anachoendelea kukisema Paulo katika 1 Wakorintho 10 kinaakisi kile tunachojifunza katika Warumi 14.)

 

      1. Pitia kwa harakaharaka Matendo 15 ili ujikumbushe juu ya mabishano yanayobishaniwa na kutafutiwa suluhu katika kanisa la awali. Kanisa la awali lilitoa uamuzi gani kuhusu suala la ulaji wa nyama iliyotolewa sadaka kwa sanamu? (Ni mojawapo ya mambo machache yaliyozuiliwa kwa umahsusi kabisa!)

 

    1. Hebu tuangalie tena Warumi 14:1. Ikiwa tuko sahihi kwamba suala ni kuepuka kula nyama iliyotolewa sadaka kwa sanamu (na ni vigumu kufikiria kwamba suala hilo laweza kuwa jambo jingine lolote lile), Paulo analiitaje suala hili? (“Ni suala lenye kuzua mjadala (lenye mashaka).”)

 

      1. Paulo anawezaje kuliita “suala lenye kuzua mjadala” suala lililotatuliwa na kanisa kwenye kikao rasmi kusuluhisha mgogoro kuhusu tohara – na kwa dhahiri masuala mengine kama vile kula nyama zilizotolewa sadaka kwa sanamu? (Hebu tuliweke suala hili mawazoni mwetu na tuone kama tunaweza kulitatua baadaye tunapoendelea kujifunza sehemu iliyosalia ya sura ya 14 ya kitabu cha Warumi.)

 

 

    1. Soma Warumi 14:3-4. Kwa nini Mkristo anapaswa kumkubali mtu anayeenenda kinyume na maamuzi yaliyotolewa na viongozi wa kanisa katika kikao rasmi? (Suala la msingi katika jambo hili lazima litegemee, kwa kiasi kikubwa, kauli iliyopo katika Warumi 14:1 kwamba suala hili “lina mashaka.” Ninadhani kwamba ikiwa kanisa limeamua jambo rasmi, basi halikuwa suala lenye mashaka. Lakini, hii ni sehemu ya fumbo tunalotakiwa kulifumbua.

 

      1. Suluhisho kuu tunalopaswa kulifikia kutokana na usomaji wa hivi vifungu katika Warumi 14 ni lipi? (Tusiwe watu wa kuhukumu. Tusiwaonyeshe dharau watu wasiokubaliana nasi.)

 

  1. Siku Takatifu

 

    1. Soma Warumi 14:5. Ninaichukulia siku ya Jumamosi kuwa Sabato ya kweli kwa mujibu wa Biblia, siku iliyo takatifu zaidi kuliko siku nyingine. Je, Paulo ananizungumzia mimi? Je, ninasahihishwa? (Ukisoma maoni ya kale kuhusu Biblia (takribani miaka 100 iliyopita) utawaona wasomi wa Biblia wa nyakati hizo wanaoishika siku ya Jumapili wakijenga hoja kwa nguvu zote kwamba Paulo hazungumzii siku ya juma ya ibada. Hawakutaka Wakristo waache kwenda kanisani siku ya Jumapili! Walichokuwa wanakihoji wasomi hawa, na ninaamini ni sahihi, ni kwamba sikukuu za Agano la Kale pia zilichukuliwa kama siku takatifu. Kwa kuwa sikukuu hizo zilifungamanishwa na mfumo wa kafara uliotimilizwa pale msalabani, basi ziliendana na tafsiri ya Paulo kuhusu siku takatifu kwamba ni “jambo lenye mashaka.” Sidhani kama kuitunza Sabato ya kila juma kunatiliwa mashaka mahali popote katika Biblia – lakini hilo ni somo jingine.)

 

    1. Soma Warumi 14:6-8. Ikiwa hatukubaliani na mambo yenye mashaka, Paulo anasema kuwa kanuni gani inatumika? (Tunatakiwa kutenda kile tunachodhani kuwa Bwana anakiruhusu na kuwa na shukrani. Lengo katika kila jambo ni kuishi maisha yenye kumpa Mungu utukufu.)

 

      1. Vipi ikiwa mtu anahoji kwamba jambo “lina mashaka,” na hoja ya “mashaka” hayo ni kwamba nyakati zimebadilika na Biblia haina maana tena katika kutatua jambo hilo? (Hoja ya aina hiyo inaibua swali la endapo mtu anayetoa madai hayo anafanya hivyo “kwa Bwana.” Inawezekana kwamba baadhi ya watu hawajali kabisa kile ambacho Mungu anatutaka tukifanye.)

 

  1. Uhusiano

 

    1. Soma Warumi 14:10-12. Tunapaswa kuzingatia hukumu ya nani? (Hukumu ya Mungu. Tunatakiwa kuwa makini kuhusu kuwahukumu watu wengine, na tunatakiwa tunatendee kwa heshima wale wasiokubaliana nasi kwenye mambo yenye mashaka).)

 

    1. Soma Warumi 14:13. Ikiwa tunadhani kuwa tuko sahihi kuhusu jambo fulani, kuna kosa gani katika “kuzibainisha sheria?” Kwa kusema hivyo namaanisha kutekeleza mambo tunayodhani kwamba Mungu anataka tuyatende? (Tatizo ni kusababisha “kikwazo.” Mkristo mwingine anaendelea kukua kiimani na anaweza asiyaelewe vizuri mapenzi ya Mungu. Hatupaswi kumkatisha tamaa mtu huyo asiendelee na safari ya Kikristo kwa kuwa watu wa kuhukumu.)

 

    1. Soma Warumi 14:14. Kanuni ni ipi ikiwa unaamini kuwa hutakiwi kula nyama iliyotolewa sadaka kwa sanamu au kwamba baadhi ya siku takatifu zinatakiwa kuadhimishwa? (Ikiwa unadhani hivyo, basi unapaswa kutenda kile unachoamini kuwa ni sahihi.)

 

 

    1. Soma Warumi 14:15-18. Tunaweza kuona kwa wazi kabisa kwamba Paulo anaunga mkono suala la ulaji nyama na hazingatii siku takatifu zinazoadhimishwa na baadhi ya watu. Nini wajibu wa mtu mwenye mtazamo kama wa Paulo dhidi ya watu wasiokubaliana naye? (Jiepushe kujiingiza kwenye mgongano katika tofauti zenu kwenye mambo yenye mashaka).)

 

      1. Angalia tena Warumi 14:17. Jambo la msingi katika maisha ya Mkristo ni lipi? (“Haki, amani na furaha katika Roho Mtakatifu.” Kisicho cha msingi ni “kula na kunywa.”)

 

      1. Hebu tupitie tena suala nililokuambia kuwa uliweke mawazoni mwako mwanzoni kabisa mwa somo hili. Paulo anawezaje kuuita “wenye mashaka” uamuzi rasmi wa kanisa kuzuia kula nyama zilizotolewa sadaka kwa sanamu? (Ni suala la “kula na kunywa,” na sio suala la haki, amani na furaha. Hii inaturejesha katika sehemu (kipengele) ya somo letu la juma lililopita. Soma Warumi 13:9-10. Hii inafundisha kwamba lengo la Amri Kumi ni kuwaonesha watu wengine upendo. Mara zote tunatakiwa kuweka mawazoni mwetu mambo yaliyo ya muhimu (mtazamo wa upendo na kutafuta amani na furaha) na mambo yasiyo ya muhimu (kanuni zinazohusu ulaji, unywaji na mambo mengine ya kiufundi).)

 

    1. Mara zote Mkristo anatakiwa kuwa radhi kuzichunguza imani zake. Kuna sababu gani kuamini kwamba Sabato sio jambo lenye mambo ya kina ya kiufundi, kama vile kula na kunywa? (Kumbuka kwamba mambo makubwa ni upendo, haki, amani na furaha. Katika kitabu cha Mwanzo, Sabato iliadhimisha kazi ya Mungu ya uumbaji. Katika kitabu cha Kutoka, Sabato iliadhimisha uumbaji na siku ya pumziko. Katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati, Sabato iliadhimisha kuokolewa kutoka utumwani Misri. Pale msalabani, Yesu alipumzika kaburini siku ya Sabato kuadhimisha kuishinda dhambi na kumwokoa kila mtu anayemkiri. Ni vigumu kwangu kufikiria suala lenye uhusiano zaidi na upendo, haki (kwa imani), amani na furaha!)

 

    1. Soma Warumi 14:19-22. Unapaswa kufanya nini ikiwa Mkristo mpya (au dhaifu) anadhani kuwa hupaswi kula au kunywa kitu fulani na wewe, Mkristo mkomavu, unadhani kuwa jambo hilo ni sahihi? (Hapa ndipo tunapotakiwa kuwa “wanafiki watakatifu.” Paulo anatuambia tusile wala kunywa kitu chenye mashaka. Nadhani anamaanisha tusifanye hivyo mbele ya Mkristo dhaifu. Badala yake “fanya hivyo kwa ajili yako peke yako.”)

 

      1. Hii inazungumzia nini kuhusu mjadala wa mambo yenye mashaka katika darasa lako la kujifunza Biblia? (Kuliweka jambo kwa ajili yako peke yako ni ushauri mzuri – hususani pale utakapomfanya Mkristo dhaifu ajikwae.)

 

      1. Vipi kuhusu kuwasaidia watu kuwa wakomavu zaidi katika imani zao? Vipi kuhusu kuwafikisha kwenye hitimisho lenye mantiki zaidi? (Soma Warumi 14:23. Tunatakiwa kukumbuka kwamba isipokuwa tu kama mtu ameshawishika kwenye jambo fulani, basi bado ni dhambi kwake. Hivyo, kuwa makini!)

 

 

    1. Soma Warumi 15:1-4. Hitimisho letu la mwisho linapaswa kuwaje kuhusu huu mjadala wa mambo yenye mashaka? (Lengo ni kujwajenga watu wengine. Tunatakiwa kuitoa sadaka mitazamo yetu (mikomavu, sahihi) ili kuwainua wale wanaotuzunguka walio na ukomavu kidogo. Katika mambo yenye mashaka, lengo la kweli ni kuonesha upendo.)

 

    1. Rafiki, je, somo hili la Warumi limebadili jinsi unavyoifikiria na kuichukulia sheria juu ya namna ya kuishi maisha sahihi? Paulo anatufundisha kuyaangalia mambo kwa kutafakari mambo makubwa. Angalia kama matendo yako yanatangaza haki, upendo, amani na furaha. Kama haujajikita kuzingatia jambo hili katika siku za nyuma, je, utamwomba Roho Mtakatifu akubadilishe mtazamo wako?

 

  1. Juma lijalo: Tutaanza somo jipya kuhusu uwakili.